CHADEMA mna mikakati gani serious ya kushinda uchaguzi 2020?

CHADEMA mna mikakati gani serious ya kushinda uchaguzi 2020?

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Huwezi kukiondoa madarakani chama kikongwe kama CCM kwa kulalamika kwenye vyombo vya habari, au kusubiri kigawanyike, unaweza kusubiri isiwe na kulalamika tu hakutoshi.

Hadi sasa hatuoni movement yeyote serious kuonyesha kweli mna nia ya kuingia ikulu, pamoja na operation Chadema ni msingi, kwa mfano, kuliko kuishia kufanya press conference pale Ufipa, mnaweza kuandaa makongamano ya kimataifa Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, mkaita vyombo mbalimbali vya ndani na nje, investors, mabalozi, mkaalika known public speakers ikiwezekana kutoka nje, mkatumia fursa hiyo kueleza sera zenu na jinsi mtakavyozitekeleza mtakapochukua madaraka. Huo ni mkakati mmoja tu wa kujitangaza ndani na nje mkaaminika, kwa dunia ya leo huwezi kushinda urais bila support ya nje. Hatuoni mkifanya hivyo.

Sioni mkakati wa kuunganisha nguvu, nilisikia wapinzani wameanzisha Azimio la Zanzibar sijui limeishia wapi, nchini Kenya haikuwa kazi rahisi kuiondoa KANU, vyama vya upinzani viliungana baadhi ya viongozi wao wali sacrifice vyeo vyao.

Siyo lazima muweke wazi mikakati yote lkn angalau wapiga kura waanze kuona mwelekeo wa chama towards 2020, siyo mbali, ikiwezekana wamjue mshika kibendera siyo waje kushitukizwa dakika za mwisho kama mlivyofanya kwenye uchaguzi uliopita.

Kushinda uchaguzi ni zaidi ya sanduku la kura, ingekuwa sanduku leo Lowassa angekuwa rais kwa sababu naimani alipata kura nyingi zaidi ya Rais Magufuli na Self leo angekuwa rais wa Zanzibar, sanduku la kura ni kitendo cha kuhalalisha (legitimise) mikakati yako uliyofanya kabla, ya halali na isiyo halali.

If you don't plan you are planning to fail.
 
Nadhani kwa sasa wanamuacha bwana yule atambe na ajidanganye kuwa anakubalika ila wakati wa kampeni ukifika,wataanza kutema cheche na hapo bwana yule na chama chake ndio watajua wanakubalika kiasi gani.

Kwa sasa, wamebanwa, ila wanapata nafasi ya kukusanya madhaifu na kasoro za bwana yule na wakati ukifika wataanza kuyasema majukwaani.
 
Nilijaribu kufuatilia vile vikao vya ndani maeneo mbalimbali ya nchi nikagundua kuwa Chadema ya sasa ni imara zaidi kuliko wakati wote.

Katika mazingira kama haya ya sasa chini ya Magufuli anayekandamiza Uhuru wa kisiasa kwa kutumia dola na unyanyasaji Chadema ingekuwa imekufa kama wanavyo tabiri lakini hamasa ilionekana ni kubwa na sio kama wakati wa Dr Slaa ambapo ushabiki ulikuwa mkubwa.

Sasa hivi hata Chawata wanaonekana tena kwa ujasiri mkubwa hadi polisi wanaona watumie mabavu kwa hao wanawake.
Ni kweli ni vizuri kuanza sasa hivi kumnadi wanaye taka kumsimamisha au wakae na vyama halisi vya mabadiliko mapema kijulikane kama ni mbwai na iwe mbwai
 
Mleta mada ana hoja ya msingi ambayo ninadhani ina mantik. Sisi wapenxi wa mabadiliko ya kweli ya kidemokrasia tunajitaji kutiwa moyo na kauli za mara kwa mara zinazoonesha kuwa kuna mkakati wa ushindi au wa kuhakikisha kuwa hata tukishindwa hatushindwi kwa kishindo.

Binafsi natamani coalition ya Chadema na vyama vingine kikiwemo ACT Wazalendo. Na ninatumaini makosa ya 2015 hatutarudia. Natamani ukimya toka chadema na vyamba mbadala upungue na sisi wapenzi tusikose la kusema!
Nadhani kwa sasa wanamuacha bwana yule atambe na ajidanganye kuwa anakubalika ila wakati wa kampeni ukifika,wataanza kutema cheche na hapo bwana yule na chama chake ndio watajua wanakubalika kiasi gani.

Kwa sasa, wamebanwa, ila wanapata nafasi ya kukusanya madhaifu na kasoro za bwana yule na wakati ukifika wataanza kuyasema majukwaani.
 
Je unataka kujua mbinu zao ili ufanyeje? Hiyo ni siri yao. Je CCM mna mikakati gani?
 
Mleta mada ana hoja ya msingi ambayo ninadhani ina mantik. Sisi wapenxi wa mabadiliko ya kweli ya kidemokrasia tunajitaji kutiwa moyo na kauli za mara kwa mara zinazoonesha kuwa kuna mkakati wa ushindi au wa kuhakikisha kuwa hata tukishindwa hatushindwi kwa kishindo.

Binafsi natamani coalition ya Chadema na vyama vingine kikiwemo ACT Wazalendo. Na ninatumaini makosa ya 2015 hatutarudia. Natamani ukimya toka chadema na vyamba mbadala upungue na sisi wapenzi tusikose la kusema!
Si mko huku JF mnapambana??
 
Chadema wamejipanga kuutangazia Umma kuwa watashinda kabla ya saa nne asubuhi uku wakijua fika kura huhesabiwa baada ya saa kumi. Na mkakati mwingine

Mkakati mwingine ni kuwambia wananchi kuwa wameibiwa Kura...
 
Huwezi kukiondoa madarakani chama kikongwe kama CCM kwa kulalamika kwenye vyombo vya habari, au kusubiri kigawanyike, unaweza kusubiri isiwe na kulalamika tu hakutoshi.

Hadi sasa hatuoni movement yeyote serious kuonyesha kweli mna nia ya kuingia ikulu, pamoja na operation Chadema ni msingi kwa mfano, mnaweza kuandaa makongamano ya kimataifa pale Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, mkaita vyombo mbalimbali vya ndani na nje, investors, mabalozi, mkaalika known public speakers ikiwezekana kutoka nje, mkatumia fursa hiyo kueleza sera zenu na jinsi mtakavyozitekeleza mtakapochukua madaraka. Huo ni mkakati mmoja tu wa kujitangaza ndani na nje mkaaminika. Hatuoni mkifanya hivyo.

Sioni mkakati wa kuunganisha nguvu, nilisikia wapinzani wameanzisha Azimio la Zanzibar sijui limeishia wapi, nchini Kenya haikuwa kazi rahisi kuiondoa KANU, vyama vya upinzani viliungana baadhi ya viongozi wao wali sacrifice vyeo vyao.

Siyo lazima muweke wazi mikakati yote lkn angalau wapiga kura waanze kuona mwelekeo wa chama towards 2020, siyo mbali, ikiwezekana wamjue mshika kibendera siyo waje kushitukizwa dakika za mwisho kama mlivyofanya kwenye uchaguzi uliopita.

Kushinda uchaguzi ni zaidi ya sanduku la kura, ingekuwa sanduku leo Lowassa angekuwa rais na Self angekuwa rais wa Zanzibar, sanduku la kura ni kitendo cha kuhalalisha (legitimise) mikakati yako uliyofanya kabla, ya halali na isiyo halali.

If you don't plan you are planning to fail.
Sidhani kama watakuelewa kwa huu ushauri makini sana,
 
Back
Top Bottom