CHADEMA, njia ya kupita ili kuingia Ikulu ni kuacha kabisa kumchafua Hayati Magufuli. Mkumbatieni mtafika

Kaangalie matusi anayoogeshwa Lisuu ndo urudi hapa useme huu ujinga wako
Hayo matusi ni sehemu ya siasa, hivyo kawasisitize hao wanaotukana wasiache maana ni haki yao hadi watakapotosheka. Kama mkitukana huko kwenye page yake mnadhani mtamzuia kusema ukweli, basi mmeukalia. Sisi wengi tunamuunga mkono kwa kumsema yule ibilisi.
 
Wapiga kura wapi, maana kwa sasa hivi hapa nchini kushiriki uchaguzi ni kupoteza muda, na Magufuli ndio aliyeshusha thamani ya box la kura. Sasa sijui ni nani mnamtisha na hao wapiga kura, ambao yeye mwenyewe hakuwaamini hadi akaamua kupora uchaguzi.
 
Anzisheni kile chama chenu cha sukuma gang ili mtumie huo mtaji wa wa huyo jiwe. Hao team jiwe wako wapi, mbona hawathubutu kujitokeza hadharani ili wachote huo mtaji wa jiwe kama kweli wanaamini upo? Mnaleta vitisho vya kijinga mkitegemea watu wataacha kuanika uhayawani wa dhalimu?
 
Na huo ndio ukweli wenyewe !! Lakini kwa kuwa wataupuuza wasitegemee miracles katika Uchaguzi !!
 
Mkumbatie wewe peke yako. Kwetu sisi yule ni fisadi wa kuchomwa moto kama kibaka.
 
Kwa kifupi siasa ni sayansi Chadema watumie mtaji wa Magufuri kwa vile falsafa yao ya raslimali za nchi wanafanana naye kuliko utawala wa awamu hii. tofauti ya magufuri na wao ni kwenye falsafa ya demokrasia na uhuru wa kujieleza au mambo ya haki za kibinadamu. wacheze na fursa.
 
Kumtumia Shetani kumtoa shetani mwenzie ni kuhalalisha kufanya ushetani mbeleni ukishafanikwa kushika madaraka.

Mazuri ya Magufuli yatasemwa, na mabaya yake yatasemwa.

Ndiyo maana Lissu anasema mazuri ya Magufuli kuwa hakuwa muingia mikataba mibovu, Lakini mabaya yake kama uuaji, kutoheshimu katiba anasema!
 
Kama wanajua kupiga hesabu vizuri watazingatia ushauri wako !!
 
Kusema CCM haikubaliki kanda ya ziwa sababu inaweza kuwa ni ubaguzi tu wa kuona mwanamke yupo pale ikulu na akifanya kazi ya maana sana.

Hakuna mradi ulioachwa na hayati JPM uliolala mpaka kwa miaka miwili tangu afariki dunia. Walitegemea kuona kila kitu kikikwama lakini uhalisia umekuwa ni kinyume chake.

Na tunao wapumbavu wengi kwenye jamii yetu ambao hata kikifanyika kizuri kiasi gani wanakimbilia kwenye udhaifu wa jinsia, kwao hakuna jema linaloweza kufanywa na mwanamke hizi ni akili za kipuuzi sana.

Hivyo kujaribu kuwaambia CHADEMA kwamba wasimtukane Magufuli kwa kudhania kwamba Samia ni mteremko kwao, ni kujidanganya pia. Samia anao wasaidizi wa kiwango cha juu sana na anawapa uhuru wa kufanya wanaloweza kufanya wakitumia weledi wao kuijenga nchi.
 
Nafikir umeamua kujitoa ufahamu kwa chuki binafsi juu ya jiwe.Kundi la jiwe lipo na lina nguvu.CCM wanatumia divide and rule technique, Team jiwe pekee haiwez watoa CCM madarakani, Chadema pekee hawana uwezo wa kuitoa CCM madarakani na ACT pia haina huo uwezo.So CCM wanawatumia ACT kuiponda CHADEMA na Wakati huohuo CHADEMA inatumika kuipoteza Sukuma gang.Chadema haiwezi chukua nchi kwa kupambana na ACT,CCM na Sukuma gang kwa pamoja. Chadema inaweza chukua nchi kwa kuungana na Sukuma gang, bila hata kuungana na ACT Inawezekana vizuri tu. Sukuma gang ni watu wa chini wenye kuamini katika Magufuli na hawa ni wengi sana.Unaweza fanya research kwenye daladala tu,Tamka MAGUFULI then kaa kimya utaelewa kama unataka kuelewa coz kuelewa sometimes ni uamuzi. Ni mwanasiasa ubwabwa tu atakayekuambia sukuma gang haina lolote lakini yule anayejua SIASA ni sayansi hawezi beza hili kundi. Hawez cheza ovyo na hii karata, kama unavyoona wanasiasa wanavyocheza na HISIA za bodaboda, machinga au mamantilie ndivyo hata hili kundi inavyotakiwa ucheze nalo. Na Bahati mbaya hili kundi limemeza hayo makundi yote.

Ukitaka SIASA za kufurahisha nafsi yako ni sahihi kabisa kubeza hili kundi ila kama unataka SIASA za kushika dora basi huwez jitoa ufahamu ktk kucheza na HISIA za hili kundi. Nachoona Chadema na Lisu wanafanya SIASA katuni au SIASA maigizo. Sayansi ya SIASA kila kundi ni muhimu katika kufikia lengo flani ila SIASA katuni au za kutumika ndio utaona mwanasiasa anapambana kuponda kete za kumfanya afike sehemu. Adui wa Adui yako ni RAFIKI yako na hii ni FACT,Sukuma gang ni Adui wa CCM,Sasa kama Chadema ni adui wa CCM kwanini asiwe rafiki wa sukuma gang?Au ye anafanyaje SIASA?
 
Magufuli ana nyota kali sana, wanaomtukana atakuwa aliwashika kama sio kwenye vyeti feki basi alibana pale mlipokuwa mnakula bure. Sijawahi kusikia uku mtaani watu wanamtukana Magu
 
Kusema CCM haikubaliki kanda ya ziwa sababu inaweza kuwa ni ubaguzi tu wa kuona mwanamke yupo pale ikulu na akifanya kazi ya maana sana.
Hii sentesi ni ya kijinga!

Acha kubagua watu mpuuzi wewe! Uongozi mbaya ukiwa umefanywa na mwanaume ndio sahihi kuuchukia na kiongozi huyo kuchukiwa? Ukifanyika chini ya mwanamke, ukisemwa inakuwa ni kuisema jinsia yake?

Na aewe ulienda shule kusomea upuuzi?

Kushindwa ni kushindwa tu, na ubaya wa kiongozi yeyeto utasemwa bila kujali jinsia!

Elewa sana mkuu
 
Kusema CCM haikubaliki kanda ya ziwa sababu inaweza kuwa ni ubaguzi tu wa kuona mwanamke yupo pale ikulu na akifanya kazi ya maana sana.
Hii sentesi ni ya kijinga!
Acha kubagua watu mpuuzi wewe! Uongozi mbaya ukiwa umefanywa na mwanaume ndio sahihi kuchukiwa? Ukifantika chini ya mwanamke, ukisemwa inakuwa ni kuisema jinsia yake?

Na aewe ulienda shule kusomea upuuzi?

Kushindwa ni kushindwa tu, na ubaya wa kiongozi yeyeto utasemwa bila kujali jinsia!

Ele
Mkuu! Umemaliza hoja!

Mungu akutunze! Wasipokuelewa hawa mabehewa wa chadema, basi tena
 
Eleza kwanza zile pesa ambazo zilifichwa China na eti zitakabidhiwa familia yake! Alizitoa wapi, zile pesa alizokuwa akizigawa barabarani alizitoa wapi na zile pesa alizoipa CCM iwalipe mishahara wafanyakazi wake wakati CCM haikuwa na pesa alizitoa wapi!
Msitetete wizi na hujuma huku pesa za wenye maduka ya kubadili pesa hawajarudishiwa pesa zao zaidi ya kakuleta, viti na meza.
 
yule ngosha hapana asee, yeye ndio katengeneza haya yote. Bila yeye tusingekuwa na hili bunge la ndioooo kapambana kudhoofisha upinzani. Matokeo yake nchi inaelekea shimoni
 
CCM hata ya Magufuli kashindwa, ndiyo maana haijaleta mabadiliko ya kimfumo.

Sasa kwa nini tunalinganisha CCM iliyoshindwa na CCM iliyoshindwa badala ya kuweka standards za uongozi mzuri na kutaka tuzipate kutoka kwa yeyote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…