GE2025 CHADEMA: Tumepata taarifa ya Tundu Lissu kutaka kupewa sumu

GE2025 CHADEMA: Tumepata taarifa ya Tundu Lissu kutaka kupewa sumu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwa hiyo ufafanuzi wa Serikali ndo utamaanisha hawataki kumuua?

Hakuna watu wenye intelejensia kali kama wazungu.

Ukiona wamesema ujue lmefanyika na wamepata taarifa au linapangwa kufanyika na wamepata taarifa.
Wasuka njama ni Mbowe na ibirisi wa ccm na ikubumbukwe FBI Scotland yard na vyombo vya uchunguzi vya kimataifa vipo Tanzania kwa nguvu ya ICC The Hague wanakusanya taarifa zote ili Lisu akitoka jela watesi waonevu wote wafikishwe kwenye mahakama ya uhalifu The Hague
 
TAARIFA KWA UMMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuujulisha umma kuwa kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa zinazodai kuwa Mhe. Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuna mipango ya kuwekewa sumu akiwa kizuizini.

Taarifa hizi zimetolewa usiku huu wa leo, tarehe 02 Julai 2025, kutoka kwa vyanzo mbalimbali vya kuaminika. Miongoni mwa waliotoa kauli kuhusu suala hili ni Mhe. David McAllister, Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya (European Parliament), ambaye kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) ameandika:

"Nina wasiwasi mkubwa kuhusu ripoti za kutisha za jaribio la kumtilia sumu kiongozi wa upinzani wa Tanzania Tundu Lissu akiwa kizuizini."

Chadema inachukulia taarifa hizi kwa uzito wa hali ya juu. Hili si jambo la kupuuzia, hasa tukikumbuka kuwa si mara ya kwanza kwa viongozi wa Chadema kulengwa na vitisho, mashambulizi au uonevu wa aina mbalimbali, huku taarifa nyingi tulizowasilisha kwa mamlaka husika zikipuuzwa au kutochukuliwa hatua yoyote.

Tunazitaka mamlaka husika, likiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Mahakama kuchukua hatua za haraka, huru na za kina kuchunguza madai haya mazito. Tunaitaka Serikali kutoa kauli ya wazi na kuwajibika kuhakikisha usalama wa Mhe. Tundu Lissu akiwa kizuizini.

Pia, soma; IDU tunafatilia njama za kumuwekea Lissu sumu Gerezani

Tunatoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa, Mashirika ya Haki za Binadamu, Mabalozi na wahusika wengine wote wa kimataifa kufuatilia kwa ukaribu suala hili na kushinikiza uwajibikaji, ulinzi wa haki za binadamu, na kuheshimiwa kwa misingi ya demokrasia nchini Tanzania.

Imetolewa leo Jumatano, tarehe 02 Julai 2025

Brenda Rupia

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi


View attachment 3391862
JPM akasome.Et alikuwa Doktator!!
 
Wasuka njama ni Mbowe na ibirisi wa ccm na ikubumbukwe FBI Scotland yard na vyombo vya uchunguzi vya kimataifa vipo Tanzania kwa nguvu ya ICC The Hague wanakusanya taarifa zote ili Lisu akitoka jela watesi waonevu wote wafikishwe kwenye mahakama ya uhalifu The Hague
Vyovyote vile muhusika mkuu ni Samia
 
Wamagharibi sio watu wazuri, khofu yangu yasitokee kama ya congo na sudan. Watanzania shtukeni


Free palestine 🇵🇸
Iran 🇮🇷 🔥
 
Hii sio habari ya kupuuzwa kabisa, huyu mshenzi kwa jinsi alivyochanganyikiwa na madaraka anaweza kufanya lolote ili kumuondolea bugdha.

VamP.jpg
 
Wamagharibi sio watu wazuri, khofu yangu yasitokee kama ya congo na sudan. Watanzania shtukeni


Free palestine 🇵🇸
Iran 🇮🇷 🔥
Washauri wa Mama iddy Amin Dada mkoloni kaburu toka Zanzibar ndiyo wameamua kumchuuza afanye mambo ya hovyo baadae wapate kisingizio cha kumwengua kwenye mbio za Urais waweke Mtanganyika
 
Hizo taarifa ninazo kabla ndo maana nikaishauri serekali imuhudumie Lissu kila kitu magereza wasipokee chochote kutoka kwa watu wa Chadema kumpa Lissu wanaweza kumuua ili waichonganishe serekali na wananchi
Kitendo cha Lisu kutokea gerezani akiwa na bashasha kinawaumiza sana majizi ya ccm. Na alipoamua kujitetea ndio imekuwa mbaya zaidi kwani anawamaliza mawakili vilaza wa ccm. Na anaivua nguo mahakama kuwa inapokea maelekezo kwa majizi ya ccm. Namna pekee ni kumuua Lisu baada ya dhalimu magu kushindwa kwa risasi.
 
Hii sio habari ya kupuuzwa kabisa, huyu mshenzi kwa jinsi alivyochanganyikiwa na madaraka anaweza kufanya lolote ili kumuondolea bugdha.

View attachment 3392004
Dikiteta mkoloni kaburu toka Zanzibar wenye ccm yao akina Bashiru na wenzao sasa wanamchochea afanye vitu vya hovyo wapate kisingizio cha kumwengua ugombea Urais
 
Washauri wa Mama iddy Amin Dada mkoloni kaburu toka Zanzibar ndiyo wameamua kumchuuza afanye mambo ya hovyo baadae wapate kisingizio cha kumwengua kwenye mbio za Urais waweke Mtanganyika
Idi amin alikua mtu poa sana, sema mlikaririshwa uongo kwamba anakula nyama za watu.

Waweke mtanganyika, huu Muungano una maana gani sasa, si bora uvunjwe tu!
 
Back
Top Bottom