CHADEMA ni wakandamizaji wa Uhuru wa maoni na kujieleza kwa watu. Hawana tofauti na CCM

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo!

CHADEMA wengi wao wanatabia ya udikteta uchwara, ukandamizaji wa uhuru wa maoni hasa yanayokinzana na sera zao.

CHADEMA wanauwezo wa kuingilia uhuru binafsi wa mtu mwingine hata kama havunji sheria za chama, katiba ya nchi na maadili.

Ukitaka ugombane na CHADEMA basi pinga au kosoa sera au jambo lolote unaloliona halipo sawa Kimtazamo wako.

Ni tabia mbaya sana. Ni zilezile tabia za kiccm wanazozilalamikia. Tofauti ni kuwa CCM wanadola alafu upande wa Pili hawana.

Sisi Watibeli tunazingatia sana haki za watu hata kama tunatofautiana mawazo na falsafa.

CHADEMA hupenda wao tuu ndio waongee kumaanisha wao tuu ndio wasikilizwe.

Ukimkosoa kiongozi wa CHADEMA Kama wao wanavyokosoa viongozi wa vyama vingine. Inakuwa nongwa.

Sio lazima chama chote kimchukie mtu mmoja. Sio lazima. Sio lazima wanachama wote wampende kiongozi fulani. Sio lazima.

Kupenda mtu ni haki ya mtu iliyo ndani ya hiyari yake.

Humu mnaweza kunipenda Mtibeli au msinipende. Hilo lipo ndani ya mipaka yenu. Sio mimi nijisikie vibaya au niwalazimishe mnipende. Huo ni ukatili.
Au wanaonipenda watake kuwalazimisha wasionipenda wanipende. Huo ni ushenzi.

Haina tofauti na mtu anayelazimisha Salamu. Kusalimia ni hiyari ya mtu. Ipo ndani ya uhuru wake.

Mtu kutoa Salamu za Rambirambi kwenye msiba ni hiyari yake.

Mtu kumsamehe mtu mwingine sio lazima ni hiyari yake.

Usishangae siku Tundu Lisu akiamua kusamehe waliompiga Risasi alafu ukaona baadhi ya watu wakachukia, wakamkasirikie wakamuona Msaliti.

Sisi Watibeli hatuumizwi na maamuzi ya mtu mwingine ambayo yapo ndani ya mipaka yake na Hayagusi mipaka yetu.

Hofu yangu ni hii, tabia za kiccm naziona pia huko CHADEMA.
Usitoe kibanzi jichoni mwa mwenzako wakati wewe unaboriti.

Tabia za kiccm, inaletwa hoja na upinzani. Wafuasi wa CCM wanajibu ninyi vibaraka wa wazungu, sijui blah blah.

Wanaccm nao wakileta hoja, wafuasi wa chadema utasikia buku 7 sijui blah blah blah.

Mwanaccm akikosoa chama chake. Anaandamwa na CCM wenzake ikiwezekani kufukuzwa kabisa uanachama.

Mwanachadema akikosoa chadema au viongozi wa chadema, wanachadema wanaanza kelele na kumuita msaliti na majina mengine.

Hatutaki vyama vinavyotaka kusifiwa na kupongezwa tuu. Tunataka vyama ambavyo wanachama wake watakuwa huru kukosoa na kusifia bila kuletewa fujo.

Nimemaliza

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kinachopigiwa kelele ni hila ya mtoa maoni, sio maoni ta mtu. Chadema inapambana na hila za watu wake, wala sio maoni yao. Ukitoa maoni ambayo wanaona wazi kuna hila nyuma yake lazima upigwe spana. 😊

🫢🫢😆😆😄

Hao policcm wakifanya hivyo kosa lao linakuwa wapi?

Acheni tabia za ajabu.
Hila ya mtu unaipataje kwenye maoni yake?
 
Hamjambo!

CHADEMA wengi wao wanatabia ya udikteta uchwara, ukandamizaji wa uhuru wa maoni hasa yanayokinzana na sera zao.

CHADEMA wanauwezo wa kuingilia uhuru binafsi wa mtu mwingine hata kama havunji sheria za chama, katiba ya nchi na maadili.

Ukitaka ugombane na CHADEMA basi pinga au kosoa sera au jambo lolote unaloliona halipo sawa Kimtazamo wako.

Ni tabia mbaya sana. Ni zilezile tabia za kiccm wanazozilalamikia. Tofauti ni kuwa CCM wanadola alafu upande wa Pili hawana.

Sisi Watibeli tunazingatia sana haki za watu hata kama tunatofautiana mawazo na falsafa.

CHADEMA hupenda wao tuu ndio waongee kumaanisha wao tuu ndio wasikilizwe.

Ukimkosoa kiongozi wa CHADEMA Kama wao wanavyokosoa viongozi wa vyama vingine. Inakuwa nongwa.

Sio lazima chama chote kimchukie mtu mmoja. Sio lazima. Sio lazima wanachama wote wampende kiongozi fulani. Sio lazima.

Kupenda mtu ni haki ya mtu iliyo ndani ya hiyari yake.

Humu mnaweza kunipenda Mtibeli au msinipende. Hilo lipo ndani ya mipaka yenu. Sio mimi nijisikie vibaya au niwalazimishe mnipende. Huo ni ukatili.
Au wanaonipenda watake kuwalazimisha wasionipenda wanipende. Huo ni ushenzi.

Haina tofauti na mtu anayelazimisha Salamu. Kusalimia ni hiyari ya mtu. Ipo ndani ya uhuru wake.

Mtu kutoa Salamu za Rambirambi kwenye msiba ni hiyari yake.

Mtu kumsamehe mtu mwingine sio lazima ni hiyari yake.

Usishangae siku Tundu Lisu akiamua kusamehe waliompiga Risasi alafu ukaona baadhi ya watu wakachukia, wakamkasirikie wakamuona Msaliti.

Sisi Watibeli hatuumizwi na maamuzi ya mtu mwingine ambayo yapo ndani ya mipaka yake na Hayagusi mipaka yetu.

Hofu yangu ni hii, tabia za kiccm naziona pia huko CHADEMA.
Usitoe kibanzi jichoni mwa mwenzako wakati wewe unaboriti.

Tabia za kiccm, inaletwa hoja na upinzani. Wafuasi wa CCM wanajibu ninyi vibaraka wa wazungu, sijui blah blah.

Wanaccm nao wakileta hoja, wafuasi wa chadema utasikia buku 7 sijui blah blah blah.

Mwanaccm akikosoa chama chake. Anaandamwa na CCM wenzake ikiwezekani kufukuzwa kabisa uanachama.

Mwanachadema akikosoa chadema au viongozi wa chadema, wanachadema wanaanza kelele na kumuita msaliti na majina mengine.

Hatutaki vyama vinavyotaka kusifiwa na kupongezwa tuu. Tunataka vyama ambavyo wanachama wake watakuwa huru kukosoa na kusifia bila kuletewa fujo.

Nimemaliza

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Kama unayaelewa mazingira ambayo chadema wana-operate kisiasa..huwezi walinganisha na ccm kwenye mizani yenye vigezo vinavyofanana..
 
Hapa nakubaliana nawe 100%.

Nina mashaka siku ikitokea Chadema wakaingia ikulu, kisha mmoja wa viongozi wao apewe tuhuma zozote, ukihoji tu, basi nao wanaweza kuunda makundi ya wasiojulikana waanze kutuwinda mitaani.
 
Chadema ni chama Cha Watanzania wote ambao wamekandamizwa na CCM na kujikuta wakilazimika kuishi bila kutumia ubongo wao na elimu zao

Je, wewe ni miongoni mwao?

Mtu mnafiki anapokuwa Chadema, hujulikana na kubainika mapema mno kwa sababu ubongo wa watu kwenye chama hiko ni ruksa kuutumia

Wewe unachosema, ni kile kile ambacho kwako wewe unaona ni kama kukandamiza mawazo na kubinya uhuru wa watu ilihali Chadema ingali bado inapambana na mambo mengi sana!
 
Hamjambo!

CHADEMA wengi wao wanatabia ya udikteta uchwara, ukandamizaji wa uhuru wa maoni hasa yanayokinzana na sera zao.

CHADEMA wanauwezo wa kuingilia uhuru binafsi wa mtu mwingine hata kama havunji sheria za chama, katiba ya nchi na maadili.

Ukitaka ugombane na CHADEMA basi pinga au kosoa sera au jambo lolote unaloliona halipo sawa Kimtazamo wako.

Ni tabia mbaya sana. Ni zilezile tabia za kiccm wanazozilalamikia. Tofauti ni kuwa CCM wanadola alafu upande wa Pili hawana.

Sisi Watibeli tunazingatia sana haki za watu hata kama tunatofautiana mawazo na falsafa.

CHADEMA hupenda wao tuu ndio waongee kumaanisha wao tuu ndio wasikilizwe.

Ukimkosoa kiongozi wa CHADEMA Kama wao wanavyokosoa viongozi wa vyama vingine. Inakuwa nongwa.

Sio lazima chama chote kimchukie mtu mmoja. Sio lazima. Sio lazima wanachama wote wampende kiongozi fulani. Sio lazima.

Kupenda mtu ni haki ya mtu iliyo ndani ya hiyari yake.

Humu mnaweza kunipenda Mtibeli au msinipende. Hilo lipo ndani ya mipaka yenu. Sio mimi nijisikie vibaya au niwalazimishe mnipende. Huo ni ukatili.
Au wanaonipenda watake kuwalazimisha wasionipenda wanipende. Huo ni ushenzi.

Haina tofauti na mtu anayelazimisha Salamu. Kusalimia ni hiyari ya mtu. Ipo ndani ya uhuru wake.

Mtu kutoa Salamu za Rambirambi kwenye msiba ni hiyari yake.

Mtu kumsamehe mtu mwingine sio lazima ni hiyari yake.

Usishangae siku Tundu Lisu akiamua kusamehe waliompiga Risasi alafu ukaona baadhi ya watu wakachukia, wakamkasirikie wakamuona Msaliti.

Sisi Watibeli hatuumizwi na maamuzi ya mtu mwingine ambayo yapo ndani ya mipaka yake na Hayagusi mipaka yetu.

Hofu yangu ni hii, tabia za kiccm naziona pia huko CHADEMA.
Usitoe kibanzi jichoni mwa mwenzako wakati wewe unaboriti.

Tabia za kiccm, inaletwa hoja na upinzani. Wafuasi wa CCM wanajibu ninyi vibaraka wa wazungu, sijui blah blah.

Wanaccm nao wakileta hoja, wafuasi wa chadema utasikia buku 7 sijui blah blah blah.

Mwanaccm akikosoa chama chake. Anaandamwa na CCM wenzake ikiwezekani kufukuzwa kabisa uanachama.

Mwanachadema akikosoa chadema au viongozi wa chadema, wanachadema wanaanza kelele na kumuita msaliti na majina mengine.

Hatutaki vyama vinavyotaka kusifiwa na kupongezwa tuu. Tunataka vyama ambavyo wanachama wake watakuwa huru kukosoa na kusifia bila kuletewa fujo.

Nimemaliza

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Hata jf tu kuna rule zake, kama unataka ujue jaribu kumtukana maxme. Halafu utaoaona kama kila kitu hakina mipaka yake
 
Chadema ni chama Cha Watanzania wote ambao wamekandamizwa na CCM na kujikuta wakilazimika kuishi bila kutumia ubongo wao na elimu zao

Je, wewe ni miongoni mwao?

Mtu mnafiki anapokuwa Chadema, hujulikana na kubainika mapema mno kwa sababu ubongo wa watu kwenye chama hiko ni ruksa kuutumia

Wewe unachosema, ni kile kile ambacho kwako wewe unaona ni kama kukandamiza mawazo na kubinya uhuru wa watu ilihali Chadema ingali inapbana na mambo mengi sana
Kipindi cha sakata la mbowe kulamba asali, chadema walikua wakali sana 😁
 
Naona watetezi wa Lema mnakuja mbio mbio kisa ni wa kaskazini mwenzenu?
Lema alitakiwa kujibu kuhusu Passport yake alipataje, na sio kumuingiza Heche, Heche wakati wake ungefika na angeulizwa kuhusu passport yake kaipataje.
Hilo la kuingiza mtu mwingine ndipo watu walipopata mushkeli huyo nabii uchwaraa.
 
Mwanazuoni kama wewe ilitakiwa uwe unajua kutofautisha CHADEMA na wanachadema, na washabiki wengineo. Mambo yanafanywa na mashabiki ila unakuja kuchambua taasisi.

Tukiingia kwenye suala la salamu za rambirambi ni kweli ni hiyari ya mtu, lakini kufanya personification ili kuelezea hisia zako nayo inakuwa sio sawa, yeye angetoa salamu zake kisha msemaji wa Chama au kutokana na protokali yao aliyepaswa kupeleka salamu kuwakilisha chama angefanya hivyo. Sasa kuvunja kwake itifaki inaonekana kuna la zaidi yaani ametaka aonekane na kujiweka yeye mbele na anajali kuzidi?

Ila kubwa kuliko yote hatupaswi kutazama hayo, inapaswa tutazame sababu za hizi hasira za watu zimekujaje?
 
Kinachopigiwa kelele ni hila ya mtoa maoni, sio maoni ta mtu. Chadema inapambana na hila za watu wake, wala sio maoni yao.
My kaka, ngoja niplay "devil's advocate" kidogo.
Ukitoa maoni ambayo wanaona wazi kuna hila nyuma yake lazima upigwe spana. 😊
Ukisema "maoni ambayo wanaona wazi kuna hila nyuma yake" unamaanisha ni nani akiona? ni akina nani ambao wana mandate ya kuamua maoni haya au kukosolewa huku kuna hila nyuma yake?

Je huyo mtu anayeona au kuamua nini kina hila akikosea na akakosolewa, mizani gani itatumika kuamua kama hayo maoni dhidi yake ni legit?
 
Hata jf tu kuna rule zake, kama unataka ujue jaribu kumtukana maxme. Halafu utaoaona kama kila kitu hakina mipaka yake

Kwa nini umtukane?
Akikosea kwa nini asikosolewe?

Hujaona ni mara ngapi humu watu wanakosoa masuala ya Nyuzi kuunganishwa na mambo mengine?

Kwani wewe unashindwa kutofautisha ukosoaji na utukanaji?
 
Back
Top Bottom