PreGE2025 CHADEMA kurudia matapishi yake? Safari hii haitakimbilia Mahakamani?

PreGE2025 CHADEMA kurudia matapishi yake? Safari hii haitakimbilia Mahakamani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kwanini watu wa CCM wanaona kama Chadema imeacha kusaini kanuni kwa bahati mbaya. Wakati imefanya makusudi kabisa ili ilazimishe Reforms zifanyike na iwapo hakuna reforms basi kwa mujibu wa Chadema nakuna nayenyewe haitoshiriki uchaguzi huo
 
Km CHADEMA imeamua kutokushiriki ni kwa nini inawauma?? Kwani chama pinzani ni hicho tuu?? No reform no Election..that's enough
Wanajua siku ya kupiga kura vituo vitakuwa vitupu, na watajiona wasivyokubalika, lazima waumie.

CHADEMA kushiriki huwa kunawapa justification kubwa ya maana ya uchaguzi, sasa hawatashiriki, badala ya kufurahi wanalialia kila kukicha.
 
Ukitafakari vizuri, utaona CHADEMA Iko kwenye mtanziko mwingine.

Tume ya Uchaguzi (INEC), imeshafanya maamuzi kuwa CHADEMA hakitaruhusiwa kushiriki uchaguzi wa mwaka huu na chaguzi ndogo zake. Kutokana na kukataa kushiriki mchakato wa kikanuni ulioanza toka tarehe 1/3/2025 na kuhitimishwa na utiaji Saini kanuni hizo tarehe 12/04.

Haiingii akilini kudhani kuwa Tume inaweza tu kirahisi kufuta maamuzi yake kama CHADEMA inavyojaribu kushinikiza.

Kitakachotokea itabidi CHADEMA kwenda Mahakamani kutafuta tafsiri na kuomba Judicial review. (kwa Maana ajenda ya "kukinukisha" haitawezekana, wasahau hili).

Sasa utajiuliza, kama CHADEMA wakienda Mahakamani, huko sio ni kurudia matapishi yake, maana kilishakataa kufika huko Mahakamani kuhusu uchaguzi huu?

Lakini Mwenyekiti Lissu, alishawatangazia Wana CHADEMA wanao tarajia kugombea mwaka huu wasahau mipango hiyo; alisema: "Tunaenda kuuvuruga uchaguzi huu, kama unatarajia kugombea ubunge sahau, kama unatarajia kugombea udiwani sahau, Mimi mwenyewe nilifikiria uraisi nimesahau".

Katika mazingira hayo chama kitaenda huko Mahakamani kutafuta manufaa gani haswa kichama na kwa hoja zipi kuwa hakikupewa Haki ya ushiriki katika mchakato mzima? Je chama hakitaonekana ni kigeugeu?

Ndio Maana Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya kati, Mheshimiwa Jingu, amekiri hadharani kuwa Mwenyekiti wao hana washauri wazuri.

MAONI YA WADAU

..kufanya Reforms ili kuongeza imani ya wadau kuhusu uchaguzi ni rahisi kuliko kuendelea na Tume na sheria zilizopo.
 
CHADEMA walishasusa hawatoshiriki uchaguzi mkuu, hakuna haja ya kwenda mahakamani kudai haki ya kushiriki uchaguzi

Akili yako huwa haina uwezo wa kutunza kumbukumbu?

Ibu leta nukuu hata moja ambapo CHADEMA ilisema imesusa uchaguzi.

"CHADEMA, haitasusia uchaguzi, na wala No Reform No Election haina maana tutasusia uchaguzi, bali kama hakuna mabadiliko ya sheria na kanuni, tutazuia uchaguzi. Hatuwezi kwenda kwenye uchaguzi unaosimamuwa na Tume ya Rais, huku mapolisi wakiua na kujeruhi vijana wetu; mapolisi na wasimamizi wa uchaguzi wakiingiza maboksi ya kura fake, wagombea wetu hata wakishindwa hawatangazwi"; Tundu Lisu, wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa kampeni ya No Reform No Election, mjini Mbeya.
 
Back
Top Bottom