CHADEMA, njia ya kupita ili kuingia Ikulu ni kuacha kabisa kumchafua Hayati Magufuli. Mkumbatieni mtafika

Wewe mpuuzi mimi ni CCM Pengine hata kabla wazazi wako hawajakuzaa, kutofautiana mawazo sio kigezo cha kuja na mapovu kama haya.
 
Kwa katiba yako sasa uongozi ni mtu sio watu
Hapana, katiba hata ya sasa hilo liko wazi, usitake kuisingizia.

Ni hivi, watu ndio wanaongoza nchi, si katiba. Kwa maana hata kama katiba ikiwa haifai, watu wataibadilisha.

Watu wakishindwa kuibadilisha katiba, ina maana wameikubali.

Wakenya wanafanya mabadiliko kwa kasi kuliko sisis, si kwa sababu wana katiba mpya.

La hasha. To the contrary.

Wakenya wamepata katiba mpya kwa sababu wanafanya mabadiliko kwa kasi kuliko sisi.

Kwa hiyo, acha kuisingizia katiba.

Hiyo katiba inaruhusu mikutano ya hadhara ya kisiasa, lakini mmemuachia mumiani mmoja apige marufuku mikutano ya hadhara ya kisiasa kwa miaka kadhaa mpaka akjifia mbali huko.

Sasa hapo napo utalaumu katiba?
 
Nimekuelewa mkuu

Ila kiukweli nyinyi nchi imewashinda boss!
Huo ndiyo ukweli, na imetushinda sababu ya kuishi kimazoea na hatuendani mahitaji ya kinyakati.
Chama tawala kinachotakiwa kuisimamia serikali katika kuiletea nchi maendeleo, chenyewe kipo very local, angalia organizations ndani ya Chama, hata hazieleweki zinachofanya, bado hizo party wings yanayoendelea ndani yake, ni upupu mtupu.
Angalia uwezo wa hoja kati ya vijana waliokuzwa ndani ya upinzani na wanaokuzwa ndani ya CCM, unaweza ukadhani wanaishi nchi mbili tofauti
 
Salute kwako mkuu!

Nimependa namna ulivyo mkweli na muwazi!

Rait tungelikuwa hivi wote, nahisi tusingelikuwa hapa tulipo
 
Dawa yako nishaisema! Njoo na lingine

Uozo wa kiongozi hauna uhusiano na jinsia yake! Wewe unaelewa kiswahili au ni mburundi wewe!!!
Sio kweli kwa Tanzania hii, wapo wajinga wengi tu wenye kuongozwa na mfumo dume. Na wengi wao ni wale ambao hawakutegemea kuwa JPM angeaga dunia March 2021.

Wameingiwa na unyonge mwingi na vinyongo vya kila aina. Kazi yao ni kuhamisha magoli, likifanyika zuri wanakaa kimya kama vile hawalioni na kesho asubuhi wanakuja na mada nyingine ya malalamiko.

Ni watu waliochagua kuteseka na wanazeeka na visirani vya kila aina.
 
Umeandika vzr, nimewahi kuwashauri hivi hivi pia. Big up
 
Lissu endelea kugawa dozi kwa hawa sukuma gang hadi wateme ndoano🤣🤣🤣
Kwani sukuma gang ni matokeo ya nani?

Ya ccm ama chadema?

Kama ni matokeo ya ccm, huwezi kufurahia hili kama mwana ccm! Utakuwa mjinga wa mwisho kabisa na usiyeelewa kabisa nini maana ya siasa

Kula ya mwanasiasa inatokana na kutegemea sana wapiga kura!

Na wakati ukiomba kura, unatazamia makundi yote yakuunge mkono ili uendelee kula!

Kama hutaki haya, basi wewe ni mjinga tu na usiyejua lolote
 
Ni pamoja na kuchezea kibano wezi, wauza ngada, wala rushwa, wanufaika wa watumishi hewa na watumishi hewa kwa ujumla

Na ikiwa katika hayo ulikuwepo, abadani huwezi kumkubali hata kidogo
Siko katika wote hao uliowataja, lakini bado simkubali. Angekuwa anaendesha hayo yote kwa haki bila double standard ningemkubali. Lakini aliendesha nyingi za hizo operations zake kwa uonevu mkubwa.
 
Chadema hakuna mwenye akili ya kuelewa ulichoandika. 2025 watashindwa Uchaguzi Mkuu na kusingizia kuibiwa kura!!!
 
Chadema hakuna mwenye akili ya kuelewa ulichoandika. 2025 watashindwa Uchaguzi Mkuu na kusingizia kuibiwa kura!!!
Kwani CHADEMA hata wakishinda, kwa mfumo huu, wewe unaona CCM watakubali na kuacha kuleta figisu?
 
Kwani CHADEMA hata wakishinda, kwa mfumo huu, wewe unaona CCM watakubali na kuacha kuleta figisu?
Ingawa si kwa asilimia zote nachokihisi!

Ila ninaamini! Sukumagang, karibu wote ni wana ccm na tena kwa asili yao ni wanamsimamo mkali!

Chadema ikiwawini hao, ni rahisi kuendesha operation za maandamano kwa nchi nzima kwa mafanikio makubwa zaidi

Na lingine ni hivi!

Kadiri upepo unavyounguruma, ndivyo unavyompa wasiwasi mwente nyumba mbovu
 
Kura gani unaongelea boss, wakati Magufuli aligeuza amri yake ndio inaamua nani awe kiongozi? Wakati Magufuli ananajisi chaguzi mliona yuko sahihi. Nadhani hamkujua kuwa kile ni kitendo kibaya sana cha kutoheshimu maamuzi ya wananchi. sasa hivi ameshaotesha mbegu mbaya ya kutoheshimu maamuzi ya wananchi, ww bado unaleta vitisho hewa vya wapiga kura.

Hakuna kiongozi wa CCM ataacha kutumia mbinu zile chafu kubaki madarakani. Magufuli alifanikiwa sana kushusha morali ya wapiga kura, na kwa sasa chaguzi zimepoteza thamani yake, na hakuna anayejitambua ataenda kupoteza muda wake kwenye mstari wa kura eti anachagua kiongozi. Kaeni mahali mtafakari mahali dhalimu alipora nguvu ya wananchi.
 
Kwani CHADEMA hata wakishinda, kwa mfumo huu, wewe unaona CCM watakubali na kuacha kuleta figisu?
Ingawa si kwa asilimia zote nachokihisi!

Ila ninaamini! Sukumagang, karibu wote ni wana ccm na tena kwa asili yao wanamsimamo mkali!

Chadema ikiwawini hao, ni rahisi kuendesha operation za maandamano kwa nchi nzima kwa mafanikio makubwa zaidi

Na lingine ni hivi!

Kadiri upepo unavyounguruma, ndivyo unavyompa wasiwasi mwente nyumba mbovu
Ok

Ngoja niamini usemacho boss! Lakini je, kifanyike kipi boss

Na ccm ndio hiyo haitaki kusikia chochote, katiba wala tume huru!

Shauri cha kufanya boss
 

Sitaki kuwaita Sukuma Gang, hili jina linachafua kabila letu watu wengi sana ambao hatukumkubali Magufuli.

Kati ya mwanasiasa anayekwepa kusema ukweli ili awachote hao wafuasi wa Magufuli kwa hadaa, na anayesema ukweli hata kama utawachukiza hao wafuasi wa Magufuli, utamuheshimu zaidi yupi?

Kati ya mwanasiasa mwenye hila za uongo ambaye anajali kushinda uchaguzi kuliko kusema ukweli, na yule ambaye anasema ukweli tu, hata kama utamfanya asishinde uchaguzi, unamuheshimu na kumkubali yupi hapo?
 
Hilo kundi la waoga ndio unataka cdm waungane nalo? Sukuma gang wangekuwa na nguvu hiyo wangekaa hadharani na kuonyesha msimamo wao. Unataka kuonyesha sukuma gang ni kundi lenye nguvu sana, lakini halithubutu hata kujipambanua!

Kwanini nyie sukuma gang hamjitokezi hadharani mpime kukubalika kwenu? Mmebaki kutaka kujishikiza kwa cdm wenye uthubutu, na ambao wako tayari kulipa gharama ya harakati zao?
 
Mkuu!

Slemani alipopelekewa kesi ya mama wawli na mtoto mmoja kubishania mtoto huyo mmoja kila mmoja kusema ni mtoto wake

Alichokifanya, aliwaamuru mtoto aletwe mbele yake ili akatwe panga!

Kati yao hao kina mama, kuna aliyesema, bora tukose wote, mwingine alilia kwa uchungu sana, na slemani akabaini kuwa, yule mama anayelia kwa uchungu, ndiye mama wa mtoto, na akapatiwa mtoto


Nachotaka kusema ni hivi! Dunuani hatuna ruksa tena ya kuumiza watu bali kuushinda ubaya kwa mema!

Kuna kitu kinahitajika ikiwa unataka ujipatie kile unataka! Kuna wakati itakubidi uwe mjinga kumbe ni mwerevu kuliko wao

Nadhani umenielewa! Yaliyopita hayawezi kutufanya tusimame njiani na kisha tukose shabaha yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…