Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,193
- 299
Kule bungeni hatupeleki sura, bali watendakazi ambao ndio jeuri ya chama chetu, anasema. Dk Slaa anasema shutuma zilizotolewa na Wangwe, ambaye alikuwa anagombea umakamu mwenyekiti, ni maneno tu ya kumtaka apate nafasi hiyo.
Na wewe pia, maana CCM ndio imekusomesha tena wenda hata allowance ilikua inakupa kwenda middle school,chuo kikuu napo wenda CCM imekulipia gharama zote hata huko Us wenda usikute ni CCM hiyo hiyo ilikupeleka.
ni kweli 80% CCM ndipo imetufikisha hapa tulipo,Maana wengi wetu CCM ndio imetuleta ulaya na marekani na baada ya sisi kuunganika na hawa jamaa waupe ndio tunang'aka kwa CCM iliyotupa mwanga Badala ya kuipa njia mbadala zaidi ya kushambuliana.
MKAMAP...hata kama Chadema kikikumbwa na migogoro, its not a TICKET kuwa CCM it has done something worth...
Kuhusu Kuunganisha Mada naona Ndugu yangu Mkjj ameshikwa na Hamaki, may be aje kuomba radhi kwa hamaki hizo, politics haziendi na hamaki...CCM nao wamekuja nayo kuwa wale wanaodakia Hoja ya Zanzibar ni Nchi wana ajenda ya Siasa..
Admin,Moderators na Kweli mada zimekuwa nyingi mpaka unaona adha kusoma. Its true that kila mmoja anapenda mada aloianzisha iwezekupata audience. Mie nashauri Mods wawe care ili kundi la wanaohisi kuonewa lisiwepo, kila mmoja awe na Haki sawa na wengine.
Ushauri wangu ni kuwa kama mada imekosa Hits ndani ya wiki 2 iwe archived, na ikitokea relevant mada imekuja later, basi kuunganisha ni muhim.
Chuma, sijahamaki, na huo ni msimamo wangu.
Kuna tabia ya watu kutaka kupigiwa magoti pale ambapo wanachokitaka hakifanyiki. Kwa kutumia gia ya "uchadema" wanataka watu watetemeke wakilalamika na wagwaye wakiandika. Jamii hi ya ndugu zetu wakiona jamboo haliendi wanavyotaka wana haraka ya kubatiza watu "msemaji wa Chadema" au "mwanachama wa Chadema" licha ya kwamba hawajui affiliation ya mtu.
Mkuu MMJJ,
Hiki kiburi cha kubeza mawazo ya haki ya mwanaJF umekitoa wapi. Nani kaomba kupigiwa magoti? Hivi ni kosa kwa mtu kuomba thread yake iachwe huru ili ijadiliwe au huko ndio kupigiwa magoti?
Tunapoomba demokrasia tuwe tayari na sisi kuwa wanademokrasia kwa vitendo.
Binafsi nawashukuru ma MoDs kwa kazi nzuri, kubwa wanayofanya ya kuhakikisha kuna sanity hapa na jinsi ambavyo wamekuwa prompt kuhakikisha kuwa mtiririko wa mada unaendelea kuwa vizuri.
Kwa wale tunaopigania demokrasia ya kweli nchini, je hii ni demokrasia kufukuzana uanachama pale unapodai haki yako tena kwa kufuata sheria?
Kama Wangwe akiamua kwenda mahakamani kutafuta haki yake, je hii ni sababu ya kutosha kwa yeye kufukuzwa kwenye chama alichokijenga mkoani Mara hadi kupata ubunge na uongozi wa serikali ya mitaa?
Hawa wanaotoa misemo kwa misingi ya upendeleo ni vema sana waangalie wanachosema kisiwe ni kinyume kabisa na kile wanachohubiri kuwa wanakipigania. Demokrasia sio upande mmoja ni kila mahali na kwenye kila chama.
Wangwe atishiwa kutimuliwa Chadema
2008-07-19 08:58:41
Na Cynthia Mwilolezi, PST, Arusha
Viongozi wa Chadema Wilaya za Arusha Mjini na Vijijini wamesema iwapo Chacha Wangwe ataendelea na vitisho vya kupeleka chama mahakamani, achukuliwe hatua kali ikiwa pamoja na kuachishwa nafasi zote za uongozi alizonazo ndani ya chama.
Walisema sambamba na hilo, hata kumsimamisha uanachama, kwani heri kuwa na wanachama na hata wabunge wachache wanaokitumikia vyema chama na taifa, kuliko kuwa na wanachama wengi aina ya Bw. Wangwe wanaotaka kukisambaratisha chama na kuvuruga jitihada za kuwaondolea wananchi umaskini.
Hayo yamesemwa jana na Katibu mwenezi CHADEMA, wilaya ya Arusha, Bw. Samson Mwigamba na Mwenyekiti Baraza la Vijana CHADEMA, Wilaya ya Arusha, Bw. Zulfikri Mjema, wakati wakiongea na waandishi wa habari ofisini kwao.
Walisema kuwa wanamtaka Bw. Wangwe atulie bungeni ili kuwawakilisha wananchi wake wa jimbo la Tarime na Watanzania kwa ujumla tofauti na ilivyoripotiwa katika vyombo vya habari kwamba tokea asimamishwe umakamu mwenyekiti haonekani bungeni.
``Hii siyo sifa ya wabunge wa CHADEMA na asitumie muda wa kuwawakilisha wananchi kuzunguuka huku na kule na kufanya vita dhidi ya chama, kwani hicho ndicho alichochaguliwa na wananchi wa Tarime afanye hivyo,`` walisema.
Walisema anachokifanya Bw. Wangwe ni sawa na mtu ambaye wenzake wakiwa vitani, dhidi ya adui yeye anarudi nyumbani kwake kuanza kupigana na watu wa nyumbani mwake na kutangaza vita kati ya wanafamilia yake,`` walisema viongozi hao.
Walisema kuwa wanamshangaa kumwona Bw. Wangwe akihangaika kukipaka matope chama chao kwa kupitia vyombo vya habari, wakati wenzake wakiwa katika vita dhidi ya ufisadi, na wananchi wake wa Tarime wakiendelea kuuana kwa vita ya kugombania ardhi na wengine wakitaabika kwa kufukuzwa toka katika maeneo yao ili kuwapisha wawekezaji wa machimbo ya madini.
Viongozi hao walisema kuwa kama Bw. Wangwe aliona kuwa kamati kuu haikumtendea haki alikuwa na nafasi ya kukata rufaa kwenye baraza kuu, ambalo hujumlisha wajumbe wengi zaidi, likijumuisha hata wenyeviti wa wilaya kwa mujibu wa katiba hiyo, hapo angepata nafasi ya kujieleza vizuri na baraza kuu kuangalia kama kweli ameonewa na kamati kuu au la.
SOURCE: Nipashe
KJ.. ni kitendo chenu (wewe na Mkamap) kukandia JF halafu wakati huo kuona ni chombo ambacho mawazo yenu yanapokelewa kama ya wengine. Mnafikiri mkikandia watu na JF au kuihusisha na Chadema basi ndio ma MoD wapige magoti ili wasifikiriwe kuwa ni Chadema. Ni jambo moja kutoa hoja au kuuliza kitu lakini ni jambo jingine kabisa kuwafanya watu duni.
Huko ndiko kupigiwa magoti, kwanini mtu afiikiri thread yake ni kuu mno kiasi kwamba haiwezi kuunganishwa, kuhamishwa, au kuwa edited? Hicho ndicho kiburi ambacho binafsi nakikataa. Kama hakuna miti mitakatifu isiyokatwa Tanzania, na hakuna miti hiyo hapa JF.
JF itaendelea kusimama na kutetewa.
KJ.. you'll be just fine...
I think MMJJ, you can do better than that.
Now that you have failed to show how I insulted (kukandia) JF, why not join my quest to persuade Mods to bring back the thread, so that we can let wanaJF cut it into pieces?
I think MMJJ, you can do better than that.
Now that you have failed to show how I insulted (kukandia) JF, why not join my quest to persuade Mods to bring back the thread, so that we can let wanaJF cut it into pieces?
I think MMJJ, you can do better than that.
Now that you have failed to show how I insulted (kukandia) JF, why not join my quest to persuade Mods to bring back the thread, so that we can let wanaJF cut it into pieces?