Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,256
- 44,597
Hawaruhusiwi kujadili kitu bila ruhusa ya Mzee Mtei,Ndesamboru na Mpaka kielewe(Mbowe) ingebidi abadili jina na kuwa 'Kimeshaeleweka'.
na siku zote KLH News au Mwanakijiji ni mtu wa breaking News lakini kwa hili amekuwa na kigugumizi.
tuendelee kusubiri ila nimesoma maoni www.freemedia.co.tz kwenye habari hii kuna maoni ya ajabu.
Asante, ES, Niliteleza. Kweli Makani ni wa Kanda ya ziwa. Thanks
hii Ndo Analysis Inayotakiwa Hapa, Chacha Anamatatizo Yake Mengi Yanayofahamika, Lakini Hoja Zake Ni Muhimu Kuzingatia, Vinginevyo Zitaibuliwa Na Watu Wengine Waliotulia Na Siyo Chacha Tena, Mtaendelea Kuwafukuza??? bado Nauliza, Kwa Dr. Slaa Na Zitto Walitaka Kujiuzulu????
Nachoipendea Chadema ni kwamba huwa wapo tayuari kukubali makosa na kufanya marekebisho haraka iwezekanavyo tofauti na CCM ambao maamuzi ya baadhi vionzogi wachache husimama kama mlima.
Wana JF,
Wangwe amesimamishwa kwa kuwa alikuwa anataka kugombea uwenyekiti wa Chadema taifa kwenye uchaguzi wa Chadema unaokuja.
Kama atakuwa hakuwa na hilo wazo, namshari afanye hivyo kwani akishinda atakuwa ameleta mapinduzi halisi ndani ya Chadema.
Je hilo kosa sasa linasema nini kuhusu hoja yako ya Ukabila?
Inadhoofika?
Wengine tulipopata habari hii tulisinyaa. Nitakuwa mnafiki mkubwa nikisema kwamba hii sio habari mbaya kwa CHADEMA. Ukweli ni kwamba ni habari mbaya ambayo bila shaka itatusumbua kwa muda kabla haijatulia. Niseme pia kwamba hii ni habari njema kwa CCM maana ndiyo siasa ilivyo; msiba wa mpinzani wako kwako ni harusi.
Sasa kuna watu wana hamu ya kusikia sisi wengine ambao ni wanachama wa wazi wa CHADEMA tunasemaje. Mimi nikiri kwamba Chacha ni mzigo kwa uongozi wa pamoja sio tu ndani ya CHADEMA bali hata kwa kambi ya upinzani bungeni kwa kuwa sio mtu wa kwenda kwa maamuzi ya pamoja (tusisahau huyu bado ni kiongozi kwa kuwa bado ni mbunge na M/Kiti wa chama chetu Mkoa wa Mara).
Pamoja na hayo, binafsi ningependa sana kutoka kwa Wangwe katika uongozi ingekuwa ni kwa njia ya kiheshima zaidi kuliko ilivyotokea. Ningependelea kwamba afike mahala akiri makosa yake na aone kwamba amekuwa ni mzigo kwa CHADEMA badala ya msaada na hivyo aone haja ya kujiuzulu mwenyewe kwa maslahi ya chama badala ya kufukuzwa. Ndivyo inavyofanyika katika vyama vinavyojiandaa kuchukua dhamana ya uongozi wa nchi. Mtaposikia kiongozi fulani wa chama fulani sehemu fulani amejiuzulu huwa mara nyingi sio kwa hiari bali kwa shinikizo ili kumtunzia heshima. Huwa ni mara chache sana inapolazimika kuanikwa makosa yote ya kiongozi mfukuzwa wazi kiasi hiki. Hata hivyo naamini Wangwe alipewa nafasi ya kujitetea na kujiuzulu na, kwa hulka yake, atakuwa aligoma na hivyo kuilazimu Kamati Kuu kuchukua maamuzi mazito na magumu kama haya.
Niseme kidogo pia kuhusu statement iliyotolewa. Kwa kiasi kikubwa maelezo yaliyopo katika tamko la CHADEMA yanajenga taswira tata kwa wananchi wa Tarime. Yatawafanya wajilaumu kuwa na mbunge wa aina ya Chacha. This is unfortunate and I must painfully acknowledge here that the statement was not carefully crafted. It would appear that there was an obsessiveness with getting rid of Chacha without due consideration to the consequences on our constituents and the future electability of Chacha and our party in Tarime. Statement kama hii itatunzwa na wapinzani wetu huko Tarime na watainyofoa kwenye uchaguzi wa 2010.
Nimalizie kwa kusema hivi uongozi ni pamoja na kuchukua maamuzi magumu ambayo ni unpopular for the time being lakini yenye tija kwa muda mrefu ujao. Ninaamini kwamba Kamati Kuu ya chama chetu ilijiridhisha kwamba hapakuwa na njia mbadala ya kutatua tatizo la kiuongozi la Wangwe isipokuwa hii walioichukua. Kamati Kuu ya CHADEMA ninaijua vizuri; siamini kwamba wangeweza kuchukua maamuzi magumu na yenye kukirudisha nyuma chama chetu kisiasa kama kungekuwa na njia ingine mbadala zaidi ya hii waliyopita.
Mimi nikiri kwamba Chacha ni mzigo kwa uongozi wa pamoja sio tu ndani ya CHADEMA bali hata kwa kambi ya upinzani bungeni kwa kuwa sio mtu wa kwenda kwa maamuzi ya pamoja (tusisahau huyu bado ni kiongozi kwa kuwa bado ni mbunge na M/Kiti wa chama chetu Mkoa wa Mara).
Wengine tulipopata habari hii tulisinyaa. Nitakuwa mnafiki mkubwa nikisema kwamba hii sio habari mbaya kwa CHADEMA. Ukweli ni kwamba ni habari mbaya ambayo bila shaka itatusumbua kwa muda kabla haijatulia. Niseme pia kwamba hii ni habari njema kwa CCM maana ndiyo siasa ilivyo; msiba wa mpinzani wako kwako ni harusi.
Sasa kuna watu wana hamu ya kusikia sisi wengine ambao ni wanachama wa wazi wa CHADEMA tunasemaje. Mimi nikiri kwamba Chacha ni mzigo kwa uongozi wa pamoja sio tu ndani ya CHADEMA bali hata kwa kambi ya upinzani bungeni kwa kuwa sio mtu wa kwenda kwa maamuzi ya pamoja (tusisahau huyu bado ni kiongozi kwa kuwa bado ni mbunge na M/Kiti wa chama chetu Mkoa wa Mara).
Pamoja na hayo, binafsi ningependa sana kutoka kwa Wangwe katika uongozi ingekuwa ni kwa njia ya kiheshima zaidi kuliko ilivyotokea. Ningependelea kwamba afike mahala akiri makosa yake na aone kwamba amekuwa ni mzigo kwa CHADEMA badala ya msaada na hivyo aone haja ya kujiuzulu mwenyewe kwa maslahi ya chama badala ya kufukuzwa. Ndivyo inavyofanyika katika vyama vinavyojiandaa kuchukua dhamana ya uongozi wa nchi. Mtaposikia kiongozi fulani wa chama fulani sehemu fulani amejiuzulu huwa mara nyingi sio kwa hiari bali kwa shinikizo ili kumtunzia heshima. Huwa ni mara chache sana inapolazimika kuanikwa makosa yote ya kiongozi mfukuzwa wazi kiasi hiki. Hata hivyo naamini Wangwe alipewa nafasi ya kujitetea na kujiuzulu na, kwa hulka yake, atakuwa aligoma na hivyo kuilazimu Kamati Kuu kuchukua maamuzi mazito na magumu kama haya.
Niseme kidogo pia kuhusu statement iliyotolewa. Kwa kiasi kikubwa maelezo yaliyopo katika tamko la CHADEMA yanajenga taswira tata kwa wananchi wa Tarime. Yatawafanya wajilaumu kuwa na mbunge wa aina ya Chacha. This is unfortunate and I must painfully acknowledge here that the statement was not carefully crafted. It would appear that there was an obsessiveness with getting rid of Chacha without due consideration to the consequences on our constituents and the future electability of Chacha and our party in Tarime. Statement kama hii itatunzwa na wapinzani wetu huko Tarime na watainyofoa kwenye uchaguzi wa 2010.
Nimalizie kwa kusema hivi uongozi ni pamoja na kuchukua maamuzi magumu ambayo ni unpopular for the time being lakini yenye tija kwa muda mrefu ujao. Ninaamini kwamba Kamati Kuu ya chama chetu ilijiridhisha kwamba hapakuwa na njia mbadala ya kutatua tatizo la kiuongozi la Wangwe isipokuwa hii walioichukua. Kamati Kuu ya CHADEMA ninaijua vizuri; siamini kwamba wangeweza kuchukua maamuzi magumu na yenye kukirudisha nyuma chama chetu kisiasa kama kungekuwa na njia ingine mbadala zaidi ya hii waliyopita.
Ni muhimu wadau mnaochangia suala la hili la kung'olewa kwa Mh.Chacha Wangwe(MB) katika nafasi ya umakamu Mwenyeketi wa Chadema,mkawa makini katika kutofautisha neo "wananchi" na "wanachama".Ni muhimu sana hili.Ndugu zangu,
Mimi sii mkali katika maswala kama haya isipokuwa kusema kweli naliona swala halikukaa vizuri kabisa...Uamuzi uliopitishwa kidogo una mushkheri yaani ni ktk maamuzi yale ambayo sikuyategemea..
Binafsi nilitegemea baada ya maamuzi ya Kikao basi Uongozi wa Chadema wangewakilisha swala hili kwa wananchi wake waliompigia kura na kuwapa taarifa yote hii ili wapate kupiga tena kura za kumsimamisha Wangwe..
Chadema kama chama hawahitaji kufanya kama CCM ambao tumewaona siku nyingi wakiondoa watu wapinzani na kuwabeba wanaounga mkono Ubabe na Ufisadi..Hii ni hatari sana kama mtu hakubaliani na baadhi ya vitu ama viongozi fulani basi aondolewe na kuwekwa yule mwenye utiifu kwa mtu ama kundi la watu...
Binafsi naamini kuwa kinachotupanga nyuma ya chama ni Mrengo, sera na ilani za chama sio upinzani kati ya watu na kama kweli Chacha Wangwe amekuwa akijaribu kupotosha mwelekeo wa Chama nadhani hilo ni jukumu la wananchama wote kulisikia na pengine kusikia Utetezi wa Wangwe mwenyewe sawa kabisa na utaratibu uliofuatwa alipochaguliwa...
Nadhani hapa kumetumika zaidi hisia za watu na upinzani ama chuki baina ya watu badala ya haki kutumika, hata kama Wangwe ni mkodefu kweli.. Utaratibu uliotakiwa ungekuwa na UWAZI zaidi kwa wanachama kuliko taarifa ya kamati kuu kwani hadi sasa hivi sidhani kama wananchi waliomchagua wanafahamu utetezi wa Chacha Wangwe kuhusiana na tuhuma zilizowakilishwa..
ChaCha Wangwe pamoja na makosa yote ambao alionyesha hata kabla ya Uchaguzi alikuwa pendekezo la wananchi na ikaleta matatizo kwa baadhi viongozi na kama nakumbuka ilibidi tu hao viongozi waheshimu uchaguzi wa wananchi waliokuwa wengi (demokrasia) lakini hayakuwa matakwa yao hata kidogo.. leo hii baada ya kukaa muda kamati (viongozi hao) inachukua madaraka ya kile walichokusudia toka ama kabla ya Uchaguzi!.. Hiki ndicho kinachonekana kwa wananchi ...hii inatisha!
Kwa hiyo kwamba Wangwe alichaguliwa na wanachama wetu wengi haitufanyi tuzibe masikio na macho ya kuona vile alivyo.
...Lakini, juu ya yote mimi nadhani watu wanataka kufanya a big fuss out of this!
Mimi nadhani tusiwe derailed kirahisi. Vita ya ufisadi ndio agenda ya sasa. Kama chadema wakiuana, waache wauane labda itatusaidia kujua kuwa nao si chama makini cha kushika nchi, lakini hatuwezi kuwasaidi kuficha udhaifu wao. Kama wanao na tuuone ili tujue kama the trust we started building is justified. Suala la chacha ni suala dogo sana. Chacha bado ni kigogo ndani ya chadema.