CHADEMA na CUF waungana kipinga nyongeza ya posho bunge la katiba

Dr Slaa hajui kama Joshua Nasari ni Mbunge wa chadema ambae nae anataka nyongeza ya posho
 

He huyu Slaa anapingana na mwenye chama! Ni muhaini huyu! Mwenyewe kasema posho ni ndogo na maisha ya Dodoma ni magumu! Ha!
 

Slaa ana siasa za ulaghai sana huyu mzee. Ni nini kitamtenga na dhambi jamani!?
 
akili yako imemezwa na posho kiasi hujui kama hiyo kamati sio wote wanaunga mkono posho, haya mama jipange watawaongezea
Hili suala la posho litasumbua sana kwa kuwa wengi wa wale wajumbe 201 walioteuliwa na Rais ni "apeche, alolo", hohehahe, hawana mbele wala nyuma.

Hata hao wachache wenye ukwasi na ajira za uhakika kwenye kundi hili la wajumbe 201 pato lao halikaribiani kabisa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri hii na wenzao wa Baraza la Wawakilishi. Tofauti hii peke yake ni ugomvi tosha.

Wabunge na Wawakilishi wanakula na kulala kwenye mahoteli. Wengi wa hawa 201 wamepangiwa kwenye vigesti huku jambo lililowapeleka Dodoma ni zito na laKIHSTORIA kwelikweli. Hivi kweli Bunge la Katiba linahitaji siku 70? Za nini hasa wakati watabadili mambo machache sana!

Tulihitaji Wajumbe zaidi ya 600? Hatua hii ya Bunge la Katiba ilihitajika? Mbona mwaka 1977 halikuwepo na Katiba tunayo?
 
Unafiki wa wanasiasa Dr.W.Slaa acha unafika usirukie ili jambo anza kwanza na wabunge wako bungeni kila siku wanachukua posho.

siyo lazima upinge kila kitu cha Dr. Slaa. Utaifa kwanza vyama baadae, hapa swala ni katiba ya nchi na siyo lingine lolote.
 
Last edited by a moderator:
 
Mleta mada analeta ushabiki wa vyama kwenye jambo la msingi. Lukuvi hataki posho iongezwe na ndiyo maana alipoteuliwa wanafiki walimpinga wakijua fika nyongeza ni ndoto. Mbowe pia hatakubaliana na hilo. Kamati nzima iliyoteuliwa sioni wa kukubali nyongeza ya posho labda walogwe.
 
Unafiki wa wanasiasa Dr.W.Slaa acha unafika usirukie ili jambo anza kwanza na wabunge wako bungeni kila siku wanachukua posho.

unawaza kwa kutumia nini?? Inamana kwako hakuna jambo la kheri??
 
Last edited by a moderator:
CHADEMA wajanja sana. Wakati ule Mh Zitto anang'ang'ana posho hizi zifutwe walijidai kumuunga mkono. Tujiulize waliishia wapi? Mbowe alirudisha gari la KUB? Alikataa milioni mbili ya KUB ya kila mwezi?

Wasaidieni hawa wajumbe 201 nao angalau kwa siku hizi 70 wafanane na Wabunge wetu. Hela ya kugharamia SIASA haijawahi kuwa tatizo nchi hii.
 
Dr Slaa hajui kama Joshua Nasari ni Mbunge wa chadema ambae nae anataka nyongeza ya posho

Huo ni upotoshaji ndugu,Nasari alishafafanua juu ya jambo hilo.Tafuta uzi wake uko humu,amesema posho ya laki 3 ni kubwa. Hao watu wa gazeti la Nipashe walidanganya.
 
Tamko zuri asiyetaka jibu ni rahisi tu aondoke wala asijitese kukaa Dodoma ARUDI NYYUMBANI KWA MKEWE,MUMEWE AU WANAWE awaache ambao wako tayari kufanya kazi kwa ajili ya Taifa na siyo matumbo yao na ulafi uliokithiri
 
Bora umemjibu huyo wengine wanarukaruka tu humu ndani
hawaangalii uzi ambazo watu wamezitoa mwanzo
huo ni upotoshaji ndugu,nasari alishafafanua juu ya jambo hilo.tafuta uzi wake uko humu,amesema posho ya laki 3 ni kubwa. Hao watu wa gazeti la nipashe walidanganya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…