samora10
JF-Expert Member
- Jul 21, 2010
- 7,602
- 4,811
THESI,
Usihangaike na watu wenye ajenda zao. i) Wachagga nao ni Watanzania na wanahaki zao katika Taifa hili. Mtu yeyote anayejenga chuki ya kikabila bila msingi amefilisika, na hana nafasi katika Taifa hili. Tuliisha kwenda mbali zaidi ya makabila. Dawa ya mtu kama huyo ni wa kumpuuza tu.
ii) Padri Slaa- Kuzini na mke wa mtu. Kama Padri Slaa mwenyewe hakasiriki wala nyie hamhitaji kukasirika. Mwenye mamlaka ya kuhukumu ni Mungu tu na si binadamu mwingine. Unajua walivyokimbia Mahakamani kwa lengo la Propaganda za Kisiasa. Leo wako wapi mbona hakuna anayezungumza tena. Ndio Maana Mimi Padri Slaa, huwa siwajibu, kwa sababu asiyejua bali anajifanya mjuaji ni juha kuliko wale wasiojua. Huyo unasababu ya kubishana naye kwa kuwa hutambadilisha hata ukibishana naye.
iii) Kutishia kumwaga Damu ni kosa la jinai. Kama anajua kuna aliyetishia kumwaga Damu na hajaripoti Polisi ili mhusika akamatwe, basi ni mzushi, mchonganishi na kadhalika na huyo huhitaji pia kuhangaika naye. Au analake jambo, au katumwa na hatumii akili zake bali kichwa anakibeba kama kabichi, kwa kuwa kichwa cha binadamu chenye ubongo kimemumbwa na Mungu kufikiri, kutafakari lakini kama kichwa cha mtu kimejaa tu ushabiki usipoteze muda. Tukumbuke mfano wa Kichaa aliyekimbia na nguo zako na wewe ukimbimkimbiza jamii haitafahamu kichaa ni nani kati yenu. iv) Busara ya mtu inapimwa kwa maneno na matendo yake, na hivyo wapimwe kwa maneno na matendo yao. Tusiwatukane, kwa sababu haisaiidii sana kumpigia Mbuzi Gitaa.... Thanks, na kama nilivyosema siku zote Wasamehewe bure, haigharimu kusamehe bure bali kunakupa thawabu....
Safi sana Dr tunashukuru kwa ushauri wako,Tuko pamoja kwa maslahi ya taifa hili