Maboso
JF-Expert Member
- Feb 18, 2013
- 5,164
- 5,762
Alianza ishu ya ukomo wa uongozi, nikaguna baada ya kuhisi ukakasi wa kipengele cha kutokuwa na ukomo wa uongozi. Nilijifariji nikidhani labda viongozi na wanachama walipitiwa kwenye hicho kipengele. Leo hii limekuja suala la mahakama, kwa kiasi fulani nilishindwa kumwelewa Lissu aliposema eti mwanachama hapaswi kwenda mahakamani, nikaguna ila kama kawaida yangu nikatafuta katiba ya Chadema, kiukweli nadiriki kusema neno DEMOKRASIA halipaswi kutumiwa na Chadema hata kidogo. Hata jina la chama tu lingebadilishwa. Huwezi kuhubiri demokrasia wakati unazuia watu kwenda mahakamani. Hii si sawa hata kidogo. Kuna baadhi ya watu wanasema eti hata TFF hupaswi kwenda mahakamani. Wanakosea, TFF au mpira wa miguu wana mahakama zao na wanasheria waliosomea sheria za mpira wa miguu. Kinachokatazwa ni kwenda kwenye hizi makahakama ambazo si za michezo, ila kwenda mahakama ya mpira wa miguu inaruhusiwa. Sasa Chadema wamekuwa wao ndio mahakama, wao ndio majaji, wao ndio vyombo vya dola. Katiba wameiweka kiasi kwamba mwanachama hana haki yoyote ile pindi linapokuja suala laa kutafuta suluhu. Sidhani kama demokrasia ipo namna hii. Wengi leo wanashangailia labda kwa sababu hawampendi Zitto, ni sawa, ni haki yao. Lakini ifike mahali tuangalie haya mapungufu ya katiba kwa mapana zaidi.