Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,122
- 5,104
Actually mfumo wa vyama vingi Africa upo kwa nguvu ya wahisani/mabeberu tu.
Hata mchakato halali ukifuatwa wa kufuta upinzani kwa maana ya bill bungeni hamuwezi hata kuzuia chochote.
You’re very right. Leo muswada wa kufuta vyama vingi ukipelekwa bungeni utapita kwa nderemo na vifijo. Ndipo Tanzania ilipofikia. Watanzania/Waafrika wamezoea kutawaliwa kidikteta. Nyerere na Mobutu katika enzi zao, kwa nyakati tofauti walilifafanua hili kwa media za Ulaya. Kwamba: “sisi Waafrika asili yetu ni kutawaliwa na chifu mmoja tu anayekabidhiwa dhamana kamili juu ya usalama na ustawi wa jamii. Sasa hii vyama vingi ni kama kuleta machifu wengi na kuwakanganya wananchi”!
Lakini 1992, Nyerere, akiwa nje ya madaraka ya urais na uenyekiti wa CCM, alikuwa mkweli na mhalisia (honest and realist) kwamba Watanzania wengi elimu na uelewa wao uko chini sana kiasi cha kutotanabahi umuhimu wa demokrasia na mfumo wa vyama vingi. Hivyo akaipiku (overrule) Tume ya Nyalali na kuwapa ushindi 20% waliotaka mfumo wa vyama vingi. Hii ni moja ya nyakati Nyerere alipoonyesha “statesmanship” ya hadhi yake. Ni wakati alipowakosoa viongozi wa CCM na serikali yake kwa kukumbatia “mabaya” ya utawala wake na kutupilia mbali “mazuri”.
Leo hii CCM na serikali yake wanaona ufahari kuongoza taifa lililojaa watu wenye uelewa finyu wa demokrasia, mfumo wa vyama vingi, utawala bora, na haki za binadamu. Watu waliojaa hofu kuhusu mustakabali wao kiuchumi na tishio la kunyanyaswa na vyombo vya dola. Lugha iliyoenea nchini ni kama ya North Korea. “Rais wetu mpendwa/kipenzi”; “kwa busara kuu za mheshimiwa ...”; Hata kurekebisha mitaro ya barabara za mitaani watu wanamlilia “Rais mpendwa”! Rais ndio anashukuriwa kwa kutoa pesa za miradi ya kitaifa na ya vitongoji. Bizarre! Bora tuachane na vyama vingi.
Hata upinzani nako hivyohivyo. Viongozi wanatajwa kwa namna ya kuabudiwa. Natambua mchango mkubwa na mhanga unaotolewa na CHADEMA kusimamia demokrasia Tanzania. Sina tatizo kabisa na Mbowe kuongoza muda mrefu. He has earned it. Aina ya siasa zinazofanywa nchini zinahitaji mtu aina ya Mbowe kuongoza upinzani. Lakini CHADEMA nao wazungumzie utekelezaji wa mipango na maamuzi ya taasisi zao kuliko kurejea maagizo na busara za mwenyekiti hata kama ni kitu kilekile. Mtindo wa kauli ni muhimu sana.