figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
TAARIFA KWA UMMA
Kamati Kuu ya Chadema iliyokutana katika kikao chake maalum cha siku mbili kuanzia juzi tarehe 11 mpaka 12 Machi 2025 ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Tundu Lissu imefanya uteuzi wa Wakurugenzi kwa mujibu wa ibara ya 7.7.16 (b) na Wataalamu mbalimbali wa Makao Makuu ya Chama kwa mujibu wa ibara ya 7.7.17 (e) ya Katiba ya Chama toleo la mwaka 2019 kama ifuatavyo;
A) WAKURUGENZI
1. John Pambalu; ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Uchaguzi.
2. John Kitoka; ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Diaspora.
3. Wakili Gaston Garubindi; ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu.
4. Bi. Brenda Rupia; ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi.
B) WATAALAMU
1. Bi. Catherine Ruge: Mtaalamu wa dawati la jinsia.
2. Leornad Magere: Mtaalamu wa Rasilimali, Miradi na Uwekezaji.
Aidha, Kamati Kuu imethibitisha Makatibu wa Kanda nne za Chama kwa mujibu wa ibara ya 7.7.16 (c) kama ifuatavyo;
1. Bi. Ashura Masoud; amethibitishwa kuwa Katibu wa Kanda ya Kati inayojumuisha mikoa ya Dodoma, Morogoro na Singida.
2. Benjamin Ntele: amethibitishwa kuwa Katibu wa Kanda ya Pwani inayojumuisha mikoa ya kichama ya Ubungo, Ilala, Kinondoni, Temeke na Pwani.
3. Totinan Ndonde: amethibitishwa kuwa Katibu wa Kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga.
4. Edger Malimusi: amethibitishwa kuwa Katibu wa Kanda ya Kusini inayojumuisha mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma
Imetolewa leo Jumatano tarehe 12 Machi 2025.
Apolinary Boniface Margwe
Msaidizi - Kurugenzi ya Mawasiliano na Uenezi