Mkapa alikaa kimya siku zote kwa mambo asiyoyajua. Wastaafu wangapi waliongea?
Mlitaka asemaje wakati wapo wanaoamini TL aliliwa shaba na watu wake?
Nyie andamaneni tu kama mnataka kumfuata huko aliko. Wanakulitafuta Wanakulipata. Msije kulialia tu badaaye.
Tena hapa unaleta hoja nyingine . Hawa viongozi wakishastaafu wanavua joho la uongozi kitaifa na kuwa makada wa vyama vyao. Ni Mwalimu Nyerere peke yake alibaki kuwa 'statesman'' akizungumzia mambo ya kitaifa na kimataifa bila kuingiza uchama.
Waliofuata hakuna hata mmoja anayezungumza kama kiongozi mstaafu, wote huzungumza kama makada wa CCM
Juzi ulimsikia Mwinyi akisisitiza katiba ibadilishwe, si kusisitiza kuhusu Tume huru ya uchaguzi.
Mkapa alizungumzia Tume huru akiwa 'amejificha' nyuma ya kitabu chake, ingawa alijua ni suala la Kitaifa
Hakuwahi kutokan na kuzungumza kama mstaafu kuhusu umuhimu wa katiba
Akaongelea usia wa Nyerere kuhusu dini na ukabila kupitia kitabu chake, si kama Rais mstaafu
Kikwete ni kama waliomtangulia, naye haongei kwasababu kuna 'maslahi' ya chama hasa Wabunge wa Familia yake
Mimi sioni sababu ya viongozi wastaafu kupewa hadhi za kitaifa , pengine CCM ingewapa hadhi za kichama
Wanapomaliza muda wao , na ni ukweli usiopingika hawana msaada kwa taifa bali kwa CCM
Ni kwa mantiki hiyo sioni sababu za kuzuia wanachama wengine wasiendelee na shughuli zinazohusu makada wao
CCM wanaweza kuendelea na shughuli zao kama ilivyo ACT na Chadema. Sioni tatizo lolote katika hilo