CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Tuna uhakika hii ndio kauli ya mwisho? Unless kuna mtu alikuwepo wakati Chacha anafariki. Kama vitu viliibwa ikiwemo laptop, nyaraka n.k basi kuna mtu anajua nyaraka hizo zilizpo na zimekuwa zikiibuliwa pole pole.

......
vipi kama ni ccm ndio walioandika waraka huo na kuusambaza kwa jina la wangwe wakitaka watu tuache kuuongelea na kufichua ufisadi wao na kuongelea marehemu na mgogoro wa chadema? ni vp watathibitisha hayo kweli ni maneno ya chacha? kwa nini hayakutoka ndani ya mwezi mzima aliosimamishwa kuwa makamu mwenyekiti yatoke baada ya kufa? kuna kitu hapo na kama lengo lao ni kutupoteza maboya tusahau usifadi wakati unatuumiza, wala hatusahau
 
Gembe waraka wa kumfungua Wangwe au maamuzi hayo watu wa Chadema wana haki kuwa nayo, na wao wakitoa ni rahisi kueleweka. Lakini inapotokea vitu vya marehemu vinapoonekana kwa jirani, watu tunauliza "jirani ulivipata lini vitu hivyo vya marehemu?" Kuna jibu rahisi tu linaloweza kutolewa kuwa vitu vya marehemu pale kwenye ajali si vyote viliibwa au kutoweka. Na miongoni mwa vitu hivyo ni a, b, c n.k

Tatizo kubwa kwangu ni baadhi ya vitu hivi vinapoibukia mikononi mwa CCM.
 

MKuu nachelea kusema unaongea pumba hapa Jibuni hoja otherwise... NINYI SIO WATU WA KUAMINIKA HATA KIDOGO!!!... in fact mnadeserve kuitwa spinners....

Na kwa kweli nasikitishwa kwamba JF tunaelekea pabaya ... ati kwamba hoja ni za CCM, CUF tu ndio zinahitaji kujibiwa... za chama TEULE... TUKUFU Chadema sio za kujibiwa... inasikitisha sana...

Tena mambo yenyewe yako... wazi.
 


Sasa mkuu unafika mbali.Ni kwa nini unataka Dr.Slaa aongelee suala la Mbowe kama Mbowe? Si ni bora basi hata ungekua unamtaja Mwenyekiti? Maanke slaa akikujibu kwamba sula la Mbowe silijui ungeona unaonewa
 
Ili kumuenzi Chacha Wangwe, UONGOZI wa CHADEMA uusome vizuri WARAKA huu waone ni lipi la KUZINGATIA na linalohitaji hatua za haraka kuchukuliwa ili kuweka sawa pale walipokuwa wanakosea. CCM walishindwa kumuenzi MWALIMU kwa vitendo na sasa akina Mkapa hata ile kwenda kuangalia mpira kiwanjani hawawezi.
 

Rudini kujibu hoja kwenye original post! over.
 
Hakuna kilichoulizwa kwenye original post!

Kwi kwi kwi...

Hakuna lolote... kumbe haya tunayoongelea siku zote hapa ... ni upupu tu! Nitarajia ku-staafu muda si mrefu... napenda watu wanaojadili kwa kuweka taifa mbele na kutolala upande mmoja... kitu ambacho hapa naona... hakuna...
 
Naamini cha muhimu ni kutizama the contents za huo waraka. Kwa mtizamo wangu that is what counts. Haijalishi nini chanzo cha hii documents. Cha muhimu hapa; je hizi shutuma zipo chadema? ni msimamo wa chadema? Lets say, kama document hii imetolewa na mtu wa ndani ya CHADEMA ambaye anataka " kumfunga paka kengel". To me what counts ni contents na si form kama wengi wanaong'ang'ania. Wadanganyika tuna safari ndefu....Cause of the cause, has caused the cause of the cause...

I humbly submit. Mpiganaji
 
waraka Umebeba Mambo Mazito Sana. Wether Huo Waraka Ni Original Or Not Lakini Umesheni Yale Yote Ambayo Marehemu Wangwe Alikuwa Amepania Kuyafanyia Kazi Kwa Manufaa Ya Wana-chadema Wote Na Ndiyo Hayo Yaliyomfanya Hadi Kusimamishwa Uongozi.
Kwa Wanasiasa Hapo Sasa Wanachofanya Ni Kujaribu Kutafuta Njia Ya Kukwepa Kujibu Zile Ambazo Ni Hoja Za Msingi...hao Ndiyo Tunaowategemea Waje Waunde Serikali Mbadala...nadhani Itakuwa Ni Zaidi Ya Haya Yaliyotokea...kauli Zinaonesha Kaharufu Ka Kulindana Na Kuogopana...no, Kuna Jambo Zito Zaidi.
 
Serious question needs to be answered. It does not seem to have been signed? who has seen a signed one, if not how can it be taken to be his?

I think the issue here is, the validity of these serious accusations and NOT who actually wrote them down!

CHADEMA leadership OWES wananchi a clear explanation of the truth!!!!
 
CONCLUSION; whether you like or not, MR FREEMAN MBOWE jiuzulu wadhifa wako,,haufai ka mwenyekiti na kama alivyotuonya bwana Mrema 2005 kwamba wewe na Lipumba hamna experience ya kuongoza watu...kama utakataa ukweli jiandae kwa anguko jingine ambalo litakupeleka kubaya zaidi
 
kauli ya mwisho ya chacha .zak. wangwe..POLITICS,WELL AS THEY SAY ITS A DIRTY GAME..maswali mengi yanayo hitaji majibu ya kina, na yaliyo ongoka.toka kwa uongozi wa juu wa chadema. fedha za ruzuku, ukabila, umangi meza, ufisidi, ubabe, ujeuri..so forth and so on..AHH..MZEE WA HELIKOPTA, NI WEWE KWELI KAMANDA...hebu tusikie the other side of the coin...isije kauli ya Rastafarian zak.wangwe.MUNGU AILAZE ROHO YAKE PEMA PEPONI. ikatupunguzia hamasa na imani kubwa ilio anza kujengeka kwetu sisi tunao lala hoi ndani ya nchi yetu.kuwa tumepata chama kinacho tupigania. MZEE WA SLAA ZA MAANGAMIZI..epa,meremeta,richmond,deepkijani..ni kweli mzee kuna kibanzi kwenye jicho la chama cha demokrasia na maendeleo?? hebu safisheni hali hii ya hewa ilio chafuka ndani ya chama.nanyi vijana ndani ya chama KAMANDA ZITTO,MZEE WA MADINI.ya fanyieni kazi yalio kuwa yakimzonga marehemu MPIGANAJI CHACHA.ZAKARIA.WANGWE kwani kama ndivyo chama kinavyo endesha mambo yake..basi mjue wazi kuwa chama kinaaishi "KWA MATUMAINI"...
 
Kasheshe na wengine, hoja zilizomo humo ni za msingi na madai yanayotolewa ni mazito na yanayohitaji majibu. Hilo halina ubishi. Binafsi nitaangalia madai ambayo yanahusiana na "facts" kuliko yanayohusiana na "mitizamo na hisia". Hayo mengine ni vigumu kuyafuatilia kwani anayedaiwa kuwa mhusika hayupo tena (nitalirudia hili mwisho).

Madai yanayodai Ukweli wa takwimu na vidhibiti.

HOJA YA KWANZA YA WARAKA:


MAJIBU YANAYOHITAJIKA:
Je ni kweli Chadema inapata ruzuku ya milioni 66 kwa mwezi? Na kama ni hivyo je ni kwa sababu gani wameshindwa kutumia kiasi (kama kilichopendekezwa na waraka au vinginevyo) kugawa fedha kila jimbo au kila wilaya ili kukiimarisha chama chao? Kwa maneno mengine, kinachohitajika kuoneshwa ni uhalalishaji wa matumizi ya fedha hiyo ukiondoa shughuli za kuimarisha chama wilani au majimboni. Yaani, ni kitu gani kinahalalisha matumizi ya fedha hizo nje ya kuimarrisha chama majimboni au wilayani. Je kati ya milioni 66 yawezekana kutoa milioni 12 au 23 kila mwezi kwa shughuli za kuimairisha chama wilayani/majimboni, kama haiwezekani ni KWANINI?.


HOJA YA PILI YA WARAKA:



MAJIBU YANAYOHITAJIKA:

Kwanza kama ni kweli Chadema inapokea milioni 66 kwa mwezi basi kiwango kilichotakiwa kuwa kimepatikana kwa miezi sita ya mwanzo ni milioni 396 na siyo 374 (isipokuwa kama kuna makato ambayo mimi sijayaingiza).

Katika hili cha kwanza kinachohitajika ni kujulikana kwanza kwa muda wa miezi sita ya mwanzo Chadema ilipata kiasi gani kama ruzuku. Na pili kati ya kiasi hicho ilitumia kiasi gani makao makuu na kwa vitu gani na kiasi gani kilitumika nje ya makao makuu. Tatizo siyo tu la kutumika kiasi hicho lakini hasa ni kuhalalisha matumizi hayo. Kama ni kweli zimetumika milioni 350 makao makuu ni wazi Chadema wanaweza kuonesha kitu hicho kilichostahil matumizi hayo. Kinyume chake pia ni kweli, kiwango chochote kilichotumika makao makuu lazima kioane na huduma au bidhaa iliyolipiwa kiasi hicho.

DAI LA TATU LA WARAKA:
Kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Mhe. MBOWE alitufahamisha wanachama kuwa alikuwa anakidai chama US $ 181,949.00 sawa na Tshs. 218,338,546. Mpaka sasa chama kimekwisha mlipa Tshs. 175,000,000/=

MAJIBU YANAHOHITAJIKA:
Hapa ni rahisi kwani ni swali la "kitu ni cheupe au cheusi"? Je Mbowe aliikopesha Chadema kiasi chochote cha fedha kwa mkataba gani? Hivyo kuna swali alikopesha au hakukupesha? Kama alikopesha ilikuwa ni kiasi gani na kwa mkataba gani?

Hili siyo gumu kulielewa na halina matatizo kwa sababu kama wanavyosema wenzetu "the devil is in the detail". Ni vizuri kuona mkataba huo (kama upo) na masharti yake. Endapo mashart hayo (kama riba n.k) ni kubwa mno basi kuna haja ya Chadema au Mbowe kuelezea ni kwanini waliingia mkataba wa aina hiyo ambao kimsingi unafanya Chadema kuwa na mzigo.

DAI LA NNE

Na kwa kuwa hata baada ya kuwa Mhe. MBOWE amekwisha lipwa zaidi ya nusu ya deni alilodai kuikopehsa CHADEMA, vifaa vyote yakiwemo magari, vipaza sauti na kadhalika vimebakia kuwa mali yake binafsi,

Hili nalo ni swali la "cheupe au cheusi"? Je vifaa vyote vikiwemo magari, vipaza sauti "n.k" vimebakia mali yake binafsi? Ni rahisi kulikanusha dai hili au kulithibitisha kwani vitu vina mmiliki na mali za Chadema zimeorodheshwa na mkaguzi. Chadema wanaweza kuliengua dai hili kwa kuonesha orodha ya mali zao.

DAI LA TANO


MAJIBU YANAYOTAKIWA:

Kwanza hapa kuna kitu tunachokiita kama 'pseudo-obviousness". Kwamba, ni ukweli usiopingika na kila mtu anajua ukweli huo. Sasa Chadema au Mbowe na wenyewe waseme kama ukweli huu ni readily available kuwa "walighushi orodha ya majina ya viti maalumu". Kama ni kweli basi wakiri ni ukweli kwani tumeambiwa na waraka kuwa hili halina "mjadala".

Zaidi ya yote kuwa Mbowe na Dr. Slaa waliomba radhi kwa "kughushi" na "kuvunja Katiba" ni madai mazito kwani yanakiri kufanya makosa yaliyotajwa. Je ni kweli radhi hiyo iliombwa na kwa kosa hilo la kughushi?

MADAI YA SITA - Ubabe


MAJIBU YANAYOHITAJIKA
Je ni kweli huyo mtu yupo? na je ni kweli alichaguliwa na ni kweli hafanya kazi yake? Lakini kubwa ni je hafanya kazi hiyo kwa sababu ya Mbowe? Na je ni kweli Chadema haifanyi kazi ya siasa mkoani Dar kwa miaka minne?

MADAI YA SABA: VYAMA DADA SHIRIKI


MAJIBU YANAYOHITAJIKA.

Hapa napo ni rahisi pia; je ni kweli vyama hivyo rafiki vinaulalamikia uongozi wa Chadema? Je ni kweli walitoa msaada wa Shs milioni 78 kwa ununuzi wa baskeli na pikipiki na vitu hivyo havijanunuliwa hadi sasa. Majibu yake ni rahisi kwani ni ndiyo au hapana na maeleezo kidogo.

MWISHO:

Utaona kuwa nimeyaacha madai yoyote ambayo yanadai mang'amuzi binafsi kwani kwanza hatujui mwandishi wa waraka huu ni nani hasa ingawa unataja kuwa ni wa "Wangwe". Hadi Polisi waseme kuwa kuna nyaraka za Wangwe ambazo zimepatikana na wanathibitisha kuwa ni za wangwe (through chain of custody) ni vigumu kukubali kuwa ni wa Wangwe. Lakini pia kwa sababu, masuala yanayohusu vionjo, hisia, mitazamo na mang'amuzi binafsi ni vigumu kluyahoji kwani ni vitu ambavyo vya kibinafsi sana. Lakini zaidi ni kwa sababu kama kweli ni waraka wa Wangwe kuna maswali ambayo yeye pekee angeweza kuulizwa.
 
Gembe kwa umakini wako nilitumaini uliisha kuelewa niliposema nilikuwepo na kuona kwa macho yangu. Sijui unataka nizungumzie nini? Katika mambo haya partisanship haisaidii sana. Unasema (waraka)...umesema ukweli wotekuhusu Chadema...It is clear you have made up your mind. Sidhani hata nikieleza itasadia nini. Prejudice ni mbaya sana.
Nadhani kwa wanaofuatilia niliisha kueleza kuwa hatuna la kuficha na wala hatuna la kujibu.Ni swala la mtu kushikilia tu mtizamo wake vs majority. Wakati utakapofika tutatoa yote systematically na wote wenye mapenzi mema wakitaka wanaweza kuja kufanya verification. Lakini upotoshaji kama wa RAI kuwa wabunge wajichotea hela... bila hata kupiga simu kujua walilipwa za nini nadhani ni kinyume na journalistic ethics. Lakini ndiyo nchi yetu ilivyo na wengi wetu tunafahamu sababu ndiyo maana, .. ukikutwa unaoga na kichaa kakimbia na nguo zako huhitaji kumkimbiza uchi, kwani wanaokuona hatatambua kichaa ni nani kati yenu...' Kimya chetu kitafsiriwe na wenye kutafakari katika misingi hiyo.
 


Haya ndiyo maneno; kwangu la maana ni kujibu hoja ambazo ni za msingi na zijibiwe zikaridhisha. Masuala ya mahesabu tumeshaambiwa kuwa Chadema wako huru vitabu vyao kuangaliwa na mtu yeyote sasa kwanini waandishi walioko karibu wasiende kuviangalia vitabu hivyo lakini kuendelea kuandika madaai? Maswali mengine yanahitaji kupangiliwa majibu ili kuondoa utata wowote ule.
 
Tuna uhakika hii ndio kauli ya mwisho? Unless kuna mtu alikuwepo wakati Chacha anafariki. Kama vitu viliibwa ikiwemo laptop, nyaraka n.k basi kuna mtu anajua nyaraka hizo zilizpo na zimekuwa zikiibuliwa pole pole.

hii habari ya kuleta habari za kuandika andika tu hapa ni kutupotezea muda na kuleta propaganda zisizo na kichwa wala mbele, hata mimi leo naweza kuandika chochote nitakacho na kukileta hapa.
 
tatizo
mwkjj ni kua
saizi wanaweza fanya watakalo maana RIP hatunaye.Huyu Mbowe kama angekua mkweli angefuata ushauri wa CHACHA kumuonyesha mahala fedha hizo zilipoingilia ktk akaunti ya chadema.Mbowe kama alishindwa kumuonyesha hayo RIP CHACHA aliyekua mwenyekiti mwezake kwangu mimi yote yatakayo kuja ni ya kupikwa, mmeyapika sasa mnatengeneza njia ya kuyatoa kwani tutaamini vipi hayajatengenezwa jana.Kama yengelikuwapo toka wakati huo asingesita kumuonyesha mwezake hadi wakagombana.

Pili Mimi naona Mbowe ni fisadi fulani yani chama hakina fedha anakikopesha harafu fedha hizo anazitembelea mwenyewe kwa helkopita na mwisho anadai zirudishwe.

Mbowe kama alivyosema RIP gharama alizutumia mwenyewe kugombea Urais kwanini adai kurudishiwa?? Ndiyo RIP akaendelea kuhoji naye ktk ubunge alitumia gharama zake hivyo nae angehitaji kurudishiwa gharama hizo.

Mbowe alijua kabisa urais hapati ila aka manipulate kugombea urais ili aongeze gharama na ajilipe fwedha ndefu .
 
Kitu cha kufanya saizi Mbowe sio kutuletea mikataba.

bali aanze kwa kutu convice kwa kuprint Bank statement pesa hizo zilipoiingilia miezi sita kabla hadi leo.
pia walete hicho walichoandika bank wakati wanaiingiza hizo pesa hapo utakua mwanzo mzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…