CHADEMA na Askofu Mwamakula acheni kuchapisha mitandaoni habari za uongo

CHADEMA na Askofu Mwamakula acheni kuchapisha mitandaoni habari za uongo

Inasikitisha sana kuona huyu Askofu wa CHADEMA, ndugu Mwamakula pamoja na chama chake wakipost mara kwa mara habari za uongo ili mradi kuishambulia CCM. Wakikamatwa na kufunguliwa mashtaka watamlaumu mtu?

Jana Askofu wa CHADEMA kazusha kuwa Rais Samia kahojiwa na THE REPORTER KE na kujibu jinsi alivyojibu kitu ambacho sio kweli. Rais hajahojiwa na media yoyote. Na hata kama angehojiwa isingekuwa media ya vichochoroni kama aliyoitaja Askofu wa CHADEMA. Huyu askofu tumpuuze.

CHADEMA nao wanadai Rais Hichilema wa Zambia kapigwa mawe kwa sababu alihudhuria kuapishwa kwa Rais Samia. Huu ni uongo mkubwa. Waliompiga mawe Hichilema ni wachimbaji wadogo wa madini huko Chingola, Copperbelt Province. Sababu ni mgogoro unaohusu madini. Wachimbaji wadogo wanataka warudishiwe baadhi ya maeneo.

Askofu wa CHADEMA na chama chako acheni huo upuuzi wa kueneza chuki bila sababu.
Chadema ni kiwanda cha uzushi na uongo
 
Back
Top Bottom