Tetesi: CHADEMA kufutwa?

Muwe mnavichunguza vyama iwapo mna mapenzi ya vyama,siyo kuvishabikia tu bila kujua kua ni vyama vya wahuni tu
Kuna taarifa zinasambaa kwenye magroup ya whatApp ya kuwepo mkakati wa kuifuta chadema kabla ya uchaguzi mkuu mwaka huu. je hizi taarifa ni kweli? Kama ni kweli nini malengo ya watu waliopanga ili jambo? hawaoni wanaiweka amani yetu mashakani?
 
kwa mujibu wa sheria Chama hakiwezi kufutwa Mwaka wa Uchaguzi. Puuza hayo mambo
Mkuu zito!hv kule zanzibar ccm wapo tayari kumsaliti dr.Hussein mwinyi ili maalim seif ashinde ????mi nadhani kile kikao cha ikulu cha akina seifu na mbatia ni changa la macho tu!!!!reserve my coment!!!ccm ni joka limezalo!!!
 
Hilo nalisikia pia,mchongo mzima umeanzia takukuru na mpira utatupwa kwa msajiri kuipeleka kibra,na mambo ya GAC kuhusu ukaguzi was mahesabu ya vyama hayazingatiwi.
 
Bunge la Tanzania kwa sasa linaendeshwa kwa mujibu wa Sheria binafsi za Ndungai siyo kwa mujibu wa Sheria za jamhuri ya muungano wa Tanzania
Shida ni akidi tu hata lile la Sitta,Makinda upinzani haujawahi kuwa na athari kwenye maamuzi yoyote.

Ni bill ipi iliwahi kukwamishwa na upinzani bungeni toka 1995?
 
Kuna taarifa zinasambaa kwenye magroup ya whatApp ya kuwepo mkakati wa kuifuta chadema kabla ya uchaguzi mkuu mwaka huu. je hizi taarifa ni kweli? Kama ni kweli nini malengo ya watu waliopanga ili jambo? hawaoni wanaiweka amani yetu mashakani?
Njia pekee ya ccm kuendelea kuwaburuza watanzania ni kuifuta Chadema , vinginevyo watakwisha
 
chadema kinafanyia kazi mambo ya mitandaoni ya uzushi.
 
Uchaguzi ukiwa huru na haki kwa Tanzania ni vigumu CCM ishinde watanzania wapo tayari kupigia hata kivuli kuliko kuipigia CCM iliyodumaza maendeleo kwa miaka 50 na sasa badala ya viwanda imekuwa ni Serikali ya Kesi kesi kesi kutwa zote
 
chadema kinafanyia kazi mambo ya mitandaoni ya uzushi.
Kama chadema ingekuwa hivyo wewe usingekuwa kutwa kuwabambikia kesi kuwapiga risasi kuwapora ushindi kwenye uchaguzi mbalimbali ungeacha wananchi waamue wenyewe
 
kwa mujibu wa sheria Chama hakiwezi kufutwa Mwaka wa Uchaguzi. Puuza hayo mambo
Yani wewe, Mbowe kila ninapowatazama huwa napata hasira flani.
Kipindi hiki wanamabadiliko tunapitia kipindi kigumu kutokana na utengano wenu.
Sipati picha kama leo hii vichwa vutatu (Mbowe, Zitto, Lissu) vingekuwa pamoja na malengo mamoja, Huyu mtesi wetu asinge Fanya haya anayiyafanya sasa.

Tafadhali ongozeni Watanzania katika kufika siasa safi tunayoitaka.

Dunia haiaribiwi na watu wabaya, Dunia huaribika sababu watu wema kuacha kusimama katika nafasi zao
 
Nikisema kuwa magu anashauriwa na wanafiki wasaka tonge mtabisha! Itazame takukuru inavyomuingilia cag na kukataa ripoti yake ambayo imeionyesha ccm na cuf kuwa na hati chafu na badala yake wameirukia cdm yenye hati safi!
Waone wanasheria wa takukuru wanavyokengeuka na kumshauri boss wao vibaya juu ya matumizi ya cdm yaliyotolewa na watu wasio wanachama wa cdm! Ni vituko juu ya vituko!
Angalau tuhuma hizo wangezitoa wakiwa ndani ya cdm zingekuwa na uhalali wa kuchunguza na takukuru lakini sio wanachama na hawahusiki na lolote ndani ya cdm!
Tiss nao waneuvaa mkenge kwa kulianzisha hili sekeseke ndani ya cdm kwani unajulikana kuwa wao ndio wawezeshaji wa mpango huu na wanamsukuma mwenyekiti wa time ya vyama vya siasa kufanya maamuzi ya kuifuta cdm eti ikithibitika Kuna ubadhirifu! Huu ni utani kwa jaji Mutungi kumlazimu avunje Sheria ambayo anasimamia kuongoza vyama vya siasa!
Kwa taarifa yenu ccm na magenge yenu, hiki mnachokifanya kitawaletea shida kubwa Sana mbeleni ikiwa cdm waliamua kwenda mahakamani kudai kuingiliwa na watu wasiokuwa wanachama wao kuwazushia na mtaaibika!
Na mkikosea kukifutia usajili basi huyo mnayemshauri kipuuzi ataangukia pia kwenye uchaguzi ujao ambao mnajiaminisha kushinda kabla! Endeleeni kumpotosha na kumpa sifa ili mjaze matumbo yenu!
 
Hebu lets think strategically..

What can we do to stop these motherfvckers?

Maana hawa ni mavichaa,yatatufuta kweli....

ACT iwe kama backup,ijengwe mipango kisipotee kitu.

Wanachama na resources zote twende nazo ACT,na vibe lote
 
Kama chadema ingekuwa hivyo wewe usingekuwa kutwa kuwabambikia kesi kuwapiga risasi kuwapora ushindi kwenye uchaguzi mbalimbali ungeacha wananchi waamue wenyewe
kesi gani chadema imebambikiwa mzee baba?
mlikuwa na wabunge wangapi uchaguzi uliopita, walitangazwa na tume ipi ?
majimbo muhimu kwenye majiji makubwa mlishinda na tume iliwatangaza chadema kama washindi.
mlishawai shika jiji la mwanza lote nyamagana na ilemera.
jiji la arusha,mbeya.jiji la tanga wapo cuf.

kwa dar wapinzani mlikamata majimbo mengi kawe,ubungo,temeke,ukonga,kinondoni,kibamba.jimbo la mbagala ccm wamelikomboa dk za majeruhi.
 
Mbona Chadema imeshajifuta yenyewe tu boss?

Pale unapolazimisha kupata mvuto wakati huna mvuto. Matokeo yake ndio hayo kufanya hila za wazi bila aibu.
 

Safari hii utatumia nguvu kubwa sana kuaminisha watu kuwa z ni 2.
 
Kuna taarifa zinasambaa kwenye magroup ya whatApp ya kuwepo mkakati wa kuifuta chadema kabla ya uchaguzi mkuu mwaka huu. je hizi taarifa ni kweli? Kama ni kweli nini malengo ya watu waliopanga ili jambo? hawaoni wanaiweka amani yetu mashakani?
Amani ya Bibi yako ndo inawekwa mashakani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…