CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Ila nimegunduwa kumbe Chadema inaitetemesha CCM kama mtu mgeni kwenye jamvi hili nimeona baada ya biharamulo kumekuwa na kufukua thread za miaka mitatu minne iliyopita kwa nini mumeona nguvu ya chadema,nadhani your too predictable some one to trust you guys mwisho wa siku sisi wanajamvi tunaona ni propaganda mulizozifanya kwa kuwachafua akina Sumaye kable ya uchaguzi wa 2005 mkidhani mumepata kumbe mumepatikana,Serikali ya CCM imepoteza hadhhi sana chama cha viongozi wa kiisala na jumuiya zake kama vijana,wanawake na wazazi klnatakiwa kijisafishe badala ya kutaka kuua demokrasia kwa kuwaandama wale wachache waliojitoa kuamsha washawasha ya vuguvugu la kisiasa.Nafurahi kwamba si mwananchama wa chama chochote ukiacha uanacha tuliolazimisha na CCM miaka hiyo tukiwa vyuoni
Nitasimamia haki siku zote
CCM kweli munawohofia chadema lakini mapinduzi ya kweli hayataletwa na chadema yataletwa na wanchi wenyewe ambao hawasikii na mwazini wala la nani wanjua kuzomea na kuuliza na kuwakaba viongozi na bado mwakani jasho litawatoka CCM wakati wa mabumbu umekwisha sikiliza kipindi cha TBC1 wanachi wakihojiwa utajua mabadiliko makubwa ya kifikra ya wanachi wa vijiji
kwa strategies za kuandika nyaraka wenyewe mukihusisha akina Wangwe wakati uhakika wa waraka wenyewe hauwezwi kuhakikiwa ni upuuzi mtupu peleka porojo kw a washamba wengine sio katika jambi hili
 
Mbowe anajulikana kwa haya mambo, niliwahi kuona humu kwenye JF kuwa alikuwa akitumia gari la kifahari la wizi lililotoka huko UK, na jamaa alimwaga data za kutosha. Kwa hiyo hili wala halipingiki. Ikiwa utaratibu wa kweli utafatwa wa kuhakiki matumizi ya vyama na ruzuku na misaada wanayopewe utafanywa, itabidi vyama vyote vifungwe, including CCM.

Aaaah, sie tusie na vyama yetu macho, masikio na kuchokonowa.

Eh na wewe umerudi? nadhani una mission maalum😀
 
Kauli Ya Mwisho Ya Marehemu Chacha Wangwe Kwa Mwenyekiti Wa Chadema Freeman Mbowe



Monday, 13 July 2009 04:21


KAULI YA MWISHO YA MAREHEMU CHACHA WANGWE KWA
MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE
HII NI TAARIFA YA MHESHIMIWA WANGWE KUHUSU JARIBIO LA MWENYEKITI WA CHADEMA, FREEMAN MBOWE KUMVUA WADHIFA WAKE NA UANACHAMA WA CHADEMA ALIYOTARAJIA KUISOMA KWA WATANZANIA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA KUFIKA DAR ES SALAAM, DHAMIRA AMBAYO ILIKATISHWA NA MAUTI YALIYOTOKANA NA INAYOSEMEKANA KUWA NI AJALI YA KUPANGWA, ENEO LA PANDAMBILI, WILAYA YA KONGWA DODOMA TAREHE 28 JULAI, 2008.
Taarifa hii ilikuwa isomwe Dar es salaam, tarehe 29 Julai, 2008 siku moja kabla ya ajali iliyomuua CHACHA WANGWE
UTANGULIZI
Jumamosi, June 28 mwaka huu wajumbe kadhaa wa Kamati Kuu ya CHADEMA walidai kuwa wamesitisha Umakau Mwenyekiti wangu katika kikao kilichofanyika mjini Dodoma siku hiyo. Kesho yake Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. FREEMAN MBOWE akaitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutaja sababu za kunisimamisha uongozi.
Inatosha tu kusema kuwa sababu zote alizotoa ni za uzushi kama ile inayodai kuwa mimi navujisha siri za chama kwa viongozi wa CCM bila hata kutaja siri hizo, au kusema nimezitoa lini, wapi, na kwa kiongozi yupi?
Kikao hicho kinachosemekana kunisimamisha uongozi, kilikuwa na wajumbe 31 ambao takribani nusu hawakuwa na uhalali wa kupiga kura kinyume cha katiba na kanuni za CHADEMA kwa vile walikuwa wameandaliwa kwa kazi hiyo. Wajumbe 7 walikataa kushiriki njama hizo.
Kufuatia jaribio hilo la kunivua uongozi kutokubalika kwa wanachama walio wengi wa CHADEMA , Mwenyekiti MBOWE na wafuasi wake wameendelea kuhaha kwa kuongeza sababu nyingine mbalimbali ili kuhalalisha njama zao. Sasa hivi wameingia hatua ya kuwashawishi wanachama wa Tarime eti wanifukuze uanachama.
Kwa kuzingatia katiba, kanuni na taratibu za CHADEMA, nilichokifanya mimi baada ya kubaini njama zao ni kukata rufaa kwa Baraza Kuu la Chama, kupinga upotoshaji unaofanywa chini ya uongozi wa Mhe. MBOWE anayeonekana kutaka kuendesha chama kinyume na matarajio ya wanachama walio wengi.
Hivyo basi zipo habari za uhakika kuwa kikao hicho cha Baraza Kuu hakitaitishwa ama kabisa, au kitacheleweshwa kwa makusudi, kwa visingizio mbalimbali ikiwemo kutokuwa na fedha za kukidhi gharama za kikao hicho.
Naomba nikiri kuwa ninakerwa sana na mtiririko mzima wa sakata hili linalozua mgogoro unaokiyumbisha chama. Ukweli ni kwamba mimi niligombea Umakamu Mwenyekiti nikiwa na agenda ya kufufua uhai wa chama kwa kukaripia vitendo visivyostahili katika kuendesha chama. Agenda yangu haijabadilika. Yote niliyoyasema wakati nagombea nafasi hii yanafahamika kwa wana CHADEMA wote. Walikuwepo walioyalalamikia na walikuwepo walioyapongeza matamshi yangu hayo.
Mwisho wa yote wana CHADEMA waliridhika kuwa ajenda yangu ilikuwa sahihi na hivyo wakanichagua kuwa Makamu Mwenyekiti. Hivyo basi hata kama ni kweli kuwa ulikuwepo mvutano wakati wa kampeni ile, lakini hilo ni jambo la kawaida katika uchaguzi. Nijuavyo mimi hayo yalitakiwa yawe si ndwele nasi tugange yajayo kwani wanachama walikwisha fanya uamuzi halali kupitia kura zao.
Baada ya kuingia kwenye wadhifa wa Makamu Mwenyekiti Taifa, nilifanikiwa kuzungumza na Mhe. MBOWE kuhusu mambo, hususan yale, niliyoyapigania wakati wa kinyang?anyiro kile na kumuomba tukae chini na kutafuta jinsi ya kufanikisha azma hiyo.
Ni imani yangu kuwa waraka huu utawasaidia wanaCHADEMA wenzangu na watanzania wote kwa ujumla, kuelewa vizuri ukweli wa mambo niliyoyapigania kabla ya kuwa Makamu Mwenyekiti, na ninayoendelea kuyasimamia hivi sasa nikiwa Makamu Mwenyekiti, na inshallah nitakayoyatekeleza baadae kama Taifa Mwenyekiti wa CHADEMA.
Kimsingi mambo tunayotofautiana na Mhe. MBOWE ni haya yafuatayo:-
MATUMIZI YA RUZUKU
CHADEMA hupata ruzuku ya Tshs. 66,000,000 kwa mwezi (Milioni sitini na sita). Mimi nasema si haba hasa tukizingatia chama kilikotoka. Naamini kuwa kiasi hiki cha fedha kikisimamiwa vizuri kinaweza kukirahisishia chama kujieneza katika ngazi zote toka Tawi, Wilaya, Mkoa na Taifa.
Si kweli kwamba matatizo yote yatamalizwa na fedha hizi lakini basi hata ofisi za chama zinaweza kuwa hai nchi nzima kitu ambacho kwa sasa hakipo. Mahesabu yanaonesha kuwa mtaji wa laki moja (Tshs.100,000/=) kwa wilaya moja nchini inatosha, hivyo kwa Wilaya 126 kwa mwezi jumla yake ni Tshs. milioni 12 (Tshs. 12,600,000/= ) zinahitajika ( Wilaya 126 x 100,000 kila wilaya = 12,000,000/=)
Hata tukisema tupeleke kiasi hicho kwa kila jimbo la uchaguzi jumla yake ni Tshs. Milioni 23 (Tshs. 23,000,000/=) kwa maana ya majimbo 213 x 100,000 = 23,000,000/=. Mhe. MBOWE anasema hizo ni pesa nyingi sana kwa uimarishaji wa chama. Mimi nasema hapana, kiwango hiki kwa kila Wilaya au Jimbo la uchaguzi ni muafaka kwani haba na haba hujaza kibaba.
Chini ya uongozi wa Mhe. MBOWE na wafuasi wake hawastaajabu kuwa kati ya Tshs. 374,144,000.40 zilizopatikana kama ruzuku katika ya Januari 1 na Juni, 30, 2008, Tshs. 350,000,000/= zilitumika Makao Makuu ya CHADEMA na Tshs. 25,000,000/= tu ndizo zilikwenda Wilayani kuimarisha chama.
Mimi naona mgao huu unayatukuza Makao Makuu ya CHADEMA isivyostahili wakati huo huo ukidhalilisha chama nchi nzima.
MADENI YA UCHAGUZI
Kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Mhe. MBOWE alitufahamisha wanachama kuwa alikuwa anakidai chama US $ 181,949.00 sawa na Tshs. 218,338,546. Mpaka sasa chama kimekwisha mlipa Tshs. 175,000,000/=
Baada ya kupata wadhifa wa Makamu Mwenyekiti, na kwa kuzingatia takwimu zionekanazo hapo juu katika kulinganisha matumizi ya fedha Wilayani na Makao Makuu niliamua kumshauri MBOWE asitishe kujilipa deni kutokana na fedha za ruzuku kwani siamini kuwa kulipa madeni yaliyopita kunaendana na utaratibu wa usimamizi wa fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa toka serikalini.
Mhe. MBOWE alichachamaa na ndipo nilipomshauri kuwa kama ni hivyo basi atuthibishie pesa hizo anazodai alikikopesha chama ziliingia kwenye akaunti gani ya CHADEMA, kupitia hundi ipi, na lini? Nilimuomba pia kutaja ni kikao gani cha chama kiliidhinisha matumizi ya fedha hizo kwani kama hakuna ushahidi wa maidhinisho, ni dhahiri kuwa matumizi hayo hayakudhibitiwa na chama na kwa mantiki hiyo kuyafanya kuwa matumizi binafsi ya Mhe. MBOWE.
Vilevile, nilimueleza kuwa matumizi ya fedha hizo alizodai alikikopesha chama yalikuwa yakinuka harufu ya UFISADI. Stakabadhi zote kuhusiana na matumizi hayo zilionesha kuwa gharama za aidha ununuzi na / au ukodishaji wa vifaa hivyo, hazikutofautiana na viwango wanavyolipishwa watalii kwa huduma kama hizo, kwa maana ya gharama ya juu sana.
Na kwa kuwa hata baada ya kuwa Mhe. MBOWE amekwisha lipwa zaidi ya nusu ya deni alilodai kuikopehsa CHADEMA, vifaa vyote yakiwemo magari, vipaza sauti na kadhalika vimebakia kuwa mali yake binafsi, basi bila kumficha nilimueleza kuwa huko ni kukinyonya chama kwa kukigeuza kitega uchumi cha watu binafsi.
Kuhusu suala la kulipa madeni kupitia ruzuku ya serikali, nilimuomba Mhe. MBOWE afuatilie kwa Msajili wa Vyama vya siasa ili tupate ufafanuzi kama kweli fedha za ruzuku ya serikali kwa vyama vya siasa, inaweza kutumika kulipia madeni ya viongozi wa vyama hivyo yatokanayo na uchaguzi ili CHADEMA isiathirike kisheria.
Niseme kweli hapa kwamba, kwa vile wanaCHADEMA wengi walinichagua kuwa Makamu Mwenyekiti, na hata mimi mwenyewe tulikuwa wagombea wa nafasi za ubunge, udiwani n.k katika uchaguzi wa mwaka 2005 ningefarijika sana iwapo na sisi tungerejeshewa angalau chochote cha kufidia gharama zetu, kwa maana kwamba kama chama kimeamua kurudisha gharama hizo kiwalipe wote badala ya kulipa madeni kwa wateule wachache.
UTEUZI WA WABUNGE WA VITI MAALUM
Naamini ukweli wa suala hili hauna mjadala. Kwamba Mhe. MBOWE na wafuasi wake walighushi orodha ya majina ya viti Maalum badala ya kupeleka yaliyopendekezwa na Kamati Kuu sio siri. Naamini hata Mhe. MBOWE anakubaliana nami kuwa suala hili si moja ya siri anazodai nimevujisha!
Yamesemwa mengi juu ya mtafaruku uliojitokeza kuhusu viti maalum hadi baadhi ya waasisi wa chama wakataka kujitoa na hivyo kumlazimisha Mwenyekiti Taifa ( FREEMN MBOWE) na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kukiomba radhi kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kwa kukiuka katiba, kanuni na maadili ya chama katika suala hili la kugushi viti maalum.
Ni ukweli ulio wazi kuwa kitendo hicho cha upendeleo bado kina iumiza taswira ya CHADEMA. Chama kinaonekana kuendekeza ujanja ujanja kiasi kwamba watu na binti zao, wakwe zao, shemeji zao, waume wenzao, wachumba wa shemeji zao, wake wenza na kwa kiwango kikubwa watu wa kabila moja ndiyo wamekuwa sura ya CHADEMA bungeni.
Katika hili nilichoweza kumueleza Mhe. MBOWE ni kuwa chaguzi mbalimbali tangu za Mitaa, Ubunge na Urais zinakaribia ni vizuri tufanye bidii kusambaza nguvu zetu nchi nzima tuwe na mtaji wa kura maeneo mengi ili kashfa kama hii isijirudie. Hii ni kwa msingi kuwa chama kikijitanua kutakuwa hakuna sababu ya kuwaona watu wa eneo fulani tu kuwa ndiyo mhimili wa CHADEMA na hivyo zikitokea fursa itakuwa rahisi chama kuwakilishwa na mtandao wake mpana badala ya koo au kabila fulani.
Sasa kwa kuwa kuimarisha chama kitaifa maana yake ni matumizi ya fedha, nalo hili likawa nongwa ingawa kwa mtazamo wa Makao Makuu kulipa madeni kwa wateule wachache si nongwa. Cha ajabu ni kwamba Mhe. MBOWE hakukana kuwa hili la viti maalum na hata upangaji wa ajira kwa ukabila una leta athari mbaya kwa mustakabali wa CHADEMA.
Katika maongezi yangu nae nilikuwa wazi nilipotahadharisha kuwa:
1. Watanzania wakiendelea kuona kwamba CHADEMA inaendeshwa kwa misingi ya kikabila hawatajiunga na chama chetu na tutakosa wafuasi.
2. Watanzania wakiona kuwa sisi tumeweka mbele ukabila kuliko utaifa hawatatupa madaraka na kutawala kwa kuhofia yale yanayotokea nchi jirani kama Rwanda, Burundi, Kenya na kadhalika ambako nafasi za raia wote zimehodhiwa na kabila moja na hatma yake watu wamechinjana kama kuku kwa kupinga hilo.
Pia nilimwambia kwamba, kwa jinsi sura ya uteuzi wa Wakurugenzi na watendaji wengine wa Makao Makuu inavyoonekana, sasa tayari chama chetu kimebatizwa jina la CHAMA CHA WACHAGA, na hii si kuwatendea haki raia wengine na makabila yao ambao wataonekana kama punguani kujihusisha na chama na ukabila.
Yote haya ninayosema kuhusu ukabila, upendeleo na kadhalika sio dhana tu. Kufuatia malalamiko mengi yaliyokuwa yakisikika nchi nzima kuhusu masuala haya, Kamati Kuu ya CHADEMA ilikwisha unda Tume kutafuta ukweli wa mambo hayo. Tume hiyo ya watu watano iliongozwa na Mhe. Merky Lugendo Mziray ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA nayo imekwisha toa taarifa yake kwamba Makao Makuu ya CHADEMA yanatawaliwa na ubaguzi wa kikabila, kidini na kielimu.
UTENDAJI WA KIBABE
CHADEMA ni chama kilicho njia panda kwa sasa kutokana na utendaji wa kibabe wa Mhe. MBOWE. Ninafahamu jinsi vyama vingine vya upinzani hapa nchini kama vile NCCR ? Mageuzi vilivyoporomoka haraka haraka mithili ya nyumba ya mabua. Chama NCCR ? Mageuzi kilifikia mahali pazuri tu hadi watu wakaanza kufikiria kuwa kingekuwa chama mbadala kwa CCM. kwa bahati mbaya uchu wa madaraka, ulafi wa ruzuku, na tabia za kimangimeza kwa pamoja vikakiathiri hadi kupoteza umaarufu wake.
Na hata vyama vingine vya upinzani vina dalili hizo hizo japo kwa viwango vinavyotofautiana. Ila badala ya kujichunguza na kujua kasoro zetu, kila siku vyama vyetu, vimekuwa vikidai kuwa ni chama tawala ndicho kinachoviroga, kama ambavyo Mhe. MBOWE ameanza kuweweseka kupitia vyombo vya habari.
Napenda kuthibitisha kuwa katika mgogoro unaopaliliwa sasa na Mhe. MBOWE ndani ya CHADEMA kutokana na ufisadi, ufuska, ulevi wa madaraka na umangimeza chanzo chake ni tabia yake ya kuendesha chama kibabe. Mathalan kumzuia Martin Mung?ong?o Mkurugenzi aliyechaguliwa kwa kura kutofanya kazi zake ndani ya chama, madai ya kupigana na watendaji wa chama ndani ya baa na vitendo vingine vya aina hiyo ni ushahidi tosha wa hulka hii. Hadi sasa Mhe. MBOWE amefanikiwa kukizuia chama hiki kisifanye kazi ya siasa mkoa wa Dar es salaam kwa miaka minne.
Ninavyoongea hivi sasa CHADEMA imekuwa ikikimbia vikao vya Democratic Union of Afrika (DUA), Muungano wa Vyama Vya Upinzani, uliofanikisha CHADEMA kujuana na Conservative Party ya Uingereza na Republican ya Marekani. Vyama dada hivi vyote vinaulalamikia uongozi wa CHADEMA kwa kufuja fedha ya misaada na kuwasilisha kwao risiti za kugushi, kama ilivyofanyiwa Conservative Party baada ya kutoa msaada wa Tshs. 78,000,000 kwa ajili ya ununuzi wa baiskeli na pikipiki ambazo hazikununuliwa.
Katika mkutano wa Kamati Kuu ya CHADEMA huko Dodoma hivi majuzi tu, Mhe. MBOWE kwa kauli yake aliwatisha wajumbe kuwa alikuwa amethibiti uwezekano wowote wa wajumbe kujisikia huru kwa kutoa mawazo ambayo yangepingana na ajenda yake aliyoitoa ghafla kikaoni kunisimamisha Umakamu Mwenyekiti.
Mhe. MBOWE Alikifahamisha kikao kuwa alitoa taarifa kwa IGP, SAID MWEMA kuwa kuna wahuni ambao walitaka kuuchafua mkutano wake, naye IGP akahakikisha kuwa mkutano ule unalindwa kwa kiwango cha kushtua kama ambavyo hata vyombo vya habari vimethibitisha.
Hayo ni baadhi tu ya mambo yanayobainisha Mhe. MBOWE ni kiongozi wa aina gani.
HITIMISHO
Kama nilivyokwisha sema hapo awali, sijaacha na sintoacha ajenda yangu ya kufufua uhai wa CHADEMA kwani ndiyo ahadi iliyofanikisha kuchaguliwa kwangu kuwa Makamu Mwenyekiti Taifa. Nilipopata wadhifa huo nilianza kuitekeleza ajenda hiyo kupitia mahojiano na Mwenyekiti MBOWE kuhusu matumizi ya ruzuku, madeni ya uchaguzi, uteuzi wa wabunge wa viti maalum, nafasi za ajira Makao Makuu, na kuhusu mwenendo wa chama Mkoa wa Dar es salaam.
Nilijikuta katika mvutano mkubwa kila nilipogusa eneo lolote katika haya. Nakiri kuwa kwa kiwango kikubwa sikuwa na uwezo wa kubadili mambo hayo yaliyokuwa yakiratibiwa kwa ukaribu na Mhe. MBOWE na wafuasi wake kwani sikupewa ushirikiano wa aina yoyote na chama pale Makao Makuu. Ni vigumu kuamini, lakini ni kweli kuwa sikuwa na ofisi Makao Makuu, sikupewa vitendea kazi kama magari, vipaza sauti na/au vyombo vya habari, na sikuwahi kupata taarifa yoyote ya kiutendaji toka Makao Makuu.
Kwa kuzingatia yote hayo, naomba nichukue fursa hii kuwashukuru kwa dhati wanachama wa CHADEMA mkoa wa Dar es salaam ambao kwa pamoja tulisimama kidete kufufua uhai wa chama hapa jijini. Niseme tu ushirikiano wao wa hali na mali uliniwezesha kushughulikia masuala muhimu ya kitaifa na kimataifa.
Rai yangu kwa wana CHADEMA na wale wote wanaokitakia mema chama chetu na nchi yetu kwa ujumla ni kwamba kazi ya kupigania demokrasia ya kweli ndani na nje ya chama, kukiepusha chama na vitendo vya ukabila, migogoro, ubadhirifu, umangimeza, ufisadi na ubaguzi wa aina yoyote bado inaendelea na nawaombeni mniunge mkono kwa hali na mali katika vita hii. Naamini tutashinda.
Mungu Ibariki CHADEMA
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika
====Chacha Wangwe amekufa lakini waraka wake huu utawasaidia WanaCHADEMA na watanzania kuelewa ukweli wa mambo aliyokusudia.
Madam Amosam,
siwezi kukuhukumu sana kwa waraka huu. ni kweli lazima wana JF waangalie authenticity yake ili kujiridhisha na content zake kabla ya kutoa maoni.
kama ni kweli una document original iliyokuwa imeandikwa na Marehemu Wangwe iambatanishe (attach) katika thread yako na binafsi pamoja na wana JF wengine wenye utaalamu wa IT wanaweza kuthibitisha juu ya original author wa hiyo document. au waweza kuituma kwa [email protected]
 
Maandishi haya ya Marehemu Chacha Wangwe kumkomoa Mwenyekiti Freeman Mbowe, more than one year ago, yamefufuliwa na Wana-JF ambao ni ccm damu dam, kwa vile CHADEMA sasa ni tishio kubwa dhidi ya chama tawala.

Kama kweli JF tunataka kuwa objective, as great thinkers must be, tuonyeshe jinsi MBOWE na Chadema walivyoibuka washindi ktk jimbo la Marehemu Chacha Wangwe, na kuwabwaga CCM licha ya kuiga kutumia helikopta na kuleta vigogo wa Makao Makuu Tarime. Walihonga hata Mchungaji Christopher Mtikila akajiingiza na DP yake pale. Poor Mtikila aliambulia ngeu kichwani ambayo hataisahau maishani.

Kuanzia Uchaguzi Mdogo wa Tarime, na kuingia kwa Charles Mwera, Mwana-Chadema shupavu, kurithi kiti cha Chacha Wangwe, chart ya kukua kwa Chadema imekuwa ni juu, juu, juu tu mpaka leo; na itaendelea hivyo hivyo mpaka chama cha mafisadi king'olewe madarakani. Hakuna Kulala, Mpaka Kieleweke.

Wanaozusha FREEMAN MBOWE eti anaendesha shangingi lililoibwa huko Uingereza wangeshauriwa wawe careful. Maana ushahidi unaweza kuanikwa hadharani kwamba mashangingi mengi ya vigogo wa ccm yanatokana na wizi wa fedha za kodi za walalahoi kutoka akaunti ya EPA. Wizi wa shangingi U.K. na wizi wa mashangingi Tz ambayo yangeweza kutumiwa na Wizara zetu za Afya, Kilimo, Elimu n.k. ni upi mbaya zaidi? Na hata kama shangingi la Mbowe liliibwa U.K., yeye alilinunua.
 
Last edited:
huu waraka ni kampeni za CCm za kuiomaliza Chadema, wanachotaka kufanya ni kupandikiza chuki ambazo zilishaanzwa kupandikizwa miaka nenda rudi za ukabila na udini, lakini kwa wenye akili timamu hata zitto kabwe kakikuta chama kina nguvu Kigoma kumbuka Amani Kaburou, sasa uwezi kusema kuna ukabila na hata aAmani alipotoka Chadema Kwenda Ccm hakuzungumza mambo ya ukabila,
kwa kifupi huo waraka sio wa Chacha Wangwe, na kama ni wa Wangwe ulikuwa wapi siku zote
 
Maandishi haya ya Marehemu Chacha Wangwe kumkomoa Mwenyekiti Freeman Mbowe, more than one year ago, yamefufuliwa na Wana-JF ambao ni ccm damu dam, kwa vile CHADEMA sasa ni tishio kubwa dhidi ya chama tawala.

Kama kweli JF tunataka kuwa objective, as great thinkers must be, tuonyeshe jinsi MBOWE na Chadema walivyoibuka washindi ktk jimbo la Marehemu Chacha Wangwe, na kuwabwaga CCM licha ya kuiga kutumia helikopta na kuleta vigogo wa Makao Makuu Tarime. Walihonga hata Mchungaji Christopher Mtikila akajiingiza na DP yake pale. Poor Mtikila aliambulia ngeu kichwani ambayo hataisahau maishani.

Kuanzia Uchaguzi Mdogo wa Tarime, na kuingia kwa Charles Mwera, Mwana-Chadema shupavu, kurithi kiti cha Chacha Wangwe, chart ya kukua kwa Chadema imekuwa ni juu, juu, juu tu mpaka leo; na itaendelea hivyo hivyo mpaka chama cha mafisadi king'olewe madarakani. Hakuna Kulala, Mpaka Kieleweke.

Wanaozusha FREEMAN MBOWE eti anaendesha shangingi lililoibwa huko Uingereza wangeshauriwa wawe careful. Maana ushahidi unaweza kuanikwa hadharani kwamba mashangingi mengi ya vigogo wa ccm yanatokana na wizi wa fedha za kodi za walalahoi kutoka akaunti ya EPA. Wizi wa shangingi U.K. na wizi wa mashangingi Tz ambayo yangeweza kutumiwa na Wizara zetu za Afya, Kilimo, Elimu n.k. ni upi mbaya zaidi? Na hata kama shangingi la Mbowe liliibwa U.K., yeye alilinunua.

Hii iko chini sana ,yani kwa vile ccm wanaiba basi na yeye mbowe kuiba ni halali.Teh teh teh
kwa kweli hii kali.
 
huu waraka ni kampeni za CCm za kuiomaliza Chadema, wanachotaka kufanya ni kupandikiza chuki ambazo zilishaanzwa kupandikizwa miaka nenda rudi za ukabila na udini, lakini kwa wenye akili timamu hata zitto kabwe kakikuta chama kina nguvu Kigoma kumbuka Amani Kaburou, sasa uwezi kusema kuna ukabila na hata aAmani alipotoka Chadema Kwenda Ccm hakuzungumza mambo ya ukabila,
kwa kifupi huo waraka sio wa Chacha Wangwe, na kama ni wa Wangwe ulikuwa wapi siku zote

Hayo maneno aliyazungumza Wangwe mwenyewe kwa mdomo wake akiwa hai.Ukitaka nenda kwenye vyombo vya habari watakupa hata audio uisikilize.
 
huu waraka ni kampeni za CCm za kuiomaliza Chadema, wanachotaka kufanya ni kupandikiza chuki ambazo zilishaanzwa kupandikizwa miaka nenda rudi za ukabila na udini, lakini kwa wenye akili timamu hata zitto kabwe kakikuta chama kina nguvu Kigoma kumbuka Amani Kaburou, sasa uwezi kusema kuna ukabila na hata aAmani alipotoka Chadema Kwenda Ccm hakuzungumza mambo ya ukabila,
kwa kifupi huo waraka sio wa Chacha Wangwe, na kama ni wa Wangwe ulikuwa wapi siku zote

Tupo ukurasa mmoja mkuu, but am sorry to let them know that their application is too late!
 
Kana-Ka-Nsungu,
2) Kama unavyofahamu Chadema huwa haina tabia ya kukurupuka. Tumekaa kimya muda wote, na hatukutaka kujibu chochote, kwa kuwa wakati waraka huu unatolewa tulikuwa bado kwenye maombolezo, na isingelikuwa vema kabla hata ya arobaini kuanza kulumbana wakati mhusika hayupo. Ambaye angelifanya hivyo ni mtu asiye sensitive kwa utamaduni wa Mtanzania. Chadema hatuko tayari na tusingeliweza kufanya wala hatutafanya hivyo hata siku moja kwa pressure tu kuwa tunatakiwa kujibu tuhuma.
ii) Kwa kawaida unahangaika kama kuna chembe cha ukweli katika tuhuma. Kama huna mashaka na tuhuma, na tuhuma unajua kwa uhakika hazina msingi, basi huna sababu hata tone kukurupuka kujua. Cha kwanza, na hasa pale ambapo hakuna ushahidi unaotolewa na watu wanaendelea "kukandamiza" lazima kujiuliza kuna nini, lazima kufanya utafiti na kuchunguza chanzo cha Tuhuma hizo. Ukitoka hadharani una msingi wa tuhuma na watu wote wataheshimu kwa vile umetoka na uchunguzi uliokamilika.
iii) Napenda kutoa taarifa ya awali kuwa sasa Chadema tuko in possition with evidence in hand, kwanini tumetuhumiwa hayo yote.Kwanini tumehusishwa na kifo na kwanini Mheshimiwa Mbowe ametuhumiwa na kuhusishwa na kifo. Indicator tumekwisha kutoa kwenye magazeti, kuwa tunayo sasa recorded evidence ya njama zinazofanywa na baadhi ya viongozi wazito wa vyama wakiwemo wa upinzani. Namba ya Fax ya Katibu Mkuu wa Chama Tawala imetajwa kuwa ndiyo iliyotuma ujumbe huo kwa fax kutoka Dodoma, kwa wale ambao hawakufuatilia ni fax no (026)2322965 ya Katibu Mkuu CCM Dodoma, tarehe 27 July, saa 9.42 alasiri yaani siku moja tu kabla ya kifo, na kutawanywa kwa Makatibu wa Mikoa wa CCM kutoka Fax no (022) 2667457 ya Stationary tarehe 31 July wakati wote wenye mapenzi mema tuko Kwenye Msiba Tarime. Mwenye akili ya kuchambua hahitaji kuambiwa hapa kuna nini. Taarifa ya Sherehe Afrika Kusini anayosemekana "kuiangusha Mbowe" baada ya kupata Taarifa ya Msiba nayo tumepata ushahidi documentary (Video na Audio) ambapo mwenyekiti wa Chama cha Upinzani alimwita kwake Mhariri wa Gazeti, tena linalomilikiwa na walioko kwenye listi ya Mafisadi tuliyoitaja 15 September, 2007. Hapa mwenye akili ya uchambuzi naye hahitaji kuambiwa kuna nini nyuma ya pazia. Tunazo nyaraka mbalimbali, ambazo ninaomba msubiri Tamko rasmi tutakolotoa. Wenye masikio wategee wakati huo.

Hilo tamko lilitoka? Tunaweza kupata copy? Maana kwangu mimi ni mara ya kwanza kuona hii habari na hasa huu waraka wa Wangwe.
 
Ila nimegunduwa kumbe Chadema inaitetemesha CCM kama mtu mgeni kwenye jamvi hili nimeona baada ya biharamulo kumekuwa na kufukua thread za miaka mitatu minne iliyopita kwa nini mumeona nguvu ya chadema,nadhani your too predictable some one to trust you guys mwisho wa siku sisi wanajamvi tunaona ni propaganda mulizozifanya kwa kuwachafua akina Sumaye kable ya uchaguzi wa 2005 mkidhani mumepata kumbe mumepatikana,Serikali ya CCM imepoteza hadhhi sana chama cha viongozi wa kiisala na jumuiya zake kama vijana,wanawake na wazazi klnatakiwa kijisafishe badala ya kutaka kuua demokrasia kwa kuwaandama wale wachache waliojitoa kuamsha washawasha ya vuguvugu la kisiasa.Nafurahi kwamba si mwananchama wa chama chochote ukiacha uanacha tuliolazimisha na CCM miaka hiyo tukiwa vyuoni
Nitasimamia haki siku zote
CCM kweli munawohofia chadema lakini mapinduzi ya kweli hayataletwa na chadema yataletwa na wanchi wenyewe ambao hawasikii na mwazini wala la nani wanjua kuzomea na kuuliza na kuwakaba viongozi na bado mwakani jasho litawatoka CCM wakati wa mabumbu umekwisha sikiliza kipindi cha TBC1 wanachi wakihojiwa utajua mabadiliko makubwa ya kifikra ya wanachi wa vijiji
kwa strategies za kuandika nyaraka wenyewe mukihusisha akina Wangwe wakati uhakika wa waraka wenyewe hauwezwi kuhakikiwa ni upuuzi mtupu peleka porojo kw a washamba wengine sio katika jambi hili

Hapa umeongea ukweli. Anti-CHADEMA posts za zamani zinafukuliwa hata kama zimepitwa na wakati na hii ni Dalili Njema kuwa Kichwa cha Nyoka (Sisiemu) kinakaribia kukatwa.
 
Mugo"The Great";523356 said:
Hapa umeongea ukweli. Anti-CHADEMA posts za zamani zinafukuliwa hata kama zimepitwa na wakati na hii ni Dalili Njema kuwa Kichwa cha Nyoka (Sisiemu) kinakaribia kukatwa.

Mkuu hii imetulia sana, tena ni yule joka wa mdimu (Mudhihiri, 2009) lol!
 
Mwanakijiji,ili la kuwa na Rekodi nalipinga kabisa,hata Leo ukiamka na ukimuuliza Mnyika au Frank Isack ni wanachama wangapi ambo ni Vijana wanao kwaT anzania hawezi kukupa Jibu la ukweli

Na hii inatufundisha nini,Mali bila Daftali hupotea bila mwenye mali kuwa na taarifa,hivyo hivyo wanachama hupotea sababu hakuna Rekodi zao.watu wangawiwa kadi katika mikutano ya hadhara na hakuna kinachoendelea.ipo haja ya vyama kuwa na rekodi Nzuri za wanachama wake na hii itasaidia katika mipango ya Kampeni
Ndiyo ilivyokuwa Biharamuro na Busanda.
 
JE CHADEMA ITASALIMIKA......! KAMA KUNA WAO......(wachaga) NA SISI ....(makabila mengine)....! DHAMBI HII IKISHAKUWALA BADO ITAENDELEA NA KWA.....!
tik...tak....tik...tak...!

...Haya ndio yanayomwandama Zitto Kabwe baada ya kumalizika Uchaguzi Mkuu.
Nini tamko la CHEDEMA kuhusu tuhuma mfululizo dhidi ya ZITTO KABWE?

'Bendera fata upepo,' nao hawaimbiwi wanacheza,
badala ya kujenga chama wao wanaondoa fito zilizojengewa nyumba.
Changes? Never...
labda baada ya miaka 50!
 
Kama nilihama chama kwa kumfuata Mbowe au la, wewe inakuhusu nini? Una haki gani ya kunichagulia sababu za kuhama chama? Wewe umefanya utafiti au kusoma tafiti za wengine kujua sababu zinazowafanya watu wajiunge na chama A na sio B? Inaonekana ilikuuma, kukukera na kukuudhi sana mimi kuhama CCM na kujiunga na CHADEMA, unaweza kutueleza ni kwa nini hasa unakuwa na uchungu namna hii?

Mimi nadhani sababu ungekuwa CCM usingekuwa na coverage kubwa kama uliyonayo Chadema siku hilo likifa utahamia chama C.
 
Tangia kampeni kuanza za uchaguzi mkuu, Ndg. Slaa alikuwa peke yake kwenye kampeni bila ya kusaidiwa na Mgombea mwenza, tofauti na vyama vingine, je huu sio ubinafsi?. Na habari za uhakika zilizozopo ni kuwa Mgombea mwenza wa Slaa alikuwa na elimu ya darasa la 7 tu, ili hali yeye mwenyewe alikuwa anahubiri elimu ya awali iwe ni form six. Hivi alichokuwa anakisema ndicho alichokuwa anakimaanisha kweli ? inakuwaje utuletee mgombea mwenza wa darasa la 7 ili hali wewe wahubiri elimu ya awali ni form six ?. Huu ni upotoshaji dhahiri ambao CDM waliufanya kwa wananchi, na yaonyesha Slaa alichokuwa anakisema sicho ambacho angetenda endapo angepata urais. Bora Mungu alituepushia mbali mtu huyu !
 
na wewe akili yako inarudi nyuma watu wako kwenye mijadala yenye afya kwa taifa bado unaturudisha kwenye kampeni ambazo zimeisha na Kuibua maswali kibao sifa za kugombea nafasi yoyote ya uongozi ni kuja kusoma na kuandika period
 
Ndugu ThinkTwice

kwa mgombea yeyote wa chama kuahidi kuwa ataleta kitu kizuri si kuwa lazima kiwepo. Mathalan JK anaposema ataleta flyover hazipo ! Unapomwambia mwanao nitakununulia soda ukifaulu siyo lazima kuwa uahidi wakati soda ipo!! kadhalika kuwa na mtu wa darasa la saba na huku Slaa akisema watatakiwa wa form six as elimu ya wali, maana yake kwa sasa haiko hivyo na huyo mgombea mwenza ilikuwa sample nzuri tu! ya kuwa kama wewe unamdharau mtu wa darasa la saba na huku uansema alikuwa mbinafsi huoni tayari indirectly umeungana na Slaa kuwa darasa la saba ni aibu (kwako) na elimu ya walai iwe form six?

Pili ciriteria za shule na uongozi ni vitu viwili tofauti ambavyo watawala wamejaribu kutundanganya ukiwemo wewe mpendwa!!

Mkwawa, Mirambo, Mputa,Rumanyika, Mangi Sina, Mandara, n.k walikuwa viongozi wazuri na hawakuwa na shule yeyote leader is born, and we all have such ability naturaly because real leadership starts at home!
 
Huyo Mgmbea mwenza hakuweza kufika elimu ya juu kutokana na udhalimu na utawala mbovu wa ccm. hivyo ingekuwa cdm ndio ilichukua nji hii tokea uhuru huyo mwenye hiyo elimu asingekuwepo..
 
Tangia kampeni kuanza za uchaguzi mkuu, Ndg. Slaa alikuwa peke yake kwenye kampeni bila ya kusaidiwa na Mgombea mwenza, tofauti na vyama vingine, je huu sio ubinafsi?. Na habari za uhakika zilizozopo ni kuwa Mgombea mwenza wa Slaa alikuwa na elimu ya darasa la 7 tu, ili hali yeye mwenyewe alikuwa anahubiri elimu ya awali iwe ni form six. Hivi alichokuwa anakisema ndicho alichokuwa anakimaanisha kweli ? inakuwaje utuletee mgombea mwenza wa darasa la 7 ili hali wewe wahubiri elimu ya awali ni form six ?. Huu ni upotoshaji dhahiri ambao CDM waliufanya kwa wananchi, na yaonyesha Slaa alichokuwa anakisema sicho ambacho angetenda endapo angepata urais. Bora Mungu alituepushia mbali mtu huyu !

hili swala lako lilijibiwa kwa ufasaha wakati wa mdahalo(katafute clip).acha kukurupuka ndugu au ndio tuseme una "regressed milestones"katiba haimkatazi mtz mwenye elimu ya std 7 kugombea!
THINK THRICE BEFORE YOU POST .
 
Back
Top Bottom