Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,907
- 1,082
Hivi wewe unavyochukia ufisadi unachonganisha? Mtanzania anachambua mambo kwa uelewa mkubwa sana na kuna faida kwa wanachadema hadi bwana Mbowe.
sasa kila anayekwenda kinyume na Mbowe ni mchonganishi? Wangwe kaweka wazi matatizo ya chadema, nadhani mngemshukuru kwa kuyaweka wazi ili yafanyiwe kazi kuliko kupita pembeni pembeni. sasa hata JF nako mnatukaza kuyajadili kwa uoni wetu,
hapa kuna ushahidi wa pande mbili kuwa Wangwe wamekuwa akishiriki kwenye vikao vya wasio wapenzi wa kweli wa Chdema hilo ni kosa la kufukuzwa kwa mujibu wa Mpaka kielewe.
lakini pia kuna ujumbe kauweka Field Marshal ES kuwa Mbowe nae alikuwa akipita nchi nzima kumpakazia WANGWE toka mwezi wa tatu, sasa ilitakiwa Wangwe nae mumpe nafasi ya kumsikiliza.
kumziba mdomo wake sio kujenga demokrasia ya chama chenu.
kama aliweza kupata kura kwenye mkutano vipi watu watano wamtoe kienyeji?
kama kusimamishwa wasimamishwe wote Mbowe na WANGWE. sio mmoja kumpendelea kwa vile baba mkwe wake(Mtei) ni mwasisi na mwenye chama.
uvundo huu mtauficha kwa muda kama hamtarekebisha yatakuja hayo hayo na kina Zitto nao hawatakuwa na muda mrefu.swali Chadema ni wanademokrasia vipi mnawasimamisha wale wote wenye dukuduku ili chama chao kiende? au ndio udikteta uliopo makao makuu uliyojadiliwa hapa?
Mpaka kieleweke.
Kwa maandishi yako inaonekana ni Mbowe au unatumiwa na Mbowe.
wewe umeleta thread hii lakini huwapi nafasi watu kuchangia kwa kuishupalia kuonesha una maslahi yako. au unatumia mtandao huu kumuua Wangwe, sio busara kumsakama mwanachama wenzio tayari mmemvua umakamu Wenyekiti ambao hamkutaka aupate lakini kwa nguvu zake Mola akaupata na sasa mmeyarudisha maamuzi yenu watu sita (wale watano wa Dodoma na wewe)na kupinga utashi wa wajumbe waliokuja kwenye mkutano kumchagua Wangwe mwezi desemba 2007.
unasema Baregu ni bingwa wa kutatua migogoro kashindwa kumsaidia wangwe, lakini Baregu huyo huyo ndio aliyeivuruga NCCR na akashindwa kusuluhisha huko.
Makani sio bingwa wa Administrative Law ni mwanasheria wa mambo ya Benki ndio maana huwezi kumuona kwenda kumtetea Mahalu au Zombe sio eneo lake, huyu bwana hawezi kwenda kinyume na bosi wake wa BOT bwana Mtei ambaye alikuwa gavana wa benki kuu na yeye akawa msaidizi.
MK hujaweka uzoefu wa Mtei na Ndesamburo ambao walikuwepo kwenye kikao, au unataka tuamini kuwa kikao na maamuzi yalitoka kwa hao watu watatu tu?
Mtanzania.
Endelea kumwaga vitu umetulia sana na tunakuelewa wasio kuelewa wana agenda yao, hawezi mtu kukuziba mdomo wako wamemziba Chacha na sisi wanataka tusiseme?
au ndio maana Mwanakijiji aliwahi kuandika makala na kipindi maalum kumlaani Wagwe wakati wa jeshi letu lilipoenda Ngazija.inawezekana ulikuwa ndio mkakati wa kumsambalatisha Wangwe, nilishangaa kuona Mwanakijiji anamlaani makamu mwenyekiti wa chama chake.
Tunaomba Kitila Mkumbo,Mnyika,Zitto na Mwanakijiji wape kutupa maoni yao ingawa inaonekana wazi kuwa watamtosa Chacha(Msemakweli) ila somo kwenu ni kuwa mwenzenu akinyolewa nyinyi tieni maji vichwa vyenu. lazima mjue kuwa Wangwe ana watu nyuma yake huko Tarime wamemuamini na wameikubali Chadema kupitia kwake.
wanadiscuss in private, labda na wao wameshtushwa na hili!
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
NA
WANANCHI WA TANZANIA
KUSIMAMISHWA KWA MHESHIMIWA CHACHA ZAKAYO WANGWE (MB.) KUWA KAIMU MAKAMU MWENYEKITI WA TAIFA (BARA) WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
3. Amekuwa akikashifu chama, viongozi na watendaji wake bila kutofautisha kashfa na ukosoaji wa kisiasa na/au wa kiutendaji
Mheshimiwa Chacha Wangwe yeye mwenyewe na/au kwa kutumia wanachama na/au viongozi waliochukuliwa hatua za kinidhamu na vikao halali vya chama amekuwa akitoa kashfa dhidi ya chama, viongozi wake na/au watendaji wake. Bila ya kujali ushahidi uliopo hadharani wala maamuzi ya vikao vya chama ambavyo yeye mwenyewe alishiriki kuyafikia, Mh. Wangwe amekuwa akikituhumu chama, viongozi wenzake wa kitaifa na watendaji wake wa ngazi za juu kwa ukabila na/au udini. Licha ya ushahidi wa wazi kwamba viongozi wa ngazi za juu akiwemo yeye mwenyewe wametoka sehemu mbali mbali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Chacha Wangwe ameendelea kutuhumu kwamba kuna upendeleo kwa Wachagga na/au watu wa kaskazini ya Tanzania. Kivuli pekee cha tuhuma hizi potofu ni madai ya uwongo kwamba Wabunge watano kati ya sita wa Viti Maalumu wa CHADEMA katika Bunge la Jamhuri ni Wachagga. Kama wananchi wanavyofahamu, Wabunge Wachagga ni watatu tu na wengine ni Mzanzibari mmoja, Mpare mmoja na Muha mmoja. Aidha Mh. Chacha Wangwe anafahamu kwamba kati ya wajumbe thelathini na sita wa Kamati Kuu ya Chama kuna Wachagga watano tu sawa na wajumbe wa Mkoa wa Kigoma! Aidha Mh. Wangwe anafahamu fika kwamba kati ya wakurugenzi na watendaji wa ngazi za juu wa Makao Makuu wapatao zaidi ya ishirini, Wachagga wako watatu tu. Kwa msingi huo, lengo la kashfa za ukabila ndani ya chama zina lengo moja tu: kuwapaka matope viongozi na watendaji wa ngazi za juu wa chama kwa nia ya kuwadhoofisha na kuwapunguzia nguvu ya kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi ndani ya serikali na CCM.
-----------------------------------------------
Freeman A. Mbowe
MWENYEKITI
WABUNGE WA CHADEMA
Is this fair to the rest of Tanzanians?
Kwa nini isingekua kila mteuliwa akatoka at least mkoa tofauti?? Ugumu unatoka wapi au mikoa mingine haina wanachama wa Chadema wenye sifa?
Mhe. Maulidah Anna Komu, Komoro & Kilimanjaro (kaolewa na Mkilimanjaro na kuhamia huko).
Mbunge Viti Maalum (2005-2010)
Mhe. Susan Anslem Lyimo, Kilimanjaro
Mbunge Viti Maalum (2005-2010)
Mhe. Halima James, Kilimanjaro
Mbunge Viti Maalum (2005-2010)
Mhe. Grace Sindato Kiwelu, Kilimanjaro
Mbunge Viti Maalum (2000-2010)
Mhe. Lucy Owenya, Kilimanjaro (Mtoto wa Ndesamburo)
Mbunge Viti Maalum (2005-2010)
Mhe. Mhonga Ruhwanya Said, Kigoma
Mbunge Viti Maalum (2005-2010)
he He Heeee, Yaani Kuna Vichekesho Huko Na Vilivyonikuna Ni Hivi:
Wacha Kubisha Mangi Hichi Chama Wachaga Tu.
Ona Ndesamburo Anatoka Moshi Mjini, Mtei Anatoka Marangu, Makani Anatoka Rombo, Ngaiza Kule Kilema, Baregu Yeye Old Moshi, Kasisiko Huyo Usangi Lakini Bado Karibu, Chiku Yeye Kirua Vunjo, Zito Pale Uru Nakwambia Wote Wachaga Hao!!!!!!!
Na Bigup, Bongo, - 29.06.08 @ 12:11 | #19197
Tulimwambia Wangwe Kuwa Hiyo Ni Ngo Au Saccoss Ya Wachaga Na Zaidi Ni Family Business.
Niliandika Sana Jamii Forums Hadi Wakanifungia Kwa Sababu Jamii Forums Au Jambo Imenunuliwa Na Wachagga Wa Chadema Na Wanawalipa Ujira Vikojozi Kama Mwanakijiji Ambaye Hutumia Majina Mengine Kama Mwafrika Wa Kike,koba,madela Wa Madilu Au Ben Ili Kuzipa Nguvu Hoja Za Chadema Na Mume Wake(mbowe Au ****)
Mbowe Hamtaki Wangwe Kwa Vile Ana Akili Kuliko Mbowe.
Ndio Maana Baada Ya Kupata Umakamu Bwana Wangwe. Mbowe Akaacha Masomo Kula Sahani Moja Na Wangwe.
Kosa La Wangwe Alisema Kuwa Anataka Kukijenga Chama Toka Kwenye Family Business Na Uchagga Na Kuwa Chama Kama Taasisi Toka Siku Hiyo Anapata Mambo Mengi Ya Kusingiziwa Na Hadi Mzee Halimoja Ameamua Kutoka Kwenye Hii Ngo Ya Wachagga Baada Ya Kuona Wangwe Hatendewi Haki.
Wabunge Wa Kuteuliwa Wako Saba Wote Wachagga Mmoja Tu Kwa Vile Ni Kimada Wa Mbowe Ndio Kabila Lingine.
Kamati Kuu Ya Chadema Wako Kina Edwin Mtei Baba Mkwe Wa Mbowe Ambaye Alikuwa Mwenyekiti Wa Chama Na Ndio Mradi Wa Familia Yake.na Akaamua Kumrithisha Mbowe(mkwe Wake Unafikiri Wangwe Atapata Haki Gani Hapo?
Wangwe Alisema Kuwa Chadema Ni Chama Cha Kikabila Na Wakristu Hilo Ndio Kosa Kubwa Linalomgharimu.
Wangwe Lazima Azuunguke Nchi Nzima Kutueleza Kuwa Chadema Kama Huna Meno Yaliyoungua Basi Huna Chako,mbona Zitto Alizuunguka Nchi Nzima Wakati Jimboni Kwake Hakuna Hata Kisima Cha Maji?.
Mbowe Alimfukuza Warid Kaburu Kwa Mtindo Huu Huu.
Cha Ajabu Jambo Forums Ni Mtandao Wa Chadema Lakini Wangwe Alikuwa Akishambuliwa Toka Apewe Uenyekiti Na Aliyekuwa Akimshambulia Ni Kale Kakijeba Kanajiita Mwanakijijji(emolo Wa Jambo Forums) Kwa Vile Alipewa Dola Elfu Mbili Na Mbowe Kutengeneza Blog Yake.
Mzee Mtei Kampa Mbowe Nafasi Ya Uenyekiti,ndesamburo Kampa Mtoto Wake Ubunge(lucy) Ule Wa Kuteuliwa.
Watu Kama Leodgar Tenga Ni Mwanachama Wa Chadema Kwani Sifa Mama Ya Kuwa Member Chadema Ni Uchagga.
Mnyika Mama Yake Ni Mchagga Ndio Maana Kapewa Ukurugenzi Vijana.
Kitila Mkumbo Au Asha Abdala Anavyojiita Jamii Forums Anafuata Mkumbo Tu Kama Jina Lake Halisi Hajui Chadema Ni Mali Ya Kina Mangi.
Phillimon Mikael(mbowe) Vipi Habari Hii Umeiweka Kwenye Jamii Forums(jambo) Na Emolo Wako(mwanakijiji A.k.a Mwafrika Wa Kike)ataweka Mchango Gani?
Na Chinga - 29.06.08 @ 15:59 | #19234
Kazi Kwelikweliiii!!!!!!!!!
Maana Maoni Ya Wasomaji Ni Matamu Kuliko Habari Yenyewe. Hongereni Tz Daima Kutoa Nafasi Ya Maoni Ya Wasomaji. Keep It Up
Na Mpita Njia, Belgium, - 29.06.08 @ 17:46 | #19246
Wachaga Juuu Juu Zaidi
Na Mangi - 29.06.08 @ 18:40 | #19253
Love Chagga Or Hate Them But You Cant Ignore Them.chadema Juu.
Na Mangi ,lambo - 29.06.08 @ 18:44 | #19254
Inaelekea Chadema ukipinga tu fikra za WALE WAZEE WA TATU WA KICHAGA UMEISHA (Ndesamburo, Mtei na Makani).
hli Liko Wazi Na Tulishalijadili. Naweka Kiambatanisho Ili Wasiokuwa Waliliona Nao Walione.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
NA
WANANCHI WA TANZANIA
KUSIMAMISHWA KWA MHESHIMIWA CHACHA ZAKAYO WANGWE (MB.) KUWA KAIMU MAKAMU MWENYEKITI WA TAIFA (BARA) WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
4. Kuvujisha siri za vikao halali vya chama kwa watu wanaotaka kuhujumu chama
Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe amehusishwa moja kwa moja na kosa la kutoa siri za vikao vya vya ndani vya chama. Kwa mfano, Mh. Wangwe ametoa siri na/au nyaraka za vikao vya Kamati ya Wazee wa Chama vilivyokutana kujadili tuhuma, uzushi na kashfa zake dhidi ya Mwenyekiti wa Taifa, Katibu Mkuu na Sekretariat ya Kamati Kuu ya Chama kwa watu ambao nao wamechapisha kwa kuzipotosha siri na/au nyaraka hizo katika vyombo vya habari....... Lengo la kuvujisha na/au kupotosha nyaraka na/au taarifa za vikao vya ndani vya chama ni kuendeleza migogoro yenye lengo la kukidhoofisha chama na kukifanya kiache mapambano dhidi ya ufisadi ndani ya serikali na CCM.
----------------------------------------------
Freeman A. Mbowe
MWENYEKITI
Hli liko wazi na tulishalijadili. Naweka kiambatanisho ili wasiokuwa waliliona nao walione.