CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

KAULI YA MWISHO YA MAREHEMU CHACHA WANGWE KWA
MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE

HII NI TAARIFA YA MHESHIMIWA WANGWE KUHUSU JARIBIO LA MWENYEKITI WA CHADEMA, FREEMAN MBOWE KUMVUA WADHIFA WAKE NA UANACHAMA WA CHADEMA ALIYOTARAJIA KUISOMA KWA WATANZANIA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA KUFIKA DAR ES SALAAM, DHAMIRA AMBAYO ILIKATISHWA NA MAUTI YALIYOTOKANA NA INAYOSEMEKANA KUWA NI AJALI YA KUPANGWA, ENEO LA PANDAMBILI, WILAYA YA KONGWA DODOMA TAREHE 28 JULAI, 2008.

Taarifa hii ilikuwa isomwe Dar es salaam, tarehe 29 Julai, 2008 siku moja kabla ya ajali iliyomuua CHACHA WANGWE

UTANGULIZI

Jumamosi, June 28 mwaka huu wajumbe kadhaa wa Kamati Kuu ya CHADEMA walidai kuwa wamesitisha Umakau Mwenyekiti wangu katika kikao kilichofanyika mjini Dodoma siku hiyo. Kesho yake Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. FREEMAN MBOWE akaitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutaja sababu za kunisimamisha uongozi.

Inatosha tu kusema kuwa sababu zote alizotoa ni za uzushi kama ile inayodai kuwa mimi navujisha siri za chama kwa viongozi wa CCM bila hata kutaja siri hizo, au kusema nimezitoa lini, wapi, na kwa kiongozi yupi?

Kikao hicho kinachosemekana kunisimamisha uongozi, kilikuwa na wajumbe 31 ambao takribani nusu hawakuwa na uhalali wa kupiga kura kinyume cha katiba na kanuni za CHADEMA kwa vile walikuwa wameandaliwa kwa kazi hiyo. Wajumbe 7 walikataa kushiriki njama hizo.

Kufuatia jaribio hilo la kunivua uongozi kutokubalika kwa wanachama walio wengi wa CHADEMA , Mwenyekiti MBOWE na wafuasi wake wameendelea kuhaha kwa kuongeza sababu nyingine mbalimbali ili kuhalalisha njama zao. Sasa hivi wameingia hatua ya kuwashawishi wanachama wa Tarime eti wanifukuze uanachama.

Kwa kuzingatia katiba, kanuni na taratibu za CHADEMA, nilichokifanya mimi baada ya kubaini njama zao ni kukata rufaa kwa Baraza Kuu la Chama, kupinga upotoshaji unaofanywa chini ya uongozi wa Mhe. MBOWE anayeonekana kutaka kuendesha chama kinyume na matarajio ya wanachama walio wengi.

Hivyo basi zipo habari za uhakika kuwa kikao hicho cha Baraza Kuu hakitaitishwa ama kabisa, au kitacheleweshwa kwa makusudi, kwa visingizio mbalimbali ikiwemo kutokuwa na fedha za kukidhi gharama za kikao hicho.

Naomba nikiri kuwa ninakerwa sana na mtiririko mzima wa sakata hili linalozua mgogoro unaokiyumbisha chama. Ukweli ni kwamba mimi niligombea Umakamu Mwenyekiti nikiwa na agenda ya kufufua uhai wa chama kwa kukaripia vitendo visivyostahili katika kuendesha chama. Agenda yangu haijabadilika. Yote niliyoyasema wakati nagombea nafasi hii yanafahamika kwa wana CHADEMA wote. Walikuwepo walioyalalamikia na walikuwepo walioyapongeza matamshi yangu hayo.

Mwisho wa yote wana CHADEMA waliridhika kuwa ajenda yangu ilikuwa sahihi na hivyo wakanichagua kuwa Makamu Mwenyekiti. Hivyo basi hata kama ni kweli kuwa ulikuwepo mvutano wakati wa kampeni ile, lakini hilo ni jambo la kawaida katika uchaguzi. Nijuavyo mimi hayo yalitakiwa yawe si ndwele nasi tugange yajayo kwani wanachama walikwisha fanya uamuzi halali kupitia kura zao.

Baada ya kuingia kwenye wadhifa wa Makamu Mwenyekiti Taifa, nilifanikiwa kuzungumza na Mhe. MBOWE kuhusu mambo, hususan yale, niliyoyapigania wakati wa kinyang’anyiro kile na kumuomba tukae chini na kutafuta jinsi ya kufanikisha azma hiyo.

Ni imani yangu kuwa waraka huu utawasaidia wanaCHADEMA wenzangu na watanzania wote kwa ujumla, kuelewa vizuri ukweli wa mambo niliyoyapigania kabla ya kuwa Makamu Mwenyekiti, na ninayoendelea kuyasimamia hivi sasa nikiwa Makamu Mwenyekiti, na inshallah nitakayoyatekeleza baadae kama Taifa Mwenyekiti wa CHADEMA.

Kimsingi mambo tunayotofautiana na Mhe. MBOWE ni haya yafuatayo:-

MATUMIZI YA RUZUKU

CHADEMA hupata ruzuku ya Tshs. 66,000,000 kwa mwezi (Milioni sitini na sita). Mimi nasema si haba hasa tukizingatia chama kilikotoka. Naamini kuwa kiasi hiki cha fedha kikisimamiwa vizuri kinaweza kukirahisishia chama kujieneza katika ngazi zote toka Tawi, Wilaya, Mkoa na Taifa.

Si kweli kwamba matatizo yote yatamalizwa na fedha hizi lakini basi hata ofisi za chama zinaweza kuwa hai nchi nzima kitu ambacho kwa sasa hakipo. Mahesabu yanaonesha kuwa mtaji wa laki moja (Tshs.100,000/=) kwa wilaya moja nchini inatosha, hivyo kwa Wilaya 126 kwa mwezi jumla yake ni Tshs. milioni 12 (Tshs. 12,600,000/= ) zinahitajika ( Wilaya 126 x 100,000 kila wilaya = 12,000,000/=)

Hata tukisema tupeleke kiasi hicho kwa kila jimbo la uchaguzi jumla yake ni Tshs. Milioni 23 (Tshs. 23,000,000/=) kwa maana ya majimbo 213 x 100,000 = 23,000,000/=. Mhe. MBOWE anasema hizo ni pesa nyingi sana kwa uimarishaji wa chama. Mimi nasema hapana, kiwango hiki kwa kila Wilaya au Jimbo la uchaguzi ni muafaka kwani haba na haba hujaza kibaba.

Chini ya uongozi wa Mhe. MBOWE na wafuasi wake hawastaajabu kuwa kati ya Tshs. 374,144,000.40 zilizopatikana kama ruzuku katika ya Januari 1 na Juni, 30, 2008, Tshs. 350,000,000/= zilitumika Makao Makuu ya CHADEMA na Tshs. 25,000,000/= tu ndizo zilikwenda Wilayani kuimarisha chama.

Mimi naona mgao huu unayatukuza Makao Makuu ya CHADEMA isivyostahili wakati huo huo ukidhalilisha chama nchi nzima.

MADENI YA UCHAGUZI

Kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Mhe. MBOWE alitufahamisha wanachama kuwa alikuwa anakidai chama US $ 181,949.00 sawa na Tshs. 218,338,546. Mpaka sasa chama kimekwisha mlipa Tshs. 175,000,000/=

Baada ya kupata wadhifa wa Makamu Mwenyekiti, na kwa kuzingatia takwimu zionekanazo hapo juu katika kulinganisha matumizi ya fedha Wilayani na Makao Makuu niliamua kumshauri MBOWE asitishe kujilipa deni kutokana na fedha za ruzuku kwani siamini kuwa kulipa madeni yaliyopita kunaendana na utaratibu wa usimamizi wa fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa toka serikalini.

Mhe. MBOWE alichachamaa na ndipo nilipomshauri kuwa kama ni hivyo basi atuthibishie pesa hizo anazodai alikikopesha chama ziliingia kwenye akaunti gani ya CHADEMA, kupitia hundi ipi, na lini? Nilimuomba pia kutaja ni kikao gani cha chama kiliidhinisha matumizi ya fedha hizo kwani kama hakuna ushahidi wa maidhinisho, ni dhahiri kuwa matumizi hayo hayakudhibitiwa na chama na kwa mantiki hiyo kuyafanya kuwa matumizi binafsi ya Mhe. MBOWE.

Vilevile, nilimueleza kuwa matumizi ya fedha hizo alizodai alikikopesha chama yalikuwa yakinuka harufu ya UFISADI. Stakabadhi zote kuhusiana na matumizi hayo zilionesha kuwa gharama za aidha ununuzi na / au ukodishaji wa vifaa hivyo, hazikutofautiana na viwango wanavyolipishwa watalii kwa huduma kama hizo, kwa maana ya gharama ya juu sana.

Na kwa kuwa hata baada ya kuwa Mhe. MBOWE amekwisha lipwa zaidi ya nusu ya deni alilodai kuikopehsa CHADEMA, vifaa vyote yakiwemo magari, vipaza sauti na kadhalika vimebakia kuwa mali yake binafsi, basi bila kumficha nilimueleza kuwa huko ni kukinyonya chama kwa kukigeuza kitega uchumi cha watu binafsi.

Kuhusu suala la kulipa madeni kupitia ruzuku ya serikali, nilimuomba Mhe. MBOWE afuatilie kwa Msajili wa Vyama vya siasa ili tupate ufafanuzi kama kweli fedha za ruzuku ya serikali kwa vyama vya siasa, inaweza kutumika kulipia madeni ya viongozi wa vyama hivyo yatokanayo na uchaguzi ili CHADEMA isiathirike kisheria.

Niseme kweli hapa kwamba, kwa vile wanaCHADEMA wengi walinichagua kuwa Makamu Mwenyekiti, na hata mimi mwenyewe tulikuwa wagombea wa nafasi za ubunge, udiwani n.k katika uchaguzi wa mwaka 2005 ningefarijika sana iwapo na sisi tungerejeshewa angalau chochote cha kufidia gharama zetu, kwa maana kwamba kama chama kimeamua kurudisha gharama hizo kiwalipe wote badala ya kulipa madeni kwa wateule wachache.

UTEUZI WA WABUNGE WA VITI MAALUM

Naamini ukweli wa suala hili hauna mjadala. Kwamba Mhe. MBOWE na wafuasi wake walighushi orodha ya majina ya viti Maalum badala ya kupeleka yaliyopendekezwa na Kamati Kuu sio siri. Naamini hata Mhe. MBOWE anakubaliana nami kuwa suala hili si moja ya siri anazodai nimevujisha!

Yamesemwa mengi juu ya mtafaruku uliojitokeza kuhusu viti maalum hadi baadhi ya waasisi wa chama wakataka kujitoa na hivyo kumlazimisha Mwenyekiti Taifa ( FREEMN MBOWE) na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kukiomba radhi kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kwa kukiuka katiba, kanuni na maadili ya chama katika suala hili la kugushi viti maalum.

Ni ukweli ulio wazi kuwa kitendo hicho cha upendeleo bado kina iumiza taswira ya CHADEMA. Chama kinaonekana kuendekeza ujanja ujanja kiasi kwamba watu na binti zao, wakwe zao, shemeji zao, waume wenzao, wachumba wa shemeji zao, wake wenza na kwa kiwango kikubwa watu wa kabila moja ndiyo wamekuwa sura ya CHADEMA bungeni.

Katika hili nilichoweza kumueleza Mhe. MBOWE ni kuwa chaguzi mbalimbali tangu za Mitaa, Ubunge na Urais zinakaribia ni vizuri tufanye bidii kusambaza nguvu zetu nchi nzima tuwe na mtaji wa kura maeneo mengi ili kashfa kama hii isijirudie. Hii ni kwa msingi kuwa chama kikijitanua kutakuwa hakuna sababu ya kuwaona watu wa eneo fulani tu kuwa ndiyo mhimili wa CHADEMA na hivyo zikitokea fursa itakuwa rahisi chama kuwakilishwa na mtandao wake mpana badala ya koo au kabila fulani.

Sasa kwa kuwa kuimarisha chama kitaifa maana yake ni matumizi ya fedha, nalo hili likawa nongwa ingawa kwa mtazamo wa Makao Makuu kulipa madeni kwa wateule wachache si nongwa. Cha ajabu ni kwamba Mhe. MBOWE hakukana kuwa hili la viti maalum na hata upangaji wa ajira kwa ukabila una leta athari mbaya kwa mustakabali wa CHADEMA.

Katika maongezi yangu nae nilikuwa wazi nilipotahadharisha kuwa:

1. Watanzania wakiendelea kuona kwamba CHADEMA inaendeshwa kwa misingi ya kikabila hawatajiunga na chama chetu na tutakosa wafuasi.
2. Watanzania wakiona kuwa sisi tumeweka mbele ukabila kuliko utaifa hawatatupa madaraka na kutawala kwa kuhofia yale yanayotokea nchi jirani kama Rwanda, Burundi, Kenya na kadhalika ambako nafasi za raia wote zimehodhiwa na kabila moja na hatma yake watu wamechinjana kama kuku kwa kupinga hilo.

Pia nilimwambia kwamba, kwa jinsi sura ya uteuzi wa Wakurugenzi na watendaji wengine wa Makao Makuu inavyoonekana, sasa tayari chama chetu kimebatizwa jina la CHAMA CHA WACHAGA, na hii si kuwatendea haki raia wengine na makabila yao ambao wataonekana kama punguani kujihusisha na chama na ukabila.

Yote haya ninayosema kuhusu ukabila, upendeleo na kadhalika sio dhana tu. Kufuatia malalamiko mengi yaliyokuwa yakisikika nchi nzima kuhusu masuala haya, Kamati Kuu ya CHADEMA ilikwisha unda Tume kutafuta ukweli wa mambo hayo. Tume hiyo ya watu watano iliongozwa na Mhe. Merky Lugendo Mziray ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA nayo imekwisha toa taarifa yake kwamba Makao Makuu ya CHADEMA yanatawaliwa na ubaguzi wa kikabila, kidini na kielimu.

UTENDAJI WA KIBABE

CHADEMA ni chama kilicho njia panda kwa sasa kutokana na utendaji wa kibabe wa Mhe. MBOWE. Ninafahamu jinsi vyama vingine vya upinzani hapa nchini kama vile NCCR – Mageuzi vilivyoporomoka haraka haraka mithili ya nyumba ya mabua. Chama NCCR – Mageuzi kilifikia mahali pazuri tu hadi watu wakaanza kufikiria kuwa kingekuwa chama mbadala kwa CCM. kwa bahati mbaya uchu wa madaraka, ulafi wa ruzuku, na tabia za kimangimeza kwa pamoja vikakiathiri hadi kupoteza umaarufu wake.

Na hata vyama vingine vya upinzani vina dalili hizo hizo japo kwa viwango vinavyotofautiana. Ila badala ya kujichunguza na kujua kasoro zetu, kila siku vyama vyetu, vimekuwa vikidai kuwa ni chama tawala ndicho kinachoviroga, kama ambavyo Mhe. MBOWE ameanza kuweweseka kupitia vyombo vya habari.

Napenda kuthibitisha kuwa katika mgogoro unaopaliliwa sasa na Mhe. MBOWE ndani ya CHADEMA kutokana na ufisadi, ufuska, ulevi wa madaraka na umangimeza chanzo chake ni tabia yake ya kuendesha chama kibabe. Mathalan kumzuia Martin Mung’ong’o Mkurugenzi aliyechaguliwa kwa kura kutofanya kazi zake ndani ya chama, madai ya kupigana na watendaji wa chama ndani ya baa na vitendo vingine vya aina hiyo ni ushahidi tosha wa hulka hii. Hadi sasa Mhe. MBOWE amefanikiwa kukizuia chama hiki kisifanye kazi ya siasa mkoa wa Dar es salaam kwa miaka minne.

Ninavyoongea hivi sasa CHADEMA imekuwa ikikimbia vikao vya Democratic Union of Afrika (DUA), Muungano wa Vyama Vya Upinzani, uliofanikisha CHADEMA kujuana na Conservative Party ya Uingereza na Republican ya Marekani. Vyama dada hivi vyote vinaulalamikia uongozi wa CHADEMA kwa kufuja fedha ya misaada na kuwasilisha kwao risiti za kugushi, kama ilivyofanyiwa Conservative Party baada ya kutoa msaada wa Tshs. 78,000,000 kwa ajili ya ununuzi wa baiskeli na pikipiki ambazo hazikununuliwa.

Katika mkutano wa Kamati Kuu ya CHADEMA huko Dodoma hivi majuzi tu, Mhe. MBOWE kwa kauli yake aliwatisha wajumbe kuwa alikuwa amethibiti uwezekano wowote wa wajumbe kujisikia huru kwa kutoa mawazo ambayo yangepingana na ajenda yake aliyoitoa ghafla kikaoni kunisimamisha Umakamu Mwenyekiti.

Mhe. MBOWE Alikifahamisha kikao kuwa alitoa taarifa kwa IGP, SAID MWEMA kuwa kuna wahuni ambao walitaka kuuchafua mkutano wake, naye IGP akahakikisha kuwa mkutano ule unalindwa kwa kiwango cha kushtua kama ambavyo hata vyombo vya habari vimethibitisha.

Hayo ni baadhi tu ya mambo yanayobainisha Mhe. MBOWE ni kiongozi wa aina gani.

HITIMISHO

Kama nilivyokwisha sema hapo awali, sijaacha na sintoacha ajenda yangu ya kufufua uhai wa CHADEMA kwani ndiyo ahadi iliyofanikisha kuchaguliwa kwangu kuwa Makamu Mwenyekiti Taifa. Nilipopata wadhifa huo nilianza kuitekeleza ajenda hiyo kupitia mahojiano na Mwenyekiti MBOWE kuhusu matumizi ya ruzuku, madeni ya uchaguzi, uteuzi wa wabunge wa viti maalum, nafasi za ajira Makao Makuu, na kuhusu mwenendo wa chama Mkoa wa Dar es salaam.

Nilijikuta katika mvutano mkubwa kila nilipogusa eneo lolote katika haya. Nakiri kuwa kwa kiwango kikubwa sikuwa na uwezo wa kubadili mambo hayo yaliyokuwa yakiratibiwa kwa ukaribu na Mhe. MBOWE na wafuasi wake kwani sikupewa ushirikiano wa aina yoyote na chama pale Makao Makuu. Ni vigumu kuamini, lakini ni kweli kuwa sikuwa na ofisi Makao Makuu, sikupewa vitendea kazi kama magari, vipaza sauti na/au vyombo vya habari, na sikuwahi kupata taarifa yoyote ya kiutendaji toka Makao Makuu.

Kwa kuzingatia yote hayo, naomba nichukue fursa hii kuwashukuru kwa dhati wanachama wa CHADEMA mkoa wa Dar es salaam ambao kwa pamoja tulisimama kidete kufufua uhai wa chama hapa jijini. Niseme tu ushirikiano wao wa hali na mali uliniwezesha kushughulikia masuala muhimu ya kitaifa na kimataifa.

Rai yangu kwa wana CHADEMA na wale wote wanaokitakia mema chama chetu na nchi yetu kwa ujumla ni kwamba kazi ya kupigania demokrasia ya kweli ndani na nje ya chama, kukiepusha chama na vitendo vya ukabila, migogoro, ubadhirifu, umangimeza, ufisadi na ubaguzi wa aina yoyote bado inaendelea na nawaombeni mniunge mkono kwa hali na mali katika vita hii. Naamini tutashinda.

Mungu Ibariki CHADEMA
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika

====Chacha Wangwe amekufa lakini waraka wake huu utawasaidia WanaCHADEMA na watanzania kuelewa ukweli wa mambo aliyokusudia.

Kila kilichoandikwa humu kilishajibiwa humu tayari. Dr Slaa alishawahi kueleza kuhusu mkopo kwa CHADEMA toka kwa Mbowe na jinsi ulivyopitia vikao vyote, Zitto alishawahi kueleza humu kuhusu viti maalum na kuhusu fedha za conservative. Mnyika amewahi kueleza hapa kuhusu ruzuku na helikopta. Hebu tazameni tu post zao mchambue majibu yao ukilinganisha na hoja za kwenye huu waraka unaoitwa wa marehemu

...ndiyohiyo
 
kwanini maelezo ya wali ya serikali kuhusu EPA hatukuyakubali?? mpaka tukataka uchunguzi huru.

Kwani DR SLAA yeye ni nani maelezo yake lazima yawe ya kweli? kwani kuna docoment yoyote ilitolewa kuthibitisha maelezo ya SLAA??
 
JARIDA LA CHACHA ZAKAYO WANGWE MBUNGE WA TARIME CHADEMA

Utangulizi:

Jarida hili la Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe lina sehemu tatu. Sehemu ya kwanza litaweka bayana na kufafanua sababu za mimi kuchafuliwa kisiasa na baadhai ya viongozi wa ngazi za juu za Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, na sehemu ya pili itaonyesha baadhi ya maswali ya msingi niliyopata kuuliza Bungeni na majibu yake na sehemu ya tatu itakuwa na michango mbalimbali niliyopata kuchangia kwa muda wa miezi miaka miwili na nusu.

Lengo hasa la Jarida hili ni kumwelewesha Mtanzania na hususan MWANADEMOKRASIA juu ya tuhuma zilizoelekezwa kwangu kwa lengo la kunichafua kisiasa huku viongozi wa CHADEMA wakidai kukisafisha chama jambo ambalo si kweli na ni kampeni chafu zilizoandaliwa na baadhi ya viongozi wa Chama na kuwarubuni wajumbe 31 wasiokuwa wanademokrasia na kunipaka matope ya siasa zao zisizo na hata chembe ya Demokrasia.

Nasema hivi nikijua wazi kwamba, CHADEMA kama chama kinaendeshwa kwa katiba na kwa wakati huo huo kikiwa kinaendeshwa kidikteta na kauli za NDIYO MZEE. Ninajua wazi kwamba, viongozi wa sasa wa chama changu wanatofautiana sana na viongozi wa mwanzo wakati CHADEMA ikianzishwa kwani wanatofautiana kiitikadi, kisera na hata kimtazamo. Kwa mfano, mzee Mtei alikuwa akikieneza chama hasa vijijini miaka ya 95 kwa kutumia magari chakavu na alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwashawishi wananchi na wakijua kuwa CHADEMA si chama cha mjini, na hapa ndipo mwanzo wa CHADEMA kuwa Chama Tawala kule Tarime hadi sasa. Ila katika uongozi huu wa kizazi kipya basi kila kitu kinaenda kwa kauli za "Mheshimiwa Mwenyekiti kasema" na matumizi mabaya huku ufisadi ukikitafuna chama kwa matumizi hewa na kwa kigezo kuwa eti wanajilipa madeni ya Kampeni. Nililia sana juu ya matumizi ya helkopta katika kampeni lakini nikaanza kuonekana kuwa mini ni mbaya. Binafsi sikuona sababu za Chama kutumia helkopta ilhali bado wanachama wa vijijini hawakijui chama wala sera zake huku viongozi wa wilaya na mikoa wakishindwa hata kutoa durufu (photocopy) za viepeperushi vya chama kwa kukosa ruzuku. Hii si sawa.

SEHEMU YA KWANZA

Sababu za baadhi ya Viongozi wa CHADEMA kuamua kunichafua kisiasa.

Baadhi ya Kampeni za chini chini dhidi yangu, tarehe 28 na 29 Juni 2008 katika kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Dodoma ambacho kiluhudhuriwa na wajumbe 31 kiliridhia mimi kuondolewa kwenye wadhifa niliokuwa nao ndani ya chama kama Makamu Mwenyekiti kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutuhumiwa kuwa navujisha siri za chama kwa CCM. Binafsi kwangu kama mwanasiasa wa kiwango cha juu ni pigo kubwa sana kisiasa kuchafuliwa na watu 31 tu ndani ya chama. Ninachokiamini hapa ni kwamba, kutokana na msimamo wangu wa siku nyingi hata kabla sijawa makamu mwenyekiti CHADEMA, ndiyo sababu rasmi ya kupigiwa kampeni na baadaye kura za kutokuwa na imani na mimi kwa taarifa nilizo nazo ni kwamba anaandaliwa Dr. Slaa kushika nafasi hiyo. Hapa ikumbukwe kuwa Mke wa Dr. Slaa ni diwani kupitia CCM hivyo kuna uwezekano wa sera za chama zikavuja kupitia Mama huyu katika njia mbalimbali.

Ofisi ya Katibu Mkuu (Ofisi ya Slaa) ndiyo ya kwanza kunituhumu kuwa nawaingilia majukumu yao katika suala zima la matumizi mabovu ya fedha za ruzuku ya chama. Chama hupata zaidi ya milioni 60 kila mwezi. Ni fedha nyingi sana kukijenga chama kama zikipata mipango mizuri na kuachana na matumizi mabovu kama matumizi ya helkopta kwenye kampeni kama ilivyotokea kwenye chaguzi zetu pamoja na baadhiya viongozi kudai kuwa wanajilipa madeni waliokikopesha chama wakati wa kampeni za 2005.

Mhe. Philemon Ndesamburo Mbunge wa Moshi Mjini inadaiwa kuwa anakidai chama milioni 100 alizokopesha wakati wa kampeni za 2005.

Mhe. Philemon Ndesamburo Mbunge wa Moshi Mjini inadaiwa kuwa anakidai chama milioni 100 alizokopesha wakati wa kampeni za 2005, Freeman Mboe ambaye hadi sasa ni Mwenyekiti wa chama changu katika ngazi ya Taifa naye kwa taarifa nilizo nazo ni kwamba kila mwezi hulipwa shilingi milioni 10 ili kufidia fedha anazodai kukikopesha chama ambazo ni zaidi ya milioni 500 katika kampeni hizo hizo na hadi sasa anaendelea kukidai chama mamilioni ya shilingi.

Mimi nilipoonyesha wasiwasi juu ya madeni haya yasiyoisha, ikaundwa tume ya kampeni za kutokuwa na imani na mimi. Binafsi sijui kama viongozi wanaojiita makini kama kina Dr. Slaa na Kabwe Zitto wangeweza kuusimamia ufisadi mkubwa kama huu ndani ya chama huku wakiwa mstari wa mbele kuwafichua mafisadi Serikalini. Au ni kawaida kuwa Mganga hajigangi? CHADEMA kuna ufisadi wa aina nyingi sana kuanzia uchapaji bendera hadi manunuzi ya vifaa vya chama!

Katika ofisi ya Vijana nako kunanuka ufisadi kwani ni vijana wachache sana ambao hupata nafasi ya kwenda nje ilhali mikoani nako kuna vijana wanaohitaji kujifunza. Ofisi hii ina watu maalumu wa kwenda kwenye Semina na Matamasha mbalimbali. Na watu hao hupangwa na John Mnyika.

Pamoja na hayo, Kurugenzi hii inayoendeshwa na John Mnyika imekuwa ikifanya hesabu za "Mbili mara Mbili toa nne". Nakumbuka matamasha mbalimbali yaliyowahi kuratibiwa na Kurugenzi hii kwa kutumia fedha za chama yamekuwa hayana maslahi yoyote kwa chama ….labda kwake mwenyewe kwani itakumbukwa kwamba Kurugenzi ilizindua mfuko ulioitwa Tumaini jipya Septemba 16, 2007 katika hafla ya wafanyakazi vijana na akaunti ya Tumaini Jipya 01810301 NBC ilifunguliwa. Jumla ya shilingi milioni 6,176,500 zimekusanywa na shilingi milioni 6,064,300 zimetumika kwa shughuli mbalimbali za vijana ikiwemo gharama za hafla yenyewe. Hafla nyingine kama hiyo ilifanyika Arusha.

Hafla hii ilifanyika tarehe 29 Machi, 2008 The New Polygon Triangel Arusha na kuhudhuriwa na washiriki 67 mgeni rasmi akiwa Mhe. Mzee Edwin Mtei. Jumla ya shilingi milioni 2,300,700 zilikusanywa na shilingi milioni 1,885,000. Zimetumika kwa shughuli mbalimbali za vijana ikiwemo gharama za hafla yenyewe. Sasa najiuliza, kulikua na mantiki gani ya kutumia fedha za chama kiasi cha shilingi 6,064,300 na kukusanya shilingi 6,176,500/=? Ni faida ya shilingi ngapi ilipatikana kama ameamua kukiingiza chama katika kufanya biashara ya matamasha?

Jingine, tangu nimekuwa mbunge Chadema na Baadaye Makamu Mwenyekiti sijawahi kuandaliwa safari za kibunge ama za kukiwakilisha chama ilhali kuna watu wasio na uwezo kiakili, kifikra na hata nafasi za uongozi lakini waliandaliwa safari za nje. Chama kimefikia hatua ya kuwakilishwa kimataifa na watu wasio na vigezo kwa ajili ya utawala mbovu! Siandiki haya kwa kuwa nimeondolewa katika uongozi, hapana! Hizi ni harakati zangu za muda mrefu juu ya utawala bora. Tazama, wafuatao wamewahi kusafiri katika mataifa mbalimbali kwa shughuli mbalimbali kukiwakilisha chama. Mhe. Suzan Lymo (Mb. Viti maalumu) Cape Towan, Afrika Kusini kwa Mkutano wa Interparliamentary Union. Susan pia amesafiri kwenda USA kwa High Level meeting ya HIV/AIDs mwezi June, 2008. Mhe. Zitto Kabwe, (Mb) alisafiri kwenda Berlin mara mbili – Mhe. Zitto pia alisafiri kwenda Marekeani kwa wiki 3 kwa mwaliko wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani pamoja na Wabunge vijana toka dunia nzima ambako walipata nafasi ya kutembelea majimbo mbalimbali ya Marekani. Mhe. Mhonga Said (Mb – Viti maalum) alisafiri kwenda Burundi kwa Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu. Mhe. Dr. Slaa amesafiri kwenda Johannesburg, Windhoek na Manzini Swaziland kwa vikao vya Kamati na Bunge la SADC. Dr. Slaa ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya InterParliamentary Cooperation Committee ya Bunge la SADC. Mhe. Maulida Komu (Mb. Viti Maalumu) alisafiri kwenda Nairobi na pia Finland. Mhe. Ndesamburo (Mb) alisafiri kwenda Australia kama Commissioner wa Bunge.

Wafuatao walisafiri kichama; Mhe. Mhonga Said (Mb – Viti Maalum), Maulida Komu (Mb – Viti Maalum), Suzan Kiwanga (Afisa Msaifizi Idara ya Uchaguzi na Kampeni) na John Mnyika Mkurugenzi wa Idara ya Vijana) walisafiri kwenda Norway na Sweden. Anthony Komu (Mkurugenzi wa Fedha na Utawala) alisafiri kwenda Norway kwa mwaliko wa Centre Party, Mhe. Balozi Ngaiza (Mjumbe wa heshma wa kamati kuu wa kuteuliwa na Mwenyekiti), John Mnyika (Mkurugenzi katika Ofisi ya Vijana), John Mrema (Afisa katika Kurugenzi ya Halmashauri na Bunge), walisafiri kwenda Windhoek Namibia kwa Mkutano wa Dua, na Mhe. Kimesera (Katibu Mtendaji wa kuteuliwa na Mwenyekiti), Suzan Lymo (Mb) Viti maalum, na John Mrema walisafiri kwenda Kampala, Uganda kwa Mkutano wa Dua.

Ndugu Regia Mtema (Afisa katika Kurugenzi ya Vijana) alisafiri kwenda Malawi kwa Mkutano wa NIMD. Mama Naomi Kaihula (Mkurugenzi katika Idara ya Wanawake) na Regia Mtema walisafiri kwenda Finland kwa mwaliko wa Shirika la Demo Finland. Johna Mrema, Msafiri Mtemelwa na Happiness Mwaipopo (Sina hakika kama ni Mwanachama) walisafiri kwenda London/Uingereza kwa mwaliko wa Conservative Party/WFD wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Mhe. Benson Kigaila (Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo) alienda Zimbabwe katika uchaguzi uliofanyika 27 June, 2008 kupita Ofisi ya Msajili wa Vyama.

Suala la ukabila ni jambo ambalo halihitaji kupingwa kwani asilimia karibu 85 ya viongozi wa CHADEMA wametoka katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha pamoja na kwamba baada ya mimi kulishupalia jambo hili wameanza kubadilisha majina.

Wapo wanachama kama mimi ambao nao wakipewa nafasi za uongozi ndani ya chama hiki watafanya vizuri zaidi ya hawa na wengine ambao ni Jobless! Pengine niweke wazi hapa kuwa, mimi ni kiongozi shupavu nisiye kuwa na hata chembe ya woga katika kuteta na kusimamia haki za mwanachama wa CHADEMA tena nisiyependa siasa za kisanii. Ukweli huu ndio uliowafanya kina Mbowe, Slaa kuwa mstari wa mbele katika kupiga kampeni na baadaye kura ya kutokuwa na Imani na mimi. Binafsi naamini katika chama cha siasa mtu muhimu ni Mwanachama na si Mwenyekiti au Katibu. Hapa mimi siandiki maneneo haya kukufanya udhani kuwa nataka kuwa king'ang'anizi kwenye wadhifa niliovuliwa, la hasha bali napenda upate picha halilisi ya uendeshwaji wa Siasa ya CHADEMA na kisha uweze kugundua uhalisia wa mgogoro ulivyo. Viongozi wa CHADEMA Makao Makuu wamening'oa kutoka katika wadhifa niliokuwa nao kwa sababu zao binafsi na si sababu za chama kama chama, na wanajitahidi kuzunguka mikoani kwa siri kuendelea kunichafua kisiasa kuwa sifai. Kweli sifai kwa wafuja ruzuku ya chama, kweli sifai kwa mafisadi ndani ya chama ila nafaa kukiendesha chama katika ngazi ya taifa katika nafasi yoyote na siku zote. Nafaa kwa sababu nimefukuzwa kwa kusema ukweli hivyo nikageuka mwiba kati kati ya majipu, nikatolewa. Ndiyo, nafaa kwa sababu siko tayari kufanya kazi na watu waliozoea kukaa ofisini kama mafaili! Nafaa kwa sababu mimi ni mpambanaji, kamanda shujaa niliye tayari kuwajibishwa kwa ajili ya kuwatetea WANADEMOKRASIA hususan WANACHADEMA nchi nzima.

Kuliendesha Taifa kama Tanzania hakuhitaji siasa za kisanii, fitina, na chuki. Kinachotakiwa ni nani abadilike alete mabadiliko katika siasa ili aweze kukabidhiwa dola na alete mabadiliko. Wananchi wamechoshwa na siasa zetu ndio maana wanaziita siasa za kisanii. Wanahitaji mabadiliko. CHADEMA maana yake ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo, lakini huku wanakoelekea tayari uongozi wa Mbowe na Slaa wameiondosha Demokrasia kwa kunitoa katika wadhifa wa umakamu Mwenyekiti kwa kupiga kampeni ndogo ya wajumbe 31 tu! Tena huku wakinituhumu kuwa navujisha siri za chama!!. Dhahama kama hii siwezi kuivumilia hata kidogo na ni wazi kuwa hata wanachama wetu hawajafurahishwa na jambo hili. Mimi nilipokuwa kwenye ngazi hiyo ndipo fedha zilipoanza kupelekwa mikoani kwa viwango halali, ndipo ukarabati wa Makao Makuu ulifanyika. Niweke wazi hapa kuwa, jambo lililonifanya niandike jarida hili si kuwashawishi Freeman Mbowe na Slaa kunirudisha kwenye nafasi waliyonitoa kwa matusi, la hasha! Lengo ni kuweka wazi kwa wanachama wajue aina ya uongozi uliopo Makao Makuu ya Chama. Kama ni suala la mimi kurudi katika nafasi hiyo ni mimi mwenyewe nikiamua na kwa kutumia Demokrasia. Ikumbukwe kuwa, Freeman ndiye aliyesema kuwa hataki kufanya kazi na mimi na kutokana na UMANGIMEZA na Kauli za NDIYO MZEE akapata kuungwa mkono na wajumbe 31 tu! Baada tu ya mimi kutangazwa kuwa nimetolewa kwenye wadhifa niliokuwa nao nilipata simu nyingi sana za wanachama na hata baadhi ya watendaji Makao Makuu wakiniambia kuwa kama Mbowe hayuko tayari kufanya kazi na mimi, wao bado wananihitaji katika Uongozi Taifa. Kuna mila ya kichagga kuwa, katika eneo la kazi/biashara, ukimuona anayekusababisha ukose maslahi Fulani unatakiwa kumuondoa kwa gharama yoyote! Na hili ndilo lililojiri kwangu na mwenyekiti wangu.

Aluta Continue…………………..

Wangwe Chacha Zakayo,
Mbunge wa Tarime-CHADEMA

KAULI YANGU KWA MSOMAJI

Awali ya yote, nasikitika sana kwa maamuzi yaliyofikiwa na wajumbe 31 kule Dodoma aidha, kwa hasira, chuki au majungu na kuamua kuniondoa katika wadhifa niliokuwa nao wa Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara wakitumia kivuli cha Katiba ya Chama. Pili nimezidi kuumia zaidi pale nilipotuhumiwa kuwa eti navujisha siri za Chama kwa CCM! Niliwapa siku Arobaini (40) kuwaza kuthibitisha juu ya tuhuma hizo lakini wameshindwa hadi leo! Inamaanisha kuwa walitumia tuhuma hizo ili kunitoa kati yao ili nisiendelee kutetea ahadi za wanachama wa CHADEMA na nisiendelee kupinga ubadhirifu wa fedha za chama. Pengine kutokana na hasira, chuki na majungu hayo hayo wakaamua kuzidi kunichafualia jina katika mkutano uliofanyika Tanga kwa kunisema kuwa mimi ni mhuni. Hapa sintakuwa na huruma wala urafiki na yeyote aliye mstari wa mbele kunichafua kisiasa nitahakikisha nawafungulia mashtaka na waweze kuthibitisha tuhuma hizo. Mpendwa msomaji, pamoja na hayo ni vyema ukumbuke kuwa, uongozi wa CHADEMA Taifa umeshindwa kukieneza chama hadi vijijini. Ni kwa ajili ya majungu haya haya!.

Kimsingi, tusiposhikamana kwa sauti moja, lengo moja na kwa msimamo, ni dhahiri kuwa chama cha mapinduzi kitaendelea kushika Dola hadi Ukamilifu wa Dahari! Chama kisipokuwa madhubuti hakitaweza kushika Dola hakiwezi kuaminika na Wananchi. CHADEMA tufike mahali tugeuke, tujue tuna lengo la kuiongoza Tanzania na si vinginevyo. Badala ya kulewa katika kuwafichua mafisadi. Tumejisahau!.

Naamini kuwa, nguvu za umma ndiyo nguvu inayoweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Naamini kuwa, katika chama chochote cha siasa, mwanachama ndiye bora kuliko Kiongozi.

Naamini kuwa msingi bora wa chama hujengwa na watu makini.

Naamini pia baada ya kusoma Jarida hili ukiwa kama mwanachama au Mwanademokrasia utaungana nami katika kupiga vita UFISADI ndani ya CHADEMA.

Imetoka Tarishi Hauwawi
 
Hizi ni tuhuma nzito, ni ushauri wa bure tu viongozi ndani ya Chadema.Kama kweli fedha zilitolewa na conservative kwa ajili ya pikipiki na baiskeri na kisha kutumika kusikojulikana na maajibu na aibu.Ni wazi kabisa CHADEMA inapata umaarufu na tuna kila sababu ya kupinga kashfa hizi kwa kuwa waadalifu.Tunahitaji kuimarisha misingi ya chama tangu shina.Mambo yaliyomo kwenye walaka wa marehemu ni mazito na ya kusisimua.Kwani ofisi za chadema wilayani zintisha.Hazina hadhi kama ofisi.Ni aibu tupu.Mimi naipenda chadema na nimwanachama wa muda mrefu ila kama tutakuwa mafisadi kama wenzetu wa CCM tutakuwa hatuwatendei haki wananchi wanyonge wa Tanzania.
Ushauri wa bure kwa Mh. MBOWE na watendaji wote wa chama.Hakikisha wanatoa tsh 300,000 kila mwezi kwenye wilaya na wahakikishe wanaofisi za kudumu na imara kila kata nchini amabapo kila wenyeviti wa kata wawe na pikipiki na wenyeviti wa vitongoji baiskeli, hapo tutakuwa na ndoto ya kufika ikulu.Tuache umabavu.
Mh. Slaa, Mh. Zitto tunaimani nyie ni nuru yetu sasa mkiunga ufisadi ndani ya chama tutafika kweli?Tuwekeni wazi kwa hili.
 
Ninapomaliza kuisoma thread hii nashindwa kabisa kujizuia kuamini kwamba haya si maneno ya marehemu, sioni kwanini mtu mwingine ambaye si marehemu apoteze muda wake kuandika yote haya huku akijidai yeye ndiye Wangwe? Motive behind? Hata hivyo sidhani kama chama chochote kilicho serious na mambo yake kingekimbilia kutaka kujua aliyeyaandika haya badala ya kujibu hoja zilizotolewa, hata kama hoja hizi zingekuwa zimetolewa anonymously bado ingekuwa ni muhimu kwa chama kurespond. Shame Chacha died before all these became public........na hapa ndio utaamini kuwa marehemu hana haki, I can bet everything here will be vehemently denied bse there is no one to hit back, sioni hata mantiki ya huu mjadala kuendelea.
Kana-Ka-Nsungu,
2) Kama unavyofahamu Chadema huwa haina tabia ya kukurupuka. Tumekaa kimya muda wote, na hatukutaka kujibu chochote, kwa kuwa wakati waraka huu unatolewa tulikuwa bado kwenye maombolezo, na isingelikuwa vema kabla hata ya arobaini kuanza kulumbana wakati mhusika hayupo. Ambaye angelifanya hivyo ni mtu asiye sensitive kwa utamaduni wa Mtanzania. Chadema hatuko tayari na tusingeliweza kufanya wala hatutafanya hivyo hata siku moja kwa pressure tu kuwa tunatakiwa kujibu tuhuma.
ii) Kwa kawaida unahangaika kama kuna chembe cha ukweli katika tuhuma. Kama huna mashaka na tuhuma, na tuhuma unajua kwa uhakika hazina msingi, basi huna sababu hata tone kukurupuka kujua. Cha kwanza, na hasa pale ambapo hakuna ushahidi unaotolewa na watu wanaendelea "kukandamiza" lazima kujiuliza kuna nini, lazima kufanya utafiti na kuchunguza chanzo cha Tuhuma hizo. Ukitoka hadharani una msingi wa tuhuma na watu wote wataheshimu kwa vile umetoka na uchunguzi uliokamilika.
iii) Napenda kutoa taarifa ya awali kuwa sasa Chadema tuko in possition with evidence in hand, kwanini tumetuhumiwa hayo yote.Kwanini tumehusishwa na kifo na kwanini Mheshimiwa Mbowe ametuhumiwa na kuhusishwa na kifo. Indicator tumekwisha kutoa kwenye magazeti, kuwa tunayo sasa recorded evidence ya njama zinazofanywa na baadhi ya viongozi wazito wa vyama wakiwemo wa upinzani. Namba ya Fax ya Katibu Mkuu wa Chama Tawala imetajwa kuwa ndiyo iliyotuma ujumbe huo kwa fax kutoka Dodoma, kwa wale ambao hawakufuatilia ni fax no (026)2322965 ya Katibu Mkuu CCM Dodoma, tarehe 27 July, saa 9.42 alasiri yaani siku moja tu kabla ya kifo, na kutawanywa kwa Makatibu wa Mikoa wa CCM kutoka Fax no (022) 2667457 ya Stationary tarehe 31 July wakati wote wenye mapenzi mema tuko Kwenye Msiba Tarime. Mwenye akili ya kuchambua hahitaji kuambiwa hapa kuna nini. Taarifa ya Sherehe Afrika Kusini anayosemekana "kuiangusha Mbowe" baada ya kupata Taarifa ya Msiba nayo tumepata ushahidi documentary (Video na Audio) ambapo mwenyekiti wa Chama cha Upinzani alimwita kwake Mhariri wa Gazeti, tena linalomilikiwa na walioko kwenye listi ya Mafisadi tuliyoitaja 15 September, 2007. Hapa mwenye akili ya uchambuzi naye hahitaji kuambiwa kuna nini nyuma ya pazia. Tunazo nyaraka mbalimbali, ambazo ninaomba msubiri Tamko rasmi tutakolotoa. Wenye masikio wategee wakati huo.
 
Kwa sababu ya sensitivity ya mamabo ya CHADEMA humu JF i can bet my life hii thread itahamishwa by Saturday

Hongera sana Bubu kwa kuwa na guts
 
Mh Dr Slaa kama haya unayosema ni sahihi kwanini huo "ushahidi" msiupeleka kwenye vyombo vya usalama na sheria ili haki na sheria vichukue mkondo wake? Haya mambo ya kutoa statement hayasaidii sana ni sawa na msema pweke siku zote yupo right.
 
Vyombo vya usalama Tanzania vinamilikiwa na nani? Wameshindwa kuwachukulia hatua wahalifu wakubwa wa EPA itakuwa ushahidi wa CHADEMA? Are you dreaming?
 
6jey1yw.gif
 
Kwanza niwahakikishie akina nyiye mlioandaa vizuri hii deal ya kutujadilisha hoja ya CHACHA WANGWE kuwa mmefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuitingisha CHADEMA na kutusahaulisha japo kwa muda mfupi mjadala wetu kuhusu mafisadi.

Kwa kweli kwa hili nakiri mafisadi wapiga bao. Labda niwahakikishie kuwa wapo wakubwa humu JF ambao kila hoja ya ufisadi zinaposhika kasi wao wanabuni hoja mbadala ya kupoza au kuzima hoja hiyo. Kwa leo nawapongeza sana kwani mmeonyesha umahiri mkubwa.

Kama yamkini mafisadi wameajiri watu wa kufanya kazi kama iliyofanyika katika hoja hii ya leo, basi nina uhakika leo malipo yatakuwa makubwa zaidi.

Well Well Well!!! Niwahakikishie akina Mkamap, Kasheshe, Gembe, Pundamilia na wenzao wote ambao mna usongo na hii hoja kuwa na tahadhari ya mambo yafuatayo.
1. Kila dakika moja tunayopoteza bila kuwabana mafisadi nchi yetu inaibiwa mabilioni kutoka kwenye madini, kukwepa kodi, kuingiza bidhaa feki, mikataba ya hovyo, matumizi mabaya ya fedha za serikali, nk. Mpenda nchi hatathubutu kutumia muda wake kujadili noon issues akauacha ufisadi kustawi.

2. Watanzania wanajua kwa uhakika kuwa mafisadi wanatumia media kila mahali kwa lengo la kujisafisha na kuhujumu vita dhidi ya ufisadi. Hata humu JF wapo makuwadi wa kuwasafisha mafisadi pia.

3. Kila mlio wa ngoma huelezea ngozi iliyoiwamba. Yeyote aliye wa kulia kwa ajili ya uchungu wake kwa ajili ya wizi wa rasilimali za nchi tutamwona hapa. Na yule wa kulia kwa kuwa mabwana zake wameguswa tutamwona hapa pia.

Ninawahakikishia makuwadi wa mafisadi kuwa haijalishi mnatekeleza wajibu wenu kwa uhakika, uangalifu na ustadi kiasi gani, lakini bado wapiganaji dhidi ya mafisadi hawataisha wala kupungua.
 
Kauli Ya Mwisho Ya Marehemu Chacha Wangwe Kwa Mwenyekiti Wa Chadema Freeman Mbowe

Monday, 13 July 2009 04:21

KAULI YA MWISHO YA MAREHEMU CHACHA WANGWE KWA MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE

HII NI TAARIFA YA MHESHIMIWA WANGWE KUHUSU JARIBIO LA MWENYEKITI WA CHADEMA, FREEMAN MBOWE KUMVUA WADHIFA WAKE NA UANACHAMA WA CHADEMA ALIYOTARAJIA KUISOMA KWA WATANZANIA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA KUFIKA DAR ES SALAAM, DHAMIRA AMBAYO ILIKATISHWA NA MAUTI YALIYOTOKANA NA INAYOSEMEKANA KUWA NI AJALI YA KUPANGWA, ENEO LA PANDAMBILI, WILAYA YA KONGWA DODOMA TAREHE 28 JULAI, 2008.

Taarifa hii ilikuwa isomwe Dar es salaam, tarehe 29 Julai, 2008 siku moja kabla ya ajali iliyomuua CHACHA WANGWE

UTANGULIZI
Jumamosi, June 28 mwaka huu wajumbe kadhaa wa Kamati Kuu ya CHADEMA walidai kuwa wamesitisha Umakau Mwenyekiti wangu katika kikao kilichofanyika mjini Dodoma siku hiyo. Kesho yake Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. FREEMAN MBOWE akaitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutaja sababu za kunisimamisha uongozi.

Inatosha tu kusema kuwa sababu zote alizotoa ni za uzushi kama ile inayodai kuwa mimi navujisha siri za chama kwa viongozi wa CCM bila hata kutaja siri hizo, au kusema nimezitoa lini, wapi, na kwa kiongozi yupi?

Kikao hicho kinachosemekana kunisimamisha uongozi, kilikuwa na wajumbe 31 ambao takribani nusu hawakuwa na uhalali wa kupiga kura kinyume cha katiba na kanuni za CHADEMA kwa vile walikuwa wameandaliwa kwa kazi hiyo. Wajumbe 7 walikataa kushiriki njama hizo.

Kufuatia jaribio hilo la kunivua uongozi kutokubalika kwa wanachama walio wengi wa CHADEMA , Mwenyekiti MBOWE na wafuasi wake wameendelea kuhaha kwa kuongeza sababu nyingine mbalimbali ili kuhalalisha njama zao. Sasa hivi wameingia hatua ya kuwashawishi wanachama wa Tarime eti wanifukuze uanachama.

Kwa kuzingatia katiba, kanuni na taratibu za CHADEMA, nilichokifanya mimi baada ya kubaini njama zao ni kukata rufaa kwa Baraza Kuu la Chama, kupinga upotoshaji unaofanywa chini ya uongozi wa Mhe. MBOWE anayeonekana kutaka kuendesha chama kinyume na matarajio ya wanachama walio wengi.

Hivyo basi zipo habari za uhakika kuwa kikao hicho cha Baraza Kuu hakitaitishwa ama kabisa, au kitacheleweshwa kwa makusudi, kwa visingizio mbalimbali ikiwemo kutokuwa na fedha za kukidhi gharama za kikao hicho.

Naomba nikiri kuwa ninakerwa sana na mtiririko mzima wa sakata hili linalozua mgogoro unaokiyumbisha chama. Ukweli ni kwamba mimi niligombea Umakamu Mwenyekiti nikiwa na agenda ya kufufua uhai wa chama kwa kukaripia vitendo visivyostahili katika kuendesha chama. Agenda yangu haijabadilika. Yote niliyoyasema wakati nagombea nafasi hii yanafahamika kwa wana CHADEMA wote. Walikuwepo walioyalalamikia na walikuwepo walioyapongeza matamshi yangu hayo.

Mwisho wa yote wana CHADEMA waliridhika kuwa ajenda yangu ilikuwa sahihi na hivyo wakanichagua kuwa Makamu Mwenyekiti. Hivyo basi hata kama ni kweli kuwa ulikuwepo mvutano wakati wa kampeni ile, lakini hilo ni jambo la kawaida katika uchaguzi. Nijuavyo mimi hayo yalitakiwa yawe si ndwele nasi tugange yajayo kwani wanachama walikwisha fanya uamuzi halali kupitia kura zao.

Baada ya kuingia kwenye wadhifa wa Makamu Mwenyekiti Taifa, nilifanikiwa kuzungumza na Mhe. MBOWE kuhusu mambo, hususan yale, niliyoyapigania wakati wa kinyang'anyiro kile na kumuomba tukae chini na kutafuta jinsi ya kufanikisha azma hiyo.

Ni imani yangu kuwa waraka huu utawasaidia wanaCHADEMA wenzangu na watanzania wote kwa ujumla, kuelewa vizuri ukweli wa mambo niliyoyapigania kabla ya kuwa Makamu Mwenyekiti, na ninayoendelea kuyasimamia hivi sasa nikiwa Makamu Mwenyekiti, na inshallah nitakayoyatekeleza baadae kama Taifa Mwenyekiti wa CHADEMA.

Kimsingi mambo tunayotofautiana na Mhe. MBOWE ni haya yafuatayo:-

MATUMIZI YA RUZUKU
CHADEMA hupata ruzuku ya Tshs. 66,000,000 kwa mwezi (Milioni sitini na sita). Mimi nasema si haba hasa tukizingatia chama kilikotoka.

Naamini kuwa kiasi hiki cha fedha kikisimamiwa vizuri kinaweza kukirahisishia chama kujieneza katika ngazi zote toka Tawi, Wilaya, Mkoa na Taifa.

Si kweli kwamba matatizo yote yatamalizwa na fedha hizi lakini basi hata ofisi za chama zinaweza kuwa hai nchi nzima kitu ambacho kwa sasa hakipo. Mahesabu yanaonesha kuwa mtaji wa laki moja (Tshs.100,000/=) kwa wilaya moja nchini inatosha, hivyo kwa Wilaya 126 kwa mwezi jumla yake ni Tshs. milioni 12 (Tshs. 12,600,000/= ) zinahitajika ( Wilaya 126 x 100,000 kila wilaya = 12,000,000/=)

Hata tukisema tupeleke kiasi hicho kwa kila jimbo la uchaguzi jumla yake ni Tshs. Milioni 23 (Tshs. 23,000,000/=) kwa maana ya majimbo 213 x 100,000 = 23,000,000/=. Mhe. MBOWE anasema hizo ni pesa nyingi sana kwa uimarishaji wa chama. Mimi nasema hapana, kiwango hiki kwa kila Wilaya au Jimbo la uchaguzi ni muafaka kwani haba na haba hujaza kibaba.

Chini ya uongozi wa Mhe. MBOWE na wafuasi wake hawastaajabu kuwa kati ya Tshs. 374,144,000.40 zilizopatikana kama ruzuku katika ya Januari 1 na Juni, 30, 2008, Tshs. 350,000,000/= zilitumika Makao Makuu ya CHADEMA na Tshs. 25,000,000/= tu ndizo zilikwenda Wilayani kuimarisha chama.

Mimi naona mgao huu unayatukuza Makao Makuu ya CHADEMA isivyostahili wakati huo huo ukidhalilisha chama nchi nzima.

MADENI YA UCHAGUZI
Kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Mhe. MBOWE alitufahamisha wanachama kuwa alikuwa anakidai chama US $ 181,949.00 sawa na Tshs. 218,338,546. Mpaka sasa chama kimekwisha mlipa Tshs. 175,000,000/=

Baada ya kupata wadhifa wa Makamu Mwenyekiti, na kwa kuzingatia takwimu zionekanazo hapo juu katika kulinganisha matumizi ya fedha Wilayani na Makao Makuu niliamua kumshauri MBOWE asitishe kujilipa deni kutokana na fedha za ruzuku kwani siamini kuwa kulipa madeni yaliyopita kunaendana na utaratibu wa usimamizi wa fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa toka serikalini.

Mhe. MBOWE alichachamaa na ndipo nilipomshauri kuwa kama ni hivyo basi atuthibishie pesa hizo anazodai alikikopesha chama ziliingia kwenye akaunti gani ya CHADEMA, kupitia hundi ipi, na lini? Nilimuomba pia kutaja ni kikao gani cha chama kiliidhinisha matumizi ya fedha hizo kwani kama hakuna ushahidi wa maidhinisho, ni dhahiri kuwa matumizi hayo hayakudhibitiwa na chama na kwa mantiki hiyo kuyafanya kuwa matumizi binafsi ya Mhe. MBOWE.

Vilevile, nilimueleza kuwa matumizi ya fedha hizo alizodai alikikopesha chama yalikuwa yakinuka harufu ya UFISADI. Stakabadhi zote kuhusiana na matumizi hayo zilionesha kuwa gharama za aidha ununuzi na / au ukodishaji wa vifaa hivyo, hazikutofautiana na viwango wanavyolipishwa watalii kwa huduma kama hizo, kwa maana ya gharama ya juu sana.

Na kwa kuwa hata baada ya kuwa Mhe. MBOWE amekwisha lipwa zaidi ya nusu ya deni alilodai kuikopehsa CHADEMA, vifaa vyote yakiwemo magari, vipaza sauti na kadhalika vimebakia kuwa mali yake binafsi, basi bila kumficha nilimueleza kuwa huko ni kukinyonya chama kwa kukigeuza kitega uchumi cha watu binafsi.

Kuhusu suala la kulipa madeni kupitia ruzuku ya serikali, nilimuomba Mhe. MBOWE afuatilie kwa Msajili wa Vyama vya siasa ili tupate ufafanuzi kama kweli fedha za ruzuku ya serikali kwa vyama vya siasa, inaweza kutumika kulipia madeni ya viongozi wa vyama hivyo yatokanayo na uchaguzi ili CHADEMA isiathirike kisheria.

Niseme kweli hapa kwamba, kwa vile wanaCHADEMA wengi walinichagua kuwa Makamu Mwenyekiti, na hata mimi mwenyewe tulikuwa wagombea wa nafasi za ubunge, udiwani n.k katika uchaguzi wa mwaka 2005 ningefarijika sana iwapo na sisi tungerejeshewa angalau chochote cha kufidia gharama zetu, kwa maana kwamba kama chama kimeamua kurudisha gharama hizo kiwalipe wote badala ya kulipa madeni kwa wateule wachache.

UTEUZI WA WABUNGE WA VITI MAALUM
Naamini ukweli wa suala hili hauna mjadala. Kwamba Mhe. MBOWE na wafuasi wake walighushi orodha ya majina ya viti Maalum badala ya kupeleka yaliyopendekezwa na Kamati Kuu sio siri. Naamini hata Mhe. MBOWE anakubaliana nami kuwa suala hili si moja ya siri anazodai nimevujisha!

Yamesemwa mengi juu ya mtafaruku uliojitokeza kuhusu viti maalum hadi baadhi ya waasisi wa chama wakataka kujitoa na hivyo kumlazimisha Mwenyekiti Taifa ( FREEMN MBOWE) na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kukiomba radhi kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kwa kukiuka katiba, kanuni na maadili ya chama katika suala hili la kugushi viti maalum.

Ni ukweli ulio wazi kuwa kitendo hicho cha upendeleo bado kina iumiza taswira ya CHADEMA. Chama kinaonekana kuendekeza ujanja ujanja kiasi kwamba watu na binti zao, wakwe zao, shemeji zao, waume wenzao, wachumba wa shemeji zao, wake wenza na kwa kiwango kikubwa watu wa kabila moja ndiyo wamekuwa sura ya CHADEMA bungeni.

Katika hili nilichoweza kumueleza Mhe. MBOWE ni kuwa chaguzi mbalimbali tangu za Mitaa, Ubunge na Urais zinakaribia ni vizuri tufanye bidii kusambaza nguvu zetu nchi nzima tuwe na mtaji wa kura maeneo mengi ili kashfa kama hii isijirudie. Hii ni kwa msingi kuwa chama kikijitanua kutakuwa hakuna sababu ya kuwaona watu wa eneo fulani tu kuwa ndiyo mhimili wa CHADEMA na hivyo zikitokea fursa itakuwa rahisi chama kuwakilishwa na mtandao wake mpana badala ya koo au kabila fulani.

Sasa kwa kuwa kuimarisha chama kitaifa maana yake ni matumizi ya fedha, nalo hili likawa nongwa ingawa kwa mtazamo wa Makao Makuu kulipa madeni kwa wateule wachache si nongwa. Cha ajabu ni kwamba Mhe. MBOWE hakukana kuwa hili la viti maalum na hata upangaji wa ajira kwa ukabila una leta athari mbaya kwa mustakabali wa CHADEMA.

Katika maongezi yangu nae nilikuwa wazi nilipotahadharisha kuwa:

1. Watanzania wakiendelea kuona kwamba CHADEMA inaendeshwa kwa misingi ya kikabila hawatajiunga na chama chetu na tutakosa wafuasi.
2. Watanzania wakiona kuwa sisi tumeweka mbele ukabila kuliko utaifa hawatatupa madaraka na kutawala kwa kuhofia yale yanayotokea nchi jirani kama Rwanda, Burundi, Kenya na kadhalika ambako nafasi za raia wote zimehodhiwa na kabila moja na hatma yake watu wamechinjana kama kuku kwa kupinga hilo.

Pia nilimwambia kwamba, kwa jinsi sura ya uteuzi wa Wakurugenzi na watendaji wengine wa Makao Makuu inavyoonekana, sasa tayari chama chetu kimebatizwa jina la CHAMA CHA WACHAGA, na hii si kuwatendea haki raia wengine na makabila yao ambao wataonekana kama punguani kujihusisha na chama na ukabila.

Yote haya ninayosema kuhusu ukabila, upendeleo na kadhalika sio dhana tu. Kufuatia malalamiko mengi yaliyokuwa yakisikika nchi nzima kuhusu masuala haya, Kamati Kuu ya CHADEMA ilikwisha unda Tume kutafuta ukweli wa mambo hayo. Tume hiyo ya watu watano iliongozwa na Mhe. Merky Lugendo Mziray ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA nayo imekwisha toa taarifa yake kwamba Makao Makuu ya CHADEMA yanatawaliwa na ubaguzi wa kikabila, kidini na kielimu.

UTENDAJI WA KIBABE
CHADEMA ni chama kilicho njia panda kwa sasa kutokana na utendaji wa kibabe wa Mhe. MBOWE. Ninafahamu jinsi vyama vingine vya upinzani hapa nchini kama vile NCCR - Mageuzi vilivyoporomoka haraka haraka mithili ya nyumba ya mabua. Chama NCCR - Mageuzi kilifikia mahali pazuri tu hadi watu wakaanza kufikiria kuwa kingekuwa chama mbadala kwa CCM. kwa bahati mbaya uchu wa madaraka, ulafi wa ruzuku, na tabia za kimangimeza kwa pamoja vikakiathiri hadi kupoteza umaarufu wake.

Na hata vyama vingine vya upinzani vina dalili hizo hizo japo kwa viwango vinavyotofautiana. Ila badala ya kujichunguza na kujua kasoro zetu, kila siku vyama vyetu, vimekuwa vikidai kuwa ni chama tawala ndicho kinachoviroga, kama ambavyo Mhe. MBOWE ameanza kuweweseka kupitia vyombo vya habari.

Napenda kuthibitisha kuwa katika mgogoro unaopaliliwa sasa na Mhe. MBOWE ndani ya CHADEMA kutokana na ufisadi, ufuska, ulevi wa madaraka na umangimeza chanzo chake ni tabia yake ya kuendesha chama kibabe. Mathalan kumzuia Martin Mung'ong'o Mkurugenzi aliyechaguliwa kwa kura kutofanya kazi zake ndani ya chama, madai ya kupigana na watendaji wa chama ndani ya baa na vitendo vingine vya aina hiyo ni ushahidi tosha wa hulka hii. Hadi sasa Mhe. MBOWE amefanikiwa kukizuia chama hiki kisifanye kazi ya siasa mkoa wa Dar es salaam kwa miaka minne.

Ninavyoongea hivi sasa CHADEMA imekuwa ikikimbia vikao vya Democratic Union of Afrika (DUA), Muungano wa Vyama Vya Upinzani, uliofanikisha CHADEMA kujuana na Conservative Party ya Uingereza na Republican ya Marekani. Vyama dada hivi vyote vinaulalamikia uongozi wa CHADEMA kwa kufuja fedha ya misaada na kuwasilisha kwao risiti za kugushi, kama ilivyofanyiwa Conservative Party baada ya kutoa msaada wa Tshs. 78,000,000 kwa ajili ya ununuzi wa baiskeli na pikipiki ambazo hazikununuliwa.

Katika mkutano wa Kamati Kuu ya CHADEMA huko Dodoma hivi majuzi tu, Mhe. MBOWE kwa kauli yake aliwatisha wajumbe kuwa alikuwa amethibiti uwezekano wowote wa wajumbe kujisikia huru kwa kutoa mawazo ambayo yangepingana na ajenda yake aliyoitoa ghafla kikaoni kunisimamisha Umakamu Mwenyekiti.

Mhe. MBOWE Alikifahamisha kikao kuwa alitoa taarifa kwa IGP, SAID MWEMA kuwa kuna wahuni ambao walitaka kuuchafua mkutano wake, naye IGP akahakikisha kuwa mkutano ule unalindwa kwa kiwango cha kushtua kama ambavyo hata vyombo vya habari vimethibitisha.

Hayo ni baadhi tu ya mambo yanayobainisha Mhe. MBOWE ni kiongozi wa aina gani.

HITIMISHO
Kama nilivyokwisha sema hapo awali, sijaacha na sintoacha ajenda yangu ya kufufua uhai wa CHADEMA kwani ndiyo ahadi iliyofanikisha kuchaguliwa kwangu kuwa Makamu Mwenyekiti Taifa. Nilipopata wadhifa huo nilianza kuitekeleza ajenda hiyo kupitia mahojiano na Mwenyekiti MBOWE kuhusu matumizi ya ruzuku, madeni ya uchaguzi, uteuzi wa wabunge wa viti maalum, nafasi za ajira Makao Makuu, na kuhusu mwenendo wa chama Mkoa wa Dar es salaam.

Nilijikuta katika mvutano mkubwa kila nilipogusa eneo lolote katika haya. Nakiri kuwa kwa kiwango kikubwa sikuwa na uwezo wa kubadili mambo hayo yaliyokuwa yakiratibiwa kwa ukaribu na Mhe. MBOWE na wafuasi wake kwani sikupewa ushirikiano wa aina yoyote na chama pale Makao Makuu. Ni vigumu kuamini, lakini ni kweli kuwa sikuwa na ofisi Makao Makuu, sikupewa vitendea kazi kama magari, vipaza sauti na/au vyombo vya habari, na sikuwahi kupata taarifa yoyote ya kiutendaji toka Makao Makuu.

Kwa kuzingatia yote hayo, naomba nichukue fursa hii kuwashukuru kwa dhati wanachama wa CHADEMA mkoa wa Dar es salaam ambao kwa pamoja tulisimama kidete kufufua uhai wa chama hapa jijini. Niseme tu ushirikiano wao wa hali na mali uliniwezesha kushughulikia masuala muhimu ya kitaifa na kimataifa.

Rai yangu kwa wana CHADEMA na wale wote wanaokitakia mema chama chetu na nchi yetu kwa ujumla ni kwamba kazi ya kupigania demokrasia ya kweli ndani na nje ya chama, kukiepusha chama na vitendo vya ukabila, migogoro, ubadhirifu, umangimeza, ufisadi na ubaguzi wa aina yoyote bado inaendelea na nawaombeni mniunge mkono kwa hali na mali katika vita hii. Naamini tutashinda.

Mungu Ibariki CHADEMA
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika

====Chacha Wangwe amekufa lakini waraka wake huu utawasaidia WanaCHADEMA na watanzania kuelewa ukweli wa mambo aliyokusudia.
 
Umekosa cha kuandika eti!!!, sasa hii ndo nini, na itatusaidia nini.
 
Kama nyarka za Marehemu JKNyerere hazijawasaidia sisi Maf.... sasa unategemea waraka wa Makamba utawasaidia sisi Maf...?
Umeshusha hadhi ya jamvi hili kwa PR za sisi Maf.....
 
Umekosa cha kuandika eti!!!, sasa hii ndo nini, na itatusaidia nini.
Usichukie,huo ndio waraka wa marehemu,sasa kama unaona unakugusa kwavile nawe upo karibu na makao makuu na inawezekana ndio wote mnaotafuna ruzuku na kuwatenga walio mikoani,mkemee mwenyekiti wako kwani ufisadi umemwelemea!
 
Kuna uhakikagani kwamba waraka huo ni wakwake, au umeandika mwenyewe.
 
huo waraka haujawahi kusomwa wakati mwenyewe yupo hai, sasa sisi tutathibitisha vipi kwamba ni kweli huo waraka ni wa Chacha Wangwe, hata kama kweli aliacha waraka tutawezaje kujua kwamba hakukuwa na uongezaji wa maneno?huo waraka hauna uzito mtu yoyote anaweza kuandika na kusema ni waraka wa Wangwe, hebu tueleze ukweli huo waraka ni Fisadi gani aliyekupa uje uuweke humu ili kupandikiza chuki chadema
 
Yasije kuwa ya NCCR-MAGEUZI..???? Yaani kama ni kweli basi ni aibu tupu kwa chama kama hichi cha chadema,tunaomba wahusika wa chadema waje watueleze kuhusu waraka huu.. la sivyo hatuwezi kuwaamini kuwapa madaraka ktk nchi yetu kwani itakuwa ni chama cha kifisadi kama ccm..
 
Si wanasema mjumbe hauwawi? muhimu ni kilichosemwa (content) na Wangwe (RIP) sio mletaji au muda wa uletaji.

By the way I find these to be more interesting...

Kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Mhe. MBOWE alitufahamisha wanachama kuwa alikuwa anakidai chama US $ 181,949.00 sawa na Tshs. 218,338,546. Mpaka sasa chama kimekwisha mlipa Tshs. 175,000,000/=
Baada ya kupata wadhifa wa Makamu Mwenyekiti, na kwa kuzingatia takwimu zionekanazo hapo juu katika kulinganisha matumizi ya fedha Wilayani na Makao Makuu niliamua kumshauri MBOWE asitishe kujilipa deni kutokana na fedha za ruzuku kwani siamini kuwa kulipa madeni yaliyopita kunaendana na utaratibu wa usimamizi wa fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa toka serikalini.
Mhe. MBOWE alichachamaa na ndipo nilipomshauri kuwa kama ni hivyo basi atuthibishie pesa hizo anazodai alikikopesha chama ziliingia kwenye akaunti gani ya CHADEMA, kupitia hundi ipi, na lini? Nilimuomba pia kutaja ni kikao gani cha chama kiliidhinisha matumizi ya fedha hizo kwani kama hakuna ushahidi wa maidhinisho, ni dhahiri kuwa matumizi hayo hayakudhibitiwa na chama na kwa mantiki hiyo kuyafanya kuwa matumizi binafsi ya Mhe. MBOWE.

UTEUZI WA WABUNGE WA VITI MAALUM
Naamini ukweli wa suala hili hauna mjadala. Kwamba Mhe. MBOWE na wafuasi wake walighushi orodha ya majina ya viti Maalum badala ya kupeleka yaliyopendekezwa na Kamati Kuu sio siri. Naamini hata Mhe. MBOWE anakubaliana nami kuwa suala hili si moja ya siri anazodai nimevujisha!
Yamesemwa mengi juu ya mtafaruku uliojitokeza kuhusu viti maalum hadi baadhi ya waasisi wa chama wakataka kujitoa na hivyo kumlazimisha Mwenyekiti Taifa ( FREEMN MBOWE) na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kukiomba radhi kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kwa kukiuka katiba, kanuni na maadili ya chama katika suala hili la kugushi viti maalum.
Ni ukweli ulio wazi kuwa kitendo hicho cha upendeleo bado kina iumiza taswira ya CHADEMA. Chama kinaonekana kuendekeza ujanja ujanja kiasi kwamba watu na binti zao, wakwe zao, shemeji zao, waume wenzao, wachumba wa shemeji zao, wake wenza na kwa kiwango kikubwa watu wa kabila moja ndiyo wamekuwa sura ya CHADEMA bungeni

Kamati Kuu ya CHADEMA ilikwisha unda Tume kutafuta ukweli wa mambo hayo. Tume hiyo ya watu watano iliongozwa na Mhe. Merky Lugendo Mziray ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA nayo imekwisha toa taarifa yake kwamba Makao Makuu ya CHADEMA yanatawaliwa na ubaguzi wa kikabila, kidini na kielimu.
 
Mbowe anajulikana kwa haya mambo, niliwahi kuona humu kwenye JF kuwa alikuwa akitumia gari la kifahari la wizi lililotoka huko UK, na jamaa alimwaga data za kutosha. Kwa hiyo hili wala halipingiki. Ikiwa utaratibu wa kweli utafatwa wa kuhakiki matumizi ya vyama na ruzuku na misaada wanayopewe utafanywa, itabidi vyama vyote vifungwe, including CCM.

Aaaah, sie tusie na vyama yetu macho, masikio na kuchokonowa.
 
Back
Top Bottom