Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,404
- 6,969
Mgombea urais wa Chadema kwa ngazi ya urais JMT alienda Zanzibar akafanya mkutano,na katika mkutano alioufanya aliongea mambo mengi,ikiwemo kutaka kuwe na muungano wa Serikali tatu. Lakini alienda mbele na kutoa kauli za kuonyesha hatambui kitu kinachoitwa Tanzania bara, bali anatambua uwepo wa Tanganyika.Na ndio maana alikazia maneno kuwa Tanganyika inaikalia kimabavu Zanzibar.
Mbali ya hayo alimalizia kwa kusema yeye anamuunga mkono mgombea wa Act wazalendo. Jambo la kushangaza ni kuwa CHADEMA wameweka mgombea Zanzibar.
Je, kama mgombea urais wa CHADEMA anamuunga mkono maalim Seif, je ni kwa nini waweke mgombea Zanzibar? Je huku sio kuwadharau wazanzibar na kuwaona wajinga? Kwanini CHADEMA wasingeacha kuweka mgombea kama wanamuunga mkono Maalim Seif.
Je, hizo kampeni wanaenda kufanya za nini huko Zanzibar kama wanamuunga mkono maalim Seif?