ccm huwa wanazigombea hizo nafasi za viti maalum, mfano Salome Mbatia aligombea akapata kura kumzidi Mama Rwekatare alipofariki Mbatia ikatizamwa nani alikuwa ana idadi ya kura nyingi nyuma ya Mbatia Akapewa ubunge Rwakatare na hakuna malalamiko ya ukabila wala ukanda sababu process ilikuwa wazi na fair .
Utaona kuwa kanuni au taratibu zimetumika, Chadema hakuna utaratibu wa kugombea hizo nafasi inaonekana ni uteuzi unaofanywa na wenye sauti ndani ya chama ndipo utaambiwa kuwa Ndesamburo kwa vile alitoa milioni mia moja akasema mtoto wake apewe ubunge, mwingine akisema nilisambaza vipeperushi nchi nzima nae itabidi mtoto wake au girl friend wake apewe nafasi, kungekuwa na uchaguzi wa kugombea nafasi hizo manung'uniko yasingekuwepo.
jibu lingekuwa rahisi sana kwa kusema kuwa wakati wa kugombea hizo nafasi ni wachaga tu waliojitokeza hapo hakuna mtu atakayelalamika.
Mwanakijiji suala la haki sawa au diversity kwa chama ni jambo la msingi sana,watu wengi wametoka CCM au NCCR kwa kusema kuwa hakuna usawa, wakija huko Chadema ikiwa kila kitu kinakwenda sehemu moja itakuwa hakuna msingi wa haki kwa wote,
Ukiwa wewe ni Admission officer wa Chuo kikuu wakaomba wanaume mia moja na wanawake 50 na una nafasi 100, ikatokea wanaume wakawa kwa kwanza kuomba katika mtiririko wako wa maombi na wanawake wakaomba ndani ya muda uliowekwa,kwa jibu lako utawapa wanaume nafasi zote na utasema hawa ndio waliomba mwanzo,unatakiwa utizame uwiano,jeshi linaajiri watu kwa uwiano wa mikoa hivi sasa tofauti na nyuma.
Nafasi za viti maluum za Chadema hazikuwa katika utaratibu ndio maana zimezua malalamiko mengi sana ambayo bado wenye Chadema yao hawataki kuyafanyia kazi, taasisi nyingi zina utaratibu wa kupokea maoni kutoka kwa wadau mbali mbali au service user hiyo hupelekea kupatikana ufanisi na ubora wa huduma kukataa kupokea kasoro za taasisi sio kwenda mbele ni kudumaza jumuiya husika.
Ukitizama muundo wa vyama vya siasa Tanzania lazima uwe na sura ya kiTaifa, CUF hawana kiti cha ubunge hata kimoja Tanzania Bara lakini wamewapa wanawake wengi kutoka Tanzania Bara kutoka mikoa ya Kagera, Tanga,Dar-es-salaam,Dodoma n.k viti vya ubunge, wangeweza kusema kuwa viti maalum vitoke Pemba tu kwenye wabunge wa kuchaguliwa, lakini wametizama suala la uwakilishi kwa sura ya kitaifa, vizuri Chadema wakawa tayari kupokea maoni au kutizama wenzao wamefanya vipi.
Chama kinatakiwa kuweka mechanism za kubalance au kuondoa malalamiko ya muda mrefu kama haya ya kabila au mkoa mmoja kuhodhi kila kitu. Taasisi nyingi lazima ziwe na equal opportunity policy kama dira ya taasisi,vizuri kitu kidogo mgawane watu wengi kuliko mtu au kikundi kimoja kumiliki au kubinafsisha kidogo kilichopo kwa maslahi ya kuweka usawa.
Ningekuwa kwenye kamati ya Chadema, ningesema kuwa CCM wamechagua mawaziri wengi kutoka mkoa wa kilimanajro na sisi Chadema tunataka kuonesha kuwa kidogo tulichopata tugawane wote tunaanza na mikoa sita kwanza, tukipata vingi nchi yote itapata mwakilishi.
Mwanakijiji hakuna anayesema kila kabila liwe na mwakilishi ila kila mkoa upate mwakilishi, huwezi kusema kuwa ANNA KOMU ni mzanzibar sababu mbunge ni mtu anayejua mazingira ya watu wake na shida zao, kama KOMU ni Mzanzibar ilkuwaje Chadema walikwenda kumchukua Marehemu Jumbe kama Mgombea mwenza hadi akawekewa pingamizi kuwa ni mtu wa Tanga.
Anayegombea Urais lazima apate mgombea mwenza kutoka Upande wa kisiwani ili kuleta sura ya kitaifa, tunaomba Chadema wawe wanafikiria walau sura ya kitaifa kuweka wabunge kutoka Zanzibar au mikoa mingine kama wanavyotoa haki CUF kwa sehemu tofauti.