CHADEMA, njia ya kupita ili kuingia Ikulu ni kuacha kabisa kumchafua Hayati Magufuli. Mkumbatieni mtafika

CHADEMA, njia ya kupita ili kuingia Ikulu ni kuacha kabisa kumchafua Hayati Magufuli. Mkumbatieni mtafika

Eleza kwanza zile pesa ambazo zilifichwa China na eti zitakabidhiwa familia yake! Alizitoa wapi, zile pesa alizokuwa akizigawa barabarani alizitoa wapi na zile pesa alizoipa CCM iwalipe mishahara wafanyakazi wake wakati CCM haikuwa na pesa alizitoa wapi!
Msitetete wizi na hujuma huku pesa za wenye maduka ya kubadili pesa hawajarudishiwa pesa zao zaidi ya kakuleta, viti na meza.
Kaiulize kamati iliyopewa kuchunguza hayo! Je ilikuja na jibu gani?

Ukumbuke, wale wote waliotakiwa kulipa fedha hizo alipokufa magufuli wakadhani mi pona yao! Wanahitajika kulizipa!
 
CCM hata ya Magufukinikishindwa, ndiyo maananhaijaleta mabadiliko ya kimfumo.

Sasa jwa ninibtunalinganisha CCM iliyoshindwa na CCM iliyoshindwa badala ya kuweka standards za uongozi mzuri na kutaka tuzipate kutoka kwa yeyote?
Inawezekana uko na hoja ila hujaamua kupangilia uwandishi wako
 
Kusema CCM haikubaliki kanda ya ziwa sababu inaweza kuwa ni ubaguzi tu wa kuona mwanamke yupo pale ikulu na akifanya kazi ya maana sana.

Hakuna mradi ulioachwa na hayati JPM uliolala mpaka kwa miaka miwili tangu afariki dunia. Walitegemea kuona kila kitu kikikwama lakini uhalisia umekuwa ni kinyume chake.

Na tunao wapumbavu wengi kwenye jamii yetu ambao hata kikifanyika kizuri kiasi gani wanakimbilia kwenye udhaifu wa jinsia, kwao hakuna jema linaloweza kufanywa na mwanamke hizi ni akili za kipuuzi sana.

Hivyo kujaribu kuwaambia CHADEMA kwamba wasimtukane Magufuli kwa kudhania kwamba Samia ni mteremko kwao, ni kujidanganya pia. Samia anao wasaidizi wa kiwango cha juu sana na anawapa uhuru wa kufanya wanaloweza kufanya wakitumia weledi wao kuijenga nchi.
Magufuli hawezi kufutika kirahis mioyoni mwa watu wew. Kile kilikuwa chuma kiboko ya wezi
 
Nawahakikishia hivyo, kwa sababu kati ya watu waliofanya tafiti kuhusu utawala wa JPM na uliopo sasa, miongoni mwao na mimi nimefanyia utafiti huo

Nasema ukweli wa moyo! Sio kanda ya ziwa tu, pwani na hata kasikazini, na nchi nzima kwa ujumla

watanzania wanahasira mno na ccm kwa uongozi uliopo ambao umeshindwa kabisa kukidhi matarajio ya wengi

Wanahasira na ccm na hasa kwa kuacha kwa maksudi Rais wa mioyo ya wengi hayati JPM kutukanwa bila wao ccm kujitokeza kukemea jambo hilo

Yako mengi ni pamoja na kupanda kwa gharama za maisha bila sauti yoyote ya kiongozi wa juu,

Hatukatai, yapo mambo ambayo kipindi cha mwendazake yalikuwa yakitokea na kuwa kero kwa wananchi, ila Rais alijitokeza hadharani kwa haraka ama kukemea na ama vinginevyo!

Kanda ya ziwa kwa sasa, ccm haitakiwi hata kwa dawa, ninao mabibi zangu ambao kabla ya utawala huu, ilikuwa ukiwaambia wakakipigie kura chama cha upunzani, ilikuwa unaambulia matusi

Nenda sasa uwaulize wazee kuihusu ccm, majibu utakayopata utaaungana na mimi kusema, watu wameichoka mno ccm na hawaitaki

Chadema, kumtukana Magufuli ni kujiharibia, kwani mkimeza tu yale mnayodhani hayakuwa sawa mtapungukiwa nini? Mbona ya kina Lowasa mliyameza na kumpa nafasi ya kugombea urais?

Mnachotaka nyinyi ni nini?

Kumbukeni, kampeni na machapisho yenu ya nyuma kipindi cha uchaguzi uliopita, nanukuu,

Mlisema, kwa sasa, tutatumia mbinu zote ili kuitoa ccm madarakani, hata kama njia za kishetani, na ndiyo maana ya kula matapishi yenu kumweka Lowasa kuongoza njia kuing'oa ccm

Kwa sasa mbashindwa nini? Mbona mnawakasirisha wananchi walio wengi na ambao huwezi kuwaambia chochote kuhusu JPM wakakuelewa zaidi watakuona kituko?

JPM ni lulu yao wananchi wengi hasa wa maisha ya chini, na wananchi wa maisha ya chini, ndio waliowengi na ndio wanaweza kuwaondoa ccm kwa uwingi wa kura zao! piga ua galagaza, JPM, ni lulu yao tu,

Hata mchukie kuona watu wakimpenda JPM, iko hivyo na hamtawabadiri kwa lolote

Nimewapuuza sana kuingiza maneno na shombo ya kijinga kumhusu JPM

Na bila shaka mmeona matusi yanayoporomoshwa kwenye ukurasa wa Tundu lissu
we akili hazikutoshi, eti mkumbatieni, mnamkumbatia mfu? Vichaaha hawakaa waishe hii dunia. Tena bila haya?
 
Magufuli hawezi kufutika kirahis mioyoni mwa watu wew. Kile kilikuwa chuma kiboko ya wezi
Ni ukweli usiomithilika!

Wajinga tu wanaodhani magufuli hajakaa mioyoni mwa watanzania wengi
 
Nafikir umeamua kujitoa ufahamu kwa chuki binafsi juu ya jiwe.Kundi la jiwe lipo na lina nguvu.CCM wanatumia divide and rule technique, Team jiwe pekee haiwez watoa CCM madarakani, Chadema pekee hawana uwezo wa kuitoa CCM madarakani na ACT pia haina huo uwezo.So CCM wanawatumia ACT kuiponda CHADEMA na Wakati huohuo CHADEMA inatumika kuipoteza Sukuma gang.Chadema haiwezi chukua nchi kwa kupambana na ACT,CCM na Sukuma gang kwa pamoja. Chadema inaweza chukua nchi kwa kuungana na Sukuma gang, bila hata kuungana na ACT Inawezekana vizuri tu. Sukuma gang ni watu wa chini wenye kuamini katika Magufuli na hawa ni wengi sana.Unaweza fanya research kwenye daladala tu,Tamka MAGUFULI then kaa kimya utaelewa kama unataka kuelewa coz kuelewa sometimes ni uamuzi. Ni mwanasiasa ubwabwa tu atakayekuambia sukuma gang haina lolote lakini yule anayejua SIASA ni sayansi hawezi beza hili kundi. Hawez cheza ovyo na hii karata, kama unavyoona wanasiasa wanavyocheza na HISIA za bodaboda, machinga au mamantilie ndivyo hata hili kundi inavyotakiwa ucheze nalo. Na Bahati mbaya hili kundi limemeza hayo makundi yote.

Ukitaka SIASA za kufurahisha nafsi yako ni sahihi kabisa kubeza hili kundi ila kama unataka SIASA za kushika dora basi huwez jitoa ufahamu ktk kucheza na HISIA za hili kundi. Nachoona Chadema na Lisu wanafanya SIASA katuni au SIASA maigizo. Sayansi ya SIASA kila kundi ni muhimu katika kufikia lengo flani ila SIASA katuni au za kutumika ndio utaona mwanasiasa anapambana kuponda kete za kumfanya afike sehemu. Adui wa Adui yako ni RAFIKI yako na hii ni FACT,Sukuma gang ni Adui wa CCM,Sasa kama Chadema ni adui wa CCM kwanini asiwe rafiki wa sukuma gang?Au ye anafanyaje SIASA?
Nimekuuliza sukuma gang wako wapi, mbona hawajitokezi waziwazi wakaonekana. Unaoongelea kundi la muhimu lenye uoga! Kama hao sukuma gang wangekuwa na nguvu hizo, Magufuli asingehangaika kupora mchakato wa uchaguzi maana hilo kundi lingempa ushindi.

Washabiki wa simba na Yanga wako wazi na wanafahamika, wafuasi wa cdm wako wazi na wanafahamika. Hayo majoga ya sukuma gang yako wapi tuyaone? Usitake kujifanya wananchi wote ndio sukuma gang, eti taja jina la Magufuli. Mbona linatajwa tu na wanaosifia wanamsifia, na wanaomponda wanamponda na hakuna lolote jipya? Unataka cdm waungane na kundi hewa linaloogopa hata kujitokeza hadharani?
 
we akili hazikutoshi, eti mkumbatieni, mnamkumbatia mfu? Vichaaha hawakaa waishe hii dunia. Tena bila haya?
Haya matusi hayaondoi ukweli wa kile nimesema!

Kakague matusi anayooga huko msaidizi wa Mbowe!

Cheza na Samia usicheze na nguvu aliyoiwekeza JPM kwenye mioyo ya watanzania kwa watu wa maisha ya chini na ya kati na hata kwa wasomi na wapenda mabadiriko nchini

Na ukimsema vibaya huyo mwamba kama alivyofanya huyo ndugu yenu na usiwe na ulinzi, utaoga bakora!
 
Ni ukweli usiomithilika!

Wajinga tu wanaodhani magufuli hajakaa mioyoni mwa watanzania wengi
Mm nilikuwa siwapendi ccm hata kdg ila kutokana na falsafa ya chuma kile ah na kofia nilinunua na kweny kampen ile 2020 niliungua jua kusubiri kumwona live tu moyo wangu utulie. Toka amefarik na kofia siitaki tena
 
Akae moyoni kwa watanzania wengi, kisha apore uchaguzi?
Kupora uchaguzi na kuwatendea haki watanzania kwa nchi hii ya watu wezi na majambazi, ni swa kabisa

Tunataka na mwingine mfano wa Jiwe aibe tena kura ili tuondokane na maswaobu yanayojitokeza sasa
 
Haya matusi hayaondoi ukweli wa kile nimesema!

Kakague matusi anayooga huko msaidizi wa Mbowe!

Cheza na Samia usicheze na nguvu aliyoiwekeza JPM kwenye mioyo ya watanzania wa maisha ya chini

Na ukimsema vibaya huyo mwamba kama alivyofanya huyo ndugu yenu na usiwe na ulinzi, utaoga bakora!
Waambie hao ni mwili tu umekufa ila falsafa zake za kizalendo bado ni mpyaaaaa mioyoni mwa watanzania wengi
 
Chadema hawana njia yoyote ya kuwafikisha Ikulu. Hicho ni chama cha wajinga ndiyo waliwao.

Wabaki kama walivyo, kutengeneza pesa za wajinga na kukusanya vijana wasiojielewa wataokwenda vyama vingine wakishajielewa.

Chadema ni chama cha kutafutia umaarufu na wapiga pesa tu.

Chadema hakina uhalali kabisa wa kupewa madaraka na wananchi wanaojielewa.
 
Ukiona mahali popote mtu anamtukana vibaya JPM wew jua alikutana na KIBANO kitakatifu 😁
 
Mm nilikuwa siwapendi ccm hata kdg ila kutokana na falsafa ya chuma kile ah na kofia nilinunua na kweny kampen ile 2020 niliungua jua kusubiri kumwona live tu moyo wangu utulie. Toka amefarik na kofia siitaki tena
Mimi mwenyewe mkuu, Magufuli alirudisha imani yangu sana juu ya uongozi wake nchini!
 
Inawezekana uko na hoja ila hujaamua kupangilia uwandishi wako
Simu ilizingua.

Nasema hivii.

CCM hata ya Magufuli ilishindwa, ndiyo maana haijaleta mabadiliko ya kimfumo.

Sasa kwa nini tunalinganisha CCM iliyoshindwa na CCM iliyoshindwa badala ya kuweka standards za uongozi mzuri na kutaka tuzipate kutoka kwa yeyote?

Kwa nini tunashindwa kufikiri kidhahania na kusema uongozi mzuri ni ule utakaotupa hiki, na hiki na hiki, hata kama hakipo?

Kwa nini tunaona ili kulinganisha uongozi, inatubidi tulinganishe uongozi mmoja ulioshindwa na mwingine ulioshindwa? Kwa nini tunaweka makundi ya kulinganisha tawala kwa muktadha wa Chawa wa Mama vs. Sukuma Gang wakati wote hao ni failures tu?

Kwa nini tunalinganisha failure na failure badala ya kuweka viwango vizuri, hata kama hatujavifikia, halafu tulinganishe uongozi wetu ulioshindwa na uongozi wa viwango vinavyotakiwa, hata kama hatujavifikia bado?
 
Yeye alifanya kipi cha maana?
Ni pamoja na kuchezea kibano wezi, wauza ngada, wala rushwa, wanufaika wa watumishi hewa na watumishi hewa kwa ujumla

Na ikiwa katika hayo ulikuwepo, abadani huwezi kumkubali hata kidogo
 
Back
Top Bottom