KakindoMaster
JF-Expert Member
- Dec 5, 2006
- 1,356
- 91
Wangwe kuishitaki CHADEMA
na Mwandishi Wetu, Dodoma
ALIYEKUWA Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chacha Wangwe, ambaye alisimamishwa uongozi juzi, amesema atakifikisha chama hicho mahakamani iwapo kitamzushia kashfa ambazo si za kweli.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, baada ya CHADEMA kutoa taarifa rasmi kuelezea kusimamishwa kwake katika nafasi ya makamu mwenyekiti, Wangwe aliwataka viongozi wa chama hicho wanaomtuhumu kwa mambo mbalimbali, kuyathibitisha madai yao, huku akionya na kusisitiza kuwa, iwapo watamzulia jambo lolote, atakwenda mahakamani.
Hawawezi kunituhumu kwa masuala ya uongo. Inabidi wa-prove (wathibitishe) tuhuma wanazotoa dhidi yangu kama wanasema nimevujisha nyaraka wathibitishe hivyo, kama wanasema nakihujumu chama wathibitishe pia, alisema Wangwe.
Hata hivyo, alikiri kusimamishwa uongozi, lakini akasema kusimamishwa kwake kumetokana na hila za Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, ambaye juzi katika mkutano wa Kamati Kuu alieleza kuwa hawezi na hataki kufanya kazi na yeye.
Alisema kuwa ni kweli uamuzi wa kusimamishwa kwake ulifikiwa kwa mujibu wa katiba ya chama hicho baada ya wajumbe wa Kamati Kuu kupiga kura ya kuafiki uamuzi huo, lakini alidai kuwa maamuzi hayo yalichagizwa na msimamo wa Mbowe.
Mkuu MJJ,
Kwani wanaojua ni akina nani? Wengine tuliambiwa na wewe ni inner circle ya CHADEMA, hebu kataa hilo au utuambie wanaojua ni akina nani?
Hawa watu wananipa raha kweli.Kwa njia hizi wanadhani wtaweza kuwatoa CCM.These are times when they are supposed to stay and hold on to each other to oust this power mongers yet they are breathing under each other's throat too bad but we will stand behind you when it comes to removing mafisadi.
Mkuu MK,
Vyama vyetu visingelikuwa vya wajinga, tusingelikuwa hapo tulipo.
Mnaotaka kuongoza Afrika lazima mbadilika na sio kuendeleza ujinga ule ule ambao ndio umetukwamisha.
Sina mapenzi na Wangwe na najua sio mwanasiasa makini lakini siungi mkono kabisa haya mambo ya viongozi wanaochaguliwa na watu walio wengi kufukuzwa na kakundi ka wapambe wachache.
Ningewaona wa maana kama mungejiuzulu wote na kuitisha uchaguzi upya ili wanachama wa CHADEMA waamue wamrudishe nani na wamlime nani. Haya mambo ya kufukuzana na kusimamishana kwenye vyama ni ujinga tu.
Kama kumsimamisha basi hicho kikao kilichomchagua ndio kingemsimamisha. Kila mtu anayefuatilia siasa za CHADEMA anajua Wangwe alikuwa haungwi mkono na kamati kuu ya CHADEMA. Sasa mmepata nafasi ya kufanya yale ambayo mlishindwa kufanya kwa kura kwenye mkutano wa CHADEMA. Ndio ujinga tunaousema wengine.
kwanza niseme naunga Mkono na Mguu upande mmoja wa hoja za Mtanzania kwenye suala hili. Mtanzania kama nimekuelewa unasema Wangwe asingesimamishwa kwa sababu chama kinamambo mengi ya kujijenga; hasa kwenye muonekano wa ukabila. Mimi naona hapo unakuwa unapotoka kidogo kwa sababu chama na katiba yake na vikao vyake vipo juu ya kila kitu. Iwapo Wangwe amesimamishwa kwa mujibu wa katiba basi sioni tatizo na itasaidia kuonyesha ni jinsi gani (at least in my eyes) kuwa chadema imekomaa.
Saying that kwenye siasa "TIMING" ni muhimu tena "pengine" kuliko hata sera!!! Sasa iwapo Mbowe amefanya hila kumsimamisha Wangwe kupitia kikao halali cha chama, mimi sioni tatizo. Iwapo Wangwe anakubalika kwenye chama kama yeye anavyoamini basi atumie haki yake kikatiba kugombea nafasi hiyo.
Hiyo habari hapo juu, Wangwe mwenyewe anajikanyaga kwenye maeneo niliyoweka bold na rangi. Sijapendezwa na kauli zake za kukimbilia mahakamani...huko mahakamani hakuna "siasa". Chadema kuna siasa na kama yeye ni "mwanasiasa" makini basi asimame imara na kujinadi kwa wana Chadema. Ni wana Chadema peke yake wanaoweza kumpa nguvu kisiasa.
Mimi nadhani ni busara kwa wachangiji kutafakari sababu zilizomfanya Wangwe kupoteza sifa za Uongozi. Nadhani kumsimamisha kiongozi anaepoteza sifa ni kitendo cha kukiimarisha chama hata mbele ya jamii. Hili ndilo tunalolisema siku zote pia kuhusu waliohusika na Richmond na EPA. Ukiwa na chama ambacho hakiwezi kuwawajibisha viongozi wake basi hilo linakuwa Genge!
Hoja ya kuwa, kiongozi amechaguliwa na mkutano mkuu halafu anasimamishwa na kamati kuu!, hili ni kwa mujibu wa katika na taratibu.
Lakini maswali mepesi, Ni kweli kuwa wana JF hawakuona mwenendo wa Wangwe? Mliamini kuwa kweli kwa mwendo ule angeifikisha CHADEMA na TZ mnapoamini? Kwanini msiwe wa kweli na wenye kupima hoja, badala ya kudakia tu kila Jambo!
Ni kweli kuwa na CHADEMA kiige mifano mibovu ya kushindwa kuwajibishana? Nadhani ni bora tuwe tunatoa hoja badala ya kufuata propaganda zisizokuwa na msingi.
Mimi nadhani hapa kuna tatizo la uelewa. Wachangiaji wengi humu wanavizia tu kujadili kitu amacho hawajakichunguza, halafu wanakuja na reasoning ya kitoto. Hivi chama uongozi kumchukulia hatua kiongozi mwenzao si sehemu ya demokrasia? Au nyie mnapenda yale a CCM ya siku hizi ya kuleana uozo na miiba ndani ya chama eti kuleta mshikamano, wakati wanalea mbomoko wa chama? Wanaomtetea Wangwe katika hili, wamchunguze kwanza. Mnajua alikotokea kabla ya kuja Chadema, na kwa nini walimtema huko? He's a problem.Vinginevyo, ni watoto wa mafisadi wanaofurahia aliyokuwa akiyafanya kuilegeza chadema, na sasa wanasikitika pandikizi lao limeng'oka?
Kumbukeni, wakati CCM ikiwa bado chama, haikusita kuchuua hatua kwa viongozi kadhaa walioleta za kuleta, wakiwamo kina Aboud Jumbe na Seif Sharrif Hamad. Huwezi kuwa kiongozi kama unaogopa kusema "huyu hapa ni tatizo."
Wangwe ni mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mara. Chama kiko Tarime tu. Sasa kama anataka kuonyesha uwezo wake si akisimike chama kwanza kwenye eneo lake la uongozi?
Ushauri: Wangwe acha kinyongo, uje hii nayo ni demokrasia, na utumie muda ulionao kujikita vema katika jimbo lako, vinginevyo naona kama CCM wanakaribia kulichukua. Halafu ukisimike chama katika mkoa wako, iwe ngome nyngine ya Chadema kwa kutumia uenyekiti wa mkoa ulionao. Kwani lazima uwe makamu mwenyekiti?
Yebo Yebo,
Nafikiri kwa kiasi hujanielewa. Ninachosema mimi ni kwamba malalamiko ya Wangwe kwa muda mrefu ni pamoja na hiyo perception ya ukabila. Walivyomtimua sasa ndio wanajiingiza kabisa kwenye yale ambayo Wangwe alikuwa anayasema kabla ya kuchaguliwa na ameendelea kuyasema hata baada ya kuchaguliwa.
Wangesubiri wanachama kwenye baraza kuu au mkutano mkuu ndio waamue. Kamati kuu kuwa na uwezo wa kumsimamisha makamu wa Mwenyekiti mimi naona ni mapungufu makubwa. Ndio njia wanazotumia CCM, sikutegemea hata vyama vinavyotaka kuleta mabadiliko navyo vitumie njia kama hiyo. Kibaya zaidi hiyo kamati haikuunga mkono uchaguzi wa Wangwe, hivyo kuamua kumsimamisha inaonekana zaidi kama political vendetta.
Panapokuwa na ugomvi kati ya Mwenyekiti na makamu wake, njia bora ni kurudi kwa wananchi, ni kuitisha uchaguzi tena ili wananchi waamue wanataka kuongozwa na nani.
Kilichonitisha mimi zaidi kwenye hili ni zile SPINS za Mbowe na wapambe wake hapo jana. Nilifikiri waleta mabadiliko wangelikuwa watu wa kwanza kuacha kutumia mbinu zile zile wanazozipinga.
Yebo Yebo,
Ninachosema mimi ni kwamba malalamiko ya Wangwe kwa muda mrefu ni pamoja na hiyo perception ya ukabila. Walivyomtimua sasa ndio wanajiingiza kabisa kwenye yale ambayo Wangwe alikuwa anayasema kabla ya kuchaguliwa na ameendelea kuyasema hata baada ya kuchaguliwa.
semeni mtakavyosema lakini ukweli unabaki pale pale tu kwamba Wangwe ni mzigo mkubwa kwa chadema maana hata wahenga walisema ni heri mchawi kuliko mnafiki maana kitendo cha yeye kufanya kikao na kabour ni moja kwa moja kuwa ni mfitini na mnafiki mkubwa kwa hiyo ni bora nusu shari kuliko shari kamili