CHADEMA: Hatutaingilia Mahakama kuhusu kesi ya Wabunge 19 kupinga kuvuliwa uanachama

CHADEMA: Hatutaingilia Mahakama kuhusu kesi ya Wabunge 19 kupinga kuvuliwa uanachama

Kimekuwa Chama cha Press kutafuta huruma. CDM hadi sasa haiamini kama inaelekea ukingoni[emoji16]
Isije ikawa ni wewe unayeelekea ukingoni lakini unaona kinyume chake.

Kama ungekuwa mjuzi, ungetambua kuwa ni rahisi zaidi CCM kufa kuliko CHADEMA. Tafakari, kwa nini nimesema hivyo.

JIBU LIPO HAPA:

CCM inapendwa zaidi na WAZEE na watu wajinga. CHADEMA inaungwa mkono zaidi na VIJANA na wasomi (TWAWEZA).
 
Kwanini hamkwenda mahakani kufungua kesi ya fogery document??????
Panua akili, argue intelligently.

Utafunguaje kesi ya forgery wakati hujaoneshwa hiyo document? Kama mkurugenzi wa NEC au Ndugai angewapa nakala ya barua ya uteuzi iliyoandikwa na kusainiwa na Mnyika, hapo wangeweza kufungua kesi ya forgery.
 
Chadema acheni kulialia

Nyie mlisema hamtaki vile viti wala hamtaki ruzuku sasa shida ni nn?

Wao wakina mdee wamechukua viti, na mmewafukuza uanachama Sawa sasa why msiendelee na Maisha yenu?

Coz hata wakitoka still vile viti nyie hamvitaki
Akina Mdee wakae bungeni kwa sababu Rais ameamua hivyo, lakini wakae humo kwa namna yoyote ile iwayo lakini kamwe wasijitambulishe kuwa ni wabunge kupitoa CHADEMA.
 
"Sasa tunakwenda kuwahoji (kina Halima Mdee), nani alisaini barua zao? Nchi hii ingekuwa inafuata sheria, wangekuwa na kesi ya jinai ya kughushi nyaraka na kujipatia fedha za walipa kodi kinyune cha sheria," - John Mrema.
Alafu mkimaliza kubwabwaja hivi mnataka waliofoji vyeti walipwe.
 
Tumeshafika patamu,
NEC mara kadhaa walikataa katakata kutoa MAJIBU kuridhisha, baada ya kuombwa kwa maandishi na CHADEMA. Wala hawakuwa tayari kutoa hata nakala ya documents zinazodaiwa ziliwezesha uteuzi wa covid 19. Sasa kesi iko mahakamani, covid 19 ndio watakaotoa majibu vizuri zaidi na aliyefanya forgery ataweza kujulikana.
La msingi ni kama ingekuwa docs hizo zilikuwa zimetokea ndani ya CHADEMA, ninaamini kuwa zingekuwa ziliishatolewa siku nyingi, ili kuwamaliza. Karibu tena.
Hapo umejibu swali au umelifafanua swali?
 
Kwani wakipokea wewe utajua popote?

Malipo yanafanywa na serekali ya CCM, kama wanaweza kuforge mambo mengi ili kuichafua CDM, watashindwa kuweka stakabadhi za malipo ili kuiumbua cdm?
 
Akina Mdee wakae bungeni kwa sababu Rais ameamua hivyo, lakini wakae humo kwa namna yoyote ile iwayo lakini kamwe wasijitambulishe kuwa ni wabunge kupitoa CHADEMA.

Hahahaha hayo ndio mambo ya mke wako anakuwa rais then Kwa vile una ugomvi nae unamwambia asitumie jina lako
 
UTAKUWA HUJUI VIZURI CHADEMA YAANI HIZO DOCUMENT WANGEKUWA WAMEFOJI NA CDM WANAVYOPENDA KESI WANGEKUWA WAMESHAENDA MUDA MREFU KUSHITAKI NA HUJIULIZI KWANINI WLAIKUWAHWAEND MAHAKAMANI KUWASHITAKI KINA MDEE SASA WANAUMBUKA
Hizo documents ziko tume ya uchaguzi ambazo ndiyo ushahidi, hata copy tu za documents walikataa kuzitoa na ndiyo ushahidi wenyewe.
It's good mambo yako mahakamani na mahakama itawalazimisha kuzitoa, tuendelee tu ku enjoy mtori nyama ziko chini.
 
Ahsante naona kama vile waanza kupata uelewa. Amen
 
Hii propoganda ya kijinga ya kutozungumiza kesi iliyo mahakamani kuna watu wengu wanaiamini.
Nani aliyekudanganya kuwa swala likiwa mahakamani halijadiliwi? Mbona kesi ya Kingai na group lake tuliijadili!?

Inategemea tu unajadili vipi.
 
Panua akili, argue intelligently.

Utafunguaje kesi ya forgery wakati hujaoneshwa hiyo document? Kama mkurugenzi wa NEC au Ndugai angewapa nakala ya barua ya uteuzi iliyoandikwa na kusainiwa na Mnyika, hapo wangeweza kufungua kesi ya forgery.
Sasa wenyewe sio ndio walisema wametumia fogery document kwa maana kwamba wana ushaidi, au wanajisemea tuu
 
Mkuu uandishi huu wa kipumbavu sio mzuri, unalifanya jukwaa hili lionekane ni kijiwe, CDM wameshatolea tamko kuhusu hii issue mara nyingi tu, HAWACHUKUI RUZUKU, looo hii dot.com mnasumbua sana kwa ufikiri wenu butu
Matusi ya nini mkuu? Kwani mhasibu wa cdm ni wewe?
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatarajia kutoa tamko leo Mei 17, 2022, ambapo waandishi wa habari wamekaribishwa kuchukua taarifa ambayo inatarajiwa kuzungumza, lakini kubwa wengi wanaamini itakuwa inahusu sakata la kina Halima Mdee na wenzake 18.

====

"Wanaojaribu kufanya propaganda huko (Sakata la kina Mdee), suala hili limekwenda mahakamani, tuko tayari na mahakamani wametupeleka eneo ambalo kwetu ni kanda ya faraja, ni eneo tunalomudu. Sidhani kama kuna kesi ambayo Chadema ilishindwa mahakaamni, rekodi bazipo," - John Mrema.

"Fomu za kudhaminiwa kwa hawa wabunge 19, zilitoka wapi na zilikuwa za chama gani? Maana fomu za kudhaminiwa za CHADEMA hadi leo zipo. Katibu Mkuu aliyepeleka majina alikuwa ni wa chama gani kwa kuwa Katibu Mkuu John Mnyika hakuwahi kupeleka majina Tume ya Uchaguzi," - Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara

"Sasa tunakwenda kuwahoji (kina Halima Mdee), nani alisaini barua zao? Nchi hii ingekuwa inafuata sheria, wangekuwa na kesi ya jinai ya kughushi nyaraka na kujipatia fedha za walipa kodi kinyune cha sheria," - John Mrema.

"Ili mtu yeyote awe mbunge wa CHADEMA ni lazima ateuliwa ha kamati kuu ya CHADEMA kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA na mamlaka ambao kamati kuu imepewa," - Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara.

"Walipoitwa (Wabunge 19) kujieleza kamati kuu walisema wanahofia usalama wao na wakaomba wapangiwe siku nyingine. Katibu Mkuu John Mnyika aliwajibu kuwa wenye mamlaka hayo ni Kamati Kuu, hawakutokea. Hivi Mahakamani mshtakiwa asipotokea shauri haliendelei kusikilizwa?" - Benson Kigaila

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Benson Kigaila amesema Chama hicho hakitaingilia taratibu zinazoendelea mahakamani kuhusu wabunge 19 waliofutiwa uanachama, huku akisisitiza kuwa hawakuwahi kumteua mtu kuwa mbunge wa viti maalum na hawautambui uchaguzi wa mwaka 2020 wala matunda yoyote ya uchaguzi huo
Chadema wamejaa wivu tu. Kama wakiendelea kuwa Wabunge lakini hawatambuliki nao ingelikuwaje?

Kwasababu viongozi wengi walishindwa kwenye uchaguzi basi wanaona bora wakose wote. Huo ni wivu na husda kali sana.
 
CHADEMA imeshakwisha, sema ina ID nyingi tu mitandaoni.
 
Malipo yanafanywa na serekali ya CCM, kama wanaweza kuforge mambo mengi ili kuichafua CDM, watashindwa kuweka stakabadhi za malipo ili kuiumbua cdm?
Wewe nawe umezidi unazi uko na hoja za kizamani sana yaani kila lawama CCM ata ukishindwa kupata haja kubwa utasema CCM.
 
Back
Top Bottom