CHADEMA ni wakandamizaji wa Uhuru wa maoni na kujieleza kwa watu. Hawana tofauti na CCM

Wafuasi na wanachadema ndio Chadema yenyewe. Hao viongozi ni wawakilishi tuu.

Sijawahi sikia viongozi wa CHADEMA wakiwaambia Wafuasi na wanachama wao kwamba waache kuwatukana na kuwadhihaki watu wanaotumia haki yao ya kikatiba kutoa mawazo yao.
Wewe ni mwana Chadema? Umejuaje hawajawahi kuwaambia.

Unaipima CDM kwenye social media…?
 
Screenshot 2026-09-14 at 10-02-25 Instagram.png
Screenshot 2026-09-14 at 10-29-03 Instagram.png
 
Siasa ni sayansi na mchezo wa akili na sio mihemko na matusi .
Chadema imejaa watu yenye mihemko ya kipumbavu.
Hakuna sayansi yoyote hapo, hilo neno siasa ni sayansi ni la kitapeli.
 
Kama kwenye mpira tu, Watanzania sote tunalazimishwa kuwa ama Yanga au Simba. Ukikosoa timu moja unawekwa timu pinzani.
 
Watanzania ni wale wale, nashangaa tunaweka classes. Hatuna tofauti, iwe CDM vs CCM, iwe SIMBA vs YANGA, iwe CHRISTIANS vs MUSLIMS hatuna tofauti iwe kwenye kufikiri wala kufanya mambo.

Watu wameichoka tu CCM na mambo yake, utawala unaoongozwa kwa katiba ya 1977 wakati asilimia kubwa ya watanzania wa leo hawajazaliwa. Wakija CDM kuna mambo yatabadilika kama kupepesa macho, then tutarudi kwenye default mode, sababu kubwa ni kwamba hatuna tofauti, hata kama kiitikadi tunatofautiana.
 
Hakuna sayansi yoyote hapo, hilo neno siasa ni sayansi ni la kitapeli.
Unajua sayansi ni nini?.. unajua kuna 'political science degree'?.. sayansi siyo pipette,test tube, pendulum bob na physics laws tu
 
Watanzania ni wale wale, nashangaa tunaweka classes. Hatuna tofauti, iwe CDM vs CCM, iwe SIMBA vs YANGA, iwe CHRISTIANS vs MUSLIMS hatuna tofauti iwe kwenye kufikiri wala kufanya mambo.

Watu wameichoka tu CCM na mambo yake, utawala unaoongozwa kwa katiba ya 1977 wakati asilimia kubwa ya watanzania wa leo hawajazaliwa. Wakija CDM kuna mambo yatabadilika kama kupepesa macho, then tutarudi kwenye default mode, sababu kubwa ni kwamba hatuna tofauti, hata kama kiitikadi tunatofautiana.

Sahihi kabisa
 
Back
Top Bottom