Mara baada ya mchakato wa uteuzi wa wagombea uchaguzi ngazi ya vyama kuanza, tulimuona Katibu wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) kwenye mikutano ya vyama vya upinzani. Kwa uelewa wangu, ushiriki huo ulukuwa sehemu ya kutekeleza wajibu wale wa kuona kuwa uchaguzi haupelekei kuvunjika kwa amani.
Tulitegemea kuwa ili kudumisha amani MNF itakuwa mstari wa mbele kuona kuwa mchakato wa uchaguzi wote unatawaliwa na haki na kufanyika kwa mujibu wa sheria.
Kinyume na matarajio yetu MNF mpaka sasa iko kimya wakati ambapo kumekuwa na matukio mengi yanayohatarisha amani kwa kufinya haki. Je, MNF nayo ni muumini wa dhana ya amani pasipo haki?