CHADEMA na CUF waungana kipinga nyongeza ya posho bunge la katiba

CHADEMA na CUF waungana kipinga nyongeza ya posho bunge la katiba

Dr Slaa hajui kama Joshua Nasari ni Mbunge wa chadema ambae nae anataka nyongeza ya posho
 
Baadhi ya vyama vya siasa, wanaharakati na wananchi wa kawaida wameshangazwa na maombi hayo ya posho, wakisema wajumbe wamesahau kilichowapeleka bungeni na kukimbilia kutetea masilahi yao.

Vyama vya Chadema na CUF kwa nyakati tofauti, vilisema kuwa vitaanzisha juhudi za kuwataka wabunge wao ambao ni wajumbe wasusie agenda yoyote inayotaka kuongezwa kwa posho hizo.

Tamko la vyama hivyo limetolewa huku Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho wajumbe wake ndio wanaodaiwa kupigia debe mpango huo, kikisema kitatoa ufafanuzi juu ya hoja hizo baada ya kupata ‘taarifa rasmi’.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema jana kuwa wajumbe hao hawakupaswa kudai nyongeza ya posho kwa vile hawakutumwa kwenda Dodoma kudai marupurupu ya fedha.

Alisema kuanza kujadili suala la nyongeza ya posho badala ya kuzungumzia hoja za msingi zilizopo kwenye Rasimu ya Katiba, ni sawa na kuwapuuza wananchi ambao wanasubiri kupata Katiba Mpya.

“Wametoka kwenye hoja na kutupeleka kwenye mambo mengine ambayo hayana msingi wowote. Sisi kama Chadema tunapinga na tunataka wabunge wetu watambue hilo,” alisema.

Alisema wale wanaolalamika kwamba Sh300, 000 hazitoshi wanajaribu kupindisha ukweli, kwani kuna baadhi ya watumishi wa Serikali wanalipwa kiasi hicho ikiwa ni mshahara wao wa kila mwezi.

Alisema Chadema kimewataka wabunge wake kutojiingiza kwenye malalamiko hayo badala yake wazingatie kile walichotumwa na wananchi kwenda Dodoma.

He huyu Slaa anapingana na mwenye chama! Ni muhaini huyu! Mwenyewe kasema posho ni ndogo na maisha ya Dodoma ni magumu! Ha!
 
Acheni Unafiki, Mbowe yumo kwenye Kamati ya wanaodai Posho pamoja na kina Lukuvi halafu mnasema Eti CUF na Chadema wanaipinga? Au mbowe mshamvua uanachama? Nassari nae yupo CCM? angalau Zitto pekee hata kama mnafiki amejitofautisha na wengine kwa kusema hata ikiongezwa hatoichukua, Kama Chadema na CUF mnayoongea yanatoka kwenye Mioyo yenu tangazeni kutochukua nyongeza ikiongezeka.

Slaa ana siasa za ulaghai sana huyu mzee. Ni nini kitamtenga na dhambi jamani!?
 
akili yako imemezwa na posho kiasi hujui kama hiyo kamati sio wote wanaunga mkono posho, haya mama jipange watawaongezea
Hili suala la posho litasumbua sana kwa kuwa wengi wa wale wajumbe 201 walioteuliwa na Rais ni "apeche, alolo", hohehahe, hawana mbele wala nyuma.

Hata hao wachache wenye ukwasi na ajira za uhakika kwenye kundi hili la wajumbe 201 pato lao halikaribiani kabisa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri hii na wenzao wa Baraza la Wawakilishi. Tofauti hii peke yake ni ugomvi tosha.

Wabunge na Wawakilishi wanakula na kulala kwenye mahoteli. Wengi wa hawa 201 wamepangiwa kwenye vigesti huku jambo lililowapeleka Dodoma ni zito na laKIHSTORIA kwelikweli. Hivi kweli Bunge la Katiba linahitaji siku 70? Za nini hasa wakati watabadili mambo machache sana!

Tulihitaji Wajumbe zaidi ya 600? Hatua hii ya Bunge la Katiba ilihitajika? Mbona mwaka 1977 halikuwepo na Katiba tunayo?
 
Unafiki wa wanasiasa Dr.W.Slaa acha unafika usirukie ili jambo anza kwanza na wabunge wako bungeni kila siku wanachukua posho.

siyo lazima upinge kila kitu cha Dr. Slaa. Utaifa kwanza vyama baadae, hapa swala ni katiba ya nchi na siyo lingine lolote.
 
Last edited by a moderator:
Acheni Unafiki, Mbowe yumo kwenye Kamati ya wanaodai Posho pamoja na kina Lukuvi halafu mnasema Eti CUF na Chadema wanaipinga? Au mbowe mshamvua uanachama? Nassari nae yupo CCM? angalau Zitto pekee hata kama mnafiki amejitofautisha na wengine kwa kusema hata ikiongezwa hatoichukua, Kama Chadema na CUF mnayoongea yanatoka kwenye Mioyo yenu tangazeni kutochukua nyongeza ikiongezeka.[/U OTE
Napata shida kuelewa kama kilichoandikwa ingawa nikiswahili umeelewa?Au ndio akiliyenu maCcm yakuazima kwawatu? Umeambiwa katibu mkuu wa Cdm ametoa tamko kama msimamo wa chama na kama mtendaji mkuu wa chama alafu wewe unaleta hangover za matap tap hapa!
 
Mleta mada analeta ushabiki wa vyama kwenye jambo la msingi. Lukuvi hataki posho iongezwe na ndiyo maana alipoteuliwa wanafiki walimpinga wakijua fika nyongeza ni ndoto. Mbowe pia hatakubaliana na hilo. Kamati nzima iliyoteuliwa sioni wa kukubali nyongeza ya posho labda walogwe.
 
Unafiki wa wanasiasa Dr.W.Slaa acha unafika usirukie ili jambo anza kwanza na wabunge wako bungeni kila siku wanachukua posho.

unawaza kwa kutumia nini?? Inamana kwako hakuna jambo la kheri??
 
Last edited by a moderator:
CHADEMA wajanja sana. Wakati ule Mh Zitto anang'ang'ana posho hizi zifutwe walijidai kumuunga mkono. Tujiulize waliishia wapi? Mbowe alirudisha gari la KUB? Alikataa milioni mbili ya KUB ya kila mwezi?

Wasaidieni hawa wajumbe 201 nao angalau kwa siku hizi 70 wafanane na Wabunge wetu. Hela ya kugharamia SIASA haijawahi kuwa tatizo nchi hii.
 
Dr Slaa hajui kama Joshua Nasari ni Mbunge wa chadema ambae nae anataka nyongeza ya posho

Huo ni upotoshaji ndugu,Nasari alishafafanua juu ya jambo hilo.Tafuta uzi wake uko humu,amesema posho ya laki 3 ni kubwa. Hao watu wa gazeti la Nipashe walidanganya.
 
Tamko zuri asiyetaka jibu ni rahisi tu aondoke wala asijitese kukaa Dodoma ARUDI NYYUMBANI KWA MKEWE,MUMEWE AU WANAWE awaache ambao wako tayari kufanya kazi kwa ajili ya Taifa na siyo matumbo yao na ulafi uliokithiri
 
Bora umemjibu huyo wengine wanarukaruka tu humu ndani
hawaangalii uzi ambazo watu wamezitoa mwanzo
huo ni upotoshaji ndugu,nasari alishafafanua juu ya jambo hilo.tafuta uzi wake uko humu,amesema posho ya laki 3 ni kubwa. Hao watu wa gazeti la nipashe walidanganya.
 
Back
Top Bottom