CHADEMA ni wakandamizaji wa Uhuru wa maoni na kujieleza kwa watu. Hawana tofauti na CCM

CHADEMA ni wakandamizaji wa Uhuru wa maoni na kujieleza kwa watu. Hawana tofauti na CCM

Chadema ni chama Cha Watanzania wote ambao wamekandamizwa na CCM na kujikuta wakilazimika kuishi bila kutumia ubongo wao na elimu zao

Je, wewe ni miongoni mwao?

Mtu mnafiki anapokuwa Chadema, hujulikana na kubainika mapema mno kwa sababu ubongo wa watu kwenye chama hiko ni ruksa kuutumia

Wewe unachosema, ni kile kile ambacho kwako wewe unaona ni kama kukandamiza mawazo na kubinya uhuru wa watu ilihali Chadema ingali bado inapambana na mambo mengi sana!

Vyama vyote vinasema hilohilo kwamba vipo kwaajili ya kupigania Watanzania. Hiyo ni siasa.

Ninachokisema ni ile tabia ya vyama kikiwemo Chadema kuwa na tabia ya kukataa ukosoaji na kuwachukulia wakosoaji kama maadui au ccm kumbe wengine hata huo muda wa vyama hawana
 
Hapa nakubaliana nawe 100%.

Nina mashaka siku ikitokea Chadema wakaingia ikulu, kisha mmoja wa viongozi wao apewe tuhuma zozote, ukihoji tu, basi nao wanaweza kuunda makundi ya wasiojulikana waanze kutuwinda mitaani.

Tutawindana humu sio poah!

Sio lazima watu wakubaliane mawazo.
Uhuru wa maoni ni kutofautiana kimawazo bila kuathiri haki na utu wa watu wengine.
 
Kama unayaelewa mazingira ambayo chadema wana-operate kisiasa..huwezi walinganisha na ccm kwenye mizani yenye vigezo vinavyofanana..

Naangalia sera ya uhuru wa maoni. Ambayo ni moja ya mambo yanayopiganiwa na CHADEMA. Pia ni moja ya Aspect za Democrasia.

Unasema watu wawe huru kuongea alafu muda huo unawazuia wanaokukosoa
 
Mwanazuoni kama wewe ilitakiwa uwe unajua kutofautisha CHADEMA na wanachadema, na washabiki wengineo. Mambo yanafanywa na mashabiki ila unakuja kuchambua taasisi.

Tukiingia kwenye suala la salamu za rambirambi ni kweli ni hiyari ya mtu, lakini kufanya personification ili kuelezea hisia zako nayo inakuwa sio sawa, yeye angetoa salamu zake kisha msemaji wa Chama au kutokana na protokali yao aliyepaswa kupeleka salamu kuwakilisha chama angefanya hivyo. Sasa kuvunja kwake itifaki inaonekana kuna la zaidi yaani ametaka aonekane na kujiweka yeye mbele na anajali kuzidi?

Ila kubwa kuliko yote hatupaswi kutazama hayo, inapaswa tutazame sababu za hizi hasira za watu zimekujaje?

Uhuru wa maoni unaenda sambamba na uvumilivu wa wanaosikiliza.

Lema na kauli zake ni mfano mmoja kati ya mingi.
Watanzania lazima tujifunze kuheshimu maoni na mitazamo ya watu wengine hata kama tunatofautiana nayo.
 
My kaka, ngoja niplay "devil's advocate" kidogo.

Ukisema "maoni ambayo wanaona wazi kuna hila nyuma yake" unamaanisha ni nani akiona? ni akina ambao wana mandate ya kuamua maoni haya au kukosolewa huku kuna hila nyuma yake?

Je huyo mtu anayeona au kuamua nini kina hila akikosea na akakosolewa, mizani gani itatumika kuamua kama hayo maoni dhidi yake ni legit?

Kuna maoni ambayo yamezua mjadala na mashambulizi kwa mtoa maoni, ndiyo mtoa mada anayoyaongelea. Sio kila maoni yanapigwa,. Maoni yenye muelekeo wa "hila" au yenye kuonyesha wazi yana kitu nyuma yake, lazima yatakutana na mashambulizi. Kutoa maoni ni "two way traffic", unayatoa na watu wanayapima na ikowezekana kuya "challenge". Sasa maoni ya mtu yanapokutana na challenge isionekane kama ni ukandamizaji au udikteta.

Kama ukotoa maoni na watu wakaona kuna namna, watatumia pia uhuru huo huo kuku challenge.
 
Nilishasema CCM imeoza lakini CHADEMA sio mbadala wake, CHADEMA ni zaidi ya Ccm kwenye kutokuvumilia maoni tofauti.

Hii reforms tunazotaka kuzifanya lazima zionekane pande zote.

Mimi namkubali Tundu Lisu lakini haimaanishi kwamba nitakubaliana na mambo yake yote.

Au kuna watu humu wananikubali lakini hiyo haimaanishi watakubaliana na kila kitu changu.

Na hilo ni muhimu kulijua na kuliheshimu.

Sasa mtu anaikubali CHADEMA lakini ikitokea hakubaliani na jambo fulani inakuwa nongwa. Anarushiwa matusi na kejeli.

Hilo lipo hata kwenye mambo ya Dini.
 
CCM ni chama cha hivyo kabisa lakini ukiangalia chadema unavyo endesha mambo yake utagundua chadema na ya hovyo mara 10 ya CCM.

Wote wapo kwenye Kapu moja.

Angalia hata mambo ya uchaguzi.
Juzi walikuwa na uchaguzi hapa, wapo waliokimbilia CCM kisa kushindwa uchaguzi.
Wapo waliohamia CHAUMMA.
Yaani mambo ni yaleyale.
 
Hamjambo!

CHADEMA wengi wao wanatabia ya udikteta uchwara, ukandamizaji wa uhuru wa maoni hasa yanayokinzana na sera zao.

CHADEMA wanauwezo wa kuingilia uhuru binafsi wa mtu mwingine hata kama havunji sheria za chama, katiba ya nchi na maadili.

Ukitaka ugombane na CHADEMA basi pinga au kosoa sera au jambo lolote unaloliona halipo sawa Kimtazamo wako.

Ni tabia mbaya sana. Ni zilezile tabia za kiccm wanazozilalamikia. Tofauti ni kuwa CCM wanadola alafu upande wa Pili hawana.

Sisi Watibeli tunazingatia sana haki za watu hata kama tunatofautiana mawazo na falsafa.

CHADEMA hupenda wao tuu ndio waongee kumaanisha wao tuu ndio wasikilizwe.

Ukimkosoa kiongozi wa CHADEMA Kama wao wanavyokosoa viongozi wa vyama vingine. Inakuwa nongwa.

Sio lazima chama chote kimchukie mtu mmoja. Sio lazima. Sio lazima wanachama wote wampende kiongozi fulani. Sio lazima.

Kupenda mtu ni haki ya mtu iliyo ndani ya hiyari yake.

Humu mnaweza kunipenda Mtibeli au msinipende. Hilo lipo ndani ya mipaka yenu. Sio mimi nijisikie vibaya au niwalazimishe mnipende. Huo ni ukatili.
Au wanaonipenda watake kuwalazimisha wasionipenda wanipende. Huo ni ushenzi.

Haina tofauti na mtu anayelazimisha Salamu. Kusalimia ni hiyari ya mtu. Ipo ndani ya uhuru wake.

Mtu kutoa Salamu za Rambirambi kwenye msiba ni hiyari yake.

Mtu kumsamehe mtu mwingine sio lazima ni hiyari yake.

Usishangae siku Tundu Lisu akiamua kusamehe waliompiga Risasi alafu ukaona baadhi ya watu wakachukia, wakamkasirikie wakamuona Msaliti.

Sisi Watibeli hatuumizwi na maamuzi ya mtu mwingine ambayo yapo ndani ya mipaka yake na Hayagusi mipaka yetu.

Hofu yangu ni hii, tabia za kiccm naziona pia huko CHADEMA.
Usitoe kibanzi jichoni mwa mwenzako wakati wewe unaboriti.

Tabia za kiccm, inaletwa hoja na upinzani. Wafuasi wa CCM wanajibu ninyi vibaraka wa wazungu, sijui blah blah.

Wanaccm nao wakileta hoja, wafuasi wa chadema utasikia buku 7 sijui blah blah blah.

Mwanaccm akikosoa chama chake. Anaandamwa na CCM wenzake ikiwezekani kufukuzwa kabisa uanachama.

Mwanachadema akikosoa chadema au viongozi wa chadema, wanachadema wanaanza kelele na kumuita msaliti na majina mengine.

Hatutaki vyama vinavyotaka kusifiwa na kupongezwa tuu. Tunataka vyama ambavyo wanachama wake watakuwa huru kukosoa na kusifia bila kuletewa fujo.

Nimemaliza

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Hii umepiga angle zote za uwanja na kukabia kwa juu yaani kwa kifupi umetoka somo kubwa sana japo wapo watakaokupinga kwa huu ukweli ambao ni ukweli mtupu
 
Wote wapo kwenye Kapu moja.

Angalia hata mambo ya uchaguzi.
Juzi walikuwa na uchaguzi hapa, wapo waliokimbilia CCM kisa kushindwa uchaguzi.
Wapo waliohamia CHAUMMA.
Yaani mambo ni yaleyale.
Ccm kitaasisi imeizidi zaidi mara 100 Chadema katika kuendesha mambo yake.

Na chadema isipo dhibiti hawa wanaharakati walio jaa mihemko na matusi inaenda kufa kifo kibaya sana.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Hii umepiga angle zote za uwanja na kukabia kwa juu yaani kwa kifupi umetoka somo kubwa sana japo wapo watakaokupinga kwa huu ukweli ambao ni ukweli mtupu

Kunipinga sio tatizo kwani ni sehemu ya mjadala.

Wanipinge kwa hoja. Hilo tuu
 
🫢🫢😆😆😄

Hao policcm wakifanya hivyo kosa lao linakuwa wapi?

Acheni tabia za ajabu.
Hila ya mtu unaipataje kwenye maoni yake?
Hila inafahamika, na dhamira njema inaeleweka. Mfano halisi, Lema kajifanya kutoa pole kwa Samia wakati Samia kaua maelfu ya watanzania na kaona sawa. Lakini hila yake iko wazi kabisa kuwa Lema sio wa hivyo, maana aligoma kumsalimia Makonda huko Monduli kwenye msiba wa Lowassa. Kwanini asipewe ukweli wake?
 
Ccm kitaasisi imeizidi zaidi mara 100 Chadema katika kuendesha mambo yake.

Na chadema isipo dhibiti hawa wanaharakati walio jaa mihemko na matusi inaenda kufa kifo kibaya sana.
Mwamba ngozi huvutia kwake. Katika vyama vya hovyo kwa sasa ni ccm, kuvaa koti la serekali ndio kunasaidia kuficha madhaifu ya ccm.
 
Kama mnajua kufanya analysis ya mambo, mnafahamu vigezo na kanuni mtagundua wengi wenu mna tatizo lile lile, mnatofautiana tu muda wa kushutumiana. Principal ya uhuru kwa wengi wenu ni “selective” Kiranga huwa anawafundisha vitu fulani ambavyo wengi wenu huwa hamuoneshi dalili ya kuvielewa 😅

Somehow hamjui kuwa ka-udikteta ni tabia ya watanzania inayotokana na poor upbringing inayotengeneza strong culture and here we are.

WaTz wengi hamuelewi neno haki, mnatumia neno haki selectively.

Kabla hatujawalaumu CDM, CCM etc wewe kama muandishi andika kuhusu usuli wa hili jambo.

Additionally; Watu wenye akili walifahamu complicity ya tabia ya mwanadamu ndio maana wakaweka sheria, taratibu, na kanuni ili ku-guide mwenendo wa watu, We don’t expect every individual to have a certain level of understanding.
 
Vyama vyote vinasema hilohilo kwamba vipo kwaajili ya kupigania Watanzania. Hiyo ni siasa.

Ninachokisema ni ile tabia ya vyama kikiwemo Chadema kuwa na tabia ya kukataa ukosoaji na kuwachukulia wakosoaji kama maadui au ccm kumbe wengine hata huo muda wa vyama hawana
Binafsi nimekuwa nikipigwa vita sana pale ninapokosoa jambo lolote kuhusu chadema
 
Mwamba ngozi huvutia kwake. Katika vyama vya hovyo kwa sasa ni ccm, kuvaa koti la serekali ndio kunasaidia kuficha madhaifu ya ccm.
Ni kweli ccm ni chama cha hovyo lakini chadema ni hovyo mara mia ya ccm.

Chadema inamapungufu mengi sana .
 
Ndio maana tunataka nchi iongozwe kwa kufuata katiba sio matakwa ya chama/wanachama. Bado sikubaliani na hoja zako sababu ya wanachadema kuwa hivyo zipo wazi, wameshapita viongozi waliowahi pendwa kama Lema lakini wakaishia saliti kambi.

Lema amekuwa na dalili kama hao, tunaambiwa yeye ndio alianzisha sakata la tonetone, juzi kaka na kumtakia salam za pole kijanja janja rais ambaye wanachadema na watu wote wenye utu hawaoni kama anastahili.

Pia hapo hapo kaja kumtuhumu Heche uhusiano wake na mkuu wa usalama wa taifa ikiwa swali lilimlenga yeye! Kimsingi ameanza kuonyesha tabia za kisnitch nikiri tu mimi ni moja ya watu tunaomkubali sana lakini ngumu kumtetea
 
My kaka, ngoja niplay "devil's advocate" kidogo.

Ukisema "maoni ambayo wanaona wazi kuna hila nyuma yake" unamaanisha ni nani akiona? ni akina ambao wana mandate ya kuamua maoni haya au kukosolewa huku kuna hila nyuma yake?

Je huyo mtu anayeona au kuamua nini kina hila akikosea na akakosolewa, mizani gani itatumika kuamua kama hayo maoni dhidi yake ni legit?
Hila ya Lema iko wazi, aligoma kumsalimia Makonda kwenye mazishi ya Lowassa, lakini Mbowe alisalimiana na huyo Makonda, unataka upewe mfano zaidi wa hila?
 
Back
Top Bottom