CHADEMA: Hatutaingilia Mahakama kuhusu kesi ya Wabunge 19 kupinga kuvuliwa uanachama

Hii ni dharau kwa kodi za wananchi na siyo kwa CHADEMA
 
Mkuu uandishi huu wa kipumbavu sio mzuri, unalifanya jukwaa hili lionekane ni kijiwe, CDM wameshatolea tamko kuhusu hii issue mara nyingi tu, HAWACHUKUI RUZUKU, looo hii dot.com mnasumbua sana kwa ufikiri wenu butu
Hao ni madalali wa CCM
 
sasa chadema wasivyo na viongozi wenye akili unasema hamtaingilia mahakama wakati tayari unazungumzia suala lililoko mahakamani chadema hambna viongozi kuna waganga njaa
Hiyo ni heading tu mmepewa, the rest mtakutana na kina Kibatala ofisini kwao japo jana mlitaka kuwakimbia lakini wapi jamaa wakaibuka tu.
 
Elimu si kigezo cha kuwa kiongozi bora,ndio maana nakuambia acha kuandika upumbavu, President Mugabe alisoma sana ila ameiacha nchi yake masikini sana na almost 20%ya raia wake wakiwa wakimbizi wa kiuchumi,icon pekee Africa, Madiba hakusoma sana kielimu (LLB)but aliiongoza SA in a very trying time, CDM hawakuchukua ruzuku na hii ni fact
 
UTAKUWA HUJUI VIZURI CHADEMA YAANI HIZO DOCUMENT WANGEKUWA WAMEFOJI NA CDM WANAVYOPENDA KESI WANGEKUWA WAMESHAENDA MUDA MREFU KUSHITAKI NA HUJIULIZI KWANINI WLAIKUWAHWAEND MAHAKAMANI KUWASHITAKI KINA MDEE SASA WANAUMBUKA
Ndugu yangu,
nadhani weye ndio sio tu huijui vizuri CHADEMA bali pia huwajui huwajui vyema WAHUNI wanaoshindana kutafuta na kutengeneza mianya ya kuimaliza CHADEMA. Kwa bahati mbaya nawe umejaa kwenye mtego huo.
Hata hivyo kesi hii waliyofungua covid 19 itasaidia SANA kuwafungua wengi macho kuwa HUU ni mwendelezo uleule wa juhudi zilezile za wahuni, tofauti yaweza kuwa mawakala wameongezeka. KATIBA MPYA ndio tiba.

Ndo tushafika patamu, tu karibu na utamu.
Pa ukweli pana tamu, kwa wajuao utamu.
Kwa wa hila si patamu, bali chungu iso tamu.
Siku wakijua tamu, watakuta ziso tamu.
 
Mkuu uandishi huu wa kipumbavu sio mzuri, unalifanya jukwaa hili lionekane ni kijiwe, CDM wameshatolea tamko kuhusu hii issue mara nyingi tu, HAWACHUKUI RUZUKU, looo hii dot.com mnasumbua sana kwa ufikiri wenu butu
Bora umuelimishe maana Ni shida tupu!
 
Ukimkuta Kobe juu ya mnazi ujue Luna aliyempandisha.
CHADEMA walieleza jambo hili Mara zote kwa ufasaha usioacha maswali lakini kina Mdee+wenzake na watetezi wao CCM,Bunge,NEC,Serikali na Sasa Mahakama tukufu hawaelewi chochote pamoja na maelezo fasaha.Spika anajifanya hamnzo kwa kudai anasubiri uamuzi Wa Mahakama kabla hats shauri halijasikilizwa/kuamuliwa.Hii ni sawa na kusema Spika amei per-empty mahakama halafu nayo ikafuatisha hivyo hivyo.
Katiba hii mbovu wanayoitetea hawaiheshim lakini bado wapo kwenye nyadhifa zao kwa sababu katiba mbovu inawalinda na Watanzania wapo kwenye silent mood,hawalalamikii hilo na hawajitetei wala hawailindi Katiba ya 1977,hawashinikizi kuipata mpya wala hawawajibishi viongozi waliojibadilisha kuwa miungu watu na ni kama tumepigwa ganzi ya ubongo vile.
Tunahitaji nchi yetu ya Tanganyika maana huku Tanzania pametushinda.Bora turudi nyumbani hata kama ni kubaya,tutajenga upya.
 
Wasisusie mwaliko wa Ikulu tu. Sakata la kina Mdee tayari lipo Mahakamani hairuhusiwi kulijadili hadi kesi iishe hapo December 2024
Nani aliyekudanganya kuwa swala likiwa mahakamani halijadiliwi? Mbona kesi ya Kingai na group lake tuliijadili!?

Inategemea tu unajadili vipi.
 
Naibu katibu mkuu wa Chadema mh Benson Kigaila amesema chama chake hakitapeleka NEC majina ya Wabunge 19 wa viti maalumu kwa sababu hawautambui uchaguzi mkuu wa 2020

Source: ITV

Sasa Mbowe huwa anaalikwa na nani Ikulu?
 
Wapuuzi Sasa kelele za nn kwa WANAWAKE 19 so wawache tu hatakama hawatakuwa na chama , wamekuwa joka la mdimu

USSR
 
Hawa waliopo alipeleka nani? Ni vipi suala hilo lisipatiwe ufumbuzi, hata kesi ya kutetea uanachama wao isingekuwepo!
 
Naibu katibu mkuu wa Chadema mh Benson Kigaila amesema chama chake hakitapeleka NEC majina ya Wabunge 19 wa viti maalumu kwa sababu hawautambui uchaguzi mkuu wa 2020

Source: ITV

Sasa Mbowe huwa anaalikwa na nani Ikulu?
Eeh waache kwani nani anawalazimisha? Kwani wasipoteua itakwamisha Serikali au kuleta njaa kwa watu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…