CHADEMA mna mikakati gani serious ya kushinda uchaguzi 2020?

Huu uchaguzi gani amabo hata CCM wenyewe wameogopa kuchaguliwa? Yaani unachafua halafu unaanika badala ya kufua?1 Hata enzi ya chama kimoja kulikuwa na uchaguzi na mtu alikuwa anajitathmini kakubalika asilimia ngapi, sasa awamu hii imefanya upumbavu halafu mnasema uchaguzi? Lyatonga ameshiriki na ni kibaraka nae mbona analia uikteta? NDIO TUTAGOMA 2020 kama upumbavu utakuwa huu kwani kuna tatizo?
 
Pemba inaongozwa na CCM tupu kwani imegeuka Hong Kong?
 

Ni vyema unapoleta uzi ujitahidi kupunguza propaganda za kijinga. Kwanza wapinzani walitangaza watashiriki uchaguzi, ila kilichowafanya wasusie uchaguzi ni rafu za wazi. Pia wananchi wengi hasa tunaopigia kura upinzani tuligoma kujiandikisha kwa sababu tulijua hila kwenye uchaguzi huu zitakuwepo, na kweli zikiwepo. Uwepo wa hila za wazi kwenye chaguzi zetu ni jambo tulilolitarajia mara baada ya Magufuli kuwa rais wa nchi yetu. Magufuli hana mvuto wa kisiasa, na wala haziwezi na pia hataki siasa za ushindani. Rejea historia yake alipokuwa mbunge hajawahi kushinda kwa ushindani zaidi ya mara moja, mara zote alishinda kwa hila. Hivyo tabia yake binafsi ndio kahamishia kwenye chaguzi za nchi nzima.

Huo mwaka 2020 wapinzani wanaweza kuamua kushiriki huo ni uamuzi wao kama vyama, ila sisi wananchi tunaojitambua hatuko tayari kuendelea kushiriki chaguzi ambazo kura zetu haziheshimiwi. Ni vizuri kupata viongozi kwa njia ya kura kwani ni njia ya amani, lakini haimaanishi kuwa viongozi wote ni lazima wapatikane kwa njia ya kura. Tuko tayari kusubiri njia yenye haki ya kupata viongozi Magufuli atakapofika baada ya miaka 10, au tutumie short cut yenye madhara kama ya Kenya, lakini itakayoleta heshima katika box la kura.
 
Kabla ya vyama vya upinzani kugomea sisi wengi tulishakosa hamasa na hilo ndio hasa waliloliona wapinzani,kwa hiyo hapa kikubwa ni hamasa kukosekana
 
Huko Lumumba hamkukubaliana nini cha kuposti leo?? Maccm wenzako wamesema wameshinda ushindi wa kisulisuli wewe unasema wapinzani wamegomea!
 
Bila shaka kuelekea uchaguzi mkuu 2020 mizengwe itafanywa tena na CCM kwa mgongo wa serikali. Kitakachofanyika ni kubadili mbinu au kuboresha mbinu ili kuwepo na utofauti na ile mizengwe iliyofanyika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Sasa swali langu liko hivi;
Je, endapo rafu ikapigwa tena UPINZANI utasusia uchaguzi mkuu wa 2020?
Na kama upinzani ukisusia hatma ya siasa za Tanzania zitakuwaje?
Mawazo yangu: Upinzani ukisusia hautapata hata jimbo moja na usiposusia pia hautapata hata jimbo moja. Hivyo basi vyama vya upinzani ni sharti vibadili mfumo wake wa uendeshaji haraka iwezekenavyo.
 

Ushauri mzuri inagwa siku hizi kufanya mikutano kama hiyo kiwazo kikubwa ni jeshi letu la polisi ambalo limegeuka jeshi la chama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…