hp4510
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 7,235
- 7,392
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatarajia kutoa tamko leo Mei 17, 2022, ambapo waandishi wa habari wamekaribishwa kuchukua taarifa ambayo inatarajiwa kuzungumza, lakini kubwa wengi wanaamini itakuwa inahusu sakata la kina Halima Mdee na wenzake 18.
"Wanaojaribu kufanya propaganda huko (Sakata la kina Mdee), suala hili limekwenda mahakamani, tuko tayari na mahakamani wametupeleka eneo ambalo kwetu ni kanda ya faraja, ni eneo tunalomudu. Sidhani kama kuna kesi ambayo Chadema ilishindwa mahakaamni, rekodi bazipo," - John Mrema.
"Fomu za kudhaminiwa kwa hawa wabunge 19, zilitoka wapi na zilikuwa za chama gani? Maana fomu za kudhaminiwa za CHADEMA hadi leo zipo. Katibu Mkuu aliyepeleka majina alikuwa ni wa chama gani kwa kuwa Katibu Mkuu John Mnyika hakuwahi kupeleka majina Tume ya Uchaguzi," - Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara
"Sasa tunakwenda kuwahoji (kina Halima Mdee), nani alisaini barua zao? Nchi hii ingekuwa inafuata sheria, wangekuwa na kesi ya jinai ya kughushi nyaraka na kujipatia fedha za walipa kodi kinyune cha sheria," - John Mrema.
"Ili mtu yeyote awe mbunge wa CHADEMA ni lazima ateuliwa ha kamati kuu ya CHADEMA kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA na mamlaka ambao kamati kuu imepewa," - Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara.
"Walipoitwa (Wabunge 19) kujieleza kamati kuu walisema wanahofia usalama wao na wakaomba wapangiwe siku nyingine. Katibu Mkuu John Mnyika aliwajibu kuwa wenye mamlaka hayo ni Kamati Kuu, hawakutokea. Hivi Mahakamani mshtakiwa asipotokea shauri haliendelei kusikilizwa?" - Benson Kigaila
Chadema acheni kulialia
Nyie mlisema hamtaki vile viti wala hamtaki ruzuku sasa shida ni nn?
Wao wakina mdee wamechukua viti, na mmewafukuza uanachama Sawa sasa why msiendelee na Maisha yenu?
Coz hata wakitoka still vile viti nyie hamvitaki