GE2025 CHADEMA kususia Uchaguzi wametuumiza wengi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Naona No Reform No Election ime tight mpaka mnaanza kumkumbuka Mkoloni.
 
Kama wangefanya uchaguzi yangetokea yale ya 2020 bado tusingepata wawakilishi bungen zaidi ya covid19 season2
 
Cdm ilikuwa na nguvu kabla ya Lowassa kumuhonga Mbowe. Na cdm imeendelea kuwa na nguvu baada ya yule mzee taplii kuondoka. Toka 2016 hadi sasa huwezi kupima maana siasa za sasa zinafanywa na vyombo vya dola, na chaguzi ni za kishenzi.
Hivi chadema ni wakumpokea tena Dr.slaa? Mtu aliyekisulibu chama na kuhamia CCM na kupewa ubalozi!!!
 
Sikio la kufa. Hakuna namna chadema wanaweza kuzuia uchaguzi hata kwa dakika 5 tu, wanataka kuwafanya chambo vijana kwa maslahi yao. Kijana mmoja akipoteza uhai kwasababu za no reforms no election moto hautazimia juu ya vichwa vya0
Tumeisha washauri ushauri wa busara, hakuna mtu atathubutu kujitokeza kuzuia uchaguzi, Ushauri wa Bure kwa Wafuasi wa NRNE, Hope for the best but get prepared for the Worst. Msidanganywe na Nyomi, mtashangaa. Hakuna atakayesusia Uchaguzi

Na wale manyumbu wao tumewaombea kwa Mungu Ee Mungu Baba Wasamehe maana hawajui watendalo! japo sasa wako moto sana! baada ya uchaguzi, sio kwisha habari yao?Sio watalia sana na kusaga meno?

P
 
"Insanity is keep doing same thing over and over again yet expecting different results" Albert Einstein

Huwa kuna uchafuzi sio uchaguzi
 
Hata mimi nimemind ni sera za uchawara kwamba ccm itafanyaje sasa na no reform no election watu wanatafuta uwakilishi chama kinasusia kweli viongozi walikosea sana miaka mitano tena ya kukaa bila wawikilishi,lissu hata urais hatufai
 
Mpumbavu ni yule anayekosea na kurudia jambo lilelile akitegemea matokeo tofauti. Sasa we mjinga nani akapange foleni kwenye uchaguzi unaosimamiwa na sheria zilezile za hovyo, watu walewale alafu utegemee miujiza? Embu azimeni ata akili kwa nchi jirani. Hakuna uchaguzi na hatupigi kura. Hatuna muda wa kuhalalisha wizi. Stupid.
 
Hata mimi nimemind ni sera za uchawara kwamba ccm itafanyaje sasa na no reform no election watu wanatafuta uwakilishi chama kinasusia kweli viongozi walikosea sana miaka mitano tena ya kukaa bila wawikilishi,lissu hata urais hatufai
HUNA AKILI.
 
Amani na utulivu SIO SUALA LA HISANI. Angalia ibara ya 8(1) (c) na 9 ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
 
Wewe hauna tofauti na prof. Flan aliwahi kuandika makala nyingi tu akitetea rushwa inavyosaidia katika kuleta maendelea kwa mtoa rushwa na mpokeaji.
 
Haahaa hapo ni sawa na manara kuwa refarii kati ya Simba na yanga, Kisha kujitosa tena uwanjani . NRNE ndo jibu
 
Tanzania hakuna uchaguzi bali ni maigizo ya uchaguzi. Kama kuna uamuzi wa busara ambao Chadema wameufanya basi ni huo wa kujiondoa kwenye maigizo ya uchaguzi. Ni kushiriki upumbavu kwa faida ya ccm. Wakashiriki wenyewe huo uchaguzi wao wa maigizo.
 
Ndio vizuri na maisha yanaendelea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…