CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

naona watanzania tunakosa mwelekeo. badala ya kujadili hoja sasa tunajadili watu na wanakotoka. kwa mtindo huu hatuendi kokote. WANGWE HAFAI




Yanii Wange Hafai hata kidogo, Mimi kipindi cha uchaguzi nilikuwa Bongo home tena Tarime yaani huyo jamaa Wana JF kasaidiwa na Mbowe na Lisu yaani sasa ananichekesha anapoanza kujiinua wakati alikuwa jamaa tu anapandisha kila siku kwa miguu kutoka Bomani mpaka hapo kwake karibu na A.M.A sasa hivi anaona amemaliza kazi nakujiinua.

Mimi ni mwana ccm lakini naomba Chadema imtimue hana jipya,maana ata hako kaubunge watu walimpa tu baada ya CCM kuamua kuwaachia ila kweli ni kwamba Wangwe katuhaibisha sana watu wa Tarime.
Simpendi tena
 

Kama Mbowe Ana Msaada Mbona Hajalipa Deni Lake La Nssf?
Kama Wewe Ccm Yana Kuhusu Nini Ya Chadema?
 
swala la kuleta Zitto Kabwe vipi? au umekimbia mada kiaina,mtu mzima huwezi kukubali hata kama ulitereza hizo ndizo safari za kisiasa, wengine hupita njia ndefu na wengine njia fupi.

Hivi ni nani aliyesema kuwa Zitto ni shahidi wake, mimi au wewe? Au hili nalo limekushinda?
 

nategemea CHADEMA kujifunza kwenye hili......kuwe na mfumo unaoeleweka . Mwanachama lazima awe na kipindi fulani (not less than five years) ili apewe uongozi wa juu. Tumeona mengi katika hili mfano NCCR na Mrema etc. Kwa njia hii itakuwa si rahisi kuwa na mapandikizi( I am not saying Chacha ni pandikizi). Lakini Wangwe alikaa muda gani uanachama hadi umakamu wa mwenyekiti? Sina hakika lakini najua ni muda mfupi.
 

Nani kakudanganya kuwa Chacha amesimamishwa kutokana na madai yake kuhusu ukabila na ruzuku?

Kwa taarifa yako Bwana huyu amesimamishwa kwa ajili ya maadili yake mabovu ya uongozi kuanzia kwenye kutoa siri za vikao, kutumiwa na CCM, kukosa ushirikiano na viongozi wenzake, kukosa uwajibikaji wa pamoja nk!

Mambo ya ruzuku na ukabila ameyazua baada ya kusimamishwa kama mkakati tu wa kutafuta kuonewa huruma mbele ya umma na mkakati wa kuwachafua viongozi wenzake.

Mambo hayo wala hakuyaibua kikao kama inavyodhaniwa. Chacha ni mnafiki sana, nimemshusha thamani baada ya kumpigia simu na kuongea naye

Asha
 
mbinu ya kukausha bwawa ndiyo inatumiwa na CCM dhidi ya CCM. katika mbinu hii kama unataka kumkamata samaki kwenye bwawa na hakamatiki basi njia rahisi ni kukausha bwawa na maji yakiisha unamkamata kirahisi

Mbowe ni samaki na dawa ya kumkamata yeye ni kuwaondoa walio karibu yake walianza na Kaburu wakaona jamaa bado yuko ngangari sasa wanamtumia Wangwe. washindwe kwa jina la wananchi wanaogandamizwa na mfumo wao wa kishetani wa kutawala!
 
Bi. Asha Abdala,
Mimi napenda sana jinsi unavyotupa dataz kifupi hua unanifungua bongo na kuona mengi ambayo siyafahamu..
Binafsi nimeelewa vizuri sababu ya kufukuzwa kwa Wangwe na inakubalika kimsingi, tatizo langu ni yale madai yake baada ya kufukuzwa. hata kama kayaleta baada ya kufukuzwa lakini hii haindowi ukweli kwamba madai hayo yalikuwepo akilini mwake na yalifahamika kwa viongozi wa Chadema.
Tumezungumza sana kuhusiana na jambo hilo hapa JF toka enzi za Bcstimes lakini kwa mshangaoi wangu sijawahi kupata jibu ambalo nikimwambia mlalahoi linaweza kuridhisha dhana alokuwa nayo kuhusiana na Uongozi wa chama. Ni sababu ambazo hadi leo nashindwa kuwaelewa CUF ambao kimsingi wana kila haki ya kufanya wanayofanya.. Lakini ni lazima tufahamu kitu kimoja kwamba kila nchi ina mazingira tofauti. Demokrasia ya Marekani ama Uingereza haiwezi kufanya kazi Tanzania wala katiba zao. Tanzania yetu pamoja na kukataa Ukabila na dini hivi vitu vinaingia ktk fungu la illigality..Kama vile unga na bwibwi.
sasa huwezi kuoenekana ukitumia Unga ama Bwibwi ukasema hakuna unga wala bwibwi Tanzania hali watumiaji wapo. Tanzania tumeukataa Ukabila na Udini kwa misingi kwamba yeyote anayeoinyesha dalili za kutumia vitu hivyo ni mhalifu... Na hii ndilo tatizo langu kubwa kuelewa kwa nini Chadema pamoja na kuelewa kwamba kuna fununu za Ukabila iweje bado tuendelee kupanda miti ya bangi ili kupata kivuli hali kuna uwezekano wa kuepuka kuendelea kupanda miti hiyo!...
Kila mnavyozungumza kuhusiana na Wangwe, yeye binafsi inazidi kunadi tuhuma hizi kwa sababu Chadema wanakosa kujibu hoja zake bali yeye mwenyewe anakuwa hoja kitu ambacho watu hawana interest naye yeye kabisa!.. Tuhuma hizi zinabakia kuelea na itakuwa vigumu sana kwa Chadema kuweza kufanya kazi huko mbele. Kesho hata akipatikana kiongozi mzuri sana lakini maadam tu ni mchagga itakuwa kazi kubwa kuwafahamisha wananchi. Ni hali ambayo imewasitisha wengi kuingia CUF na vyama vinginevyo kwa sababu karibu kila chama cha upinzani kimesimama kama vile wanasimamia maslahi ya kikundi fulani..
CCM wanachekela sasa hivi, sina maana Chadema ni chama cha Wachagga lakini dhana hiyo imesemwa sana na kurudiwa mara nyingi kiasi kwamba inaanza ku sink vichwani mwa watu.. Matokeo yake wataamini kama mtashindwa kujibu hoja hizi.. achaneni kabisa na Wangwe...litazameni swala hili na kulipatia ufumbuzi mapema ili kesho hata akichaguliwa Dr. Mangi sina patakuwa hakuna shaka lililosimama leo hii.
 
Samahani nimeweka hoja ambayo haikustahili kuwa hapa!
duh ama kweli Uzee ni mzigo mkubwa!
 
The same question nauliza hapa ni kuwa, watu wanajuaje kuhusu makabila ya wabunge wa chadema kama wao wenyewe wabunge) hawajasema makabila yao?

Kwahiyo makabila yanatambulika tu pale mwenye kabila anaposema? Nilizani Nyerere alikuwa mzanaki! Sasa nitaomba afufuke na aseme yeye ni kabila gani, otherwise I will be very wrong.
 

soma vizuri report ya central committee ya CHADEMA.
 

Hii ndiyo report ya Mbowe, Asha.
 
Hata sisi tusio na vyama vya siasa twaona Wangwe ni tatizo CHADEMA!!! Hivi huyo wangwe aliyetimuliwa CHADEMA si ndie yule aliyezuwa zogo wakati ZITTO alipoteuliwa ktk kamati ya kufuatilia mikataba ya madini???!!
 
Hivi ni nani aliyesema kuwa Zitto ni shahidi wake, mimi au wewe? Au hili nalo limekushinda?

sijawahi kushindwa jambo, ni wewe tu ndiye kila uchaguzi unashindwa uliomba wenyekiti umoja wa vijana mkoa wa Dar-es-salaam ukabwagwa,
ukaomba ujumbe la baraza la vijana la mkoa wa Dar-es-salaam nako utatupwa.
Wewe ulisema kuwa Zitto atakuja hapa kukanusha ukweli wangu kuwa wewe umepita vyama vyote CCM,NCCR NA TLP, lakini umekaa kumuhukumu Wangwe tu kuwa alikuwa NCCR, wakati wewe umemaliza vyama vyote yaani MTALII wa vyama vya siasa.
 
Hata sisi tusio na vyama vya siasa twaona Wangwe ni tatizo CHADEMA!!! Hivi huyo wangwe aliyetimuliwa CHADEMA si ndie yule aliyezuwa zogo wakati ZITTO alipoteuliwa ktk kamati ya kufuatilia mikataba ya madini???!!


Hebu tusiunge tu behewa na kuacha kuangalia aliyosema Wangwe kama yalikuwa na umuhimu;
  1. Alisema uwepo wa Zitto kwenye kamati ya madini unaweza tumiwa kuficha mambo. Je hili limetokea? Nafikiri bado kuna muda wa kutambua kama alikuwa sawa au la, lakini tunachojua ni kuwa Zitto hana sauti tena kulizungumzia hili suala mpaka Ripoti yao itakapokuwa public. Lini yatakuwa, JK knows.
  2. Wangwe alipinga Commoro's expedition ingawa alikosea kwa kutumia vifungu visivyo vya katiba. Je alikuwa na point kupinga kujiingiza kwetu Commoro? Offcourse. Lakini kwa vile baadhi ya viongozi wa juu wa CHADEMA walikubaliana na JK kwenye hili bila kudadisi, Wangwe ndiye akaonekana mwenye vurugu na akina MMJJ wakatumiwa kumpiga mawe. Sasa tunaposikia ya akina Artunas kuwa wana deals zao na Commoro thru JK, tunaanza kumuona Wangwe kama prophet.
Ukweli ni kuwa Wangwe hana elimu kubwa na pesa ya kutisha, lakini ana upeo fulani usiopimika kwenye taratibu za kawaida tulizozoea. Such people are very important in correcting a society if given due processes.
 
Never let yesterday's disappointments overshadow tomorrow's dreams

Baadae.
 
AS I SAID NA SASA NASEMA TENA....! migogoro (mitafaruku) ndiyo iliyouwa/ianayouwa upinzani wa KWELI nchini.......!
quote me......!

INTRA CONFLICTS......!
 
Zamercopolo,
Mheshimiwa heshima yako kwanza.... Mkuu kama utasoma kifungu cha 4 cha madai ya Chadema kuhusiana na Wangwe..huyu mtu atafukuzwa Uongozi na Uanachama wa chama chochoite duniani.. Hiki kifungu kimoja tu kinatosha kumfunga mtu maisha kama chama hicho kinaongoza nchi hata sisi wananchi tunaotaka kuona swala la Richmond na EPA linapata ufumbuzi tunaweza kabisa kumtia kiberiti..
tafadhali kisome tena upate kupima- weka fikra zako huru ondoa ukada wa chama ama ushabiki..kinasema hivi:-

4. Kuvujisha siri za vikao halali vya chama kwa watu wanaotaka kuhujumu chama

Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe amehusishwa moja kwa moja na kosa la kutoa siri za vikao vya vya ndani vya chama. Kwa mfano, Mh. Wangwe ametoa siri na/au nyaraka za vikao vya Kamati ya Wazee wa Chama vilivyokutana kujadili tuhuma, uzushi na kashfa zake dhidi ya Mwenyekiti wa Taifa, Katibu Mkuu na Sekretariat ya Kamati Kuu ya Chama kwa watu ambao nao wamechapisha kwa kuzipotosha siri na/au nyaraka hizo katika vyombo vya habari vinavyomilikiwa na watu wanaokabiliwa na tuhuma za kuhusika na ufisadi mkubwa wa Richmond na EPA. Vile vile Mh. Wangwe ametoa siri na/au nyaraka hizo kwa kikundi cha wanachama na/au viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam waliofukuzwa uongozi na vikao halali vya chama. Lengo la kuvujisha na/au kupotosha nyaraka na/au taarifa za vikao vya ndani vya chama ni kuendeleza migogoro yenye lengo la kukidhoofisha chama na kukifanya kiache mapambano dhidi ya ufisadi ndani ya serikali na CCM.

Mkuu kama wewe ni mwana JF wa kweli mtu kama huyu hatufai hata kama angekuwa CCM au ofisi za Magereza! hafai.....
 

Mkandara,
asante kwa ufafanuzi.
Nimekuelewa barabara na kifungu pia nimekielewa.Lakini ni vyema tukawa makini kuwa haya ni MADAI ambayo Chacha ameyakataa.Haifai kwetu sisi kuamua kuwa madai haya ni ya ukweli wakati kuna two schools of thoughts- Mbowe's and Chacha's.
Vitu hupewa nafasi kwenye ripoti kulingana na uzito wake, nadhani utakuwa umegundua kuwa kifungu hicho kimewekwa cha mwisho kabisa to tell us kuwa madai hayo ni legelege na sio msingi wa kesi.
Kumbuka kuwa Seif pia alikuwa na kesi hiyo ya nyaraka,hii ni miongoni mwa methods zilizotumiwa kumeliminate.Watu kadhaa ninaowafahamu pia wameshutumiwa kukutwa au kuvujisha nyaraka za siri.Hii ni mbinu inayotumiwa na vyama vingi kwa miaka mingi.Hivyo basi tunaposikia shutuma kama hizi tuzipe muda kufanyiwa uchunguzi huru kabla ya kutoa adhabu,iwapo lengo ni kutatua matatizo ya chama.
 

Kama ni Kitila A.K Mkumbo yule aliyekuwa Rais wa DARUSO akafanya kazi IGU pale UDSM akawa mhadhiri nk huyu Bwana hajawahi kuwa TLP wala NCCR. Alitoka NYF akiwa na wenzake wakina Mwakagenda, Ilunde, Zitto na Mnyika akajiunga na CCM kabla hata ya wenzake kuwa active kwenye siasa. Akagombea uenyekiti wa vijana DSM akafanyiwa zengwe, akamuunga mkono Salim Ahmed Salim badala ya Kikwete akafanyiwa tena zengwe. Akaamua kujiunga na CHADEMA na kuwa shabiki wa Mbowe. Huko akakutana na wenzake wakina Zitto, dogo Mnyika na Mwakagenda. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

PM
 

This is the biggest misstep the comrade has made.Unortunately its irreparable.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…