Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,582
RUZUKU, UKABILA WAIGAWA CHADEMA
CHADEMA ndicho chama pekee nchini kilichokuwa kinaonekana kutokuwa na migogoro, lakini hili la ruzuku na mengine yanaelekea kukigawa katika makundi mawili ya CHADEMA MBOWE na CHADEMA WANGWE.
Hali hii imejitokeza baada ya kutokea malalamiko ya wanachama wa CHADEMA kususu masuala kadhaa ya msingi. Masuala hayo yameibua mgawanyo uliozaa makundi hayo mawili na baadaye Mwenyekiti wa chama hicho FREEMAN MBOWE akatangaza kumsimamisha Makamu Mwenyekiti (CHACHA WANGWE).
Kwa tafakuri pana kila Mtanzania alitarajia kwamba kabla ya kumsimamisha Makamu Mwenyekiti, CHACHA WANGWE, Mwenyekiti wa chama hicho alitakiwa kujibu tuhuma moja baada ya ingine ili kujisafisha yeye mwenyewe pamoja na viongozi wengine wa juu wa CHADEMA.
Kimsingi,CHACHA WANGWE anamtuhumu MBOWE katika masuala yafuatavyo:-
Mosi, Kuna matumizi mabaya ya ruzuku (ufisadi wa ruzuku) ndani ya CHADEMA Makao Makuu. Hivyo, CHACHA WANGWE anamtaka Mwenyekiti FREEMON MBOWE atoe maelezo ya matumizi ya Ruzuku, ambayo ni fedha ya walipa kodi inayotolewa na serikali kwa vyama vyenye wabunge. Aidha WANGWE anamtaka MBOWE aonyeshe mapato na matumizi ya Ruzuku hiyo katika vikao vya chama au aunde kamati ya kuchunguza tuhuma hizo. Pia, WANGWE ana mashaka na hesabu zinazoonyesha mgawanyo wa matumizi ya ruzuku yanayopelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa kutoka chama cha CHADEMA.
Pili, CHACHA WANGWE hakubaliani na kitendo cha Mwenyekiti na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kuzuia ruzuku isifike mikoani. Anasema hali hii ina maana matawi ya chama yasifunguliwe na chama kisiwe na ofisi hali ambayo inadhoofisha chama. Vivyo hivyo, WANGWE hakubaliani na kitendo cha MBOWE kufuja fedha za chama kwa ziara za helkopta huku akiwaacha wagombea ubunge na udiwani wa chama chake hawana msaada wowote wa kifedha kutoka katika chama. Katika mazingira haya WANGWE anauliza nani anakihujumu chama kati ya MBOWE na WANGWE? Nani anadhoofisha CHADEMA?
Tatu, CHACHA WANGWE ana hoja kwamba MBOWE, anawajibika kuwaeleza watanzania, ni kwa vipi wabunge watano kati ya sita wa kuteuliwa (viti maalum) wote watoke mkoa wa Kilimanjaro ( MBOWE ni Mchaga wa Kilimanjaro). Ikumbukwe kwamba Tanzania bara ina mikoa 21 na Zanzibar mikoa 5. Kwa kawaida, idadi ya viti maalum inategemea idadi ya wabunge ambao chama kinapata katika uchaguzi mkuu, ambapo asilimia 90 ya viti vya ubunge zilizoleta viti maalum vya CHADEMA zilitoka kanda ya Ziwa. Hivyo, MBOWE kasahau kanda zilizosaidia CHADEMA ikipata viti maalum na kuvipeleka KILIMANJARO.
Nne, CHACHA WANGWE anamtaka MBOWE, aeleleze inakuwaje kati ya wakurugenzi nane wa Idara mbalimbali za CHADEMA wanne ni Wachaga wa Kilimanjaro?
Tano, WANGWE anamtaka MBOWE, aeleze umma wa watanzania inakuwaje Madereva wote wa Makao Makuu ya CHADEMA ni Wachaga kutoka Kilimanjaro?
Sita, WANGWE anataka MBOWE, ajibu tuhuma kwamba yeye mwenyewe, DR WILBROAD SLAA na PHILIMON NDESAMBULO wanajilipa fedha kwa ajili ya kurudisha gharama walizotumia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. WANGWE anauliza mbona wanachama wengine hawarudishiwi gharama hizo akiwemo yeye WANGWE? Je, huu siyo ufisadi? Je huku ni kutenda haki?
Saba, WANGWE anataka kujua ni kwa nini miaka minne iliyopita MBOWE alivunja tawi la CHADEMA mkoa wa DAR ES SALAAM na kubaki na CHADEMA Makao Makuu. Hatua hii imekifanya chama hicho kukosa viongozi na wawakilishi wa chama mkoa wa Dar ES salaam.
Nane, WANGWE anataka kujua kwa nini Wakurugenzi wote wa CHADEMA wameteuliwa na MBOWE badala ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya chama kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA. Aidha, Kwa Mujibu wa katiba ya CHADEMA kifungu 7.7.3 (vii), Katibu mkuu anatakiwa kuwajibika kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekti. Hata hivyo, DR SLAA ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA hakuwa akitoa ushirikiano kwa WANGWE hadi kufikia kumnyima ofisi alipoteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.
Tisa, Katika moja ya hatua za kumfukuza WANGWE katika Uongozi, Katibu Mkuu aliitisha kikao cha Kamati ya wazee wanne wa CHADEMA lakini kati yao wawili wakiwa wa kabila la Mwenyekiti . Wazee hao wa Kichaga ni EDWIN MTEI ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Wazee wa CHADEMA na PHILIMON NDESAMBULO. Hapo kulikuwa na mgongano wa kimaslahi (conflict of interest). Ikumbukwe kwamba, Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA Bw. EDWIN MTEI ni baba mzazi wa mke wa FREEMON MBOWE kwa maana kwamba MTEI ni mkwe wa MBOWE. Mke wa MBOWE anaitwa DR LILIAN EDWIN MTEI ( Hivi sasa anajulikana kwa jina la DR LILIAN FREEMON MBOWE) ni binti wa EDWIN MTEI.
Kumi, CHACHA WANGWE analalamika kwamba suala la kumfukuza liliibuka ghafla katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA wakati halikuwemo katika agenda. Inadaiwa kwamba MBOWE ndiye aliibua agenda hiyo. Kwa mujibu wa kanuni za CHADEMA, kama suala hilo lilitakiwa kuwa agenda ilitakiwa lijulishwe kwa wajumbe siku 21 kabla ya kikao ili wapate mawazo ya wanachama. Hata hivyo, liliibuka katika kikao bila mtuhumiwa CHACHA WANGWE kujiandaa. Aidha, katika kuhakikisha kuwa WANGWE anavuliwa madaraka yake kwenye kikao, baadhi ya viongozi waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho kwa mujibu wa katibu hawakupata mwaliko kwa sababu ilihofiwa kuwa wangekuwa upande wa WANGWE.
Kwa ufupi WANGWE anadai kwamba kuna ufisadi Makao Makuu ya CHADEMA. Kwamba MBOWE hajatoa maelezo kuhusiana na tuhuma hizo na badala yake anamtuhumu WANGWE kwamba anakigawa chama na kuamua kumsimamisha uongozi.
Katika uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti uliopita, CHACHA WANGWE hakuwa chaguo la Mwenyekiti MBOWE, lakini aliweza kushinda. Kutokana na kitendo cha CHACHA WANGWE kutangaza kwa mara ingine kugombea Uenyekiti wa CHADEMA katika uchaguzi wa Disemba 2008 amezidi kujenga maadui kutoka Makao Makuu ya chama hicho. Hofu ya MBOWE inatokana na ukweli kwamba, hivi sasa WANGWE anaungwa mkono na matawi mengi ya CHADEMA nchini kutokana na msiamamo wake wa kutenda haki na kusimamia ukweli daima.
Hivyo, MBOWE akamjengea zengwe kwamba, WANGWE anavujisha siri za chama lakini katika kikao cha Kamati Kuu hawakuweza kueleza siri ambazo WANGWE anadaiwa kuvujisha. Kwa sababu hiyo, WANGWE anadai kwamba hakuelezwa siri alizovujisha hatua ambayo inakidhi matakwa ya kisheria kwamba MBOWE amemhukumu WANGWE bila hatia. Hatua hii ina lengo la kukwaza ustawi wa demokrasia na utawala bora katika vyama vya siasa.
Katika hili la kuvujisha siri WANGWE anajitetea kwamba kama kuzungumza na wana CCM ni kosa basi mtu aliyetakiwa kuwajibika ni DR SLAA ambaye mke wake ni diwani wa kuchaguliwa wa CCM wakati mkewe CHACHA WANGWE ni mwanachama mwaminifu wa CHADEMA. Kitendo cha DR SLAA kuwa na mke mkereketwa wa CCM yamkini Nyaraka za siri za CHADEMA zinaweza kuangukia kirahisi kwa mkewe na hatimae CCM na pia wageni wa CHADEMA wanaofika nyumbani kwa DR SLAA ambako kuna tawi la CCM kwa maana ya mkewe DR SLAA ambaye anawajibika kuwakirimu wageni na hivyo kusikia mazungumzo yao. WANGWE anataka kujua ni nani kati yake na DR SLAA anaeweza kuvujisha siri za CHADEMA?
Aidha, imeonekana kwamba, kutokana na nafasi yake ya Ubunge WANGWE na wabunge wengine wa upinzani wanaweza kujipatia marafiki kutoka chama tawala CCM kama ambavyo Wabunge wa CCM wanaweza kuwa na marafiki kutoka vyama vya upinzani. Urafiki huu unaweza kuwa wa binafsi/kawaida kuliko mambo ya siasa kwa sababu ya uzalendo, hivyo tofauti ya itikadi siyo uadui bali ni suala la kusimamia ukweli kama ambavyo ZITTO KABWE alivyojumuika na wabunge wa CCM katika kamati ya madini ya Bomani.
Pia WANGWE anadai, kwamba kama kuzungumza na wana CCM ni kosa mbona MBOWE amewahi kuonekana akiwa katika mazungumzo na Rais JAKAYA KIKWETE hata kufikia kumkumbatia mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Halikadhalika MBOWE ameonekana katika mazungumzo na viongozi wengine wa CCM, vivyo hivyo wana CHADEMA wengine?
Kwa ujumla kashfa hizi zinakuja wakati bado baadhi ya Watanzania wanahoji uadilifu wa FREEMAN MBOWE. Kashfa ya kukopa na kushindwa kulipa deni la NSSF kwa muda stahiki ilitia mashaka ya uadilifu wa MBOWE kwa taifa lake. Hakika bila kujibu hoja nzito za WANGWE, Mwenyekiti MBOWE asitarajie kupata kura za Watanzania wenye fikra mbadala katika uchaguzi ujao ndani ya chama chake na asijisumbue kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Natoa mwito kwa MBOWE kuitisha mkutano wa waandishi wa Habari kujibu tuhuma moja baada ya nyingine. Vinginevyo MBOWE atakuwa ameingia katika kundi la Wenyeviti wa vyama vya siasa wanaoua demokrasia nchini.
Kwa upande mwingine, DR SLAA na KABWE ZITTO wamekuwa watu muhimu kwetu watanzania katika kutoa hoja zinazohusiana na ufisadi bungeni lakini inashangaza wameshindwa kudhibiti ufisadi wa MBOWE ndani ya CHADEMA na badala yake wamemwachia WANGWE pekee. Hakika watu hawa walitusaidia sana katika kuunda tume za kuchunguza Richmond na EPA inakuwaje kwa muda mrefu tangu Desemba 16, 2007 wanakalia ripoti ya Kamati ya Mziray iliyoundwa kuchunguza mambo yanayoweza kusababisha migogoro ndani ya CHADEMA? Kamati hiyo ilibaini ubaguzi wa kikabila na kidini katika CHADEMA lakini haikuwekwa wazi kwa Watanzania na wala haijafanyiwa kazi. Je tuwaelewe vipi viongozi hao wa CHADEMA? Ufisadi ni ule unaofanywa na viongozi wa serikali ya CCM tu? Je sio kweli kwamba Hisani siku zote inapasa kuanzia nyumbani???
RUZUKU, UKABILA WAIGAWA CHADEMA
CHADEMA ndicho chama pekee nchini kilichokuwa kinaonekana kutokuwa na migogoro, lakini hili la ruzuku na mengine yanaelekea kukigawa katika makundi mawili ya CHADEMA MBOWE na CHADEMA WANGWE.
Hali hii imejitokeza baada ya kutokea malalamiko ya wanachama wa CHADEMA kususu masuala kadhaa ya msingi. Masuala hayo yameibua mgawanyo uliozaa makundi hayo mawili na baadaye Mwenyekiti wa chama hicho FREEMAN MBOWE akatangaza kumsimamisha Makamu Mwenyekiti (CHACHA WANGWE).
Kwa tafakuri pana kila Mtanzania alitarajia kwamba kabla ya kumsimamisha Makamu Mwenyekiti, CHACHA WANGWE, Mwenyekiti wa chama hicho alitakiwa kujibu tuhuma moja baada ya ingine ili kujisafisha yeye mwenyewe pamoja na viongozi wengine wa juu wa CHADEMA.
Kimsingi,CHACHA WANGWE anamtuhumu MBOWE katika masuala yafuatavyo:-
Kwa ufupi WANGWE anadai kwamba kuna ufisadi Makao Makuu ya CHADEMA. Kwamba MBOWE hajatoa maelezo kuhusiana na tuhuma hizo na badala yake anamtuhumu WANGWE kwamba anakigawa chama na kuamua kumsimamisha uongozi.
- Mosi, Kuna matumizi mabaya ya ruzuku (ufisadi wa ruzuku) ndani ya CHADEMA Makao Makuu. Hivyo, CHACHA WANGWE anamtaka Mwenyekiti FREEMON MBOWE atoe maelezo ya matumizi ya Ruzuku, ambayo ni fedha ya walipa kodi inayotolewa na serikali kwa vyama vyenye wabunge. Aidha WANGWE anamtaka MBOWE aonyeshe mapato na matumizi ya Ruzuku hiyo katika vikao vya chama au aunde kamati ya kuchunguza tuhuma hizo. Pia, WANGWE ana mashaka na hesabu zinazoonyesha mgawanyo wa matumizi ya ruzuku yanayopelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa kutoka chama cha CHADEMA.
- Pili, CHACHA WANGWE hakubaliani na kitendo cha Mwenyekiti na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kuzuia ruzuku isifike mikoani. Anasema hali hii ina maana matawi ya chama yasifunguliwe na chama kisiwe na ofisi hali ambayo inadhoofisha chama. Vivyo hivyo, WANGWE hakubaliani na kitendo cha MBOWE kufuja fedha za chama kwa ziara za helkopta huku akiwaacha wagombea ubunge na udiwani wa chama chake hawana msaada wowote wa kifedha kutoka katika chama. Katika mazingira haya WANGWE anauliza nani anakihujumu chama kati ya MBOWE na WANGWE? Nani anadhoofisha CHADEMA?
- Tatu, CHACHA WANGWE ana hoja kwamba MBOWE, anawajibika kuwaeleza watanzania, ni kwa vipi wabunge watano kati ya sita wa kuteuliwa (viti maalum) wote watoke mkoa wa Kilimanjaro ( MBOWE ni Mchaga wa Kilimanjaro). Ikumbukwe kwamba Tanzania bara ina mikoa 21 na Zanzibar mikoa 5. Kwa kawaida, idadi ya viti maalum inategemea idadi ya wabunge ambao chama kinapata katika uchaguzi mkuu, ambapo asilimia 90 ya viti vya ubunge zilizoleta viti maalum vya CHADEMA zilitoka kanda ya Ziwa. Hivyo, MBOWE kasahau kanda zilizosaidia CHADEMA ikipata viti maalum na kuvipeleka KILIMANJARO.
- Nne, CHACHA WANGWE anamtaka MBOWE, aeleleze inakuwaje kati ya wakurugenzi nane wa Idara mbalimbali za CHADEMA wanne ni Wachaga wa Kilimanjaro?
- Tano, WANGWE anamtaka MBOWE, aeleze umma wa watanzania inakuwaje Madereva wote wa Makao Makuu ya CHADEMA ni Wachaga kutoka Kilimanjaro?
- Sita, WANGWE anataka MBOWE, ajibu tuhuma kwamba yeye mwenyewe, DR WILBROAD SLAA na PHILIMON NDESAMBULO wanajilipa fedha kwa ajili ya kurudisha gharama walizotumia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. WANGWE anauliza mbona wanachama wengine hawarudishiwi gharama hizo akiwemo yeye WANGWE? Je, huu siyo ufisadi? Je huku ni kutenda haki?
- Saba, WANGWE anataka kujua ni kwa nini miaka minne iliyopita MBOWE alivunja tawi la CHADEMA mkoa wa DAR ES SALAAM na kubaki na CHADEMA Makao Makuu. Hatua hii imekifanya chama hicho kukosa viongozi na wawakilishi wa chama mkoa wa Dar ES salaam.
- Nane, WANGWE anataka kujua kwa nini Wakurugenzi wote wa CHADEMA wameteuliwa na MBOWE badala ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya chama kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA. Aidha, Kwa Mujibu wa katiba ya CHADEMA kifungu 7.7.3 (vii), Katibu mkuu anatakiwa kuwajibika kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekti. Hata hivyo, DR SLAA ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA hakuwa akitoa ushirikiano kwa WANGWE hadi kufikia kumnyima ofisi alipoteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.
- Tisa, Katika moja ya hatua za kumfukuza WANGWE katika Uongozi, Katibu Mkuu aliitisha kikao cha Kamati ya wazee wanne wa CHADEMA lakini kati yao wawili wakiwa wa kabila la Mwenyekiti . Wazee hao wa Kichaga ni EDWIN MTEI ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Wazee wa CHADEMA na PHILIMON NDESAMBULO. Hapo kulikuwa na mgongano wa kimaslahi (conflict of interest). Ikumbukwe kwamba, Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA Bw. EDWIN MTEI ni baba mzazi wa mke wa FREEMON MBOWE kwa maana kwamba MTEI ni mkwe wa MBOWE. Mke wa MBOWE anaitwa DR LILIAN EDWIN MTEI ( Hivi sasa anajulikana kwa jina la DR LILIAN FREEMON MBOWE) ni binti wa EDWIN MTEI.
- Kumi, CHACHA WANGWE analalamika kwamba suala la kumfukuza liliibuka ghafla katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA wakati halikuwemo katika agenda. Inadaiwa kwamba MBOWE ndiye aliibua agenda hiyo. Kwa mujibu wa kanuni za CHADEMA, kama suala hilo lilitakiwa kuwa agenda ilitakiwa lijulishwe kwa wajumbe siku 21 kabla ya kikao ili wapate mawazo ya wanachama. Hata hivyo, liliibuka katika kikao bila mtuhumiwa CHACHA WANGWE kujiandaa. Aidha, katika kuhakikisha kuwa WANGWE anavuliwa madaraka yake kwenye kikao, baadhi ya viongozi waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho kwa mujibu wa katibu hawakupata mwaliko kwa sababu ilihofiwa kuwa wangekuwa upande wa WANGWE.

Dr. Slaaa kuna hoja imeibuliwa kuwa Wangwe anavujisha siri ya Chadema kwa watu wa CCM ktk sense ya kukutana nao, nae Wangwe anasema Mkeo ni DIWANI wa CCM...kuna possibility kuwa mkeo akawa na siri nyingi anawapa CCM....hapo unaweza kutuelewesha vipi wanJF...
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
NA
KUSIMAMISHWA KWA MHESHIMIWA CHACHA ZAKAYO WANGWE (MB.) KUWA KAIMU MAKAMU MWENYEKITI WA TAIFA (BARA) WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
Ndugu wanahabari na wananchi wenzangu,
Tarehe 28 Juni 2008 Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo katika kikao chake cha kawaida kilimsimamisha Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe kama Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Taifa (Bara) wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kumpigia kura ya siri ya kutokuwa na imani naye. Huu ni uamuzi mzito na ambao haujawahi kufanywa katika historia ya miaka 16 ya CHADEMA. Tunapenda kuwafahamisha wananchi wetu kwamba uamuzi huu mzito ulichukuliwa baada ya mjadala na tafakuri ya muda mrefu. Kamati Kuu ya chama chetu ilifikia hatua hiyo dhidi ya baada ya kuridhika na ushahidi kwamba Mh. Chacha Wangwe amekiuka maadili ya uongozi na hivyo kupoteza sifa mahsusi za kuendelea kuwa kiongozi wa kitaifa wa CHADEMA kwa sababu zifuatazo:
1. Amekuwa akijihusisha na/au kushiriki katika vikundi na/au vitendo vya uchonganishi na/au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa chama na/au wanachama wake.
2. Amekuwa akitoa tuhuma nzito lakini zisizokuwa na msingi dhidi ya viongozi wenzake wa kitaifa na watendaji wa chama pasipo kupitia vikao halali na wala kuzingatia taratibu za chama
3. Amekuwa akikashifu chama, viongozi na watendaji wake bila kutofautisha kashfa na ukosoaji wa kisiasa na/au wa kiutendaji
4. Kuvujisha siri za vikao halali vya chama kwa watu wanaotaka kuhujumu chama
Ndugu wananchi na wanahabari,
Kamati Kuu ya CHADEMA haikufikia uamuzi huu mzito kwa haraka na/au bila kufikiria kwa kina madhara yake kwa chama na kwa taifa letu. Kamati Kuu imefikia uamuzi huu baada ya jitihada mbali mbali za kumsaidia Mh. Chacha Zakayo Wangwe kujisahihisha na kujirudi kushindikana kabisa. Jitihada hizi mbali mbali ni kama vile:
a. Vikao mbali mbali na vya muda kati yake mwenyewe, Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu kujadili tofauti na/au migongano kati yao na/au ndani ya chama;
b. Kusuluhishwa na Kamati ya Wazee wa Chama ambapo Mh. Wangwe alitakiwa kuandika maandishi kwamba ataacha vitendo vyake dhidi ya chama, viongozi wa kitaifa na watendaji wa chama;
c. Kamati Kuu ya chama kumuonya kuacha vitendo vyake hivyo dhidi ya chama;
d. Baada ya jitihada zote hizi kushindikana, Kamati Kuu ilimsihi kujiuzulu kwa hiari yake yeye mwenyewe na hivyo kujiepusha na adha ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na kusimamishwa na Kamati Kuu.
Kwa vitendo na matukio yote haya, Kamati Kuu ya CHADEMA imejikuta haina njia yoyote ile ya kuepuka mgogoro mkubwa zaidi na usio na maana au msingi zaidi ya kumchukulia hatua za kinidhamu Mh. Chacha Zakayo Wangwe. Kwa matendo haya ni wazi Mh. Chacha Zakayo Wangwe amepoteza sifa mahsusi za kuendelea kushikilia dhamana kubwa ya uongozi ambayo vikao halali vya chama vilimpatia. Kamati Kuu imelazimika kutumia mamlaka yake ya kikatiba ya kumsimamisha uongozi wa kitaifa Mh. Wangwe kwa kumpigia kura ya siri ya kutokuwa na imani naye. Azimio la kumsimamisha Mh. Wangwe kuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti Taifa (Bara) liliungwa mkono na wajumbe ishirini na nne kati ya thelathini na moja waliohudhuria na kushiriki katika kikao cha Kamati Kuu. Idadi hii ni zaidi ya theluthi mbili ya kura za wajumbe wa Kamati Kuu inayohitajika kikatiba ili kumsimamisha uongozi kiongozi yeyote wa kitaifa kama alivyokuwa Mh. Chacha Zakayo Wangwe. Kamati Kuu imechukua hatua hii ngumu na nzito ili kukiokoa chama kutokana na migogoro ambayo imesambaratisha vyama vingine vya siasa hapa nchini.
Asanteni sana
-----------------------------------------------
Freeman A. Mbowe
MWENYEKITI
Naona hatimaye Waraka huu umeletwa JF. Huu ndio Waraka alioandika Balillle na kumpa Mzee Yusuph Halimoja, ndio waraka ambao Chacha Amekuwa akipita katika vyombo vya habari kutoa hoja zake akiusoma.
Katika waraka huu mtaona ule mkakati niliowadokeza wa kumweka Mbowe mwenyewe kikaangaoni, hii ilikuwa ni baada ya mkakati wa mwanzo wa kumng'oa kwanza Dr Slaa kushindwa.
Katika waraka huu Kamati ya Mziray imetajwa, mtakumbuka niliwaeleza siku za nyuma kuhusu hili. Hii ndio njia mpya ya Wagawe, Uwatawale inayoendelea.
Na katika taarifa hii Balille anafanya spinning sasa kuwa ripoti hii iliminywa toka mwezi Disiemba kumbe ukweli ni kuwa ni Mwenyekiti wa Kamati Bwana Mziray ndiye ambaye katika vikao vyote vya kamati kuu vilivyofuata hakutaka kuleta ripoti yake mpaka Mkakati na Rostam wa kumtoa Dr Slaa Dodoma Juni 28 akaipeleka ripoti hiyo Dodoma siku moja kabla ya kikao ili ripoti hiyo isipitie kwenye sekretariati kama zilivyo nyaraka nyingine za kamati kuu.
Sasa kuhusu taarifa ya Mziray, pamoja na kuwa ilifika dodoma bila kupitia sekretariati mwenyekiti Mbowe akiamini katika demokrasia alikubali ijadiliwe(kwa mujibu wa wachambuzi hili lilikuwa kosa la kisiasa la mbowe).
Taarifa hiyo ilijikita katika kusema CHADEMA kuna ubaguzi wa ukabila, elimu na dini. Kwamba CHADEMA inapendelea zaidi wasomi katika kugawa nafasi za utumishi makao makuu na hata viti maalumu. Pia taarifa ili eleza kuhusu ukabila kwa kutumia takwimu zilizotajwa hapo juu.
Mjadala ulipoanza ikabainika kwamba Kamati ya Mziray iliandika taarifa za uwongo kabisa na majungu kwa kutoa takwimu na hoja za uwongo. Kura zikapigwa na wajumbe 29 wa Kamati Kuu wakaikataa hiyo taarifa kama si nyaraka ya chama(total dismissal). Wajumbe wawili tu wakapiga kura za ndio, Mwenyekiti wa kamati Mziray na mjumbe wa Kamati Mzee Shilembi wa Shinyanga. Hata wajumbe wengine wawili wa kamati hiyo waliikataa ripoti hiyo, Katibu wa Kamati mama Sophia Khatau alipiga kura ya hapana na Wakili Mbogoro Mjumbe wa kamati naye alikataa kwa kuwa hakushiriki kwenye vikao vya Kamati. Mjumbe mmoja toka Pemba wa Kamati hiyo alifariki kabla ya Kamati kuwasilisha kazi yake.
RUZUKU, UKABILA WAIGAWA CHADEMA
CHADEMA ndicho chama pekee nchini kilichokuwa kinaonekana kutokuwa na migogoro, lakini hili la ruzuku na mengine yanaelekea kukigawa katika makundi mawili ya CHADEMA MBOWE na CHADEMA WANGWE.
Hali hii imejitokeza baada ya kutokea malalamiko ya wanachama wa CHADEMA kususu masuala kadhaa ya msingi. Masuala hayo yameibua mgawanyo uliozaa makundi hayo mawili na baadaye Mwenyekiti wa chama hicho FREEMAN MBOWE akatangaza kumsimamisha Makamu Mwenyekiti (CHACHA WANGWE).
Kimsingi,CHACHA WANGWE anamtuhumu MBOWE katika masuala yafuatavyo:-Kwa ufupi WANGWE anadai kwamba kuna ufisadi Makao Makuu ya CHADEMA. Kwamba MBOWE hajatoa maelezo kuhusiana na tuhuma hizo na badala yake anamtuhumu WANGWE kwamba anakigawa chama na kuamua kumsimamisha uongozi.
- Mosi, Kuna matumizi mabaya ya ruzuku (ufisadi wa ruzuku) ndani ya CHADEMA Makao Makuu. Hivyo, CHACHA WANGWE anamtaka Mwenyekiti FREEMON MBOWE atoe maelezo ya matumizi ya Ruzuku, ambayo ni fedha ya walipa kodi inayotolewa na serikali kwa vyama vyenye wabunge. Aidha WANGWE anamtaka MBOWE aonyeshe mapato na matumizi ya Ruzuku hiyo katika vikao vya chama au aunde kamati ya kuchunguza tuhuma hizo. Pia, WANGWE ana mashaka na hesabu zinazoonyesha mgawanyo wa matumizi ya ruzuku yanayopelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa kutoka chama cha CHADEMA.
- Pili, CHACHA WANGWE hakubaliani na kitendo cha Mwenyekiti na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kuzuia ruzuku isifike mikoani. Anasema hali hii ina maana matawi ya chama yasifunguliwe na chama kisiwe na ofisi hali ambayo inadhoofisha chama. Vivyo hivyo, WANGWE hakubaliani na kitendo cha MBOWE kufuja fedha za chama kwa ziara za helkopta huku akiwaacha wagombea ubunge na udiwani wa chama chake hawana msaada wowote wa kifedha kutoka katika chama. Katika mazingira haya WANGWE anauliza nani anakihujumu chama kati ya MBOWE na WANGWE? Nani anadhoofisha CHADEMA?
- Tatu, CHACHA WANGWE ana hoja kwamba MBOWE, anawajibika kuwaeleza watanzania, ni kwa vipi wabunge watano kati ya sita wa kuteuliwa (viti maalum) wote watoke mkoa wa Kilimanjaro ( MBOWE ni Mchaga wa Kilimanjaro). Ikumbukwe kwamba Tanzania bara ina mikoa 21 na Zanzibar mikoa 5. Kwa kawaida, idadi ya viti maalum inategemea idadi ya wabunge ambao chama kinapata katika uchaguzi mkuu, ambapo asilimia 90 ya viti vya ubunge zilizoleta viti maalum vya CHADEMA zilitoka kanda ya Ziwa. Hivyo, MBOWE kasahau kanda zilizosaidia CHADEMA ikipata viti maalum na kuvipeleka KILIMANJARO.
- Nne, CHACHA WANGWE anamtaka MBOWE, aeleleze inakuwaje kati ya wakurugenzi nane wa Idara mbalimbali za CHADEMA wanne ni Wachaga wa Kilimanjaro?
- Tano, WANGWE anamtaka MBOWE, aeleze umma wa watanzania inakuwaje Madereva wote wa Makao Makuu ya CHADEMA ni Wachaga kutoka Kilimanjaro?
- Sita, WANGWE anataka MBOWE, ajibu tuhuma kwamba yeye mwenyewe, DR WILBROAD SLAA na PHILIMON NDESAMBULO wanajilipa fedha kwa ajili ya kurudisha gharama walizotumia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. WANGWE anauliza mbona wanachama wengine hawarudishiwi gharama hizo akiwemo yeye WANGWE? Je, huu siyo ufisadi? Je huku ni kutenda haki?
- Saba, WANGWE anataka kujua ni kwa nini miaka minne iliyopita MBOWE alivunja tawi la CHADEMA mkoa wa DAR ES SALAAM na kubaki na CHADEMA Makao Makuu. Hatua hii imekifanya chama hicho kukosa viongozi na wawakilishi wa chama mkoa wa Dar ES salaam.
- Nane, WANGWE anataka kujua kwa nini Wakurugenzi wote wa CHADEMA wameteuliwa na MBOWE badala ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya chama kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA. Aidha, Kwa Mujibu wa katiba ya CHADEMA kifungu 7.7.3 (vii), Katibu mkuu anatakiwa kuwajibika kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekti. Hata hivyo, DR SLAA ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA hakuwa akitoa ushirikiano kwa WANGWE hadi kufikia kumnyima ofisi alipoteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.
- Tisa, Katika moja ya hatua za kumfukuza WANGWE katika Uongozi, Katibu Mkuu aliitisha kikao cha Kamati ya wazee wanne wa CHADEMA lakini kati yao wawili wakiwa wa kabila la Mwenyekiti . Wazee hao wa Kichaga ni EDWIN MTEI ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Wazee wa CHADEMA na PHILIMON NDESAMBULO. Hapo kulikuwa na mgongano wa kimaslahi (conflict of interest). Ikumbukwe kwamba, Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA Bw. EDWIN MTEI ni baba mzazi wa mke wa FREEMON MBOWE kwa maana kwamba MTEI ni mkwe wa MBOWE. Mke wa MBOWE anaitwa DR LILIAN EDWIN MTEI ( Hivi sasa anajulikana kwa jina la DR LILIAN FREEMON MBOWE) ni binti wa EDWIN MTEI.
- Kumi, CHACHA WANGWE analalamika kwamba suala la kumfukuza liliibuka ghafla katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA wakati halikuwemo katika agenda. Inadaiwa kwamba MBOWE ndiye aliibua agenda hiyo. Kwa mujibu wa kanuni za CHADEMA, kama suala hilo lilitakiwa kuwa agenda ilitakiwa lijulishwe kwa wajumbe siku 21 kabla ya kikao ili wapate mawazo ya wanachama. Hata hivyo, liliibuka katika kikao bila mtuhumiwa CHACHA WANGWE kujiandaa. Aidha, katika kuhakikisha kuwa WANGWE anavuliwa madaraka yake kwenye kikao, baadhi ya viongozi waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho kwa mujibu wa katibu hawakupata mwaliko kwa sababu ilihofiwa kuwa wangekuwa upande wa WANGWE.
Hivyo, MBOWE akamjengea zengwe kwamba, WANGWE anavujisha siri za chama lakini katika kikao cha Kamati Kuu hawakuweza kueleza siri ambazo WANGWE anadaiwa kuvujisha.
Aidha, imeonekana kwamba, kutokana na nafasi yake ya Ubunge WANGWE na wabunge wengine wa upinzani wanaweza kujipatia marafiki kutoka chama tawala CCM kama ambavyo Wabunge wa CCM wanaweza kuwa na marafiki kutoka vyama vya upinzani.
Natoa mwito kwa MBOWE kuitisha mkutano wa waandishi wa Habari kujibu tuhuma moja baada ya nyingine. Vinginevyo MBOWE atakuwa ameingia katika kundi la Wenyeviti wa vyama vya siasa wanaoua demokrasia nchini.
Kwa upande mwingine, DR SLAA na KABWE ZITTO wamekuwa watu muhimu kwetu watanzania katika kutoa hoja zinazohusiana na ufisadi bungeni lakini inashangaza wameshindwa kudhibiti ufisadi wa MBOWE ndani ya CHADEMA na badala yake wamemwachia WANGWE pekee. Hakika watu hawa walitusaidia sana katika kuunda tume za kuchunguza Richmond na EPA inakuwaje kwa muda mrefu tangu Desemba 16, 2007 wanakalia ripoti ya Kamati ya Mziray iliyoundwa kuchunguza mambo yanayoweza kusababisha migogoro ndani ya CHADEMA?
RUZUKU, UKABILA WAIGAWA CHADEMA
CHADEMA ndicho chama pekee nchini kilichokuwa kinaonekana kutokuwa na migogoro, lakini hili la ruzuku na mengine yanaelekea kukigawa katika makundi mawili ya CHADEMA – MBOWE na CHADEMA – WANGWE.
Hali hii imejitokeza baada ya kutokea malalamiko ya wanachama wa CHADEMA kususu masuala kadhaa ya msingi.
Masuala hayo yameibua mgawanyo uliozaa makundi hayo mawili na baadaye Mwenyekiti wa chama hicho FREEMAN MBOWE akatangaza kumsimamisha Makamu Mwenyekiti (CHACHA WANGWE).
Kwa tafakuri pana kila Mtanzania alitarajia kwamba kabla ya kumsimamisha Makamu Mwenyekiti, CHACHA WANGWE, Mwenyekiti wa chama hicho alitakiwa kujibu tuhuma moja baada ya ingine ili kujisafisha yeye mwenyewe pamoja na viongozi wengine wa juu wa CHADEMA.
Kimsingi,CHACHA WANGWE anamtuhumu MBOWE katika masuala yafuatavyo:-
Mosi, Kuna matumizi mabaya ya ruzuku (ufisadi wa ruzuku) ndani ya CHADEMA Makao Makuu.
Hivyo, CHACHA WANGWE anamtaka Mwenyekiti FREEMON MBOWE atoe maelezo ya matumizi ya Ruzuku, ambayo ni fedha ya walipa kodi inayotolewa na serikali kwa vyama vyenye wabunge. Aidha WANGWE anamtaka MBOWE aonyeshe mapato na matumizi ya Ruzuku hiyo katika vikao vya chama au aunde kamati ya kuchunguza tuhuma hizo. Pia, WANGWE ana mashaka na hesabu zinazoonyesha mgawanyo wa matumizi ya ruzuku yanayopelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa kutoka chama cha CHADEMA.
Pili, CHACHA WANGWE hakubaliani na kitendo cha Mwenyekiti na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kuzuia ruzuku isifike mikoani.
Anasema hali hii ina maana matawi ya chama yasifunguliwe na chama kisiwe na ofisi hali ambayo inadhoofisha chama.
Vivyo hivyo, WANGWE hakubaliani na kitendo cha MBOWE kufuja fedha za chama kwa ziara za helkopta huku akiwaacha wagombea ubunge na udiwani wa chama chake hawana msaada wowote wa kifedha kutoka katika chama.
Katika mazingira haya WANGWE anauliza nani anakihujumu chama kati ya MBOWE na WANGWE? Nani anadhoofisha CHADEMA?
ITatu, CHACHA WANGWE ana hoja kwamba MBOWE, anawajibika kuwaeleza watanzania, ni kwa vipi wabunge watano kati ya sita wa kuteuliwa (viti maalum) wote watoke mkoa wa Kilimanjaro ( MBOWE ni Mchaga wa Kilimanjaro).
kumbukwe kwamba Tanzania bara ina mikoa 21 na Zanzibar mikoa 5. Kwa kawaida, idadi ya viti maalum inategemea idadi ya wabunge ambao chama kinapata katika uchaguzi mkuu, ambapo asilimia 90 ya viti vya ubunge zilizoleta viti maalum vya CHADEMA zilitoka kanda ya Ziwa. Hivyo, MBOWE kasahau kanda zilizosaidia CHADEMA ikipata viti maalum na kuvipeleka KILIMANJARO.
Nne, CHACHA WANGWE anamtaka MBOWE, aeleleze inakuwaje kati ya wakurugenzi nane wa Idara mbalimbali za CHADEMA wanne ni Wachaga wa Kilimanjaro?
Tano, WANGWE anamtaka MBOWE, aeleze umma wa watanzania inakuwaje Madereva wote wa Makao Makuu ya CHADEMA ni Wachaga kutoka Kilimanjaro?
Sita, WANGWE anataka MBOWE, ajibu tuhuma kwamba yeye mwenyewe, DR WILBROAD SLAA na PHILIMON NDESAMBULO wanajilipa fedha kwa ajili ya kurudisha gharama walizotumia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. WANGWE anauliza mbona wanachama wengine hawarudishiwi gharama hizo akiwemo yeye WANGWE? Je, huu siyo ufisadi? Je huku ni kutenda haki?
Saba, WANGWE anataka kujua ni kwa nini miaka minne iliyopita MBOWE alivunja tawi la CHADEMA mkoa wa DAR ES SALAAM na kubaki na CHADEMA Makao Makuu. Hatua hii imekifanya chama hicho kukosa viongozi na wawakilishi wa chama mkoa wa Dar ES salaam.
Nane, WANGWE anataka kujua kwa nini Wakurugenzi wote wa CHADEMA wameteuliwa na MBOWE badala ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya chama kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA.
Aidha, Kwa Mujibu wa katiba ya CHADEMA kifungu 7.7.3 (vii), Katibu mkuu anatakiwa kuwajibika kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekti. Hata hivyo, DR SLAA ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA hakuwa akitoa ushirikiano kwa WANGWE hadi kufikia kumnyima ofisi alipoteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.
7.7.3 Viongozi Wakuu wa Ngazi ya Taifa watakuwa wafuatao:
(a) Mwenyekiti wa taifa
(b) Makamu Mwenyekiti Bara
(c) Makamu Mwenyekiti Zanzibar
(d) Katibu Mkuu
(e) Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
(f) Naibu Katibu Mkuu (Bara)
Tisa, Katika moja ya hatua za kumfukuza WANGWE katika Uongozi, Katibu Mkuu aliitisha kikao cha Kamati ya wazee wanne wa CHADEMA lakini kati yao wawili wakiwa wa kabila la Mwenyekiti . Wazee hao wa Kichaga ni EDWIN MTEI ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Wazee wa CHADEMA na PHILIMON NDESAMBULO. Hapo kulikuwa na mgongano wa kimaslahi (conflict of interest). Ikumbukwe kwamba, Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA Bw. EDWIN MTEI ni baba mzazi wa mke wa FREEMON MBOWE kwa maana kwamba MTEI ni mkwe wa MBOWE. Mke wa MBOWE anaitwa DR LILIAN EDWIN MTEI ( Hivi sasa anajulikana kwa jina la DR LILIAN FREEMON MBOWE) ni binti wa EDWIN MTEI.
Kumi, CHACHA WANGWE analalamika kwamba suala la kumfukuza liliibuka ghafla katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA wakati halikuwemo katika agenda. Inadaiwa kwamba MBOWE ndiye aliibua agenda hiyo.
Kwa mujibu wa kanuni za CHADEMA, kama suala hilo lilitakiwa kuwa agenda ilitakiwa lijulishwe kwa wajumbe siku 21 kabla ya kikao ili wapate mawazo ya wanachama. Hata hivyo, liliibuka katika kikao bila mtuhumiwa CHACHA WANGWE kujiandaa. Aidha, katika kuhakikisha kuwa WANGWE anavuliwa madaraka yake kwenye kikao, baadhi ya viongozi waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho kwa mujibu wa katibu hawakupata mwaliko kwa sababu ilihofiwa kuwa wangekuwa upande wa WANGWE.
Mapendekezo ya marekebisho ya Katiba yatafikishwa kwa kamati za Wilaya sio chini ya siku 30 kabla ya tarehe ya Mkutano Mkuu unaohusika kujadili mabadiliko. Kamati za Wilaya zitatakiwa kurejesha maoni yake katika siku 21 tangu tarehe ya mapendekezo kutumwa.
Kwa ufupi WANGWE anadai kwamba kuna ufisadi Makao Makuu ya CHADEMA. Kwamba MBOWE hajatoa maelezo kuhusiana na tuhuma hizo na badala yake anamtuhumu WANGWE kwamba anakigawa chama na kuamua kumsimamisha uongozi.
Katika uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti uliopita, CHACHA WANGWE hakuwa chaguo la Mwenyekiti MBOWE, lakini aliweza kushinda.
Kutokana na kitendo cha CHACHA WANGWE kutangaza kwa mara ingine kugombea Uenyekiti wa CHADEMA katika uchaguzi wa Disemba 2008 amezidi kujenga maadui kutoka Makao Makuu ya chama hicho.
Hofu ya MBOWE inatokana na ukweli kwamba, hivi sasa WANGWE anaungwa mkono na matawi mengi ya CHADEMA nchini kutokana na msiamamo wake wa kutenda haki na kusimamia ukweli daima.
Hivyo, MBOWE akamjengea zengwe kwamba, WANGWE anavujisha siri za chama lakini katika kikao cha Kamati Kuu hawakuweza kueleza siri ambazo WANGWE anadaiwa kuvujisha. Kwa sababu hiyo, WANGWE anadai kwamba hakuelezwa siri alizovujisha hatua ambayo inakidhi matakwa ya kisheria kwamba MBOWE amemhukumu WANGWE bila hatia. Hatua hii ina lengo la kukwaza ustawi wa demokrasia na utawala bora katika vyama vya siasa.
Katika hili la kuvujisha siri WANGWE anajitetea kwamba kama kuzungumza na wana CCM ni kosa basi mtu aliyetakiwa kuwajibika ni DR SLAA ambaye mke wake ni diwani wa kuchaguliwa wa CCM wakati mkewe CHACHA WANGWE ni mwanachama mwaminifu wa CHADEMA. Kitendo cha DR SLAA kuwa na mke mkereketwa wa CCM yamkini Nyaraka za siri za CHADEMA zinaweza kuangukia kirahisi kwa mkewe na hatimae CCM na pia wageni wa CHADEMA wanaofika nyumbani kwa DR SLAA ambako kuna tawi la CCM kwa maana ya mkewe DR SLAA ambaye anawajibika kuwakirimu wageni na hivyo kusikia mazungumzo yao. WANGWE anataka kujua ni nani kati yake na DR SLAA anaeweza kuvujisha siri za CHADEMA?
Aidha, imeonekana kwamba, kutokana na nafasi yake ya Ubunge WANGWE na wabunge wengine wa upinzani wanaweza kujipatia marafiki kutoka chama tawala CCM kama ambavyo Wabunge wa CCM wanaweza kuwa na marafiki kutoka vyama vya upinzani. Urafiki huu unaweza kuwa wa binafsi/kawaida kuliko mambo ya siasa kwa sababu ya uzalendo, hivyo tofauti ya itikadi siyo uadui bali ni suala la kusimamia ukweli kama ambavyo ZITTO KABWE alivyojumuika na wabunge wa CCM katika kamati ya madini ya Bomani.
Pia WANGWE anadai, kwamba kama kuzungumza na wana CCM ni kosa mbona MBOWE amewahi kuonekana akiwa katika mazungumzo na Rais JAKAYA KIKWETE hata kufikia kumkumbatia mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Halikadhalika MBOWE ameonekana katika mazungumzo na viongozi wengine wa CCM, vivyo hivyo wana CHADEMA wengine?
Kwa ujumla kashfa hizi zinakuja wakati bado baadhi ya Watanzania wanahoji uadilifu wa FREEMAN MBOWE. Kashfa ya kukopa na kushindwa kulipa deni la NSSF kwa muda stahiki ilitia mashaka ya uadilifu wa MBOWE kwa taifa lake. Hakika bila kujibu hoja nzito za WANGWE, Mwenyekiti MBOWE asitarajie kupata kura za Watanzania wenye fikra mbadala katika uchaguzi ujao ndani ya chama chake na asijisumbue kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Natoa mwito kwa MBOWE kuitisha mkutano wa waandishi wa Habari kujibu tuhuma moja baada ya nyingine. Vinginevyo MBOWE atakuwa ameingia katika kundi la Wenyeviti wa vyama vya siasa wanaoua demokrasia nchini.
Kwa upande mwingine, DR SLAA na KABWE ZITTO wamekuwa watu muhimu kwetu watanzania katika kutoa hoja zinazohusiana na ufisadi bungeni lakini inashangaza wameshindwa kudhibiti ufisadi wa MBOWE ndani ya CHADEMA na badala yake wamemwachia WANGWE pekee.
Hakika watu hawa walitusaidia sana katika kuunda tume za kuchunguza Richmond na EPA inakuwaje kwa muda mrefu tangu Desemba 16, 2007 wanakalia ripoti ya Kamati ya Mziray iliyoundwa kuchunguza mambo yanayoweza kusababisha migogoro ndani ya CHADEMA? Kamati hiyo ilibaini ubaguzi wa kikabila na kidini katika CHADEMA lakini haikuwekwa wazi kwa Watanzania na wala haijafanyiwa kazi. Je tuwaelewe vipi viongozi hao wa CHADEMA? Ufisadi ni ule unaofanywa na viongozi wa serikali ya CCM tu? Je sio kweli kwamba Hisani siku zote inapasa kuanzia nyumbani???
1. Kumi, CHACHA WANGWE analalamika kwamba suala la kumfukuza liliibuka ghafla katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA wakati halikuwemo katika agenda.
2. Inadaiwa kwamba MBOWE ndiye aliibua agenda hiyo. Kwa mujibu wa kanuni za CHADEMA, kama suala hilo lilitakiwa kuwa agenda ilitakiwa lijulishwe kwa wajumbe siku 21 kabla ya kikao ili wapate mawazo ya wanachama.
3. Hata hivyo, liliibuka katika kikao bila mtuhumiwa CHACHA WANGWE kujiandaa.
4. Aidha, katika kuhakikisha kuwa WANGWE anavuliwa madaraka yake kwenye kikao, baadhi ya viongozi waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho kwa mujibu wa katibu hawakupata mwaliko kwa sababu ilihofiwa kuwa wangekuwa upande wa WANGWE.
Dr.W.Slaa Dr.W.Slaa has no status.
Re: Chacha Wangwe si Makamu Mwenyekiti-Katiba ya CHADEMA
1. kuhusu Katiba ya Chadema Ibara ya 6.3.5. Hata havyo naomba nirekebishe kidogo kuhusu 6.3.5(b). Nafasi inayokaimiwa kwa muda usiozidi miezi sita ni viongozi "walioteuliwa tu" tafsiri yako.
2. Haihusiki na viongozi waliochaguliwa. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa Katiba ni uchaguzi unaofanyika na Mkutano Mkuu, na inapotokea nafasi inajazwa na Baraza Kuu na ndicho kilichofanyika kwa Mhe. Chacha.
3. Nafasi hizo hazikufungwa kama zilivyo kwa viongozi wa kuteuliwa kama ilivyo kwa Ibara ya 6.3.5(b) .Hivyo Chacha bado ni Makamu Mwenyekiti kwa mujibu wa kifungu hicho.
4. Swala la kufanyika kwa uchaguzi ni swala tofauti. Natumaini tafsiri ya Katiba imeeleweka vizuri.
wewe uliyeshindwa chaguzi zote za CCM hadi ukahamia TLP ndio umeishiwa hoja. ungekuwa na hoja ungechaguliwa.Kaishiwa hoja huyu ameshaamua kuleta vioja. Anajifanya ananijua kuliko ninavyojijua mwenyewe. His intention was to blacken my name and character and he thought I would let it go just like that. Ukweli siku zote hujitenga. Anafikiri ataficha uzushi wake kwa kuibua madai mengine.
So far ninaamini maneno yote ya pande mbili ni hisia tu bado hatujapata ukweli, ninasema hivi kama haya maneno juu ni ya kweli, basi huko kuna tatizo kubwa na sio dogo na yanahitaji kutatuliwa sasa kwenye hii tatizo.
Kwenye Kamati Kuu baada ya taarifa ya wazee kuwasilishwa akaikana taarifa ya wazee, akawakana wazee, akamwambia Mzee Mtei kuwa hata kama yeye ni mwasisi hawezi kumsikiliza kwa kuwa sasa yeye yuko juu. Akamtukana Profesa Baregu kwa kumwambia tu anyamaze kwa kuwa ni "Mhaya Tu"(alimnukana pia matusi ya nguoni siyataji), Mama Chiku Abwao alipoingilia kati naye akatukanwa. Mwenyekiti wa Madiwani wa CHADEMA Tanzania ambaye pia ni Naibu Meya Wa Halmashauri ya Kigoma Ujiji alipoingilia kati naye akasemwa Vibaya na Chacha.
Sasa imani kwa Chacha ilipotea kutokana na mtiririko wa mambo toka asubuhi ya tarehe 28 mpaka taarifa ya wazee ilipojadiliwa kwa masaa zaidi ya matano. Na kabla ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani alipewa wasaa wa kujieleza, na ndipo alipotukana. Na ndipo alipoamka na kutaka kumpiga Tundu Lissu kwenye kikao.
... lakini kwa maelezo niliyoyasoma toka kwa Mbowe, Tundu Lissu, Dr Slaa, Profesa Baregu, Bob Makani katika Tanzania Daima, Mwananchi, Mtanzania na Mwanahalisi na jinsi ambavyo nimelinganisha na Katiba. Taratibu zote zilufuatwa.
Maswali mbali mbali yamejitokeza, na ningeshauri kila mwenye maswali ya ziada aongezee ili wahusika waweze kutujibu. Unaweza kulielekeza kwa upande unaopendelea kama unaona swali lako ndipo linakohitaji jibu;Haya ni yangu machache na ninategemea kusikia mengi zaidi toka kwa wahusika.
- Kuna ushahidi gani wa Rostam Aziz kuhusishwa na huu mgogoro?
- Hiyo ripoti ya tume ya Mziray, kwa nini isiwekwe wazi na kujadiliwa ukweli au uongo wake?
- Je haingekuwa vema kwa Mh. Mbowe naye kufanya mahojiano na MMJJ (KLH) ili kujibu shutuma zilizoelekezwa kwake?
- Je hapangeweza kufikiwa utatuzi mwingine wowote badala ulio bora na kukinusuru chama kisigawanyike badala ya kumfukuza Mh. Wangwe hasa tukitilia maanani kuwa uchaguzi uko karibu?
- Ni kwa nini Mziray kama amepika ripoti kwa kutumia pesa ya Rostam Aziz, asichukuliwe hatua za kinidhamu kama alivyofanyiwa Mh. Wangwe?
- Kama malalamiko ya Mh. Wangwe juu ya wabunge wa kuteuliwa, madereva na wakurugenzi, je haingekuwa vema kurekebisha hizo nafasi badala ya kumfukuza Wangwe na kuanzisha mgogoro?
- Kwenye mahojiano na KLH, Wangwe alipendekeza kuwa angalau TShs. 100,000 (jumla TShs. 14 million approx.), zitengwe kwa ajili ya kila wilaya, je hili sio wazo zuri ili kuwa na matawi yatakayovuta wanachama kila pande ya nchi badala ya CHADEMA kuwa chama cha mikoa fulani tu?
- Kwa chama chenye mapato madogo kama CHADEMA, je sio wazo zuri kuachana na Helcopter ambayo ni ya gharama kubwa sana na kutumia njia nyingine kuhamasisha wananchi?
Ulipoeleza hapo juu nilifikiri ulikuwepo.
Ni hivi, kama unataka kutu convince Chacha kaharibu huwezi kwenda kuchukua hadithi za yule anaesema Chacha kaharibu halafu ukategemea hiyo itakuwa balanced narration of what transpired.
Na hayo ma tabloid ya Tanzania Daima, Mwananchi, Mtanzania na Mwanahalisi, hao ni wadaku as far as I'm concerned, ambao sidhani hata walikuwepo kwenye mkutano.
Na magazeti mengine hayo si nasikia ni ya Mbowe. Sasa kweli unaweza kuyaleta kama kielelezo kweli?
Tundu Lissu alihadithia kilichotokea na hakusema alitaka kupigwa ila majibizano ya Wangwe.
Narration yako ni ya upande mmoja. To say the least.
Nimetumia credible sources, kwako wewe kuhani Majira na Rai ndio credible zaidi?
Mpigie simu Tundu Lissu umuulize
Profesa Baregu mwenyewe amekiri kwenye mahojiano yake na Mtanzania kuwa Chacha alitumia lugha chafu kikaoni.
Mzee Makani ni mwanasheria naye alieleza ukweli...
Kwa sisi tulio nje ya mifumo ya vyama vya kisiasa, inatusikitisha sana kuona mikoroganyo inapotokea ndani ya mojawapo ya vyama vinavyotegemewa kuleta demokrasia nchini. Hivi karibuni tumeona mvutano ndani ya chama cha CHADEMA kati ya upande unaomuunga mkono mwenyekiti wa chama hicho, Mh. Freeman Mbowe na upande mwingine akiwapo aliyekuwa makamu wake ambaye amevuliwa madaraka, Mh. Chacha Wangwe.
[IZE]
Hao wote ndio alleged victims!
Juma anashitaki Baraka kampiga.
Kutafuta ukweli, unarudi kwa Juma kumuuliza "eti Juma ulipigwa na Baraka?"
Juma keshadai alipigwa huwezi kumuuliza yeye tena. Wala Baraka.
Muulize Roza kama alikuwepo. Third party!
(Unawajua Juma na Roza na Baraka?)
Kama wote hao ni victims basi akaulizwe Rostam Aziz atakuwa na jibu mwafaka!
Maana naona Chacha Wangwe mtu mmoja anaaminiwa kuliko wajumbe watano wa kikao ambao walikuwepo na ni watu wa kuheshimia katika jamii! Basi waulizwe wakina Rostam Aziz na Kaborou.
Last choice, nikuunganisha na Naibu Meya wa Halmashuri ya Kigoma Bwana Shaban Mambo ambaye pia ni mwenyekiti wa Madiwani wote wa CHADEMA?
Au nikuunganishe na Mwenyekiti wa Ruvuma Bwana Fuime au Wa Iringa Dr Kapwani au wa Kigoma Bwana Kasisiko? Chagua yupi, maana hawa wote walikuwepo kikaoni na wanaweza kuthibitisha maneno yangu!
Ndio maana mi nilishasema siku nyingi hapa, wewe ni KUHANI wa MARUHANI, huupendi ukweli unaohusu CHADEMA. Unatoa hoja nzuri unapojadili ufisadi lakini linapokuja suala la CHADEMA basi ni kawaida yako kutoa hoja maruhani
Asha
Umekosea tena.
Hao madiwani wote ni wale wale. Upande uliomuondoa na kudai umetaka kupigwa. Ni Ngedele. Usiwapelekee kesi ya Nyani.
(Nimeongea figuratively hapo, maana hamchelewi ku twisti vitu nyinyi watu.)
Rostam na Kaborou hawahusiki hapa. Unatumia hoja-tasnifa, umepungukiwa na hoja murua? Unanichekesha.
Na kama unaamini CHADEMA wanapigana na ufisadi, huwezi kusema mtu anatoa hoja nzuri za kupambana na ufisadi halafu wakati huo huo mtu huyo huyo anakataa ukweli wa CHADEMA. Ni kujipinga. Njoo na hoja nyingine, hiyo pia mbovu.
Naomba sources za neutral parties.
Na sio wanaosema wametaka kupigwa, wala majarida ya waandishi, au watu wowote ambao hawakuwepo mkutanoni.
Kama vile Asha Abdallah.