CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?


Haya na hili nalo
Tarime waunga mkono kusimamishwa kwa Wangwe

2008-07-04 09:21:55
Na Simon Mhina


Uongozi wa CHADEMA wilayani Tarime, umemgeuka mbunge wao, Bw. Chacha Wangwe kuhusiana na kusimamishwa kwake uongozi.

Bw. Wangwe pia ni Makamu Mwenyekiti wa wa chama hicho.

Pamoja na kuunga mkono, uongozi huo umepinga madai yake kwamba rukuzu inayotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa haifikishwi mikoani.

Aidha, uongozi wa chama hicho mkoani Mara, umeelezea kusikitishwa na madai ya Bw. Wangwe na kusema hivi sasa wanamtazama kama mtu asiyekitakia mema chama hicho.

Akizungumza na Nipashe jana, Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Tarime, Bw. Joseph Anthony alisema inasikitisha kuona kiongozi wa juu wa chama kama Bw. Wangwe anaanzisha hoja ya malumbano yenye nia ya kukiangamiza chama.

Akifafanua alisema inasikitisha kuona Bw. Wangwe akitoa taarifa zisizo sahihi kwenye vyombo vya habari kwamba ruzuku ya chama hicho inaishia makao makuu.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Wilaya yake ya Tarime inapokea Sh. 400,000 kila mwezi kwa ajili ya matumizi ya kukijenga chama.

Kwa msingi hiyo, Bw. Joseph alisema wilaya ya Tarime inaunga mkono kusimamishwa kwa Bw. Wangwe katika nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti.

Aidha, alimshauri Bw. Wangwe kuacha mipango yake ya kukata rufaa Baraza Kuu la chama kupinga uamuzi wa kusimamishwa na badala yake asubiri uchaguzi mkuu ujao.

Alisema Bw. Wangwe anatakiwa kujirudi na kujisafisha kwa njia ya kushirikiana na viongozi wenzake, kuacha malumbano kwenye vyombo vya habari na kukanusha tuhuma dhidi ya viongozi wenzake.

Naye Mwenyekiti wa Mkoa wa Kigoma, Bw. Jafar Kasisiko alisema wao wana wasiwasi mkubwa kwamba Bw. Wangwe anatumiwa kukivuruga chama.

Bw. Kasisiko alisema anachokifanya kiongozi huyo hadi akasimamishwa kina lengo la kuwafanya mafisadi wafurahie.

Mwenyekiti huyo alisema wilaya zake zote zinapata gawiwo la ruzuku tofauti na madai ya Bw. Wangwe.

SOURCE: Nipashe

eeh kama hii ni kweli basi wangwe kwisha habari yake
 

na Gazeti la The Citizen Ni la ROstam??na hawa wa Kagera wanasema Uongo?


Hawa mbona wanasema ukweli wa mambo.

Mpaka kieleweke kawaamshe wenzio waje wakusaidie kujibu haya,Hawa viongozi hawajui hata ni sh. ngapi huwa inatoka Nje?au ndiyo mnatumia nyie watu wa kaskazini
 
Mod. naomba uliunganishe hili na thread ile inayohusu Kusimamishwa kwa Wangwe ili kuwe na mtiriliko Mzuri,Tusishindane kumjadili Wangwe..tumeshaacha Mafisadi wanapumua
 
Mod. naomba uliunganishe hili na thread ile inayohusu Kusimamishwa kwa Wangwe ili kuwe na mtiriliko Mzuri,Tusishindane kumjadili Wangwe..tumeshaacha Mafisadi wanapumua

Nashukuru umeliona hilo japo hili ndio mkakati wenyewe ambao umepangwa kuhakikisha kuwa hatudai ripoti ya EPA hata baada ya muda wa kamati kwisha .

Najibu moja kuhusu Kabourou ni kuwa aliondoka CHADEMA baada ya kushindwa ubunge hivyo madai ya huyu aliyejiita kiongozi ambaye anaogopa kutaja jina lake ni uzushi .
 

Ndio hizo siasa za majitaka,,,huyo aliesema ni katibu wa chama wa wilaya na sio Tarime naomba urekebishe msemo wako, hayo ni maoni yake binafsi na sio tamko la wanachama wote wilayani tarime, halafu nenda KLHN kwa mwanakijiji usikilize Wangwe na Lisu wanachosema,,,"kila wilaya inapata 100,000/= kila mwezi" na sio 400,000/= huyo katibu wa wilaya ni msaliti, mnafiki, kuwadi wa mbowe na mfuasi wa siasa za majitaka
 

First Lady...pls Tell The President To DO THE People's Job And Not Thre Party's Job!(ccm) Or at least you should advise him to do so!
It Is The Duty For Your Husband To Give Us The Freedom We Want....then The Political Parties Later!
 
Najibu moja kuhusu Kabourou ni kuwa aliondoka CHADEMA baada ya kushindwa ubunge hivyo madai ya huyu aliyejiita kiongozi ambaye anaogopa kutaja jina lake ni uzushi .

Si kweli yeye alisema amechoshwa na viongozi wababaishaji, wababe na wenye kuendekeza ukabila katika chama...ndicho kilichomuondoa chadema kwa mujibu wake otherwise also haya ni majitaka tu...
 
It Is The Duty For Your Husband To Give Us The Freedom We Want....then The Political Parties Later!

Acha jazba wewe....kwa mtazamo wangu umemtukana mtu hapo...sio vizuri chekecha maneno na uonyeshe hekima yako kwa kuficha upu....... wako sio vizuri hapa hoja iliyoko mezani kujadili kuhusu msimamo wa chadema kuhusu Wangwe,,acha Lugha chafu na
 
jmushi1 It Is The Duty For Your Husband To Give Us The Freedom We Want....then The Political Parties Later![/QUOTE said:
Bahati mbaya sijaolewa!ila nikiolewa and as i beliave he will be a future president of TZ!nitamueleza siku akiwa Raisi
 

MK,

Kabouru amewahi kushindwa ubunge mara ngapi Kigoma? Mbona safari hizo zote hakuondoka?

Binafsi naona ni very cheap politics kusema aliondoka baada ya kushindwa ubunge. Tatizo hapo ni kushindwa kwenu kushughulikia malalamiko ya wanachama wenu na mnakimbilia kwenye majibu ya haraka haraka.

Pia kama mliona EPA ni muhimu sana, kwanini muanze kufukuzana kipindi ambacho EPA inatakiwa ijadiliwe kwa nguvu zote?

Kama mnaendesha siasa kwa mtindo huo, tegemeeni kuwa upinzani kwa muda mrefu sana.
 
Mtanzania,

Umeuliza swali zuri sana kwa MK kuwa kwa nini waanze kufukuzana kipindi ambacho EPA ilitakiwa ijadiliwe kwa nguvu zote ? Jibu alilitoa mwanzoni aliposema kuwa Wangwe alikuwa na kikao na Rostam Kempinsiki kwa masaa 4. Wangwe hawezi kupangiwa watu wa kukutana naye. Lakini katika mazingira haya kwa nini tusiamini kuwa haya yote yanayotokea ni mkakati wa mafisadi wa EPA kuhakikisha EPA haijadiliwi ? Kama MK anafahamu hadi fedha iliyowekwa kwenye akaunti ya mke wa Wangwe toka kwa mafisadi basi tatizo ni zito kuliko wengi tunavyofikiria. Kama Wangwe alikuwa mmoja wa makamanda tuliowaamini, na bila kutaraji anageuzia mtutu kwa wale aliotakiwa kuwalinda, afanyweje ?
 
naipenda sana CHADEMA lakini sasa naona wameanza kuharibu kiukweli kama swala ni marafiki na maongezi mbona mbowe washkaji au niite marafiki zake wengi ni wana CCM tena wale ambao huwezi kuwanunua hata kwa kiasi gani cha pesa hili halionekani na wanajuaje kama yupo pale kwakukimaliza chama na si kukiimarisha wana CHADEMA kuweni makini na huyo kiongozi wenu wa juu.
 
Acha jazba wewe....kwa mtazamo wangu umemtukana mtu hapo...sio vizuri chekecha maneno na uonyeshe hekima yako kwa kuficha upu....... wako sio vizuri hapa hoja iliyoko mezani kujadili kuhusu msimamo wa chadema kuhusu Wangwe,,acha Lugha chafu na

Umekunwa? Nini kimekuchokonoa?
Mbona kama ni jazba ni wewe nyerererist!Nyererelism failed before it actually started na unyerererist ndio ulioliuza TAIFA LETU!
 
Nyerererist
Hebu nielewe maneno hayo sijayasema mimi,nimenukuuu habari ya gazeti,na ndio maana nikasema kama haya ni kweli basi jamaa kwisha,ila kwenye post zangu za nyuma kumbuka nimeomba Dr.slaa atupe maelezo ya ripoti ya Mzirai na pia wanaojua mambo ya wangwe waweke hadharani ili tumjudge fairly
 
CCM tukiangalia viongozi wa juu wa chama hicho na erikali kama ni waislamu na wote wanatoka mkoa mmoja au jirani jirani je, huo nao utakuwa ni udini au ukabila?
 
Umekunwa? Nini kimekuchokonoa?
Mbona kama ni jazba ni wewe nyerererist!Nyererelism failed before it actually started na unyerererist ndio ulioliuza TAIFA LETU!

Huo ni mtazamo wako na ukubwa wa upeo wako ndipo unapokomea na siwezi kukulaumu wewe.....na siwezi kubishana na wewe maana we know u mkurupukaji usipoangalia utakua Banned tena ubadili jina na uwe mushij1 kama siku ile,,,,mie nimekwambia tumia lugha nzuri tatizo liko wapi? haya bwana Mushi (Mchaga)
 

Samahani bwana,,nilichanganya lugha tu but my aim was namwambia huyo katibu wa wilaya,,,heshima yako mkuu
 
CCM tukiangalia viongozi wa juu wa chama hicho na erikali kama ni waislamu na wote wanatoka mkoa mmoja au jirani jirani je, huo nao utakuwa ni udini au ukabila?

Hata madereva, walinzi na viti maalum??? Hata mie nawasupport Chadema but Watatue hilo swala kwa manufaa ya chama
 
Kura zilikuwa ni 24 kwa 7. Mbowe alitowa taarifa akisaidiwa na Lusu na watendaji wakuu wengine. Wangwe ndo anasema wengine wote kwenye kamati wamenyamaza. Nahisi Wangwe nae anyamaze asubiri vikao halali kama kweli anahoja ya msingi ili chama kiwe imara na kama kweli anaitakia mema nchi hii.

Hata wanachama wa ccm wangependa mpaka kwenye mashina wapate pesa ya ruzuku lakini hawapati akitokea hata RA na EL wakisema hilo wataungwa mkono na wengi.
Akitaka afanikiwe atulie afate vikao halali.

Kama kuna matatizo kama hayo watu kutumia pesa binafsi basi wajisahihishe ila kusema kuwa CHADEMA ni NGO ya akina Mbowe, mh hata akina sisemi. AKILI KICHWANI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…