KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 3,250
- 5,509
Siasa ni kama biashara ,ni ngumu sana kama haujajipanga vema kukabiliana na mazingira ya ushindani na mshindani wako ukitambua ni Chama chenye nguvu.
Nasema haya kwa sababu siku za karibuni siioni CHADEMA Ile ya kina Dkt. Slaa ambayo ilikuwa msingi wa kujenga Chama imara, siioni Ile CHADEMA ilivyokuwa inakusanya kijiji mahali popote, siioni CHADEMA Ile yenye hoja zenye ushawishi, siioni CHADEMA Ile makini ila ya sasa inasikitisha.
CHADEMA ya sasa ni ya kufanya mikutano kwenye mikusanyiko kama masokoni na stendi kweli? Je, wanahofu kutopata watu?
CHADEMA ya sasa ni ya kupitisha bakuli la michango kwa wananchi hali wakijua wananchi wanahitaji sera ila sio kuchangishana. Je, hayo ni majuto ya kutopokea ruzuku?
Sasa , ni muda muafaka kwa CHADEMA kujipanga na kurudi kwenye misingi yake ili muda wote kisilalamike kuonewa kumbe kinakimbia udhaifu wake.