Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.

Nani aende wakati mwenyekiti yupo ndani kwa tuhuma za ugaidi? Magaidi wana nafasi gani kwenye " mkutano wa nyama vya siasa" ? Ukitaka ama miti kuwa ni watuhumiwa wa kisiasa, muwaache huru ili waje au muendelee na msimamo kuwa ni magaidi nao wasije.
Si kuna vyama vingi ambavyo ni rafiki na vitahudhuria tu, waacheni magaidi msiwabembeleze. Mnaweza kuendesha nchi bila kuongea nao.
 
Watakwambia "nafasi za u-DC zimejaa." Wanatunyeshea mvua ya matusi huko Twitter. Labda hii ndio demokrasia inayotafutwa kwenye #KatibaMpya, yaani uhuru wa kutukana kila wasiyeafikiana nae kimtazamo.
 
Hivi mpendwa unaongelea CHADEMA ipi? Ile ile unayoinanga ilishakufa na kuzikwa 'six feet under'?Hayo maushauri ya kichawi kutoka kwa wachawi wenzio yafaa ubaki nayo mwenyewe, hukohuko mnapowaimbia watesi wetu, mapambio.
Sie twadai KATIBA MPYA NA BORA ili kuondoa u mungu mtu kurudisha utawala wa sheria na haki;
twataka TUME HURU ili WANANCHI (NDIO) WAPIGE KURA, WANANCHI (NDIO) WACHAGUE
 


Katibu mkuu wa Chadema alisema vyama havipewi muda wa kutoa maoni yao na kwasababu hiyo amesema ni kwa picha tu
 
Yaani mwenyekiti wao yupo ndani kwa kesi ya 'kughushi', wao waende picnic!
Mwenyekiti alisimamia madai ya katiba, akapewa kesi ya ugaidi.
Yaani Mbowe kudai katiba ni kosa, ili hali viongozi wa vyama uchwara - ambavyo hata havijawahi kufanya mkutano wa hadhara popote - kujadili hadidu za rejea na kutoa mapendekezo ya katiba mpya ni sahihi.
Hata mimi ningewashangaa sana CHADEMA.
 
Paskali wewe ulistaafu, au umerudi kwenye ajira kimyakimya?
 
Huu ni uthibitisho kuwa Rais Mama Samia ni mpenda haki, mtenda haki, atabarikiwa, nchi itabarikiwa na itaneemeka kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kila nikimtafakari Rais Samia, I was never wrong about her niliposema haya kumhusu Samia Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!”

She is so humble Psychoanalysis Trends za Viongozi Wetu, Humbleness ya Rais Samia ni Bonafide Genuine, ni asili yake, ni nature yake, ndivyo alivyo, Ila...

Na hapa "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

Na hapa Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!

Na hapa Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.
P
 
Mzee baba, kila Rais si unasema hivyo?

Huu ni uzi wako kuhusu Magufuli

 
Chadema waliacha kususa, wakakubali kukaa mezani kufanya maridhiano, haya ndio matokeo chanya
Update
Hatimaye Chadema wameacha kushupaza shingo na wamekubali matokeo!, kwa kuufuata ushauri wa bandiko hili CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Nimepokea taarifa, hii kutokea twitwani Kisha nikasoma na bandiko hili humu JF Tundu Lissu: CHADEMA tumeanza kupokea Ruzuku

Chadema wameufuata ushauri wa bandiko hili, waneacha ujinga wa kujifanya hawayatambui matokeo ya uchaguzi wa 2020!, sasa wameacha kushupaza shingo, wameyatambua matokeo kimya kimya!, wamewasamehe mashujaa hawa kimya kimya msamaha ambao utatangazwa rasmi siku ya Jumatano tarehe 8 Machi na Mwenyekiti wa Chadema, mbele ya Rais Samia!.

Iliwa kusemwa kuwa hakuna mkate mgumu wowote mbele ya chai!, tayari Chadema imeisha anza kupokea ruzuku hivyo sasa ita survive!. Na ile kesi ya kina Halima Mdee na wale 19 iliyopo mahakamani itafutwa!.

Hongera sana Chadema, for doing the right thing!, mtabarikiwa, viongozi wenu watabarikiwa, chama chenu kitabarikiwa na Tanzania Itabarikiwa!.
Mungu ibariki Chadema
Mungu ibariki CCM kwa kukubali reconciliation
Mungu ibariki Tanzania
Paskali
 
Aisee umenifanya niisubiri hiyo tarehe 8 kwa hamu sana, nione kama watawasamehe wale wanawake 19.

Kwangu wale wanawake walishindwa kuheshimu maamuzi ya chama, lile lilikuwa ni kosa ambalo halihusiki kabisa na maridhiano.

Na hiyo kesi ya kina Mdee sioni kwanini ifutwe, kwani nani "aliyemuomba" Rais aifute?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…