Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,193
- 299
Mtanzania,
Wangwe ni mbunge wa Tarime. Sijasikia popote kuwa amevuliwa ubunge wake. Wangwe alichaguliwa makamu mwenyekiti wa CHADEMA na kikao hicho hicho ambacho kimeamua kumsimamisha wadhifa huo. Wangwe hajavuliwa uanachama wa CHADEMA. Sasa ujinga unaouzungumzia ni upi?
Baada ya kufuatilia historia ya mgogoro huu, matatizo (kama ni matatizo) yaliyosababisha Chacha atolewe kwenye uongozi ni yaleyale aliyokuwa nayo kabla ya kuchaguliwa kuwa kaimu makamu mwenyekiti, na ukifuatilia vizuri ndio sababu hizohizo ndizo zilimfanya achaguliwe, kwa hiyo kama aliyemtoa Chacha kwenye nafasi aliyokuwa akishikilia siyo aliye muweka ni dhahiri kuwa uamuzi huo unapingana na walio wengi (waliomchagua Chacha). Ni sababu zipi zilimfanya Dr. Slaa na Zitto watake kujiuzulu???? Hoja za Chacha zichambuliwe na zifanyiwe analysis objectively na independent analyst anayekifahamu CHADEMA bila biasness yoyote. Kwangu mie (mzalendo nisiye na chama cha siasa) nayaona madai ya Chacha yana uzito zaidi (relatively) na sababu zilizotolewa za kumfukuza. Ushauri kwa CHADEMA ijipange upya na isizichukulie juu juu hoja za Chacha, otherwise i am sorry to say bila kufanya hivyo mtajifanya yameisha leo ila kesho yataibuka tena na yatawamaliza.
Huyu bwana kwa kweli alikuwa anakera sana wakati mwingine! Yaani si mtu makini kama tulivyowazoea viongozi wengine wa CHADEMA. Najua yafuata maneno mengi na labda watu wa tarime watareact sana, lakini lazima tukubali ili kuwa na upinzani makini lazima na watu wake wawe makini sana! Mimi naamini wabunge wa upinzani (individually) ni competent zaidi ya wale wa CCM kwa sababu wanafanya kazi na kushinda katika mazingira magumu sana. Pia hata ukinagalia wanavyojenga hoja, za wapinzani nyingi utakuta zimejaa akili. CCM imejaza watu weak sana! Upinzani pia labda kuna problem kidogo kwa baadhi ya wabunge wanaotokea upande wa Zanzibar ukiachia akina Hamad Rashid na wengine wachache
mi nakuwa nashindwa kuelewa kama hizi ni Spinning na ushabiki wa hapa JF, maana watu wanasubiri kitu kiandikwe kisha wanatafuta mabaya ndani yake...ilimradi tu la kuongea liwepo ama Chama Mbadala kinapoteza dira...
na tumesiKia upande mmoja wa Chama na kwa jinsi nnavyomfahamu Chacha sidhani kama atakuwa amekaa kimya, kwa nini asije nae kisha tukasikia upande wake kisha tukajadili.
husiana na kachaguliwa na nani na kusimamishwa na nani nadhani tunahitaji kupitia katiba ya chama.
"Mjumbe mwingine wa kikao cha Kamati Kuu ambaye jana alizungumza na Tanzania Daima Jumapili, alisema kimsingi uamuzi wa kusimamishwa kwa Wangwe unatokana na pendekezo la vikao hivyo vya wazee, ambako awali aliitwa na kuonywa na yeye akaomba radhi kwa makosa yaliyokuwa yakimkabili.
Zitto, Kitila, Mnyika, Mbowe na allegedly Mwanakijiji, mnajulikana kuwa viongozi wa juu wa CHADEMA, kwa nini hamchangii mada na kuiweka sawa?
Zitto imesemekana ulitaka kuachia ngazi, je ni kweli? Kama ndivyo ni sababu zipi zilikufikisha bapo? Tunaomba michango yenu wakuu ASAP.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
NA
WANANCHI WA TANZANIA
KUSIMAMISHWA KWA MHESHIMIWA CHACHA ZAKAYO WANGWE (MB.) KUWA KAIMU MAKAMU MWENYEKITI WA TAIFA (BARA) WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
Ndugu wanahabari na wananchi wenzangu,
Tarehe 28 Juni 2008 Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo katika kikao chake cha kawaida kilimsimamisha Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe kama Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Taifa (Bara) wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kumpigia kura ya siri ya kutokuwa na imani naye. Huu ni uamuzi mzito na ambao haujawahi kufanywa katika historia ya miaka 16 ya CHADEMA. Tunapenda kuwafahamisha wananchi wetu kwamba uamuzi huu mzito ulichukuliwa baada ya mjadala na tafakuri ya muda mrefu. Kamati Kuu ya chama chetu ilifikia hatua hiyo dhidi ya baada ya kuridhika na ushahidi kwamba Mh. Chacha Wangwe amekiuka maadili ya uongozi na hivyo kupoteza sifa mahsusi za kuendelea kuwa kiongozi wa kitaifa wa CHADEMA kwa sababu zifuatazo:
-----------------------------------------------
Freeman A. Mbowe
MWENYEKITI
Ndugu wananchi na wanahabari,
Kamati Kuu ya CHADEMA haikufikia uamuzi huu mzito kwa haraka na/au bila kufikiria kwa kina madhara yake kwa chama na kwa taifa letu. Kamati Kuu imefikia uamuzi huu baada ya jitihada mbali mbali za kumsaidia Mh. Chacha Zakayo Wangwe kujisahihisha na kujirudi kushindikana kabisa. Jitihada hizi mbali mbali ni kama vile:
a. Vikao mbali mbali na vya muda kati yake mwenyewe, Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu kujadili tofauti na/au migongano kati yao na/au ndani ya chama;
b. Kusuluhishwa na Kamati ya Wazee wa Chama ambapo Mh. Wangwe alitakiwa kuandika maandishi kwamba ataacha vitendo vyake dhidi ya chama, viongozi wa kitaifa na watendaji wa chama;
c. Kamati Kuu ya chama kumuonya kuacha vitendo vyake hivyo dhidi ya chama;
d. Baada ya jitihada zote hizi kushindikana, Kamati Kuu ilimsihi kujiuzulu kwa hiari yake yeye mwenyewe na hivyo kujiepusha na adha ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na kusimamishwa na Kamati Kuu.
Kwa vitendo na matukio yote haya, Kamati Kuu ya CHADEMA imejikuta haina njia yoyote ile ya kuepuka mgogoro mkubwa zaidi na usio na maana au msingi zaidi ya kumchukulia hatua za kinidhamu Mh. Chacha Zakayo Wangwe. Kwa matendo haya ni wazi Mh. Chacha Zakayo Wangwe amepoteza sifa mahsusi za kuendelea kushikilia dhamana kubwa ya uongozi ambayo vikao halali vya chama vilimpatia. Kamati Kuu imelazimika kutumia mamlaka yake ya kikatiba ya kumsimamisha uongozi wa kitaifa Mh. Wangwe kwa kumpigia kura ya siri ya kutokuwa na imani naye. Azimio la kumsimamisha Mh. Wangwe kuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti Taifa (Bara) liliungwa mkono na wajumbe ishirini na nne kati ya thelathini na moja waliohudhuria na kushiriki katika kikao cha Kamati Kuu. Idadi hii ni zaidi ya theluthi mbili ya kura za wajumbe wa Kamati Kuu inayohitajika kikatiba ili kumsimamisha uongozi kiongozi yeyote wa kitaifa kama alivyokuwa Mh. Chacha Zakayo Wangwe. Kamati Kuu imechukua hatua hii ngumu na nzito ili kukiokoa chama kutokana na migogoro ambayo imesambaratisha vyama vingine vya siasa hapa nchini.
Asanteni sana
Mtanzania,
Wangwe ni mbunge wa Tarime. Sijasikia popote kuwa amevuliwa ubunge wake. Wangwe alichaguliwa makamu mwenyekiti wa CHADEMA na kikao hicho hicho ambacho kimeamua kumsimamisha wadhifa huo. Wangwe hajavuliwa uanachama wa CHADEMA. Sasa ujinga unaouzungumzia ni upi?
Kamati Kuu ya chama chetu ilifikia hatua hiyo dhidi ya baada ya kuridhika na ushahidi kwamba Mh. Chacha Wangwe amekiuka maadili ya uongozi na hivyo kupoteza sifa mahsusi za kuendelea kuwa kiongozi wa kitaifa wa CHADEMA kwa sababu zifuatazo:
1. Amekuwa akijihusisha na/au kushiriki katika vikundi na/au vitendo vya uchonganishi na/au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa chama na/au wanachama wake.
Kitendo cha kuandaa, kushiriki na/au kufadhili mikutano ya siri ya watu ambao wamechukuliwa hatua za kinidhamu na vikao halali vya chama na/au ambao wamekihama chama baada ya kupoteza ridhaa ya kuwaongoza wananchi kina tafisiri moja tu ya msingi: Kuendeleza migogoro na/au hujuma dhidi ya chama kwa lengo la kukidhoofisha na kukifanya kishindwe kuendeleza vita kubwa dhidi ya ufisadi uliojikita ndani ya Serikali na CCMambayo imekipatia chama chetu sifa kubwa na uhalali kwa watanzania.
-----------------------------------------------
Freeman A. Mbowe
MWENYEKITI
Waheshimiwa!!!
Chacha Wangwe ni Mzigo... sikiliza tu hata hoja zake Bungeni... si mpenda fuata taratibu hata kidogo...
Mimi kwa hili niko na CHADEMA...
Jamani muikivuruga CHADEMA tutakuwa tumekwisha!!! nakubaliana nao kwamba hawajafikia kukabidhiwa nchi lakini tunatamani kwamba wapate wabunge angalau 20 to 30% kwenye Uchaguzi ujao...
Sasa kuanza kuwavuruga kwa kweli hamuitendei nchi yetu!
Bado nina imani na CHADEMA.
Sijaona chama makini kama hiki. Hata CCM hamna kitu.
Si unajua shida zenu ni nyingi? Kiongozi akivurunda mnampokea kwa ushujaa eti kwa sababu alichaguliwa na wengi. Upuuzi huo.
Kiongozi akivurunda nje. Na hii ni kwa sababu katiba ambayo wamejiwekea na wananchi hao hao waliomchagua wakaipitisha inasema hivyo.
Maana yake ni kwamba hao waliomchagua ni hao hao walioweka utaratibu kwamba kama uteuzi wake utaonekana haufai basi kamati kuu imuondoe. Sasa wewe MTANZANIA shida yako iko wapi? acha kuingilia mambo yasiyokuhusu. Hiyo nikuchonganisha tu. Na hilo halisaidii maana bado tunaukubali uongozi wa Chadema kuwa ni makini.
Mchungaji kwa hili ni juu yake kuangalia na kuamua kama bado anafaa kuendelea kuwa mwanachama au afanye kama Kabarou kwa kuwarudishia ccm kadi ya chadema🙂Kama kapoteza sifa ya Uongozi, je ana sifa gani kuendelea kuwa Mwanachama?
2. Amekuwa akitoa tuhuma nzito lakini zisizokuwa na msingi dhidi ya viongozi wenzake wa kitaifa na watendaji wa chama pasipo kupitia vikao halali na wala kuzingatia taratibu za chama
Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe aidha moja kwa moja ama kwa kuwatumia viongozi na/au wanachama walioadhibiwa na vikao halali vya chama amekuwa akiwatuhumu viongozi na watendaji wa chama kwa mambo ya uzushi na yasiyokuwa na ukweli na/au msingi wowote. Yeye mwenyewe amekuwa akisambaza uzushi kwamba kuna ufujaji na/au matumizi mabaya ya fedha za chama ambao amekuwa akidai unafanywa na viongozi wa kitaifa hususan Mwenyekiti wa chama Taifa na Katibu Mkuu na/au watendaji wa Makao Makuu ya chama. Aidha Mh. Chacha Wangwe amekuwa akisambaza uzushi kwamba viongozi wenzake wa kitaifa na watendaji Makao Makuu wamekuwa wakikataa ruzuku ya chama kupelekwa mikoani na wilayani nabadala yake wamekuwa wakiitumia ruzuku hiyo kwa shughuli za Makao Makuu na/au kwa manufaa yao binafsi. Uzushi huu umetolewa licha ya Kamati Kuu ya chama ambayo Mh. Chacha Wangwe alikuwa ni mjumbe kupokea na kupitisha taarifa zote zinazohusiana na mapato na matumizi ya fedha za chama na licha ya chama kutoa ruzuku ya vifaa na/au fedha taslimu tangu mwaka 2006 kabla hata ya yeye kuchaguliwa kuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA tarehe 17 Desemba mwaka 2007. Aidha Mh. Chacha Wangwe amesambaza uzushi huu licha ya kufahamu fika kwamba si yeye mwenyewe, wala si Makamu Mwenyekiti Taifa (Visiwani), wala si Mwenyekiti Taifa wala si Katibu Mkuu wala manaibu Makatibu Wakuu wote wa chama ambao wamepokea hata senti moja ya fedha za chama kama posho au mishahara. Tuhuma hizi za uzushi na uwongo juu ya kuwepo ufujaji na/au matumizi mabaya ya fedha za chama zina lengo moja tu: Kuwapaka matope viongozo wa chama wa kitaifa na watendaji wa ngazi za juu wa chama kwa lengo la kudhoofisha jitihada za chama kujijenga kwa wananchi na kuendeleza vita dhidi ya ufisadi ambayo imekipatia chama na viongozi wake umaarufu miongoni mwa wananchi wa Tanzania.
-----------------------------------------------
Freeman A. Mbowe
MWENYEKITI