CHADEMA: Hatutaingilia Mahakama kuhusu kesi ya Wabunge 19 kupinga kuvuliwa uanachama

CHADEMA: Hatutaingilia Mahakama kuhusu kesi ya Wabunge 19 kupinga kuvuliwa uanachama

Hakuna popote wanapopokea ruzuku, fuatilia ujue sio unahisi. Msimamo huu wa kutopokea ruzuku kwa uchaguzi ule wa kihayawani umeifanya tuendelee kuiheshimu CDM.
Kwani wakipokea wewe utajua popote?
 
Naibu katibu mkuu wa Chadema mh Benson Kigaila amesema chama chake hakitapeleka NEC majina ya Wabunge 19 wa viti maalumu kwa sababu hawautambui uchaguzi mkuu wa 2020

Source: ITV

Sasa Mbowe huwa anaalikwa na nani Ikulu?
Anajialika
 
Ndiyo maana serikali imeustukia huo mchezo, mbowe keshaaibika
 
-CHADEMA au Mwenyekiti wa CHADEMA Hana msimamo,alipotoka gerezani alialikwa Ikulu kuonana na Raisi SSH,na alipotoka alionyesha ishara ya maridhiano na kuitambua Serikali ya awamu ya sita , -Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA bwana Tundu Lissu,naye alionyesha ishara ya maridhiano na kuitambua Serikali ya Awamu ya sita, wakati alipofanya mazungumzo na Raisi SSH ubelgiji,na kuomba arejeshewe hati zake za kusafiria na kuahidi kutoa ushirikiano na Serikali ya Awamu ya sita.
-kwa maana tunajenga nyumba moja kwa nini tugombee fito.
-Ni ukweli usiopingika kuwa,aliyevuguruga uchaguzi 2020 hayupo tena na kikosi chake Cha Mataga kimesambaratika.
-Serikali ya Awamu ya sita imejipambanua,kuwa itaendeleza mazuri ya awamu zilizopita na itaachana na mabaya yote ya watungulizi wake.
-Kwa mfano Mama ameamua kuwarejeshea faini ambayo walitozwa viongozi wa CHADEMA kwa kesi gushi.
-Ni busara,CHADEMA wakubali kupeleka majina ya wabunge wengine mbadala kama imeamua kuwaondoa wale ambao walijichagua wenyewe,ili kukidhi takwa la kuwa na kambi rasmi ya upinzani bungeni.
-Kama CHADEMA, wataendelea na msimamo wake wa kutotambua Serikali ya Awamu ya tano, ambayo haipo,sioni uwezekano wa Covid-19 kuondolewa bungeni,
-Covid -19 wataendelea kuwa wabunge mpaka 2025, Mahakama Kuu haitatoa hukumu mapema (Delaying tactics) abadani.
- CHADEMA,ni vema watambue kuwa kwenye siasa hakuna adui au rafiki wa kudumu,kibaraka/mamluki wa leo kesho anaweza kuwa comrade.
 
Hivi wakati Magufuli na CCM kwa ujumla wanakusanya viti vyote hili takwa walikuwa wamelisahau?..Strange indeed.....kila mtu ashinde mechi zake.....
Freeman asipeleke hao wabunge...
Wacha hao 19 waendelee chini ya mwamvuli wa mahakamani mpaka 2025...

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Inashangaza kuona ccm ikitetea kwa nguvu zote hawo wabunge mchongo ili hali Cuf walipowafukuza wabunge wao ccm hawakuonekana popote wakitetea, kweli CDM ni kiboko ya ccm.
 
Naibu katibu mkuu wa Chadema mh Benson Kigaila amesema chama chake hakitapeleka NEC majina ya Wabunge 19 wa viti maalumu kwa sababu hawautambui uchaguzi mkuu wa 2020

Source: ITV

Sasa Mbowe huwa anaalikwa na nani Ikulu?
Rais akishaaposhwa basi hata kama alipindua nchi huna jinsi kwenda nae. Ipo hivyo hata Museveni mwanzo aliupata urais kwa mapinduzi ya kijeshi na alitambulika hata kwa wapinzani wake
 
Kurudisha wabunge wengine sio tatizo kama ulimsoma vizuri Mbowe alivyohutubia mkutano mkuu, alisema, ' kuna kikao cha maliziano kitafuata' hii itajitokeza pale spika atakapowataka CDM walete upya hayo majina 19. Kupitia muafaka hilo linawezekana 100%
 
Sasa kwa hili Mbowe alitaka ajichukulie ujiko, yaani alimtega Mama Samia bonge la mtego yaani Mama angekubali tu akina Halima wafukuzwe bungeni basi hapo hapo Mbowe angesema tunahitaji uchaguzi mpya maan wa 2025 hatuutambui na hatuteui wabunge kwa sababu serikali na rais wake hajatokana na kura
 
Wasalaam wa Ntinginya.Nawasalimu sana.Kama ilivyo ada sipendi kuwachosha ila napenda uwazi na uhalisia bila kuchosha.

Sote tumeshuhudia Baraza kuu LA cdm likifanya uamzi wa pili baada ya ule wa kamati kuu juu ya usaliti wa wabunge almaarufu kama covid 19 (Mdee Et al)

Lakini ninachoona uhalisia wa kesi waliyofungua kupinga kufukuzwa uanachama na hivyo kwenda mahakamani si kutaka kutambulika kama wanachama lakini ni kutaka kulinda maslahi,heshima,protocal na kanuni za Bunge( serikali) ya awamu hii.Kulingana na Sheria za mabinge ya Afrika zipo kamati ambazo bungeni lazima ziongozwe na mbunge kutoka chama cha upinzani mfano kamati ya PAC na LAAC.kwa sababu hiyo kesi iliyopo mahakami ni kati ya Serikali(kulinda ujinga wa bunge) na Mhimili wa mahakama,cdm ni mashahidi wa Mahakama wasioaminiana,kwa nini?kwa sababu mahakama now ni tawi la serikali siyo mhimili na kuukubali ushahidi wa cdm itakula kusaliti Mkubwa wao.Kimsingi mahakama itahitaji kujua katiba ya cdm na bila shaka itaikuta iko sawa na maamzi yake dhidi ya codid19,lakini mahakama italazimika kudharau ushahidi wa cdm ili kulinda ugali.kwa nini?Jaji,Dpp, mawakili wa serikali ni wateule wa ikulu hawana self decision.

Je,Membe alipovuliwa uanachama hata kama hakuwa Mbunge alienda mahakamani?je Sophia simba alienda mahakamani?why?serikali na mahaka ni ndoa.

Cdm na mahakama ni single party katk kesi hii dhidi ya Bunge(serikali) lakini hawaaminiani kwa nini?kwa sababu mahakama tz siyo mhimili tena bali tawi LA serikali.Hata jaji anaamini kuwa sheria Bungeni imekiukwa lakini tumbo linamuuma,vp nafasi yake baada ya maamzi yake!

Tz hakuna mahakama za sheria Luna mahakama majengo.

Swali ni je mahakama itakuwa inafosi waendelee kuwa wanachama wa cdm au kuwa wabunge? Je mtu anaweza kuwa mwanachama wa chama fulani kwa kwa amri ya mahakama?je kadi ya uanachama atapewa mahakamani?

Tafakuri.
 
CHADEMA TOKEA MWANZO WALISEMA HAWATAMBUI UCHAGUZI WA MWAKA 2020 NA HAWATAMBUI MATOKEO, SASA MBONA MMEMUANDIKIA SPIKA BARUA ALIYECHAGULIWA MWAKA 2020, MBONA KILA SIKU IKULU KUJIPENDEKEZA, MBONA MNAWAFUATA FUATA KINA HALIMA MDEE WALIOTOKANA NA UCHAGUZI HUO, MNGEWAACHA KWA KUWA HAMLITAMBUI BUNGE NK

Good! Sasa kama hamtambui uchaguzi wa mwaka 2020 na hutambui matokeo maana yake hata kina @halimamdee83 @esteramosbulaya yaani wabunge 19 hamuwatambui kwa kuwa kilichowapeleka pale ni huo uchaguzi, sasa @jjmnyika @freemanmbowetz mnamuandikia barua Spika gani? Bunge gani?

Uchaguzi wa 2020 na matokeo yake ndiyo yaliyompata Mbunge @TuliaAckson na leo ni Spika wa @bunge_tz, hilo bunge limepatikana 2020, kama hamuutambui uchaguzi mnakomaa na nini? Achaneni na wabunge hao ambao hamjawapeleka na sio wa chama chenu, tena mngewafukuza uanachama bila Barua kwa Spika.

Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Filauni, hamtambui uchaguzi mkuu wa 2020, hamtambui matokeo kutwa kwenye media mnalia lia, mnalilia nini wakati mmeshawafukuza kwenye chama muwaache waliopelekwa na uchaguzi haramu kama mnavyouita, na kama mmeamua kuukubali mseme dunia isikie.

Mwisho:-kwako Spika Dr Tulia Ackson hata Barua usingeisoma kwa kuwa Barua ilikuwa haramu kutoka kwa katibu Mkuu wa chama haramu, kutoka kwa Baraza kuu haramu ambalo halikutambui, Chama ambacho hajitambui ubunge wako wa mwaka 2020, Chama ambacho kimesema uchaguzi ulikuwa si halali na hawatambui matokeo na hivyo hawawatambui wabunge hao 19 sasa kisebu sebu cha nini?
IMG_20220517_222022_996.jpg
IMG_20220517_222022_983.jpg
IMG_20220517_222022_943.jpg
 
Wabunge viti maalumu kupitia chama gani? CHADEMA.

WAMEKATALIWA NA NANI? CHADEMA

wewe unahoji mambo ya chama kingine yasiyo kuhusu?
 
Nafikiri ishu ni kutumia jina la chadema kuwepo bungeni, Kama hawakubaliani na maamuzi ya chadema Basi watafute jina la chama kingine liwaingize bungeni Kama itawezekana
 
Back
Top Bottom