Point of correction...mwanachadema gani aliteuliwa? JPM aliwanunua na wengine walilazimishwa kuhama cdm kwa kutishwa na wote walioteuliwa ilidaiwa kuwa ni hongo waliyoahidiwa kuwa watapata ili wahame cdm. Petrobas Katambi wala waitara na wenzao hawajawahi kupinga hili.
pili, unapomuomba mtu msamaha lazima uwe umemkosea. cdm walimkosea nini jpm? Tanzania si mali ya jpm na wala haitakujakuwa mali ya mtu. Ni mali ya Mungu na anayepewa uongozi anakuwa amedhaminiwa na wananchi. Hata katika ajira, mwajiri akikwambia nataka wadhamini ili nikuajiri, ukiajiriwa kisha ukaanza kuleta shida, wadhamini wako lazima wakulalamikie.
Chadema kama sehemu ya wananchi ambao ndiyo wadhamino, walikuwa na haki ya kiroho, kijamii, kikatiba na kisiasa kulalamikia mwenendo wa JPM kama mwajiriwa.
Hakuna kosa hapo