Zanzibar 2020 CHADEMA inawaona Wazanzibar ni wajinga?

Zanzibar 2020 CHADEMA inawaona Wazanzibar ni wajinga?

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Mgombea urais wa Chadema kwa ngazi ya urais JMT alienda Zanzibar akafanya mkutano,na katika mkutano alioufanya aliongea mambo mengi,ikiwemo kutaka kuwe na muungano wa Serikali tatu. Lakini alienda mbele na kutoa kauli za kuonyesha hatambui kitu kinachoitwa Tanzania bara, bali anatambua uwepo wa Tanganyika.Na ndio maana alikazia maneno kuwa Tanganyika inaikalia kimabavu Zanzibar.

Mbali ya hayo alimalizia kwa kusema yeye anamuunga mkono mgombea wa Act wazalendo. Jambo la kushangaza ni kuwa CHADEMA wameweka mgombea Zanzibar.

Je, kama mgombea urais wa CHADEMA anamuunga mkono maalim Seif, je ni kwa nini waweke mgombea Zanzibar? Je huku sio kuwadharau wazanzibar na kuwaona wajinga? Kwanini CHADEMA wasingeacha kuweka mgombea kama wanamuunga mkono Maalim Seif.

Je, hizo kampeni wanaenda kufanya za nini huko Zanzibar kama wanamuunga mkono maalim Seif?
 
Nini hujaelewa hapo!! Tundu anamuunga mkono maalim Sef lakini CHADEMA kama chama kinamuunga mkono mgombea wao ngazi ya urasi wa Tanzania visiwani. Elewa Chadema ni Mbowe
 
..kulikuwa na uwezekano wa Tume kutokumteua Maalim Seif kugombea Uraisi wa Znz.

..sasa maadam jina la Maalim Seif liko ktk ballot, basi Chadema hawana haja ya kuendelea kusimamisha mgombea wa Uraisi wa Znz.

..Pia huku Tanganyika kulikuwa na uwezekano wa Tundu Lissu au Bernard Membe kuenguliwa na tume.

..Sasa kwasababu wote wapo ktk ballot paper, na imebainika kwamba Lissu anaungwa mkono zaidi, basi hakuna haja ya vyama vya ACT na Chadema kugawana kura ktk nafasi ya Uraisi wa muungano.
 
Nini hujaelewa hapo!! Tundu anamuunga mkono maalim Sef lakini CDM kama chama kinamuunga mkono mgombea wao ngazi ya urasi wa Tanzania visiwani. Elewa Chadema ni Mbowe
Duh,hapo si kuwachanganya watu?
 
..kulikuwa na uwezekano wa Tume kutokumteua Maalim Seif kugombea Uraisi wa Znz.

..sasa maadam jina la Maalim Seif liko ktk ballot, basi Chadema hawana haja ya kuendelea kusimamisha mgombea wa Uraisi wa Znz.

..Pia huku Tanganyika kulikuwa na uwezekano wa Tundu Lissu au Bernard Membe kuenguliwa na tume.

..Sasa kwasababu wote wapo ktk ballot paper, na imebainika kwamba Lissu anaungwa mkono zaidi, basi hakuna haja ya vyama vya ACT na Chadema kugawana kura ktk nafasi ya Uraisi wa muungano.
Unatoa wazo? Au unasema nini?
 
Kwasababu hujahoji kitu,kwa kifupi umeandika pumba.
Mnawaona Watanzania Zanzibar wajinga? Chama kinaweka mgombea,alafu mgombea wenu anamuunga mkono maalim Seif.
 
Kuna tofauti kati ya Tundu Lisu kama " mtu" na Chadema kama " chama"

Ndio maana mwenyekiti wa TLP na mgombea ubunge wa Vunjo Dr Mrema anamuunga mkono Dr Magufuli wa CCM!
 
Kuna tofauti kati ya Tundu Lisu kama " mtu" na Chadema kama " chama"

Ndio maana mwenyekiti wa TLP na mgombea ubunge wa Vunjo Dr Mrema anamuunga mkono Dr Magufuli wa CCM!
Amesimamisha mgombea urais wa JMT?
 
Hata bara ACT wametamka kumuunga mkono mgombea urais Tundu Antipas Lissu.
 
Kuna tofauti kati ya Tundu Lisu kama " mtu" na Chadema kama " chama"

Ndio maana mwenyekiti wa TLP na mgombea ubunge wa Vunjo Dr Mrema anamuunga mkono Dr Magufuli wa CCM!

..Mrema alisema chama cha TLP kinamuunga mkono Jpm ktk nafasi ya Uraisi wa muungano.

..tena alitangaza msimamo huo ktk mkutano mkuu wa ccm na Shisty Nahodha alikuwa pembeni ya Mzee Mrema wakati akitoa tamko hilo.

Je Tlp wameweka mgombea urais wa JMT?
 
Back
Top Bottom