CHADEMA mna mikakati gani serious ya kushinda uchaguzi 2020?

CHADEMA mna mikakati gani serious ya kushinda uchaguzi 2020?

Huu uchaguzi gani amabo hata CCM wenyewe wameogopa kuchaguliwa? Yaani unachafua halafu unaanika badala ya kufua?1 Hata enzi ya chama kimoja kulikuwa na uchaguzi na mtu alikuwa anajitathmini kakubalika asilimia ngapi, sasa awamu hii imefanya upumbavu halafu mnasema uchaguzi? Lyatonga ameshiriki na ni kibaraka nae mbona analia uikteta? NDIO TUTAGOMA 2020 kama upumbavu utakuwa huu kwani kuna tatizo?
 
Huu uchaguzi gani amabo hata CCM wenyewe wameogopa kuchaguliwa? Yaani unachafua halafu unaanika badala ya kufua?1 Hata enzi ya chama kimoja kulikuwa na uchaguzi na mtu alikuwa anajitathmini kakubalika asilimia ngapi, sasa awamu hii imefanya upumbavu halafu mnasema uchaguzi? Lyatonga ameshiriki na ni kibaraka nae mbona analia uikteta? NDIO TUTAGOMA 2020 kama upumbavu utakuwa huu kwani kuna tatizo?
Pemba inaongozwa na CCM tupu kwani imegeuka Hong Kong?
 
Katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika jana, na Chama cha Mapinduzi kuibuka kidedea katika nafasi za uenyekiti wa mitaa, vijiji, vitongoji na ujumbe, vyama vya upinzani vilisusa kushiriki katika uchaguzi huo japo baadhi ya maeneo wapinzani walishiriki na kushinda baadhi ya nafasi.

Swali la msingi ni je wapinzani katika uchaguzi wa 2020 watasusa? Je kususa kwao wanamkomoa nani? Au tutarajie wakija na hoja mpya ya wao kushiriki katika uchaguzi huo?

Ni vyema unapoleta uzi ujitahidi kupunguza propaganda za kijinga. Kwanza wapinzani walitangaza watashiriki uchaguzi, ila kilichowafanya wasusie uchaguzi ni rafu za wazi. Pia wananchi wengi hasa tunaopigia kura upinzani tuligoma kujiandikisha kwa sababu tulijua hila kwenye uchaguzi huu zitakuwepo, na kweli zikiwepo. Uwepo wa hila za wazi kwenye chaguzi zetu ni jambo tulilolitarajia mara baada ya Magufuli kuwa rais wa nchi yetu. Magufuli hana mvuto wa kisiasa, na wala haziwezi na pia hataki siasa za ushindani. Rejea historia yake alipokuwa mbunge hajawahi kushinda kwa ushindani zaidi ya mara moja, mara zote alishinda kwa hila. Hivyo tabia yake binafsi ndio kahamishia kwenye chaguzi za nchi nzima.

Huo mwaka 2020 wapinzani wanaweza kuamua kushiriki huo ni uamuzi wao kama vyama, ila sisi wananchi tunaojitambua hatuko tayari kuendelea kushiriki chaguzi ambazo kura zetu haziheshimiwi. Ni vizuri kupata viongozi kwa njia ya kura kwani ni njia ya amani, lakini haimaanishi kuwa viongozi wote ni lazima wapatikane kwa njia ya kura. Tuko tayari kusubiri njia yenye haki ya kupata viongozi Magufuli atakapofika baada ya miaka 10, au tutumie short cut yenye madhara kama ya Kenya, lakini itakayoleta heshima katika box la kura.
 
Ona hawa wapumbavu
IMG-20191125-WA0097.jpeg
 
Kabla ya vyama vya upinzani kugomea sisi wengi tulishakosa hamasa na hilo ndio hasa waliloliona wapinzani,kwa hiyo hapa kikubwa ni hamasa kukosekana
 
Huko Lumumba hamkukubaliana nini cha kuposti leo?? Maccm wenzako wamesema wameshinda ushindi wa kisulisuli wewe unasema wapinzani wamegomea!
 
Bila shaka kuelekea uchaguzi mkuu 2020 mizengwe itafanywa tena na CCM kwa mgongo wa serikali. Kitakachofanyika ni kubadili mbinu au kuboresha mbinu ili kuwepo na utofauti na ile mizengwe iliyofanyika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Sasa swali langu liko hivi;
Je, endapo rafu ikapigwa tena UPINZANI utasusia uchaguzi mkuu wa 2020?
Na kama upinzani ukisusia hatma ya siasa za Tanzania zitakuwaje?
Mawazo yangu: Upinzani ukisusia hautapata hata jimbo moja na usiposusia pia hautapata hata jimbo moja. Hivyo basi vyama vya upinzani ni sharti vibadili mfumo wake wa uendeshaji haraka iwezekenavyo.
 
Huwezi kukiondoa madarakani chama kikongwe kama CCM kwa kulalamika kwenye vyombo vya habari, au kusubiri kigawanyike, unaweza kusubiri isiwe na kulalamika tu hakutoshi.

Hadi sasa hatuoni movement yeyote serious kuonyesha kweli mna nia ya kuingia ikulu, pamoja na operation Chadema ni msingi, kwa mfano, kuliko kuishia kufanya press conference pale Ufipa, mnaweza kuandaa makongamano ya kimataifa Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, mkaita vyombo mbalimbali vya ndani na nje, investors, mabalozi, mkaalika known public speakers ikiwezekana kutoka nje, mkatumia fursa hiyo kueleza sera zenu na jinsi mtakavyozitekeleza mtakapochukua madaraka. Huo ni mkakati mmoja tu wa kujitangaza ndani na nje mkaaminika, kwa dunia ya leo huwezi kushinda urais bila support ya nje. Hatuoni mkifanya hivyo.

Sioni mkakati wa kuunganisha nguvu, nilisikia wapinzani wameanzisha Azimio la Zanzibar sijui limeishia wapi, nchini Kenya haikuwa kazi rahisi kuiondoa KANU, vyama vya upinzani viliungana baadhi ya viongozi wao wali sacrifice vyeo vyao.

Siyo lazima muweke wazi mikakati yote lkn angalau wapiga kura waanze kuona mwelekeo wa chama towards 2020, siyo mbali, ikiwezekana wamjue mshika kibendera siyo waje kushitukizwa dakika za mwisho kama mlivyofanya kwenye uchaguzi uliopita.

Kushinda uchaguzi ni zaidi ya sanduku la kura, ingekuwa sanduku leo Lowassa angekuwa rais kwa sababu naimani alipata kura nyingi zaidi ya Rais Magufuli na Self leo angekuwa rais wa Zanzibar, sanduku la kura ni kitendo cha kuhalalisha (legitimise) mikakati yako uliyofanya kabla, ya halali na isiyo halali.

If you don't plan you are planning to fail.

Ushauri mzuri inagwa siku hizi kufanya mikutano kama hiyo kiwazo kikubwa ni jeshi letu la polisi ambalo limegeuka jeshi la chama
 
Back
Top Bottom