Umetema madini matupu!
Kusema kweli nami nilishangazwa sana kwa kitendo cha Lisu kwenda kumnanga Magufuli Usukumani!
Kitendo hicho kimeishushia Chadema credit pakubwa!
Nikawa najiuliza huu uroporopo anadhani anawafurahisha wafiwa!
Kumtukana Magufuli kanda ya ziwa ni sawa na kumtukana mtume!
Hili la Dotto Biteko litainyenyua Ccm ilipokwama iwapo tu atawaondolea kero wananchi kwa matendo ya uongozi wake.
Kama utendaji wake utakuwa ni wa kupiga siasa za kipole na kistaarabu kama vile anahubiri enjili kwa kuwaonea haya mafisadi waliolikwamisha Taifa, ndiyo atazidi kuichimbia kaburi Ccm.
Kosa jingine kubwa wanalolifanya Chadema ni kuendeleza ideology yao ya kususia vikao, kwa mfano wa hiki cha wadau wa siasa, hawakuwa na mantiki ya kufanya hivyo.
Ilitakiwa wakapambanue hoja zao pale, ingelipendeza sana .
Halafu la mwisho kwa Chadema, waondoe udikteta na ukiritimba wao katika uongozi wa chama kitaifa.
Kama wana nia ya kweli ya mabadiliko, ziwekwe sura mpya safu ya juu zitakazokubalika kwa wananchi kuuonesha umma thamani halisi ya demokrasia.
Wakiendelea kuongoza wao tu miaka na miaka kimakame nguvu, kwa kadri siku zinavyokwenda, kitashuka popularity na kubakia chama cha kugawania ruzuku kama vyama vingine vya upinzani vilivyo hivi sasa.