CHADEMA sasa hivi wanashikiwa akili na Lissu, Lema na Wanaharakati

Mkuu katika mada yako una maanisha "maslahi ya taifa" ama " maslahi ya CCM" na pia unazungumzia "national security" ama "CCM security"?
 
Kipindi Rais Samia ameingia madarakani tulisihi tumpe MUDA aweze kuweka uchumi na nchi katika mstari.
Kipindi cha JPM mliomba muda wa kufanya jambo hilo hilo - je mliwahi kukiri kuwa hakulifanya?
Ameingia huyu mnaomba muda wa kufanya yale yale - Kuna nini? Hayafanyiki? au wewe unatudanganya?; na kama hutudanganyi basi kiri kuwa JPM hakuweka uchumi na nchi kwenye mstari!
 
Siyo Mbowe tena.
 
Na wewe ulitaka vijana wa CHADEMA washikiwe ajili na nani?
 
Watanzania wanataka Maendeleo sio siasa na Porojo. Watanzania wanataka Uhuru, Haki na Usawa. Watanzania wanataka amani na utulivu wa nchi ili waweze kupambana kubadilisha maisha yao. Siasa zijikite kutatua kero za wananchi sio kujenga mipasuko na kugawa wananchi huko Space
 
Ujue na mama yako Ni Chadema mwenzetu. Uliyotukana yanamhusu hata mama yako
 
CHADEMA wakajazwa upepo na ‘Team Space’ kuanzisha vuguvugu la Katiba Mpya.

Kosa ni kujaribu ku-Sabotage Rais Samia ashindwe ku-control
Acha kuongopa sheikh..... katiba na sabotage wapi na wapi?..

.. Muogope Allah sheikh, acha kutetea uhuni na uonevu.
 
Si dhani kama uko sahihi!
Binafsi nafahamu mbowe yuko korokoroni kwa kuwa na tuhuma za ugaidi.
Wewe hayo ya katiba umeyatoa wapi!
Labda kama unataka kufungua mashtaka mapya, tueleze
Haongelei mbowe[emoji851][emoji851],
Cdm kuna shida, ndo maana viongozi makini kama mnyika wametulia tulii
 
Hiyo ni mbaya sana kwa vile Tissu, lema na wanaharakati ni maadui zao CCM.
 
Inaonekana umefufuka kutoka wafu walio kufa wakiwa mashetani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…