Kamati Kuu ya CHADEMA iliyoongozwa na Tundu Lissu, yateua Wakurugenzi wapya

Kamati Kuu ya CHADEMA iliyoongozwa na Tundu Lissu, yateua Wakurugenzi wapya

Napata shida sana kujibu mawazo ya namna hii kwa Tanzania yetu hii.
Nashukuru tu kwamba hao unaowaita "...anayejitambua" (bila shaka wewe ukiwa ni mfano wao) siyo wawakilishi wa waTanzania waislamu. Mtatafuta kila njia za kuwagawa waTanzania katika makundi kama haya kwa faida zenu, lakini hamtafanikiwa.
Nyie ndo mmeshafanikiwa kutugawa. Chama kinaonyesha udini waziwazi. Haya bila shaka ni mapendekezo ya Padri Slaa na Padri Kitime mana ndo walomuweka Mkatoliki mwenzao hapo
 
TAARIFA KWA UMMA

Kamati Kuu ya Chadema iliyokutana katika kikao chake maalum cha siku mbili kuanzia juzi tarehe 11 mpaka 12 Machi 2025 ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Tundu Lissu imefanya uteuzi wa Wakurugenzi kwa mujibu wa ibara ya 7.7.16 (b) na Wataalamu mbalimbali wa Makao Makuu ya Chama kwa mujibu wa ibara ya 7.7.17 (e) ya Katiba ya Chama toleo la mwaka 2019 kama ifuatavyo;

A) WAKURUGENZI
1. John Pambalu;
ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Uchaguzi.

2. John Kitoka; ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Diaspora.

3. Wakili Gaston Garubindi; ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu.

4. Bi. Brenda Rupia; ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi.

B) WATAALAMU
1. Bi. Catherine Ruge:
Mtaalamu wa dawati la jinsia.

2. Leornad Magere: Mtaalamu wa Rasilimali, Miradi na Uwekezaji.

Aidha, Kamati Kuu imethibitisha Makatibu wa Kanda nne za Chama kwa mujibu wa ibara ya 7.7.16 (c) kama ifuatavyo;

1. Bi. Ashura Masoud; amethibitishwa kuwa Katibu wa Kanda ya Kati inayojumuisha mikoa ya Dodoma, Morogoro na Singida.

2. Benjamin Ntele: amethibitishwa kuwa Katibu wa Kanda ya Pwani inayojumuisha mikoa ya kichama ya Ubungo, Ilala, Kinondoni, Temeke na Pwani.

3. Totinan Ndonde: amethibitishwa kuwa Katibu wa Kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga.

4. Edger Malimusi: amethibitishwa kuwa Katibu wa Kanda ya Kusini inayojumuisha mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma

Imetolewa leo Jumatano tarehe 12 Machi 2025.

Apolinary Boniface Margwe
Msaidizi - Kurugenzi ya Mawasiliano na Uenezi


Shida shaka kuwa huu uteuzi haujazingatia vigezo vya Dini kwenye nafasi zote Muislam ni Moja tu, kweli Mh Mwenyekiti Hana Udini , ni Mwadilifu sana kwenye kulinda Imani yake.

Bila shaka ni wakati wa Kina John Kula mema ya Chama
 
Tone tone imegoma John Mrema alisema mnataka kumfukuza uanachama muweke mtu wenu kama mkurugenzi wa fedha

Lisu kanywea kamuacha kumtoa baada ya kuona tone tone limedoda sababu ya matajiri wa kichaga kuzira kwa mchezo mchafu Lisu alimchezea Mbowe kushinda uenyekiti

Matqjiri wakubwq wa kichaga Tone tone wakagoma kuchangia

Kaunda muundo feki feki cheo cha Mkurugenzi wa fedha karuka

Wenye macho na akili zetu tunaona wajinga wa Chadema tu ndio hawawezi ona
Mchezo mchafu upi?
 

Attachments

  • images (13) (1).jpeg
    images (13) (1).jpeg
    10.9 KB · Views: 0
John Mrema mkurugenzi wa fedha

wamemgwaya

Chezea wewe

Lisu na ubabe wake baada ya kuona tone tone linadoda anaogopa kumtoa ukurugenzi wa fedha John Mrema kuwinda pesa za wachaga
Una comment bila hata kusoma...

Upo kama robot ambalo liko kwenye auto - setting....

Wewe Shotocan hufikiri wala kuwaza kwanza kabla ya kuandika/kusema kwa kuzingatia uhalisia wa kilichopo mezani...

Moyo wako umejaa chuki na mabaya tu kwa watu wengine usiowapenda. Kwanini unajiumiza hivyo bila sbb..?

Nani kakuambia ni Mkurugenzi wa Fedha? Umeona wapi?
 
Back
Top Bottom