CHADEMA, njia ya kupita ili kuingia Ikulu ni kuacha kabisa kumchafua Hayati Magufuli. Mkumbatieni mtafika

CHADEMA, njia ya kupita ili kuingia Ikulu ni kuacha kabisa kumchafua Hayati Magufuli. Mkumbatieni mtafika

Hilo kundi la waoga ndio unataka cdm waungane nalo? Sukuma gang wangekuwa na nguvu hiyo wangekaa hadharani na kuonyesha msimamo wao. Unataka kuonyesha sukuma gang ni kundi lenye nguvu sana, lakini halithubutu hata kujipambanua!

Kwanini nyie sukuma gang hamjitokezi hadharani mpime kukubalika kwenu? Mmebaki kutaka kujishikiza kwa cdm wenye uthubutu, na ambao wako tayari kulipa gharama ya harakati zao?
Si kila wakati unafaa kwa mapambano boss
 
Ingawa si kwa asilimia zote nachokihisi!

Ila ninaamini! Sukumagang, karibu wote ni wana ccm na tena kwa asili yao wanamsimamo mkali!

Chadema ikiwawini hao, ni rahisi kuendesha operation za maandamano kwa nchi nzima kwa mafanikio makubwa zaidi

Na lingine ni hivi!

Kadiri upepo unavyounguruma, ndivyo unavyompa wasiwasi mwente nyumba mbovu

Ok

Ngoja niamini usemacho boss! Lakini je, kifanyike kipi boss

Na ccm ndio hiyo haitaki kusikia chochote, katiba wala tume huru!

Shauri cha kufanya boss
Ushauri wangu nyie sukuma gang ambao mnajifanya mna nguvu hiyo, jitokezeni waziwazi muonyeshe misimamo yenu tuone uwezo na uvumilivu wenu. Sio mmejificha na hakuna anayethubutu kuja kupambana na ukatili ambao shujaa wenu Magufuli aliutumia kutawala wengine kwa shuruti. Hamuwezi kujificha kwa uoga, kisha mtegemee watu watajali uwepo wenu, jitokezeni hadharani mlipe gharama za mabadiliko.
 
Mkuu!

Slemani alipopelekewa kesi ya mama wawli na mtoto mmoja kubishania mtoto huyo mmoja kila mmoja kusema ni mtoto wake

Alichokifanya, aliwaamuru mtoto aletwe mbele yake ili akatwe panga!

Kati yao hao kina mama, kuna aliyesema, bora tukose wote, mwingine alilia kwa uchungu sana, na slemani akabaini kuwa, yule mama anayelia kwa uchungu, ndiye mama wa mtoto, na akapatiwa mtoto


Nachotaka kusema ni hivi! Dunuani hatuna ruksa tena ya kuumiza watu bali kuushinda ubaya kwa mema!

Kuna kitu kinahitajika ikiwa unataka ujipatie kile unataka! Kuna wakati itakubidi uwe mjinga kumbe ni mwerevu kuliko wao

Nadhani umenielewa! Yaliyopita hayawezi kutufanya tusimame njiani na kisha tukose shabaha yetu
Yani unachosema hapo ni kwamba, hata kama Tundu Lissu hana nia ya kuleta mabadiliko, anataka kupiga hela ndefu tu, anaruhusiwa kukudanganya hata wewe kwamba anataka kuleta mabadiliko, halafu umpe matumaini yako na kura, aingie ikulu, halafu akiingia ikulu akusahau wewe na ajenda zenu mlizokubaliana, aweke mbele ajenda yake ya kupiga pesa.
 
Yani unachosema hapo ni kwamba, hata kama Tundu Lissu hana nia ya kuleta mabadiliko, anataka kupiga hela ndefu tu, anaruhusiwa kukudanganya hata wewe kwamba anataka kuleta mabadiliko, halafu umpe matumaini yako na kura, aingie ikulu, halafu akiingia ikulu akusahau wewe na ajenda zenu mlizokubaliana, aweke mbele ajenda yake ya kupiga pesa.
Nitarejea boss!

Ila sina maana hiyo!

Kumbuka tu boss! Ukitaka kupajenga palipobomoka! Utahitaji kudhalilika kwanza ili uheshimike baada ya
 
Nitarejea boss!

Ila sina maana hiyo!

Kumbuka tu boss! Ukitaka kupajenga palipobomoka! Utahitaji kudhalilika kwanza ili uheshimike baada ya
Suala si kuwa una maana hiyo au huna maana hiyo, suala ni kwamba umeruhusu hilo.
 
Si kila wakati unafaa kwa mapambano boss
Sasa mnapotaka cdm waungane na nyinyi waoga hadi lini mtakuwa tayari kwa mpambano? Cdm wako kwenye mapambano muda wote, nyie mmejificha mkiendelea kula keki ya taifa, lakini mnataka muwatumie waliotayari kulipa gharama ya mabadiliko kwa tamaa yenu ya madaraka.

Kosa walilofanya cdm la kumuokota Lowassa halitajirudia tena. Nyie waoga endeleeni kujificha huku mkijifanya mna nguvu. Jitokezeni hadharani mlipe gharama ya mabadiliko, sio mkae vichakani, kisha mkiona mabadiliko yanakaribia mjifanye mnabeba propaganda za Magufuli kurukia treni la mabadiliko.
 
Chadema hawana njia yoyote ya kuwafikisha Ikulu. Hicho ni chama cha wajinga ndiyo waliwao.

Wabaki kama walivyo, kutengeneza pesa za wajinga na kukusanya vijana wasiojielewa wataokwenda vyama vingine wakishajielewa.

Chadema ni chama cha kutafutia umaarufu na wapiga pesa tu.

Chadema hakina uhalali kabisa wa kupewa madaraka na wananchi wanaojielewa.
Chama gani kina uhalali?
 
Hahaha..
Labda Katiba ibadilike.
As long as kuna hao NEC, policcm na wakurugenzi, ccm itaendelea kupeta tu
Mkuu, unadhani nchi zilizoko kwenye viguvugu la mabadiriko la kisiasa hawana jeshi?

Haki inapokosekana kabisa matokeo yake ndo hayo mkuu
 
Mkuu, unadhani nchi zilizoko kwenye viguvugu la mabadiriko la kisiasa hawana jeshi?

Haki inapokosekana kabisa matokeo yake ndo hayo mkuu
Haki ipi uliyoikosa Tanzania, hususan enzi hii ya mama Samia?
 
Nawahakikishia hivyo, kwa sababu kati ya watu waliofanya tafiti kuhusu utawala wa JPM na uliopo sasa, miongoni mwao na mimi nimefanyia utafiti huo

Nasema ukweli wa moyo! Sio kanda ya ziwa tu, pwani na hata kasikazini, na nchi nzima kwa ujumla

watanzania wanahasira mno na ccm kwa uongozi uliopo ambao umeshindwa kabisa kukidhi matarajio ya wengi

Wanahasira na ccm na hasa kwa kuacha kwa maksudi Rais wa mioyo ya wengi hayati JPM kutukanwa bila wao ccm kujitokeza kukemea jambo hilo

Yako mengi ni pamoja na kupanda kwa gharama za maisha bila sauti yoyote ya kiongozi wa juu,

Hatukatai, yapo mambo ambayo kipindi cha mwendazake yalikuwa yakitokea na kuwa kero kwa wananchi, ila Rais alijitokeza hadharani kwa haraka ama kukemea na ama vinginevyo!

Kanda ya ziwa kwa sasa, CCM haitakiwi hata kwa dawa, ninao mabibi zangu ambao kabla ya utawala huu, ilikuwa ukiwaambia wakakipigie kura chama cha upunzani, ilikuwa unaambulia matusi

Nenda sasa uwaulize wazee kuihusu CCM, majibu utakayopata utaaungana na mimi kusema, watu wameichoka mno ccm na hawaitaki

CHADEMA, kumtukana Magufuli ni kujiharibia, kwani mkimeza tu yale mnayodhani hayakuwa sawa mtapungukiwa nini? Mbona ya kina Lowasa mliyameza na kumpa nafasi ya kugombea urais?

Mnachotaka nyinyi ni nini?

Kumbukeni, kampeni na machapisho yenu ya nyuma kipindi cha uchaguzi uliopita, nanukuu,

Mlisema, kwa sasa, tutatumia mbinu zote ili kuitoa ccm madarakani, hata kama njia za kishetani, na ndiyo maana ya kula matapishi yenu kumweka Lowasa kuongoza njia kuing'oa ccm

Kwa sasa mbashindwa nini? Mbona mnawakasirisha wananchi walio wengi na ambao huwezi kuwaambia chochote kuhusu JPM wakakuelewa zaidi watakuona kituko?

JPM ni lulu yao wananchi wengi hasa wa maisha ya chini, na wananchi wa maisha ya chini, ndio waliowengi na ndio wanaweza kuwaondoa ccm kwa uwingi wa kura zao! piga ua galagaza, JPM, ni lulu yao tu,

Hata mchukie kuona watu wakimpenda JPM, iko hivyo na hamtawabadiri kwa lolote na kwa njia zozote hawawezi kuwaelewa zaidi ya kupandisha hasira zao juu yenu

Nimewapuuza sana kuingiza maneno na shombo ya kijinga kumhusu JPM

Na bila shaka mmeona matusi yanayoporomoshwa kwenye ukurasa wa Tundu lissu
Wasipoupokea ushauri huu basi watakuwa ni wapumbavu.

Kimsingi kwa vyovyote vile na kwa vyovyote Lissu atawaona watu ni wajinga, ajue kabisa ameteleza pakubwa mno
 
Wasipoupokea ushauri huu basi watakuwa ni wapumbavu.

Kimsingi kwa vyovyote vile na kwa vyovyote Lissu atawaona watu ni wajinga, ajue kabisa ameteleza pakubwa mno
Sahihi mkuu!
 
Lissu analetewa tarifa za uwongo na mashushu ya ccm ili avuruge zaidi
 
Kwani mwili umefukuliwa hadi chadema waende kuukumbatiq😧😧😧😧 harufu ya mzoga je?🥺🥺🥺 Haupendi watu na huwapendi chadema wewe Mzoga kabisa watu hai wakumbatie??
 
Back
Top Bottom