CHADEMA, njia ya kupita ili kuingia Ikulu ni kuacha kabisa kumchafua Hayati Magufuli. Mkumbatieni mtafika

Unajua mkuu, wewe unakuwaga na hoja na huwa ninakukubali sana!

Hasa unapoongelea mifumo! Hilo nakuunga mkono, kwenye hilo, naliona kosa kubwa la JPM la kutokuweka kuw mfumo ambao kila kiongozi atakayekuja, aongozwe na mfumo na siyo yeye kuiendesha mifumo atakavyo

Tunataka mfumo wa kufuatwa na kila kiongozi ajaye na siyo mtu kuwa yeye ndio mfumo
 
toka ametukanwa huyo magufuli chadema imeyumba wapi au unaishi pwan, njoo kanda ya ziwa uniambie wapi magufuli anapendwa kama hautajikuta pekeako na wajinga wenzio mlionufaika na wizi wa kura wa huyo magufuli, kama haujui kanda ya ziwa hatutaki hata kumsikia huyo mbwa wenu magufuli pamoja na mama yenu muuza bandari.
 
Unamchafuaje mtu aliyechafuka?
Hizo nguvu na lulu unazoziongelea ni zipi? Wewe unadhani yeye alikua ni mjunga hadu akauiba na kuuvuruga uchaguzi?
Alifanikiwa kuwaroga nyie muaamini anapendwa, ila ukweli aliokua nao ulimtisha.
Lissu msumchukulie poa. Kutoka kupona kuuawa kwa risasi hadi kuja kusimama na hasimu wako na kupelekea hasimu wake kusimamisha simamisha kampeni kila baada ya wiki kwa sababu za kiafya na hadi baadaye kufariki huyo siyo mtu wa kumchukulia poa. Ni mtu finyu tu ndiyo atamchukulia poa.
 
🤣

Nakushauri uende kwenye ukurasa wa nduguyo ujionee alivyoshuka ghafula umaarufu wake
 
Uongozi wa Magufuli ulifaulu kwanza alikuwa mzalendo sana na nchi yake pili aliwapenda watanganyika kwa moyo wa dhati tatu aliboresha sectorz nying sana ikiwemo afya na usafiri nne alibana wezi mpaka mifuko ya surual ya nyuma ikakutana tano hakuweka rehani mali na urithi wa nchi yetu
 
Hujaongelea uongozi, umemuongelea mtu.

Uongozi ni zaidi ya mtu mmoja.

Tofautisha uongozi na mtu.
 
Goli la ccm lipo wazi upinzani wao na beki tu.
Mama wa kambo hawezi zuia penalt
 
Unapomaliza kuandika haya, kafungue ukurasa wa Msaidizi wa Mbowe uone alivyoshushwa thamani na kushuka ghafla kwenye umaarufu wake

JPM yaweza kuwa ni mbaya, lakini ya nini kushupaza shingo kushindana na wasioelewa ubaya wake?

Unaitaka Ikulu?

Wakati mwingine unapaswa kutumia hata zile njia usizo zipenda ili ufike uendako!

Endeleeni na ujinga wenu! Kuna mabua yanawasubiri
 
Acha uongo mm nimesoma mwanza kipindi magu anatangazwa kuwa ni rais mpya shule nzima walipiga mayowe ya furaha na kukata matawi ya miti na kushangilia
 
JPM yeye alifanya total abuse, na kosa lake kubwa kabisa hakupenda kupungwa, na alitaka ashauriwe atakavyo.
Mbaya zaid ni aina ya watu aliojizungushia, waliuona udhaifu wake wa kupenda sifa wakautumia.
Mwanasiasa makini kamwe hatataka support ya 'Sukuma Gang', hili ni kundi la hovyo na majambazi tupu. Ndiyo yaliyoipeleka nchi kule ilipokuwa inapotelea.Kuna wakati nilikua nikimuonea huruma sana JPM, maana nilikua naona jinsi wanamtumia.
 
Mjinga ni wewe uliyeumizwa na ukweli wa hiyo sentensi. Mojawapo ya wanaopinga uwekezaji wa DP World pale bandarini sababu ni jinsia yake.

Mikataba mibovu imeshaingiwa mingi sana kabla hajaingia ikulu na hatujasikia kelele za wajuaji.
 
Baada ya kushinda uchaguzi na upo Ikulu tayari, ndio unapaswa kushikilia hii hoja yako

Vinginevyo, Chadema hamuitaki Ikulu ya Chamwino mnatuzuga tu

Mlimtumia Lowasa na mkakubali kula matapishi, sembuse hili?
 
Kwa katiba yako sasa uongozi ni mtu sio watu
Mkuu, mimi ushauri wangu ni kwamba, Chadema alenge kuipata ikulu kwa njia zozote zile, kila kundi alenge kulichukua yeye

Akifika hapo atatengeneza aonavyo!
 
Magufuli mwenyewe aliipata Ikulu isivyo halali, vipi utake kutegemea kivuli chake? Labda kama unaitaka Ikulu kwa mabavu na unataka kutumia mabavu ya vyombo vya usalama na Chama tawala.
Gharama maendeleo ya kweli siyo sawa na sherehe za harusi.
 
Baada ya kushinda uchaguzi na upo Ikulu tayari, ndio unapaswa kushikilia hii hoja yako

Vinginevyo, Chadema hamuitaki Ikulu ya Chamwino mnatuzuga tu

Mlimtumia Lowasa na mkakubali kula matapishi, sembuse hili?
Usifikiri kila anayechangia kwa mawazo huru ni CHADEMA, kwa taarifa yako tu, mimi kiitikadi ni CCM kuliko unavyoweza ukafikiri.
 
Well Said
 
Usifikiri kila anayechangia kwa mawazo huru ni CHADEMA, kwa taarifa yako tu mimi kiitikadi ni CCM kuliko unavyoweza ukafikiri
Nimekuelewa mkuu

Ila kiukweli nyinyi nchi imewashinda boss!
 
Kaiulize kamati iliyopewa kuchunguza hayo! Je ilikuja na jibu gani?

Ukumbuke, wale wote waliotakiwa kulipa fedha hizo alipokufa magufuli wakadhani mi pona yao! Wanahitajika kulizipa!
Unao uhakika na ukisemacho? Acha maneno ya vijiweni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…