Elections 2015 CHADEMA ikipewa Nchi, Oktoba 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu!

Pasco

uchambuzi uliotoa kuhusu shida ya katiba ya Chadema na usimamiaji wa Katiba husika haujazingatia kiini cha migogoro ndani ya Chadema na namna chama kinavyotumia miongozo yake kutanzua hiyo migogoro.

Hivi, andiko hili ulobandika hapa, unataka tuamini ati ni hao waliofukuzwa pekee ndio wanafahamu kuhusu kunyofolewa kwa vifungu vya katiba ya Chadema peke Yao?

ndio kusema maelfu ya wanachadema waliobaki Hawajui lolote kuhusu vifungu tajwa?

Jipya lingine ninaloliona kwenye post yako ni kuwa: Chadema wanafanya makosa kama sio dhambi kusimamia misingi ya chama chao, hivi sio Pasco huyuhuyu anayewakemea CCM WANAPOSHINDWA kusimamia misingi ya chama chao? Ama Pasco unafikiri CCM wakianza kusimamia misingi yao Leo hii, utasema CCM wanaongoza ki-dikteta?

Nauliza tu!
 
Chadema ni genge la watu wa hovyo hovyo

Kwa nini?
Kwa kusimamia katiba yake? Mmezoea kuishi kwa kudanganyadanganya...Vyama vipo vingi. Kuna chama watu wamekwiba pesa za ummahalafu wanasema pesa sio ya umma, mara mna wivu wa kike....Majina ya waliobeba pesa kwenye lumbesa na magunia pale Stanbic mpaka leo hayajulikani. Ndio mnapenda chama cha design hio. Nchi ya ujanja ujanja...Na maigizo ya tume ya maadili na CC ya chama chao..


Sheria na katiba ikifuatwa mnanuna. Mnaita ovyo ovyo
 

Mkuu kwa hilo ulilolisema nakubaliana na wewe kwa asilimia zote kua nchi haihitaji sana viongozi wanasiasa katika maendeleo bali wataalam.
Hata hivyo kwa chadema bado haijawa na wataalam wa kutosha katika safu yake ya uongozi, mi nafikiri njia pekee ya kulifanikisha hilo ni mabadiliko ya katiba kwanza ili chama tawala tukibanie huko.
Lakini kaka kwa chadema kuchukua nchi kwa sasa bado mapema sana japo sisi sote tunataka mabadiliko
 

Katiba ya Chadema iliandikwa na wanachadema kwa matumizi ya wanachadema kwa malengo ya CHADEMA na manufaa ya wana CHADEMA na ilipitishwa na Wanachadem
 

Mkuu devcon,
Natambua wasiwasi wako juu ya political maturity cha CHADEMA na vyama vingine vya Kisiasa hata ikiwepo CCM. Wakati Mwalimu nyerere anapewa kuongoza dola ya Tanganyika hakuwa na zaidi ya miaka 40 ki umri, akiwa na Madatari wazawa wasiozidi 3 na bila Wahandisi. Aliiongoza nchi katika kipindi cha mpito na kufanya maamuzi mengi mazuri na mabaya machache. Kipindi hiko ukumbuke kulikuwa na utawala wa machifu na makabila hivyo kuileta nchi pamoja haikuwa jambo rahisi kama watu tunavyoweza kufikiri. Sasa,ukirejea kwa Vyama Pinzani ni kweli Political maturity inaweza kuwa kidogo lakini kuna watanzania wengi tu wenye nia njema kila mahali hata huko CCM watakaounga mkonona kukusaidia chama kuongoza nchi.Mabadiriko ni muhimu katika hii nchi kwa sasa ama la utaishi wewe kwa raha kwa sababu unajuana na fulani ila wanao ukiwaacha leo their survival is deeply at risk. Nchi hii sasa tunamilikisha kwa watawala na familia zao,akiji mwingine nae afanye hivyo na wanawe tutafikia wapi? We need changes NOW whether taking risk or no,the higher the risk the higher the reward. Wapinzani wajiunge and perform as a Team (Common goal) kuwaletea Watanzania maendeleo na kufungua minyororo ya utumwa mpya unaotengenezwa
 

Kaka Marshal nakupata sana kiongozi na ninakubaliana na wewe katika point yako ulosema kua wapinzani wajiunge as a team to archive a common goal.
Hiyo ndo point ya msingi na ndo nguvu pekee itakayowatoa ccm madarakani,lakini kaka hivi unafikiri ni kwanini toka vyama vingi kuanzishwa ndani ya nchi hii wapinzani hawataki kuungana na wala hawana mpango huo wakati dhamira yao ni moja?
Hapo mimi ndo huwa napata hofu na wasiwasi juu ya viongozi wetu wa upinzani, any way mana mungu anasema kila ugonjwa una dawa yake isipokua kifo na uzee naamini ipo siku wapinzani wataliona hili na ndo itakua dawa ya CCM.
 

Mkuu devcon,
Sisasa za vyama vingi ni ngumu na inachukua muda kwa vyama pinzani kuweza kukitoa chama Ongoza madarakani. Iwapo unatambua mfumo wa divide and rule ndio kikubwa hasa kinachowapa CCM nguvu. Wanamapandikizi yao katika vyama pinzani na kwa sababu ya umaskini watu wengi ni wasaliti hasa unapopewa brifkesi imejaa pesa. Wengi wa wanasiasa tulionao wa vyama vyote kwenye ikiwemo CCM ni wadhaifu kwene pesa kuliko hata changudoa.. believe me or not wengi wapo pale kwa ajili ya matumbo yao na ndio maana itachukua muda mrefu sana kwa wapinzani kuwa na lengo moja... Njaa mwanaharamu eti :smile-big:
 

Hahahahah umenifurahisha sana kaka njaa ni mwanaharamu, ni kweli kabisa na umasikini ni nusu ya ukafiri, Dah sasa tufanye kaka na hali ndo hii tulo nayo na hawa jamaa wanatumia udhaifu huo?
 
Mambo yao ya ndani yanaammuriwa kiaina aina nchi wataiweza kweli.....
 
nijuavyo mimi a litigant has no right to a favourable decision but a right decision, kwa hiyo wafuasi wa Zito kama Pasco kama yangetolewa maamuzi tofauti mngetoa misimamo tofauti pia, ukiisoma vizuri katiba ya CDM huwezi kuona kama kuna kipengele chochote kinachokiuka katiba isipokuwa mwanachama ahakikishe kuwa amefuata taratibu zote za chama, katiba nyingi za kitaasisi ziko hivyo. pia suala la ukomo wa madaraka hapa niwe muwazi demokrasia siyo ukomo wa madaraka isipokuwa njia zinazotumika kupata maamuzi ya mwisho. malkia wa Uingereza hachaguliwi na wananchi na hana ukomo wa madaraka je ni dikteta? Pasco rudi ukatafiti upya hapa umechemsha mno.
 
Mfia pesa tumeshakozea yule jamaa yako anaewapa nyama choma mwaka mpya na chris mass anaumwa vibaya sana hawezi hata kunyanyua kikombe cha kahawa
 
KWA hiyo unataka tuendelee kuwapa nchi ccm tuendelee kuibiwa? wewe unampigania mzee wa watu afya mgogoro,spana mkononi kwa taairifa yako hatutaki kuwapa nchi wagonjwa tupate hasara ya kurudia uchaguzi kila kukicha kama zambia
 
bw pasco tanzania inahitaji kiongozi dikteta ili kurudisha misingi ya azimio la arusha​,
 
Labda ni bora tuwe na Serikali ya Kidikteta, ili watu wanyooke, wawajibike, waache kugeuza kila kitu DILI!

Ukienda Polisi, akikamatwa mtu, hawamwulizi kama ana hatia. Wanauliza ana pesa kiasi gani ili wamuachie. Askari wanashirikiana na majambazi. HATUNA Jeshi la Polisi linalostahili kuitwa Jeshi la Polisi.

Ukienda Hospitali, mgonjwa - haswa mjamzito - anaulizwa ana pesa kiasi gani, ili aweze kupata huduma stahiki. Asiye na pesa atajifungulia hapo hapo chini, sakafuni, na kama sio siku yake ya kuitwa na Yehova, atapona. La sivyo MTAZIKA! Wauguzi na madaktari wameigeuza kazi yako kuwa ajira!

Ukienda Mahakamani, hapo laana tupu. Mtu amekamatwa na ushahidi umetimia, lakini nduguze "wanamweka sawa" Hakimu. Kesi itakapoanza kusikilizwa kuna kitu kinaitwa Preliminary Hearing, ambapo Waendesha Mashtaka (Mawakili wa Serikali) ndio wanapaswa kusema iwapo watuhumiwa ana kesi ya kujibu au la. Baada ya hapo, kesi inaahirishwa ili Hakimu apitie vielelezo vya State Attorneys. Kesi inaporudi kuanza kusikilizwa, Hakimu anasema ushahidi hautoshi, kwa hiyo bora Mahakama isipoteze muda na fedha za serikali. Mtuhumiwa anachoropoka.

Wizarani huko ni balaa! Wanajipangia masurufu kwenye kasma za Semina, Warsha, Makongamano, ambayo yote ni HEWA. Pia kuna wafanyakazi HEWA, ambao ni wale waliostaafu, waliofariki, waliopunguzwa, n.k. Wanaendelea kulipwa na TAMISEMI inalijua hili. Hata HAZINA nako wanajua.

Sasa mnaitaka Serikali LEGELEGE ya CCM au mnaitaka Serikali DIKTETA ya CHADEMA, itakayofuta ufedhuli wote huu?

Kuna mengi sijayasema.... yanakera MNO!
 
PRINCE CROWN ninakuunga mkono. Demokrasia haifai kuwapo Tanzania kwa sasa. Kilichobaki ni UDIKTETA TU!

Mbona tayari sera isiyo rasmi ya CCM, "wapigwe tu" inatumika, na wananchi wanaifumbia macho? UDIKTETA wa KIFICHO wa CCM usihalalishwe kuliko huo ambao ni wa WAZI wa CHADEMA.

PEOPLE's POWER!
 
Last edited by a moderator:
Pasco tukitaka kuwa fair,basi tukubali hili:Sheria za nyumbani kwako zikivunjwa na wewe ndiyo kichwa cha nyumba basi lazima utachukua hatua stahiki.Usipofanya hivyo na Mama watoto ndiyo akawa mchukua majukumu ya kutoa adhabu stahiki pale sheria za nyumba yenu zinapovunjwa basi waswahili watasema Pasco amepewa limbwata au mkeo ndiyo mwenye sauti na wewe mzee huna usemi juu ya lolote.

Na ukishaambiwa hivyo kwa mbantu kama wewe shemeji yangu ambaye kupewa maji ya kunywa binti lazima apige magoti mpaka umalize kunywa maji na kumrudishia glass,na isipofanyika hivyo basi mwali wako huyo hafundishwa heshima vyema na mamaye lazima asakamwe.

Ndiyo hivyo hivyo kwa vyama na serikali.Na kama tungekuwa na viongozi ambao wanafuata sheria tuliojiwekea basi RUSHWA,UFISADI,Mauaji ya ALBINO na hata vyama vingi vingekuwa hadithi tu.

Lakini sababu viongozi wetu sheria tulizojiwekea zenyewe wanavunja,kwanini tuwakodolee macho wanaotetea katiba na sheria za chama chao?

Pasco kama mwanasheria nadhani ungewapa hongera sana kwa kuikingia kifua katiba na sheria zao.
 



yaani ninauhakika kabisa wanaturudisha kule kwa IDDI AMINI watu tufanye uamuzi vizuri na hawa CHADEMA wameanza kujichanganya wenyewe.......
wamekuja vizuri na sera sera zao saivi wameshaanza kuonyesha MAKUCHA.......
 
Nchi yetu,bila kutawaliwa kidikiteta hataenda,hapa ilipofikia hakuna mwenye Kauai ya mwisho,mafisadi wanalindwa,waauwaji wa alubinyo hawashughulikiwi ipasavyo,wataalumu wetu wamegeuka wanasiasa baada ya kuona ndipo mahali pa kuwatoa fasta kimaisha,wafanyabiashara wakubwa wamegeuka viongozi wa kisiasa kukwepa kulipa kodi,na kufanya biashara haramu .afu useme uitawale tanzania kawaida kawaida tu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…