CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Hii Thread mbona ina mambo mawili tofauti, kuna issue ya Wangwe na ile ya polisi kutokuwa na risiti? Kulikoni?
 
Kuna mambo mawili aliyotaka kuyasema marehemu na ni muhimu kuyapa yote kipa umbele...Kama moja ni hilo la chadema ama waraka wake wa mwisho kwa Mbowe...Then kuna hoja yake ya madini pia ambayo sijui kama ina nafasi kwenye thread hii ama tuifungulie thread yake?

Swali kubwa la kujiuliza ni moja lenye vipengele Aa na Be.....Lipi muhimu kwa wananchi....

a)Waraka wake kwa Mbowe/chadema.

b)Hoja yake ya madini iliyokuwa ikizuiliwa na mara akafa kabla ama wakati ikitakiwa kusomwa.
 
Waraka wa Madini ,kwa taratibu za Buneg Mhe. spika anweza kuwa nao.ila huu ni warak wa Mbowe na viongozi wote wa juu wa CHADEMA na wale wenye mlengo wa kumnyenyekea Mtu.
 
wewe unataka nani aje athibitishe?nani anaweza pia kuthibitisha tuhuma za pesa za EPA?

tukianza kusema hivyo basi tuache na yale ambayo hatuna uhakika nayo,ila yaliyosemwa ni kweli?

Gembe;
Do not be Naive, E&Y Audit report explains everything about EPA, We want a signed Wangwe's Document to verify its authenticity.
 
Gembe;
Do not be Naive, E&Y Audit report explains everything about EPA, We want a signed Wangwe's Document to verify its authenticity.
hiyo mbona ishu ndogo na inawezekana?mie nafikirir tuangalie nadhalia ya jambo lenyewe na wangwe alikuwa akisema nini kuhusu CHADEMA
 
Mimi naweza kuamini kuwa huu ni waraka wa Wangwe kweli kwani sentiments zake siyo ngeni na lugha yake haitofautiani na jinsi Wangwe anaandika. Swali langu hata hivyo ni walioupata wameupata wapi wakati tuliambiwa kila kitu kiliibwa pale kwenye ajali? Kama kuna mtu alikuwa nao kabla ya safari ni nani huyo, na kama kuna mtu ulimfikia baada ya ajali ni nani huyo? na wote hao waliupata wapi kwanza?

Kwa sababu kama kuna mtu mbaya ambaye aliupata waraka huu masaa machacha kabla ya Wangwe kulazimika kuondoka na akaona uzito wa madai yake ni wazi angeweza kuchukua kitu chochote na kufanya kweli ili aiharibu Chadema kabisa kwani sasa mwandishi "wake" hayupo kutetea alichoandika au kusema "hapana hicho sikukiandika".

Gembe, unafikiri waraka huu umepatikana lini? Kabla ya kifo au baada ya kifo..?
 


Mwanakijiji

Mzee nimekusoma, kweli huyu kautoa wapi huu waraka jamani? Da........... hapa kuna siri nzito, hawa watakuwa wanajua kitu.

Kuanzia ule waraka wa CCM kabla ya kifo cha marehemu, hapa kuna jambo

Gembe Uko wapi uyajibu haya Mkuu?
 
hili ni swali ambalo tunatakiwa tumuulize aliyeleta waraka huu
 
hili ni swali ambalo tunatakiwa tumuulize aliyeleta waraka huu

Gembe

Naomba utudurusu hata kidogo mkuu, naona kuna hoja unaweza kuzijua, unajua si vizuri kukaa kimya, sisi tunakusubiri, ainisha basi hata kidogo, nini lengo la CCM kuuleta waraka huu hapa jamvini?
 
Mwanakijiji

Mzee nimekusoma, kweli huyu kautoa wapi huu waraka jamani? Da........... hapa kuna siri nzito, hawa watakuwa wanajua kitu.

Kuanzia ule waraka wa CCM kabla ya kifo cha marehemu, hapa kuna jambo

Gembe Uko wapi uyajibu haya Mkuu?

Kwanini hatujiulizi kwanini baaada ya wangwe kuandika waraka huu wa kuuponda uongozi wa CHADEMA alikufa kabla hajufikisha mbele ya watu?

Je kuna kiongozi yeyote wa CHADEMA alijua?Ndiyo walijua sababua lsiahawaambi baadhi ya watu..

Mkuu Mwanakijiji,

kuna jambo moja ambalo ningesema wazi,Baadhi ya wanachama wa CHADEMA ni wanafiki sana,unakumbuka therad ile ya wangwe kusimamishwa,watu kama kina MK walileta mapema resolution ya kusimamishwa kwa wangwe,sijui waliitoa wapi ambapo ilikuwa ni jmuda mchache baada ya kikao cha dodoma,inaonesha kuna mbinu chafu zilipangwa kabla.

Ukiendelea kupitia thread ile ambayo kwa sasa haionekani(Invisible kulikoni).utagundua jinsi wana CHADEMa ambo wako hapa JF walivyomdhihaki wangwe na hili ndilo kosa kubwa walilofanya,nina mshukuru sana kitila kwa kutoka nje na kuelezea upungufu walioufanya CHADEMA.

kwa maoni yangu CHADEMA Hawakustahili kufanya jambo lile wakati walikuwa wakishindana na chana tawala katika hoja za ufisadi,navyokwambia sasa hoja ya ufisadi ilimalizwa haswa na ugomvi wa CHADEMA kwa kiasi kikubwa magazeti yakabalidili mwelekeo mzima,kifo ndiyo basi tena ukawa mwisho wa mafisadi kujadiliwa.

Mie siyo kwamba nakumbatia ufisadi wala CCM(ambacho ni chama changu) ,ila siku zote nimekuwa nikitaka tujadili hoja zinazohusu wizi wa mali zetu kama watanzania,tujadili kwanini nchi na rasilimali zetu zote ila bado uchumi wetu uko chini?nyie mkaamua kuwaunga mkono kujadili kile walichokitaka,wameshashinda tena na hili ni bao la tobo.

Ndugu watanzania wenzangu,wana mapinduzi wenzangu kuna haja sasa ya kuanzisha mijadla ya kitaifa yenye kuleta tija na ambayo tutaifuatilia mpaka mwisho.Bajeti Muhimu zimepita ila zilizo na madudu kibao kwa kuwa tulipenda sana kukitetea chama zaidi,na mtu kwa ujumla,Hibvi kweli leo tumekuwa watumwa wa kuja kumtete mtu hapa?

tukate ishu
 
Waraka wa Madini ,kwa taratibu za Buneg Mhe. spika anweza kuwa nao.ila huu ni warak wa Mbowe na viongozi wote wa juu wa CHADEMA na wale wenye mlengo wa kumnyenyekea Mtu.

Kwa hiyo unakiri kwamba kuna waraka wa kisiasa na hoja yenye maslahi ya Taifa?
If thats the case then huna nguvu tena kwasababu umeshakiri kuwa hoja iko kwa Spika Six...Swali ambalo mmeshindwa kujibu...Waraka wa Wangwe ambao ulipotea ajalini mliupata vipi?
 

FYI...Ukitaja chadema hapa ni Politics na ukitaja hoja ya madini ni real issues...Kama watu wa Tarime wamesoma na kuelimika(Tofauti na wewe) basi ni wazi wanakuona HAMNAZO KABISA...Wao hawajali vyama...NI HOJA YA MASLAHI YAO AMBAYO NI MASLAHI YANAYOPIGANIWA KATI YA WANANCHI,WANAUSALAMA MAFISADI NK.
 
Kwa hiyo unakiri kwamba kuna waraka wa kisiasa na hoja yenye maslahi ya Taifa?

Jmush1,

Hili liinchi bora tuliuze tugawane, haiwezekani mtu maka Gembe atuambie hivi mara vile sasa sisi tushike wapi jamani?
 
[/COLO

Kama hakuna majibu ya maswali hayo tunaamini vipi ukweli juu ya ujumbe uliokuwemo ndani ya waraka huo, na vipi iwe changamoto kwa Chadema?

Tunahitaji kujadili kwa kina kuhusu waraka huu ulivyopatikana kabla ya kujadili kilichomo ndani yake na kuanza kuishutumu chadema.

hongera Dk Slaa kwa kujibu.
 
Jmush1,

Hili liinchi bora tuliuze tugawane, haiwezekani mtu maka Gembe atuambie hivi mara vile sasa sisi tushike wapi jamani?

Cha muhimu ni kwa wazalendo kuwaelewesha wananchi kuwa kwenye issue hii kuna siasa na maslahi ya Taifa...Hivyo Isaya Mwita huna haja ya kuishiwa na nguvu sasa...Badala yake pigeni moyo konde na muwaeleze wananchi ukweli kuwa tishio la Wangwe halikuwa waraka wa kisiasa kwa chadema...Bali kilio cha hoja yake....Kilio kilichoonyeshwa wazi na spika kwa niaba ya wazalendo...Kilio hicho...Si kilio cha kisiasa kwani hoja ya msingi aliyoiwakilisha marehemu inapoelekea kutaka kuuwawa kwa kigezo cha kifo cha mtoa hoja ni jambo la kisikitisha.

Kama kweli ccm mafisadi hawachezi na usalama wa Taifa...Basi waache mchezo mchafu mara moja na wahakikishe siasa haitumiwi kuligawa Taifa na kusababisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
 

Jmush1,

Habari za kifo ndugu yetu Wangwe hatukijadili tena, tunajadili ni vipi CCM watunyang'anye Migodi yetu, ardhi yetu, Wangwe ni mpiganaji naye kamaliza kazi yake hapa duniani, kazi kwangu mimi na wewe Jmush1 tuiendeleze vita kati aya sisi na hawa mafisadi, tia akili, acha uzembe wa kufikri Mkuu.

Jmush1,tukiwapa muda hakika hawa mafisadi watatuuza hata sisi na wake zetu, na ikibidi hata wewe huko US watakupandilia hukohuko
 
Nina uhakika kwa kiasi kikubwa haya ni maneno ya Wangwe, a week before kifo chake nilikutana naye Mlimani city, Shoprite akiwa na familia yake, kwa wanaomgahamu Wangwe alikuwa ni mtu wa watu, nilimuuliza nini tena jamani CHADEMA ku nani? Sehemu kubwa ya maelezo yake yapo kwenye huu waraka na alinieleza kabisa Mh Mbowe anauwa chama yeye alikuwa anataka kumshitaki kwa wanachama waamue hasa kwenye kuimarisha chama kwenye ngazi ya vijiji Wangwe alikuwa anaamini wapig kura wengi wapo huko. Pia kitu kingine alichokuwa hakubalianani na Mbowe ni suala zima la Mh kugombea uraisi, alidai CHADEMA kina hitaji wabunge wengi watakao toa changamoto kwa chama tawala, alimtaka mbowe agombee ubunge. Mengi aliongea na na siku ya pili yake nilimpigia simu tukaongea kirefu tu. Ninashawishika huu waraka una ukweli hata kama umeongezewa chumvi kidogo. Swali linalo nitatatiza huyu aliyeweka huu waraka ameutoa wapi, ama ndo wale waliyoondoka na laptop ya marehemu? Deus Malya anaweza kuwa na Msaada sana kwenye hili.

Mungu ampuzishe kwa amani Rastafarian Chacha Wangwe


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…